Jambo moja ambalo CCM wanashindwa kulielewa ni ile kanuni ya maisha kwamba kila kitu kina climax yake na ikifika hapo basi kinachofuata ni kuporomoka. Zimepita dola nyingi tu dunia, wanahistoria watatusaidia lakini za karibuni ni ile ya Warumi, Wajerumani, Waingereza na sasa Wamarekani ambao nao tayari wameanza kuwahofia Wachina.
Kwa kanuni hiyo ni wazi CCM itaanguka tu, na tayari dalili zimeanza kuonekana, na hata wakilazimisha vipi haitawezekana kuzuia mabadiliko. Wametumia sana usanii katika miaka ya karibuni, bado hali sio nzuri kwao kinachokuja ni kuporomoka hata watumie risasi, wakati ukifika watatoka tu.