Kasheshe
JF-Expert Member
- Jun 29, 2007
- 4,694
- 790
Unajua Mwanakiji Kuna Watu Tunao Humu Jf Lkn Akili Zao Zimeshikwa Na Mafisadi,sasa Nyie Mnaona Raha Gani Ccm Kushinda?halafu Miongoni Mwa Hao Wanaoshangilia Huo Ushindi Hata Kadi Ya Ccm Hana Sasa Si Aibu Hh,au Ndio Mnafikiri Wote Walio Hapa Jf Ni Wapinzani Wa Ccm?tuliowengi Si Wana Ccm Wala Wa Pinzani Wa Ccm,ss Tunataka Kuona Maendeleo Yanapatikana Huko Bongo.kwa Maana Nyingine Tunataka Habari Zinazowachomoa Mafisadi Katika Mashimo Yao .
Kaboka,
Wewe na wananchi wa Kiteto waliopiga kura nani anafahamu hao wagombea... wewe au wao!!!
Mbona CCM kuna sehemu haitii mguu inagombea tu kwa mazoa kama majimbo ya Karatu(Dr. Slaa), Moshi Mjini(Ndesamburo)!!! ni kwa sababu mtu yuko capable... wananchi wanafahamu kwanini wamchague nani, Kule Kiteto hawakuwa wanachagua mbunge wa Taifa walikuwa wanachagua mbunge wa Kiteto....
Upinzani kama uko makini kuna majimbo ya kukomba kwa urahisi... na ni ya Mjini, kuna jimbo kama la Kinondoni... ukiweka mtu mzuri kama Kitila lazima alambe...
Tuwe makini tusitukane wananchi!!! wananchi hao hao ndio Upinzani na CCM wanawahitaji ili wawekwe madarakani...
Ukiwa makini pia utasema CCM walikuwa nayo siku zote,,, lakini Mbowe, Zitto n.k. wamefika wakati wa uchaguzi tu...
Kuhusu idadi ya wapiga kura kuwa ndogo,,, ni muhimu kujua sasa ni kipindi cha kiangazi au la!!! si unajua wakati wa kiangazi... tena tunahamisha mifugo yetu....
Mkitaka wawe wengi, mubadilishe sheria ya uchaguzi kwamba kwenye majimbo ya wafugaji,,, uchaguzi ufanyike wakati wa nyasi za kulishia zikiwa za kutosha