Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Status
Not open for further replies.

Hii kiboko!
Yaani kura 1000 walizopishana ndio za "KUGARAGAZWA"? Ingekuwa kura 10000 je ungesemaje?
Hata hivyo hongereni kwa ushindi, tuchape kazi tujenge taifa, uchaguzi ushaisha.
 

Kitila,

Historia iko upande wa CHADEMA na sidhani kama huu ni wakati wa kukata tamaa. Uchaguzi umefanyika na ccm wametangazwa washindi na hakuna mtu atakayekumbuka alichofanya Komba na Msekwa.

Hili lilikuwa jaribio zuri na hongera CHADEMA kwa kazi nzuri.
 

Nilidhani mapinduzi yanatakiwa yafanywe ndani ya ccm ili nchi isiendelee kuuzwa kama ilivyo sasa?
 

..nadhani unakumbuka ulipokuwa ukibadilishana mawazo na jamaa wa kijiji[au kutoka huko]ulipokuwa unarudi nyumbani likizo. what you learned in those days,still applies todate! ujinga ni mwingi. na dawa ya ujinga si propaganda[unaumwa malaria,unahitaji dawa yake na si panadol ya kupunguza maumivu]ni elimu na habari!

..sasa,huku sisi[na mola jaalia tuna ka-elimu kidogo]tuna elimishwa kila leo na habari ziko upenuni tu! wao wala hawana habari. unafikiri huwa wanayaona hayo majumba ya mbezi beach na hizo vogue au mark x kama mimi nawe?

..kazi ngumu! vyama vingine[ccm kando]vitahitaji kufanya kazi na kupiga fitna sawia, ili viweze kupata angalau "maji ya kunywa" achilia mbali hicho "chakula".

..na kwa wale wasiofahamu,hata ingekuwa chadema,wasingekubali jimbo liende kwa ccm kirahisi!hata wao wangetumia mbinu zote walizonazo chini ya mvungu kushinda. ila ustaarabu umeonekana katika kukubali mapema,kupitia tanzania daima ofcourse!
 

Mzee Pundamilia, katika netiquette kuandika kwa herufi kubwa tupu maana yake ni "kushout" kwa maana ya kupiga kelele. Sidhani kama hilo ni kusudio lako kwani ulichosema ni muhimu mno na ni hoja inayohitaji kujibiwa lakini kwa vile unapiga kelele basi reaction ya kwanza ya wasomaji kama mimi ni "negative" (ni kama mtu anakuambia jambo la maana huku anakubwakia sikioni). Ila hoja yako ni hoja nzito ila haiwi nzito kwa vile umepiga kelele, bali kutokana na mantiki ndani yake.
 
Wewe watukane wazee wako tu.. wakichagua chadema/wapinzani ndio wanakuwa werevu?

Mafisadi aliwachagua nani? Basi naona tuamue moja kuchagua mafisadi na kuacha kulalamika kuwa wametuibia sijui Buzwagi/Richmond/EPA etc au kutibu kansa yetu all-together..kwa kuwafurusha kwa kura zetu..

Tuamue moja, sio kuwa vigeugeu..We can't have both..
 

Mabadiliko ya kweli hayaji bila kuwa na mazingira muafaka ya kufanya watu wakataka mabadiliko kwa gharama yoyote ile. Kwa sasa sisiemu wanatengeneza hayo mazingira kwa kufilisi nchi na kutajirisha watu mia moja (sera ya Kikwete).

Baada ya muda, kanga na kofia havitamnunua mtu ambaye hana chakula cha mwezi mzima!
 
Ama kweli mwanakijiji leo kachanganyikiwa amefikia kutoa Thanks na lile jina lake la "mwafrika wa kike" ambapo mjadala huu halijachangia kitu. teh teh teh teh

Chadema inabidi wampoze Mwanakijiji kama kweli anatumia majina tofauti humu kwenye JF kuipigia debe chadema, makala yake kwenye Tanzania Daima, redio yake KLH NEWS na hasa makala maalum alioyowandikia wana Kiteto vyote havikufanya kazi.

Mbowe muongeze mshahara anapigana sana kijana huyu usijekumkosa na kuna member kasema hana kibali cha kutoka na kuingia Marekani, wana chadema wamfanyie utaratibu wa kupati vibali halali vya kuishi ili 2010 awasaidie kwenye Ground au kuzunguuka nae kwenye Helkopta, Naamini ni mpiganaji mzuri anzisheni mchango wa Mwanakijiji kuliko kumtumia tu bila kujali hali yake na mazingira yanayomkabili.

Mwanakijiji.

Usirudi nyuma ndio siasa.
 

Hii argument muhimu sana, inahitaji thread ya kujitegemea.
Tuendelee na mjadala!
 
Tatizo si la wananchi mimi naamini kabisa kuwa wananchi hawaichagui CCM ,hilo ni jambo ambalo nina uhakika nalo kabisa.
Ila Nilisema zamani hivi vyama vya upinzani viwachane na mambo ya kupiga kura ,waelekeze majeshi kwenye Katiba ya Nchi na tume ya Uchaguzi ,halafu mambo hayo yakishakuwekwa sawa basi hata mkuu wa Chama kama anatumika kuiunganishia CCM itakuwa vigumu kwani hata wapiga kura wanaonekana kusononeka ni kwa namna gani wameshindwa ,ukweli mchozo upo ndani ya tume ya Uchaguzi hakuna jengine haiwezekani CCM wakamate mpini na wapinzani wamekamata makali halafu mushangae kwa nini CCM hakukatika mikono itakuwa miujiza mikubwa sana.
Vyama vya upinzani vigomee kabisa kushiriki katika chaguzi hizi za sasa ,wadai tume au marekebisho ya Tume ,tume hii inayotoka katika mfumo wa Chama kimoja ikataliwe kwa nguvu zote na kuanzia ni kuwacha kushiriki katika chaguzi hizi ambazo hata upinzani ukipata mbunge inakuwa hakuna nguvu ya kudhibiti harakati za Chama Tawala ,hivyo sababu ya kudai tume huru inayoshirikisha wadau wote ianzie katika hizi chaguzi zinazoibuka kabla ya kukaribia Uchaguzi mkuu ,leo Serikali ambayo inaongozwa na Chama Tawala CCM inasema tume haina matatizo ,katiba haina haja ya kufanyiwa marekebisho ,Serikali inajifanya kama haina habari kuwa sasa Tanzania ipo katika mfumo wa vyama vingi na kila kitu chake ni lazima kifanyiwe ukarabati ili kukidhi haja ya kuwepo kwa vyama vingi katika Taifa la Tanzania.
Serikali kusema kila kitu ni sawa na hakina matata wala matatizo ni kujibebesha msalaba ambao utaipeleka nchi pahala pabaya , kila kitu kitakuwa sawa na kitakuwa hakina usumbufu wala mazonge kama kitakarabatiwa na kujulikana kuwa kimepatika na kutungwa katika mfumo wa vyama vingi ,hakuna mtu atakuja kulalama na kupiga makelele ,atakaeshindwa atakuwa hana sababu zaidi ya kushindwa katika mbinu za kampeni
Lakini leo hata ufanye kampeni za aina gani basi bado utakuja kupigwa mueleka na harakati na mikakati ya tume iliko chini ya Chama kimoja ,hata wananchi wote wachague mgombea kutoka upinzani bado tume itatekeleza mkakati wa kuhakikisha Chama chao kinabaki na kunyakua ubunge au uwakilishi na hata Uraisi ,kama mnakumbuka Zanzibari kule Karume alisema hata watu wote wasipomchagua basi kura yake na ya mkewe inatosha kumfikisha Ikulu ,hapa utapata kuona kuwa mikakati ya tume hizi za sasa si kuona uchaguzi unafanywa kwa kuzingatia matakwa ya wananchi bali mkakati ni kuhakikisha kwa njia yeyote ile mgombea kutoka chama chao anabaki kuwa mshindi liwalo na liwe.
 
.....

Mbowe muongeze mshahara anapigana sana kijana huyu usijekumkosa na kuna member kasema hana kibali cha kutoka na kuingia Marekani, wana chadema wamfanyie utaratibu wa kupati vibali

Sijui hili la kutoka na kuingia marekani linahusiana vipi na kinachoendelea hapa. Viroja huwa havishindani na hoja!?!
 

Huwezi kutumia wizi wa watu wachache ukasema ni chama ,chama sio physical entity ambacho kinaweza iba kitu.

Mfano ktk familia ya watu 8 mmoja kati yao anaweza akawa mjinga lakini huwezi sema familia ile ni jinga.

Failure ya tanzania sio ya CCM as CCM ila ya familia nzima yani watanzania.

Wapinzani wangapi wametulaghai wakati ule kwamba wao ni wema wamekimbia ccm maana ni chama kibaya leo hii NDIO viongozi na wafuasi wazuri wa CCM Je tutafahamu vipi huyu ni mlaghai,huyu ni propaganda ,huyu ni mtafuta madaraka??? kwa maneno matupu?? lahasha.

Haya mambo ya kuibua skendo si hoja kabisa ya kumfanya mtu apewe madaraka,kwani skendo hizi zimeanza kuibuliwa na wapinzani mbona mbunge wa CCM kama sikosei ni Mzee ndakaya ama kingunge ameibua skendo ngapi amefukuzisha mawaziri wangapi??

Kawaida ya mnafiki hua anakumonita tu ndg Kitila sehemu utapokesea ili ukumalize lakini mara kwa bahati mbaya juhudi za namna hii hua hazifanikiwi
 
Huwezi kutumia wizi wa watu wachache ukasema ni chama ,chama sio physical entity ambacho kinaweza iba kitu.

Mfano ktk familia ya watu 8 mmoja kati yao anaweza akawa mjinga lakini huwezi sema familia ile ni jinga.

.......

Vipi kama pesa ya wizi ndiyo inatumika kulisha na kuendesha familia?
 
Sijui hili la kutoka na kuingia marekani linahusiana vipi na kinachoendelea hapa. Viroja huwa havishindani na hoja!?!
Mwafrika wa Kike.
Hoja hii nilimpa mwanakjj naona wewe umekuja kujibu unanifanya niamini kuwa wewe ndio Mwanakijiji. kwani sikukutaja umekuja kujibu.
 
Mwafrika wa Kike.
Hoja hii nilimpa mwanakjj naona wewe umekuja kujibu unanifanya niamini kuwa wewe ndio Mwanakijiji. kwani sikukutaja umekuja kujibu.

Nani alikuambia kuwa kuna sheria hapa JF ya kuzuia watu kujibu au kuchangia hoja ?
 
Mabadiliko ya kweli hayaji bila kuwa na mazingira muafaka ya kufanya watu wakataka mabadiliko kwa gharama yoyote ile. Kwa sasa sisiemu wanatengeneza hayo mazingira kwa kufilisi nchi na kutajirisha watu mia moja (sera ya Kikwete).

..huwezi kufilisi nchi na kutajirisha watu[hata kama wachache]at the same time! unawachimbia kaburi tu!

Baada ya muda, kanga na kofia havitamnunua mtu ambaye hana chakula cha mwezi mzima!

..baada ya muda hakutakuwa na hizi kofia wala kanga!kutakuwa na mapanga na mikuki!
 
 
..hata chadema ili kishinde kinahitaji mapinduzi!muulize kitila[simaanishi yeye chadema!]!

Huu ni ukweli ingawa nina wasiwasi kuwa mapinduzi yakimalizika Chadema na vyama vya siasa basi kanda ya ziwa yote itakuwa imeuzwa kwa sinclair na wenzake. Sad but true
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…