Elections 2010 Uchaguzi wa Spika wa bunge la 10 la Tanzania

Elections 2010 Uchaguzi wa Spika wa bunge la 10 la Tanzania

INA MAANA MABERE HAKUCHAGULIWA NA CUF. WALIOMPA NI KAMA IFUATAVYO;

CHADEMA ==45
NCCR ==3
UDP==1
S. SITA NA MKEWE==2
JENISTER MHAGAMA ==1
DR. MWAKYEMBE ==1

KAFULILA WA NCCR NA MREMA WA TLP NAO HAWAKUMPA.

DU.........KAZI KWEIKWEI......
:yield:
Jamani hawa CUF mie nilishasema wabunge toka Z'bar hawana msaada wowote hebu cheki hapo...
 
hatimaye spika amepatikana na katika kujua kuwa kazi aliyonayo mbele yake ni kuwa amesema kuwa kuanzia sasa ataanza kujifunza sheria na kanuni za ni jinsi gani ataliongoza bunge la JMT. mh. spika A. Makinda amesema hayo katika hotuba fupi baada ya kuapishwa kuwa spika wa bunge la jamhuri wa Tz leo Mjini dodoma. hili bunge silipatii picha maana staili ya huyu mama kuwaamuru wabunge kaa chini akiona hoja ni ya kimbunga kwa chama tawala wakati wa bunge lililopita itamtokea puani. huu ni mzigo mkubwa sana ambao mafisadi wa nchi hii wameamua kuubwaga kwa akina mama eti wakaidai ni wakati wa mwanamke sasa. kweli kweli hii yatoka wapi sasa? ccm hii karata hamjachanga vizuri.
 
Anna Makinda kura 265

Mabere Marando kura 53

Kura zilizoharibika 9

Distrubution ya Wabunge ni Kama Ifuatavyo:
CCM 251
CHADEMA 45
CUF 30
NCCR 4
UDP 1
TLP 1

Ina Maana Hata baadhi ya wabunge wa CUF wamempigia mgombea wa CCM Kura

Shame on CUF!!!
 
Tanzania ni watu wa ajabu sana badala ya kuchagua kiongozi kwa kufuata uwezo tunachagua kwa kufuata jinsia hivi kuna nchi zenye kutetea haki za wanawake kama nchi za magharibi? Lakini hutakuta wanatoa nafasi za ubunge viti maalumu kwa wanawake au wanachagua kiongozi kwa kufuata jinsia isipokuwa uwezo wa mgombea kwa mtindo huu hatufiki popote.

Njia pekee ya kuwasaidia wanawake ni kupitisha sheria zenye haki kwa jinsia zote mbili si kugawa vyeo kwa kufuata jinsia badala ya uwezo ndo maana Tanzania hatutaendelea hata siku moja
 
Ameapa Freeman Mbowe tayari....anafuata Zitto...
 
wana great thinkers tunaomba mturushie picha za makamanda wetu wakila kiapo.
 
Hivi sie tusioamini mungu tuna kiapo chetu nasi?
 
Nimepokea habari hizi bila kushituka kwani ndicho kilichotegemewa

Namuomba sana Anna Makina, awageuke mafisadi kama alivyofanya Sitta, ikipita miaka mitano atakumbukwa kama shujaa... akiwakumbatia ataondoka kwa aibu

ANNA... WAGEUKE MAFISADI KAMA SITTA ALIVYOFANYA
 
Jamani mi sioni haja ya kushangaa.kwani tangu mwanzo move ilikuwa inaonesha MAKINDA anautwa uspika.Kuhusu CHADEMA kuunda kambi ya upinzani jambo la msingi.kwani Tunajua usiri wa muafaka ccm na cuf,Support ya MREMA wa TLP na ccm?.mi naona upinzani ni chadema tu.naamin hata bila CUF,TLP,UDP na NCCR,chadema wanaweza
 
Anna makinda huyooooooooooooo!! spika wa bunge la leo. mtoto wa aliyewahi kuwa regional commissioner wa Tabora miaka ya 70s na kwa mara ya kwanza akaibadili sura ya mji wa Tabora kati ya wafanya biashara wajeuri wa siku hizo ambao walikuwa na msemo wa " serikali ote iko fukoni - makinda weja wapi"!!! siku hizo maduka makubwa ya mjini Tabora yalikuwa mabanda yaliyoezekwa kwa madebe. Makinda aliwapa muda wafanya biashara hao kuezua madebe na kuezeka mabati kwa hiyari yao. walipobisha aliamuru wafungwa kuezua madebe na hivyo wafanya biashara kulazimika kuezeka mabati. hii iliwafungualia wafanyabiashara kuendelea kuboresha muonekano wa Tabora City centre.

kilichonifurahisha katika tukio la leo kabla ya upigaji kura ni shangwe aliyokuwa nayo mzee wa vijisenti - aligonga na anna kwa nguvu zake zote anna alipomaliza kujieleza na wakati akitoka nje.
 
kwa mujibu ya matokeo ya kura za uspika ,265-makinda, 53-marando, sasa imejidhihirisha wazi kuwa CUF, TLP, NCCR. Wana unga mkono CCM. Hii inaleta picha halisi ni nani anaye panda gari la mafisadi na nani anayepanda gari la wana mageuzi. Nadhani chadema haina haja ya kuwashirikisha CUF(ccm-2) n Co. Kwenye kambi ya upinzani!
 
kwa mujibu ya matokeo ya kura za uspika ,265-makinda, 53-marando, sasa imejidhihirisha wazi kuwa CUF, TLP, NCCR. Wana unga mkono CCM. Hii inaleta picha halisi ni nani anaye panda gari la mafisadi na nani anayepanda gari la wana mageuzi. Nadhani chadema haina haja ya kuwashirikisha CUF(ccm-2) n Co. Kwenye kambi ya upinzani! Lakini je, Anna Makinda ataweza kuuzima moto wa wabunge makini wa msimu huu!!?
 
Back
Top Bottom