Kumbuka TLS si Chama cha siasa Bali Chama cha Kitaaluma.
 
Hahahaa mkuu kwani shida iko wapi?
Wazanzibar wanakuwaje wanachama kwenye chama cha wanasheria wa Tanganyika? Au Mzanzibari anakuwaje Rais wa serikali ya Tanganyika? Maana watetezi wa mfumo wetu wa ovyo wa muungano wanadai serikali ya Tanganyika ipo ndani ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaani maana yake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande mwingine ndiye Rais wa Tanganyika ambayo itashughulika na mambo yasiyo ya Muungano sasa katika hali kama hiyo Mzanzibar anakuwaje Rais wa Serikali ya Tanganyika ambayo inashughulika na mambo yasiyo ya Muungano? Halafu Rais huyo huyo tunayemuita Rais wa serikali ya muungano pamoja na Uzanzibar wake lakini hana mamlaka wala madaraka yoyote upande wa kwao Zanzibar!
 
Hatimaye matokeo ya TLS yametoka. Mwabukusi kaibuka Kidedea. Kumbe inawezekana umma utaamua.
Inawezekana sana.
Lakini pia kumbuka, hapa kuna fundisho pande zote. Waliopoteza kura sasa watakwenda kujipanga vizuri zaidi kwa kutumia mbinu zote wanazo zifahamu.
Walioibuka na ushindi wawe na imani kuwa inawezekana kushinda iwapo tu mbinu chafu zitadhibitiwa.

Ili kuzuia mbinu chafu, ni lazima wazijue hizo mbinu ni za namna gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…