Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Ni uchaguzi wenye makelele mengi mitandaoni, lakini hauna ushindani kabisa kiuhalisia field.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba kwa upande moja mgombea ni dhaifu sana ndani ya chama, yaani kwamba mgombea huyo anaungwa mkono nje ya chama, kwenye mitandao ya kijamii na wana harakati wasio na ushawishi kwa wajumbe, wala hawana athari kwenye sanduku la kura,
huku upande mwingine kukiwa na mgombea madhubuti, huku akiwa anaungwa mkono na wajumbe wa mkutano mkuu wa chadema taifa, ambao ndio haswa wenye maamuzi ya mwisho juu ya nani awe mwenyekiti wa chadema taifa.
infact,
hapatakua na mchuano mkali kabisa, wala hapatakua na ushindani siku ya uchaguzi, kwasababu kimsingi utakua ni uchaguzi baina ya mitandao ya kijamii isiyo na kura hata moja siku ya uchaguzi, dhidi ya mgombea mahiri mwenye idadi kubwa mno ya wajumbe wa mkutano mkuu wa chadema Taifa ambao wanamuunga mkono, na ndio wenye maamuzi ya mwisho.
Kama mdau wa siasa,
unadhani ni kwa kiasi gani mitandao ya kijamii imewapumbaza, imewaaminisha na kuwazubaisha wagombea uongozi wa nafasi mballimbali nchini, hususani kuelekea uchaguzi wa chadema Taifa?
Na Je,
kuna darasa au somo kwa wanasiasa, hususan wa chadema kujifunza? maana katika chaguzi nyingi chadema huzubaa na kujipiga kifua mitandaoni kwamba wanakubalika, wakati wakienda field wanajikuta hawajulikani, hawaeleweki wala hawafahamiki ?
Uchaguzi wa chadema ngazi ya taifa unatarajiwa kuanza tar.Jan.13,2025 kwa BAVICHA na BAZECHA kufungua pazia la uchaguzi ngazi ya taifa, wakifuatiwa na BAWACHA na hatimae uchaguzi wa chama Taifa katika ujumla wake Jan.22,2025.🐒
Mungu Ibariki Tanzania