Idimi
JF-Expert Member
- Mar 18, 2007
- 15,328
- 11,192
baada ya tamaa ya fisi kuona kuwa mkono wa binaadamu utaanguka wapinzani waliona kuwa CCM ambayo kwa sasa ina kazi kubwa ya kujisafisha na kujipanga itapoteza jimbo la kiteto.
wakawa na tamaa ya kuwa CCM itaanguka tu, wakaenda kwa majigambo na kedi, wakajiamini kupita kiasi.
magazeti yakanadi hapa JF kina Mkjj na wenziwe wakajilabu vya kutosha kuwa kipindi hiki wapinzani watatoa somo ambalo CCM hawatalisahau.
lakini baada ya kuona kinyume wazee wetu wamenywea hakuna breaking news wala cha nn kimya utadhani hakuna uchaguzi.
kilichobaki ni kusubiri matetezi ya ndugu zetu wapinzani.
wapinzani jee umoja wao utadumu?
jee watasoma alama za nyakati au watasubiri huruma ya wananchi bila ya jasho?
hivi ni kweli wananchi ni wajinga wakikichagua CCM ?
lini hii jeuri ya kuwadharau wananchi itakoma kwa wananchi?
lengo la CCM ni kuhakikisha bunge la 2010 kuwe hakuna wapinzani bungeni isipokuwa wapemba tena na huko tutagawana nusu kwa nusu.
tutawafunza kuwa jeuri si maungwana na siasa si lelemama
Hii kiboko!
Yaani kura 1000 walizopishana ndio za "KUGARAGAZWA"? Ingekuwa kura 10000 je ungesemaje?
Hata hivyo hongereni kwa ushindi, tuchape kazi tujenge taifa, uchaguzi ushaisha.