Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 60
umaskini kwa kwenda mbele,endeleeni tuu kuwachagua ila msije hapa mnalia Buzwagi wala BOT na Richmond...miaka karibu 50 ya uhuru hakuna umeme wala maji,sanasana ni rushwa tuu na wizi,mungu awasaidie kuwaonyesha njia maana hiyo ni disease.
Nashindwa kuwaelewa watu ambao bado wanaipigia kura CCM.
Baada ya maskendo yote haya,je hawa watu hawaoni?
Je ni kitu gani CCM imewafanyia?
Nimechanganyikiwa !
Unajua wapinzani hawana sera hichi kibano wakizoee mpaka siku ile watakapobadirika na sera zao.
watu hatuoni kwanini wapewe CHADEMA/CUF/NCCR ambao hawafahamiki namna ya uendeshaji wao.
umaskini kwa kwenda mbele,endeleeni tuu kuwachagua ila msije hapa mnalia Buzwagi wala BOT na Richmond...miaka karibu 50 ya uhuru hakuna umeme wala maji,sanasana ni rushwa tuu na wizi,mungu awasaidie kuwaonyesha njia maana hiyo ni disease.
...... Hujiuliza ni kwa nini wananchi wameandamana maelefu kwa maelfu na kumshangilia sana Lowasa wakati sisi hapa wote tumekuwa tukimuona Lowasa ndio kiongozi wa ufisadi nchini mwetu? .....!
Nashindwa kuwaelewa watu ambao bado wanaipigia kura CCM.
Baada ya maskendo yote haya,je hawa watu hawaoni?
Je ni kitu gani CCM imewafanyia?
Nimechanganyikiwa !
Hata wewe mkuu? Nilitegemea uwe critical kidogo kwa jinsi ninavyokujua. Yaani wewe kweli unaamini wapinzani wameshindwa kwa sababu ya sera? Hujiuliza ni kwa nini wananchi wameandamana maelefu kwa maelfu na kumshangilia sana Lowasa wakati sisi hapa wote tumekuwa tukimuona Lowasa ndio kiongozi wa ufisadi nchini mwetu? Hebu tulia kidogo, achana na ushabiki cheap na ujiulize zaidi, najua kabisa kwa jinsi ninavyokujua unaweza kufanya bora zaidi ya hapo!
Nashindwa kuwaelewa watu ambao bado wanaipigia kura CCM.
Baada ya maskendo yote haya,je hawa watu hawaoni?
Je ni kitu gani CCM imewafanyia?
Nimechanganyikiwa !
Chadema wanapaswa kuondokana na upuuzi wa kudhani kuwaonyesha wananchi 'helikopta' ndio mvuto mkubwa wananchi wawape kura. If anything, this in itself should be reason enough to vote against them.
Nakubaliana na mawazo ya Mkjj. Kila uchaguzi unategemea umejipanga vipi, na ni mikakati ipi umeiweka kufanikisha azma yako ya uchaguzi. Je, unawajua vizuri wapiga kura wako? Unayajua vizuri mahitaji yao?
Huwezi kwenda tu kuomba kura kwa kelele za jukwaani. Mgombea wa Chadema alishagalagazwa mara kadhaa katika jimbo hilo hilo. Je, kabla ya kumteua tena kugombea mara nyingine, walijiuliza ni sababu zipi zilizokuwa zinamfanya ashindwe; na kama walizijua, ni yapi waliyokuwa wameyafanya safari hii ili aweze kukubalika zaidi!
Chadema, kama chama inawabidi pia wakae chini ili wajitazame upya. Their top leadership may not be inspiring enough to the wananchi.
Mie naona udhaifu wa wapinzani ni huu mtindo wao eti kuibua uozo wa mwazako na kuufanya SERA,kuibua uozo ni vyema lakini kuufanya ndio mgongo wa kupandia ni makosa makubwa ,hii naifananisha kama mtu yule anayemtaka mwanamke kwa gia za kumuambia maovu ya mwanaume aliyenaye.Mwanaumme aliyenaye anaweza akawa muovu sana lakini wewe kupitia mgongo huo ili ufanikishe adhima yako na kama mwanamke huyo ni makini hakika hutompata
..kitila,
..wapinzani[au vyama vingine nchini]vina kazi kubwa ya kujipanga kiuongozi[kwa kuwa na viongozi bora zaidi] na kimkakati wa kukuza vyama vyao na kujijenga kwenye mashina. bado kazi ngumu.
..issue ya lowassa ni suala la muda tu! tik tak tik tak!
Hata wewe mkuu? Nilitegemea uwe critical kidogo kwa jinsi ninavyokujua. Yaani wewe kweli unaamini wapinzani wameshindwa kwa sababu ya sera? Hujiuliza ni kwa nini wananchi wameandamana maelefu kwa maelfu na kumshangilia sana Lowasa wakati sisi hapa wote tumekuwa tukimuona Lowasa ndio kiongozi wa ufisadi nchini mwetu? Hebu tulia kidogo, achana na ushabiki cheap na ujiulize zaidi, najua kabisa kwa jinsi ninavyokujua unaweza kufanya bora zaidi ya hapo!
Hapa ndipo nitakubaliana na Einstein kwamba "Siasa ni Ngumu Kuliko Fizikia"!
I agree. Picha ambayo naanza kuipata ni kwamba kuna mambo ambayo sisi tunafikri ni matatizo wananchi wa kawaida hawaoni kama ni shida. Kwa mfano, hili swala la ufisadi sidhani kama watanzania wa maeneo ya Kiteto na kwingineko wanafikiri ni matatizo yanayowahusu. Yaani hawawezi kuoanisha kabisa kati ya shida walizo nazo na wizi wa pesa za serikali unaofanywa na CCM. Vinginevyo isingewezekana waichague CCM au kumshangilia Lowasa kwa kiwango tulichoona. Hapa ndipo nitakubaliana na Einstein kwamba "Siasa ni Ngumu Kuliko Fizikia"!
Kitila Mkumbo,
Nakubaliana nawe, lakini tujiulize pale makao makuu ya CHADEMA -Kinondon, Dar es Salaam... Neno "Kiteto" limeanza kutamkwa mara nyingi lini kama sio juzi wakati Mh. Mbunge wa kule alivyofariki...
Mimi nadhani niwapongeze wananchi wa Kiteto kwa sababu moja, kura sio za kuchukuliwa kirahisi tu, you have to be close to them!!! haiwezekani miezi miwili ya kuona helikopta iwe ndio kigezo cha kupewa kura, au kashfa ya Buzwagi, BOT, etc... udhani wapinzani wasafi pia... NARC ilivyoingia madarakani Kenya kwani ilifanya nini?
Tunahitaji chama tawala imara kinacho-be closely monitored.Kwa vyovyote vile wewe uliosoma science, kweli siasa ni rocket science... that what I can say!!!
Wa town wako kama 99% ya wana JF ambao wanajua mambo .Hawajali Chama ila wanataka kuona Nchi yao inasonga mbele kwa maendeleo.Leo ukiweka kura JF naamini CCM hawataona ndani na ushahidi umeuona hata Mwema na kundi lake wakaamuwa kuwamata vijana wetu kwa sababu ambazo sizijui wala wewe .Wajanja wote wanaokataa CCM .Ukimuona mjanja anaipenda CCM jua yuko highly connected na UFISADI .
Kalamu, simplicity is the enemy of truth. Unarahisisha mambo mno hapa. Helicopter haiwezi kuwa moja ya sababu za CHADEMA kushindwa. Una uhuru wa kushangilia ushindi wa CCM lakini huna haki ya kupotosha mambo kwani hujafanya utafiti wowote wa kisayansi wa kukuwezesha kufikia hitimisho kubwa kama hili. Wote tulikiri hapa kwamba CHADEMA walitekeleza wajibu wao, wamewaeleza wananchi kwa nini wawachagua wao na sio CCM, wamefanya bidii kubwa hata matokeo yanaonyesha hivyo lakini walizidiwa kura na CCM. Sasa kwa vyovyote tatizo haliwezi kuwa upande wa CHADEMA pekee. The problem here is bigger than you seem to suggest. Clue mojawapo ya kuangalia ni hii; inawezekanaje wananchi, watanzania hawahawa wamshangilia Lowasa kwa kiwango tulichoshuhudia, mtu ambaye tumemzomea kila kona kwamba ni fisadi? Sasa hapa lazima ujue kwamba upeo wetu wa kuona mambo ni tofauti sana na wananchi. Narudia tena tatizo hapa ni kubwa zaidi kuliko unavyotaka tuamini hapa.
You
Kimsingi, kati ya mgombea wa CCM na CHADEMA, mgombea wa CCM alikuwa anakubalika zaidi ya mgombea wa CHADEMA. Huenda kama CHADEMA ama upinzani ungemsimamisha mtu anayekubalika zaidi labda matokeo yangekuwa tofauti na yalivyokuwa.