Uchaguzi wa TLS 2024: Boniface Mwabukusi ashinda Urais, apata kura 1274
Screenshot_20240802_215301_X.jpg
 
Mwabukusi atakuwa rais kwa miaka 3, CCM mlichagiza wenyewe badala ya kuwa urais wa TLS kuwa wa mwaka mmoja CCM wakitumai kibaraka awekwe TLS.

Wakili msomi Boniface Mwabukusi urais wake TLS utakuwa kuanzia mwaka huu 2024 - hadi 2027 kipindi kizuri wadau wa demokrasia TLS kuunga mkono pressure ya kuelekea uchaguzi mkuu uwe huru 2024 / 2025
Kumbuka TLS si Chama cha siasa Bali Chama cha Kitaaluma.
 
Hahahaa mkuu kwani shida iko wapi?
Wazanzibar wanakuwaje wanachama kwenye chama cha wanasheria wa Tanganyika? Au Mzanzibari anakuwaje Rais wa serikali ya Tanganyika? Maana watetezi wa mfumo wetu wa ovyo wa muungano wanadai serikali ya Tanganyika ipo ndani ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaani maana yake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande mwingine ndiye Rais wa Tanganyika ambayo itashughulika na mambo yasiyo ya Muungano sasa katika hali kama hiyo Mzanzibar anakuwaje Rais wa Serikali ya Tanganyika ambayo inashughulika na mambo yasiyo ya Muungano? Halafu Rais huyo huyo tunayemuita Rais wa serikali ya muungano pamoja na Uzanzibar wake lakini hana mamlaka wala madaraka yoyote upande wa kwao Zanzibar!
 
Hatimaye matokeo ya TLS yametoka. Mwabukusi kaibuka Kidedea. Kumbe inawezekana umma utaamua.
Inawezekana sana.
Lakini pia kumbuka, hapa kuna fundisho pande zote. Waliopoteza kura sasa watakwenda kujipanga vizuri zaidi kwa kutumia mbinu zote wanazo zifahamu.
Walioibuka na ushindi wawe na imani kuwa inawezekana kushinda iwapo tu mbinu chafu zitadhibitiwa.

Ili kuzuia mbinu chafu, ni lazima wazijue hizo mbinu ni za namna gani.
 
Back
Top Bottom