Uchaguzi Wa Viongozi Wa CCM Wateka Anga la Siasa za Tanzania, CHADEMA yashikwa Mateka

Uchaguzi Wa Viongozi Wa CCM Wateka Anga la Siasa za Tanzania, CHADEMA yashikwa Mateka

Ndugu zangu CCM imeonesha umwamba wake wa siasa za hapa Tanzania,imeonesha kuwa ndio chama kikubwa na chenye ushawishi hapa Tanzania, imeonesha namna CCM ilivyo na nguvu hapa nchini, Imeonesha misuli yake ya kisiasa, imeonesha namna kinavyokubalika na kupendwa na watanzania,imeonesha namna ambavyo Ni ngumu kuizuia CCM mlangoni.

Katika uchaguzi wa ndani ya CCM wa viongozi mbalimbali katika ngazi tofauti tofauti unaoendelea nchini kwote umekuwa Ni gumzo hapa nchini. Mijadala yote ya kisiasa katika vijiwe vyote,mitaa yote,vyombo vyote vya Habari,mitandao yote ya kijamii Ni juu ya CCM na uchaguzi, Ni juu ya Nani kapitishwa na Nani kakatwa na Nani apigiwe kura za Ndio na Nani awe na Subira.

Ni uchaguzi ambao umeviteka vyama vya upinzani hasa chadema na kujikuta Vimesimamisha shughuli zake zote za kisiasa na kujikita kufuatilia uchaguzi wa viongozi wa CCM, kwa kuwa hakuna habari inayovuma kwa Sasa Kama uchaguzi wa CCM, Chadema imegeuka na kuwa Tawi la kuwatambulisha wagombea wa CCm, chadema ndio wamekuwa Kama maafisa habari wa habari za CCM juu ya Nani kakatwa na sababu za kukatwa kwake, chadema kwa Sasa imejikita katika kufuatilia kwa kina kinachoendelea katika uchaguzi huu na kusahau shughuli zao za ndani ya chama Chao

Hii Ni kutokana na Nguvu waliyonayo na wanayokuwa nayo viongozi wa CCm, hii Ni kutambua ushawishi wa viongozi wa CCm katika masuala mbalimbali yanayogusa maisha ya watanzania,kwa kuwa Hawa ndio wafuatiliaji wa utekelezaji wa ilani ya CCM, Hawa viongozi wa CCm Ndio wenye wajibu wakufahamu ikiwa wananchi wanapata huduma na kuhudumiwa Kama ilivyo ahidiwa katika ilani kupitia uchaguzi mkuu,Hawa ndio wenye ofisi ambazo zimekuwa wazi muda wote na kimbilio kwa waliokata Tamaa au kuonewa au kudhulumiwa au kucheleweshewa haki au kupokonywa haki.


Hawa ndio sauti kwa wasio na sauti na nguvu kwa wasio na nguvu, Hawa ndio unaoweza ukawakimbilia na kupokelewa kwa uharaka,Hawa ndio wanaoweza kumsikiliza mwananchi mnyonge yeyote mwenye shida, Hawa ndio wanaojuwa Hali za kimaisha za watanzania na kuishi nao, Hawa ndio Tumaini la wote,Hawa ndio wanaoweza kumuita kiongozi yeyote wa serikali atoe majibu kwa maswali ya wananchi,Hawa ndio wenye masikio sikivu na macho ya kutazama kila kitu


Hakika CCM itaendeleaa kuongoza nchi hii Daima Milele na Hakuna chama Wala mtu mwenye uwezo wa kuitikisa CCM hapa nchini ,hayupo na Wala hajazaliwa, Kama huamini Basi ondoka ndani ya CCM uone kama CCM itatikisika au kuteteleka. Hii ndio CCM chama kiongozi , Chama Cha Hayati Baba wa Taifa mwalimu Nyerere, Chama kinachoheshimika ndani na nje ya Tanzania,


Chama mkombozi wa nchi za kusini Mwa Afrika, chama kilichobeba matumaini ya watanzania, chama kinachokubalika na kuaminika na makundi yote ya watanzania,chama chenye dira na muelekeo unaoeleweka, chama kilicho na misimamo na misingi madhubuti , chama kinachotanguliza maslahi ya Taifa mbele. Ni chama kilicho katika mikono salama ya Mwenyekiti wake Shupavu,Mzalendo na Hodari mh Mama Samia Suluhu Hassan.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu: 0742-676627
Kumbe kila siku mnatafuta haueni ya CHADEMA kutosikika ili msilale na viatu?
 
Weka na profile yako mkuu
Sasa nafikiri utaelewa unajibiwa na nani humu JF
Screenshot_20221119-160357.jpg
Screenshot_20221119-160338.jpg


Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Wewe kama unajipendekeza ili uteuliwe acha kutumia mgongo wa CHADEMA tumia njia zingine.

Wenzako wakati wanafanya analigus hufanya kwa juhudi zao binafsi.

Achana kabisa na CHADEMA.
Hakuna chama Hapo zaidi ya ubabaishaji tu na utafunaji wa Ruzuku
 
Wanachadema sifa yenu kuu Ni matusi tu
Ni ushauri tu kijana, siku Moja utakumbuka, narudia Tena, acha siasa za kijinga, Jenga hoja zako bila kuwa biased, acha kusifia Kila "ujinga". Tumia hiki kipaji chako cha uandishi na huu muda wako kufanya maandiko yenye mashiko. Utanikumbuka
 
Tulipo Ni pabaya Sana

Tuna vijana wanaotafuta kujaza matumbo yao na hawafikiri Tanzania ya Baadae. Wanaogopa kusema ukweli wanaoshia kusifia tu

Ndio maana mi sitakagi chama chochote Cha siasa ,naogopa kufungwa na minyonyoro ya kusifia hata ujinga wakati uhalisia nauona.
Uchawa sahv umekuwa ajira mkuu

Huyu atakuja kuchoka mwenyewe

Ova
 
Utakuja kuchoka mwenyewe

Utapotea humu jukwaani kama

Waliyotangulia,

Ova
Sipo katika mashindano na mtu Mimi.Ndio maana unaona simtukani mtu yeyote humu kwa kuwa najuwa Kuna kutofautiana kunakonihitahi kuwa na uvumilivu napokosolewa
 
Wacha kujirusha ufahamu dogo muulize mwenzako wa Kakonko Eliya Michael

Njaa zako ni zako usiihusishe CHADEMA na kama unashida sana njoo nikupe Skills ujiajiri.
Mimi nilishajiajiri katika kilimo. Shamba langu ndio daftari langu na jembe langu ndio kalamu yangu na mabega yangu ndio begi langu
 
Back
Top Bottom