Uchaguzi Zambia 2026: Hakainde Hichilema ashinda Urais kwa muhula wa pili

Uchaguzi Zambia 2026: Hakainde Hichilema ashinda Urais kwa muhula wa pili

Anaandika Malisa GJ

Tume ya Uchaguzi nchini Zambia (ECZ) imemtangaza Hakainde Hichilema wa chama cha UPND kuwa mshindi wa kiti cha Urais wa nchi hiyo kwa kura 2,965,326 sawa na 60.1%, akifuatiwa na Brian Mundubike wa NRPUP aliyepata kura 1,856,217 sawa na 38.6% ya kura zote zilizopigwa. Wagombea wengine wamepata chini ya asilimia moja.

Hichilema mwenye umri wa miaka 64 amewahi kugombea Urais wa nchi hiyo mara 5 akishindwa, kabla ya mwaka 2021 kufanikiwa kumwangusha Rais Edgar Lungu aliyekuwa akigombea kwa muhula wa pili. Kwa matokeo ya leo, Hichilema ataongoza taifa hilo kwa awamu ya pili hadi mwaka 2031.

Hata hivyo mwitikio wa kupiga kura haukuwa mkubwa kwani ni watu milioni 4.9 tu waliojitokeza kwenye vituo vya kupiga kura kati ya watu milioni 8.4 waliojiandikisha.

Hichilema ametangazwa mshindi wa kiti cha Urais majira ya saa 9 usiku kwa saa za Zambia sawa na saa 10 alfajiri kwa saa za Afrika Mashariki. Tume ya Uchaguzi nchini humo (ECZ) haijaeleza kwanini imeamua kumtangaza mshindi wa Urais usiku wa manane watu wakiwa usingizini.

Hata hivyo wakati Tume ikitangaza matokeo hayo usiku, mgombea wa upinzani Brian Mundubike amejificha ofisi za umoja wa mataifa (UN) kuomba hifadhi akihofia kukamatwa na Polisi. Jana polisi walimtuhumu kwa uhaini, akidaiwa kusuka mipango ya kuiangusha serikali. Zaidi ya watu 20 walio karibu nae wamekamatwa na kupewa kesi za uhaini.

Pia mapema leo Wizara ya mambo ya ndani nchini humo, imemtangaza Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Mhashamu Trevor Selwyn Mwamba kuwa Mhaini na kwamba atakamatwa na kuunganishwa katika kesi ya kujaribu kuangusha serikali, inayomkabili Brian Mundubike na wenzake.!
Wamecopy na kupaste kutoka Tanzania, kumbe ni kweli TZ ilituma watu wa kusaidia ushindi
 
Wakenya,wanafanya kila liwalo,kuiondoa CCM madarakani, ili kuzisaidia nchi jirani kupata utawala bora! Vinginevyo uchafu uliopo utaenea Africa,na mwisho, Africa haitatawalika tena
 
Ukizungumzia utamaduni , hauoni kwamba utakuwa unajielekeza vibaya?
Maana hata haya mambo ya Vyama vyama sio tamaduni ya Mwafrika.
Au tafsiri yako ya tamaduni ni ipi?
Tamaduni za China jamaa kaeleza vizuri sana China unaweza kuwa kiongozi mkubwa na hakuna hata mtu mmoja kwenye familia yako nae akawa huko kwenye serikali todauti na Nchi za Afrika utawaongeza bila vigezo China wana mfumo wao na tamaduni zao ambazo hata chama kimoja kitafata yale matakwa ya Serikali na Wananchi wake.
 
Huyu mpinzani alipozingua pale aliposema Zambia ni taifa la kikristo. Huyu mgombea jau sana
Kwa katiba yao Zambia ni nchi ya kikristo. Sema hii nchi tulivu sana. Mtu yeyote anayepambana sana kuingia madarakani si rahisi kuwa mstaarabu.
 
Mahali popote CCM ikiingia, lazima laana iingie. Ilijipenyeza kwenye uchaguzi wa Mozambique, ikawa laana kubwa, mpaka watu kuuawa. Sasa ni Zambia, waombe sana kuepusha mauaji.
 
CCM kausikaje uko Zambia

Uyo mpinzani kazingua mwenyewe kuitaja Tanzania kwamba inamuunga mkono Hakainde H.

Kutokea pale. Wapiga kura wengi wakakipigia kura chama Tawala

Wazambia wengi wanaipenda Tanzania
Tofauti na Kenya✍️
 
Nilishawahi kusema hata Lissu akipewa nchi atakuwa dictator wa kupindua matokeo ya uchaguzi
Kwahiyo ni ruksa wengine kuendelea kuwa madictator kwa hofu ya kuwa Lissu akipewa nchi nae atakuwa dictator na kupindua matokeo?

Upumbavu ni kipaji.
 
Back
Top Bottom