Kaka Ahsante na wewe. Inabidi nilale maana saa hizi, ni kulala kwa dakika chache si saa chache. Hayo ni matokeo ya saa 7.15 (01.15hrs) ambako CCM walikua wakiongoza kwa tofauti ya kura takriban 2000, lakini kasi ya Chadema ilikua kubwa kwani saa 6.06(00.06) CCM walikua wakiongoza kwa tofauti ya kura 4,000 ambazo baada ya saa moja za Chadema ziliongezeka. Lakini wakati huo sehemu kubwa walikua wamekwisha kuhesabu. Kuna UKIUKWAJI mkubwa wa taratibu katika uchaguzi huo na kwa hali ilivyo KAMA CCM watashinda itakua ni ushindi wa AIBU. Kwa idadi kubwa ya wabunge walionao hawakua na sababu ya kufanya yaliyotokea Kiteto, pamoja na kuwa ni MKAKATI WA kuzuia UPEPO wa MABADILIKO.
Halisi,
Asante sana kwa kutufahamisi hizo za huko Kiteto. Nafikiri CCM hawakuwa tayari kuona wimbi la mabadiliko linaendelea maana wananchi wakishajua mwisho wa CCM unakaribia, basi wangeongeza speed ya kuwamaliza.
Pia mimi nina matatizo makubwa na strategy ya CHADEMA hasa kwenye suala la umoja wa vyama. Wameenda kule kama CHADEMA zaidi badala ya umoja wa vyama. Naelewa sheria haziruhusu mgombea wa muungano wa vyama, lakini bado ningelikuwa mimi jina la CHADEMA lingeishia kwenye hizo forms na makaratasi ya kupigia kura.
Kampeni nzima ingeendeshwa kama vyama vya upinzani na ingesimamiwa na kiongozi wa chama kingine. Kwa mfano kwasababu mgombea alikuwa wa CHADEMA basi Mrema au Lipumba ndiye angeongoza kampeni, huku Mbowe anafuata nyuma.
Kuwakosa CCM wakati huu ambao kila mtu anawaona ni mafisadi naona ni pigo kubwa sana kwa upinzani. Kama waliko na mashabiki wengi, watu wachache walipiga kura, huenda hapo CCM walinunua kadi za kupigia kura na kuzichoma moto.
Kuwashinda hawa jamaa lazima upinzani wawe wamejiandaa kuwatoa CCM kwa knock out.