Uchaguzi wa Wanafunzi Kidato cha Tano na vyuo ni kilio kwa Wazazi masikini

Tatizo linaanzia kuwapa tamisemi wasimamie shule.. tamisemi hawa wanaojenga vyoo vya masoko na stand watapata wapi huo utalaam wa kuwapeleka wanafunzi kwenye mambo muhimu?


Waziri aliye pita alikua kama mganga wa kienyeji kwa kuhimiza nyumbu, unadhani kuna elimu hapo?
 
Usilitajetaje hili dikteta hata kwenye Mambo ambayo halikufanya cha maana. Hili dubwana liliharibu na kuizika kabisa sekta ya elimu.

Kama huna hoja kaa kimya, usituletee stori za dikteta uchwara kwenye mijadala muhimu.

Usilitajetaje hili dikteta hata kwenye Mambo ambayo halikufanya cha maana. Hili dubwana liliharibu na kuizika kabisa sekta ya elimu.

Kama huna hoja kaa kimya, usituletee stori za dikteta uchwara kwenye mijadala muhimu.
Fafanua alivyoiua elimu.
 
Usilitajetaje hili dikteta hata kwenye Mambo ambayo halikufanya cha maana. Hili dubwana liliharibu na kuizika kabisa sekta ya elimu.

Kama huna hoja kaa kimya, usituletee stori za dikteta uchwara kwenye mijadala muhimu.
Mwenye SACCOS kawaharibu sana hadi mnafikiri kwa masaburi na hata utu mumekosa utadhani mlizaliwa na wanyama.
 
Mimi mdogo angu kapata Div 1-14 PCB ana point 9 aliichagua ila wamempeleka Hgl km vile wao ndo wanamjua kutoka shule za kata, dogo imebidi aende tu kusoma hiyo hiyo maana shule aliyopelekwa Ni Ilboru, sasa haifai kubadili kwenda Pcb na point zake 9 na kuhama kwenda shule nyingine ni mtiti. Yaani sasa hivi badala ya serikali kusaidia kutimiza ndoto za wanafunzi imeamua kuua ndoto zao bora ht wangempeleka CBG
 
Finland mbona umeenda mbali sana, hata hapa jirani yetu Uganda kila mwanafunzi huwa na combi yake, unawezakuta darasa moja kuna combi zaidi 7
 
Hakuna MTU anayepanga chaguo la mwanafunzi akasome nini chuo au mchepuo kidato cha 5 pale TAMISEMI bali ni mfumo ulivyotengenezwa uteua kulingana na mwanafunzi alivyofaulu masomo na alivyojaza selform yake !

Kila mchepuo una alama zake. Kwa mfano PCB ni afaulu alama BCC yaani alama nane (8) na alama Tisa (CCC/Ccd) na kuendelea haiwezekani kupangiwa PCB kwa mwaka huu ! Hivyo utampangia mwanafunzi mchepuo ule aliofaulu sana katika maombi yake kulingana cutting points zake. Hapa ndipo aliyetarajia kupangwa mchepuo wa Sayansi anashangaa amepangwa mchepuo wa sanaa (hgl/hge) au chuo !

Mwisho ni wengi wanafanya makosa kwenye kuomba machaguo yao kupitia selform wanapopewa nafasi kurekebisha machaguo yao. Mfano mwanafunzi kajaza chaguo la kwanza ni chuo badala kidato cha tano. Nani alaumiwe akipangwa vyuo pamoja na kufaulu kwa daraja la kwanza ?

 
Halafu wakiulizwa wanakanusha ! Huyu Ndalichako ni shida sana , Kwa mara ya kwanza nailaumu sana JF kwa kumteua Ndalichako kuwa Waziri wa Elimu , tulikosea sana , ikumbukwe kwamba Ndalichako aliteuliwa kwanza hapa jf halafu ndio Dr Magufuli akafuatia

Sasa Ndalichako ndiye anapanga haya machaguo au ni TAMISEMI?!
 
Huu ni upumbavu,,,, unless wanafanya kuwapangia hivyo ili kupunguza tatizo la ajira nchini, labda wameona watoto wanasoma mafizikia, mahesabu, bailojia ambayo hayawasaidii wanapohitimu, so ni bora kumsomesha mtoto hotel management kama hii fani Ina ajira nyingi, ataajiriwa anapomaliza kuliko kusoma masomo magumu... uhangaike chuo then ukose kazi, ukae benchi ... but I still think kuwapangia watoto vitu wasivyopenda itawapungizia morale ya kusoma na pia it is ethically wrong..
 
Umeharibu maana ulipomtaja "mwendazake".
 
Tatizo ni resources. Ukiruhusu mtu asome chochote utapangaje madarasa, vyumba vitatosha walimu watatosha, time table itakuaje,mitihani watafanyaje...n.k.

Combi bado zipo sana tu
Unaona ni sahihi mtu aliyepata A ya chemistry kusomea hotel management?
 
Kuna mtoto wa jirani yangu alipo angalia matokeo ya kidato cha nne aliona amepata division one, selection zilipotoka hakuchaguliwa, mamaake akanipigia simu kuniuliza inakuaje nikamwambia anitumie namba yake ya mtihani kuangalia kumbe alipata div three ya 24 na combination hazijabalance maana yangu muwe mnachunguza kabla ya kuwalaumu Tamisemi
 
Nakupongeza kwa hoja hii. Imenikuna hadi kumtima. Mifumo yao imelewa
 
Emu ngoja kwanza ule mkopo kutoka WB wa kujenga mashule umetumikaje. Kuna wilaya haina hata HIGH SCHOOL hata moja. Au ndo mkopo uliishia kwenye uchaguzi.
Shule za Alevel ni chache sana kiasi kwamba wanaohitimu kidato cha nne na kupata ufaulu ni wengi sana na hakuna nafasi za kutosha kwenda form 5
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…