Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 60
Pundamilia07;146641 [SIZE="4" said:NI YAPI MANENO MUAFAKA YA KUWAAMBIA WAPIGA KURA WAKATI WAKUHITIMISHA KAMPENI ZAKO? JE UNAPASWA KUWAAMBIA UKWELI AU MANENO YA KUBABAISHA?[/SIZE]
VICTOR KIMESERA ANAISHI WAPI?
..huwezi kufilisi nchi na kutajirisha watu[hata kama wachache]at the same time! unawachimbia kaburi tu!
..baada ya muda hakutakuwa na hizi kofia wala kanga!kutakuwa na mapanga na mikuki!
Kaka Mzee MwanaKijiji nimeona mkuu!!! lakini nakuona umenyong'onyea sana mzee wangu, pole mkuu, as if umefukuzwa uwaziri mkuu kwi kwi kwi, naona umeonja yale mtani wako aliyoyapata hivi karibuni!!!
Jifunze kupokea matokeo yote... Siamini leo hii unatuambia tuchambue sisi wenyewe... Wakati wewe ni mchambuzi wetu mahiri...
Pole mkuu!!! kama unapata kinywaji please go and take some bottles!!!
Hili ndilo linaogopesha hapa!
..unajua kuogopa ni vyema lakini hakuna msaada sana!
..laiti kama wenye macho wangeona hili linakuja,and believe me liko njiani!
..mi wala siogopi,nasikitika tu! africa seem to have its unique ways of falling into violence!
..ni kama historia ya europe inajirudia africa!
Mzee Pundamilia, katika netiquette kuandika kwa herufi kubwa tupu maana yake ni "kushout" kwa maana ya kupiga kelele. Sidhani kama hilo ni kusudio lako kwani ulichosema ni muhimu mno na ni hoja inayohitaji kujibiwa lakini kwa vile unapiga kelele basi reaction ya kwanza ya wasomaji kama mimi ni "negative" (ni kama mtu anakuambia jambo la maana huku anakubwakia sikioni). Ila hoja yako ni hoja nzito ila haiwi nzito kwa vile umepiga kelele, bali kutokana na mantiki ndani yake.
Vipi kama pesa ya wizi ndiyo inatumika kulisha na kuendesha familia?
Tukianza kuulizana maswali ya nani anaishi wapi nadhani itakuwa tunaelekea Kenya na kwingine kwenye ukabila .....
..usiwe na wasi,Huu ni ukweli ingawa nina wasiwasi kuwa mapinduzi yakimalizika Chadema na vyama vya siasa basi kanda ya ziwa yote itakuwa imeuzwa kwa sinclair na wenzake. Sad but true
Ushindi wa CCM kiteto umeshakubalika na Chadema. What next? Ukweli vyama vya upinzani havijajijenga vijijini na pia wapiga kura wa leo hawajali sera bali hela wanazopokea wakati wa uchaguzi. CCM hizo zimejaa. Bado uwezekano wa kushinda hapo baadaye upo katika kujenga vyama kwenye msingi wa yote, vijijini. Wakazi wa mijini Tanzania hawazidi 30% na hao pia ni rahisi kufikiwa, kwa kutumia mbinu za soko, 70% iliyoko vijini ndio mtaji mkuu wa CCM na huko ndiko upinzani uelekeze nguvu yao. Niliwahi kwenda kutembelea jamaa zangu kijijini, katika mazungumzo kuhusu siasa na upinzani, mzee mmoja aliniuliza swali moja "una baba wangapi?" akimaanisha kwao CCM ni kama baba katika taifa letu na hakuna haja ya upinzani. Nilitambua ugumu wa kubadirisha fikira kwanibado 'partenal' thinking ndiy inayotawala. Labda ni ule msemo wa 'zimwi likujualo halikuli ukakwisha' ndio unaofuatwa na wapiga kura wetu.
Unataka kuonewa huruma sio? Uchaguzi sio lelemamaKasheshe unategea monitoring itatoka wapi kama upande mmoja umeamua kuwa ushindi ni wa lazima kwa gharama yoyote.
Unataka kuonewa huruma sio? Uchaguzi sio lelemama
You are a very good Joker, nafikiri ungewaambia wananchi wa Kiteto maneno haya kabla ya kura kupigwa, maana unadhani wananchi wa Kiteto ni mambumbumbu.
Kimsingi, kati ya mgombea wa CCM na CHADEMA, mgombea wa CCM alikuwa anakubalika zaidi ya mgombea wa CHADEMA. Huenda kama CHADEMA ama upinzani ungemsimamisha mtu anayekubalika zaidi labda matokeo yangekuwa tofauti na yalivyokuwa.
HONGERA CCM, WAPINZANI ENDELEENI KUJIPANGA YA KITETO NI HISTORIA SASA.
Ndio nasema hoja zetu nyingi zimejengwa katika misingi ya hisia kiasi kwamba inakuwa vigumu sana kutoa counter-argument. Angalau kwa habari ambazo tulikuwa tunasoma kwenye magazeti tunajua hili sio kweli. Sio kweli kwa sababu huyu mgombea wa CCM alikuwa hawezi kabisa kuongea na ilifika mahala akipanda jukwaani wananchi wanamzomea. Siku za mwisho za kampeni ilibidi viongozi wa CCM waache kumsimamisha jukwaani ili kuepuka aibu ya kuzomewa. Kwa hiyo kimsingi wananchi wale wamechagua chama zaidi kuliko mgombea. Hii pia inajibu hoja ya Kasheshe.
Tunatambua sana kwamba hii biashara ya kujenga chama mbadala haitakuwa rahisi maana tunapambana na chama ambacho kimejijengea sura ya unchi kwa muda mrefu kwa juhudi zetu sote. Sasa tunachotarajia kutoka kwa colleagues kama JF members sio kejeli bali kutiwa moyo ili tuendelee na mapambano. Ndiyo CHADEMA wameshindwa Kiteto; lakini tutakuwa naive kukataa ukweli kwamba walipambana na juhudi hizo zinajionyesha katika idadi ya kura walizopata. Ni kweli pia kwamba lazima CHADEMA na upinzani kwa ujumla wajipange vizuri zaidi kwa ajili ya chaguzi zijazo na pengine kubadilisha mbinu na tunashukuru kwa wale wanaotoa mchango wa namna ya kuisadia CHADEMA ijipange. Tunapokea vijembe vya watu kama akina Mtu wa Pwani maana hawa tunajua ni watani zetu. But I don't expect other JF analysts to be simplistic and in their analysis in their attribution of CHADEMA's failure in Kiteto.
Sasa wewe hebu tuelezee katika kipindi cha miaka miwili tangu uchaguzi wa 2005, CCM imegubikwa na kashfa nzito nzito zinazotangwa kila kukicha katika magazeti, redio na TV hivyo kila mpiga kura wa Kiteto ama alisoma au kusikia kashfa hizo. Sasa kama bado aliona kuna umuhimu wa kuipigia kura CCM, basi kuna kasoro fulani maana unaipigia kura CCM kwa kipi hasa walichokifanya kinachostahili kuwapa kura? 😕