Uchambuzi: Adhabu kwa wabunge Silaa na Gwajima ni funzo kubwa kwa watanzania

Mods unganisheni huu Uzi tafadhali na ile mingine inayomzungumzia Gwajima na Slaa kwa yale yaliyotokana na Bunge la leo.
Yes. Mods waunganishe zile nyuzi hapa ili tuzipate zote kwa pamoja.
 
Ugomvi wangu kuhusu hii sababu ni kuwa kama wamewasimamisha hadi january hawa wananachi wa majimbo yao nani atawasemea? Nani atachangia nani atatoa mawazo ya wananchi wa hayo majimbo, nadhani kama kuwapa adhabu nzuri wangeishia kuwakata tu hiyo mishahara then wahudhurie vikao vyote kama kulikuwa na ulazima wa kuwapa adhabu za kubumba

Huko bungeni mbunge awepo au asiwepo hakuna madhara yoyote. Mbona wapo na tozo ziko juu, ni wananchi wamewatuma? Kama ni sheria huwa zinatungwa na serikali, kazi ya bunge ni kupiga blabla na kuzipitisha. Sana sana mbunge ndio atapoteza posho sio zaidi ya hapo.
 
Ndio maaana hawahofii
 
Gwajima is right on which grounds? Please can you substantiate your statement?
Mbona kwa ask. Gwajima hujachambua kama kwa Jerry. Unaisema kamati, halafu unafanya yaleyale!
 
Kwema wakuu? Naingia kwenye hoja moja kwa moja bila kupindisha maneno. Leo tarehe 31/08/2021 bunge la JMT limetoa adhabu ndogo kwa wabunge wawili wa CCM – ndugu Jerry Silaa wa Ukonga na ndugu Josephat Gwajima wa Kawe. Bunge limetoa azimio la kuwasimamisha mikutano miwili ya Bunge.

Wengi tuliofuatilia maamuzi yale ya bunge tumebaki vinywa wazi kwani kuna mambo mengi yamefichwa ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya. Watanzania wamefichwa mambo mengi sana kufuatia adhabu hii ilyotolewa kwa wabunge hawa wa CCM.

Naomba nianze kuchambua adhabu iliyotolewa kwa Silaa na sababu zilizotolewa na kamati kuhusu adhabu husika. Hoja ya Silaa ilikuwa kwamba wabunge wanalipwa pesa nyingi sana ambazo hazikatwi kodi na hili hufanyika kwa makusudi ili wasilipe kodi stahiki kwa serikali kama wafanyakazi na watanzania wengine wanavyolipa.

Kwa bahati mbaya sana, Silaa amehukumiwa kwa kusema ‘uongo’ bila kamati kuonyesha ukweli ni upi. Kinachoonekana wazi ni kuwa kamati imeamua kufunika kombe ili mwanaharamu apite. Hawataki kusema ukweli kwa sababu wakisema ukweli wananchi watakuwa wakali kwani wananchi wanabebeshwa mzigo mkubwa wa kodi na tozo, huku wabunge wakila bata. Na kwa masikitikko makubwa, pamoja na mishahara minene wanayolipwa kuna mbunge aliwahi kudiriki kusema kuwa mishahara yao ni midogo na kuwa walipwe kwa dola. Nchi hii haitakuja kuisha maajabu.

Wananchi wamjia juu mbunge anayesema posho, mishahara yao haitoishi

Kwa mujibu wa taarifa zilizowahi kutolewa na Mh Zitto Kabwe mwaka 2017 wakati akiwa mbunge wa Kigoma Mjini, mshahara wa mbunge ni Tsh 3.8 kwa mwezi, posho ya ubunge ni milioni 8 kwa mwezi, posho ya kujikimu ni Tsh 120,000 kwa siku, kukaa kikao cha bungeni posho ni Tsh 200,000 kwa siku. Bado kuna fedha kwa ajili ya mfuko wa jimbo ambayo ni milioni 46 lakini hii hutegemeana na jimbo lenyewe na mbali na hapo kuna posho ya jimbo.

Kwa kuwa huu ulikuwa mshahara wa mwaka 2017 na kwa kuwa kila mwaka wabunge hujiongezea mishahara kimyakimya, kuna uwezekano mshahara wa mbunge kwa sasa upo juu sana kuliko tunavyofikiri.

Huu ndio ufafanuzi ambao ulipaswa kutolewa na kamati ya Bunge kwa umma wa watanzania ili kukata mzizi wa fitna. Lakini wameamua kukaa kimya ili wananchi wasijue jinsi wanavyokwepa kodi kwa kujilimbikizia posho za kukufuru huku wakijilipa kimshahara uchwara ambacho hukatwa kodi uchwara isiyotosha kuchangia chochote kwenye uchumi wa taifa.

Mimi nafikiri Silaa yupo sahihi sana anaposema kuwa wabunge hawalipi kodi. Kama kweli wabunge wa CCM wanataka kushiriki ulipaji kodi, hizo posho za kufuru wanazojilipa zihamishiwe kwenye mshahara ili zikatwe kodi. Sote tunafahamu kuwa posho huwa hazikatwi kodi. Ndio maana wameamua ku-divert mshahara kwenda kwenye posho ili wakwepe kodi. Hawa jamaa ni wahujumu uchumi wallah!

Kabla sijaenda mbali sana naomba nirejee kwenye suala la Gwajima na hoja nyingine zilizoibuka kutokana na kauli zake tata za kuwakataza watanzania kuchanjwa. Kukaangwa kwa Gwajima ni haki kabisa kwa makosa aliyofanya kuwapotosha wananchi kuhusu chanjo. Nasikitika tu amepewa adhabu ndogo sana licha ya kuwa kosa alilofanya ni zaidi ya uhujumu uchumi. Ni uuaji wa makusudi.

Je ni funzo gani tulilopata kutokana na adhabu hizi kwa wabunge wa CCM? Mosi, funzo kubwa ni kuwa kuna baadhi ya wanaCCM hawapendi uongozi wa mama Samia kwa sababu wanazozijua wao wenyewe (Ushahidi: Sikiliza clip hapo juu). Hawa ni wale masalia wa mwendazake waliojipa jina na MATAGA na kujifanya kuwa wao ni watanzania zaidi kuliko wengine. Dawa yao inachemka.

Pili, kuna baadhi ya watanzania aina ya Gwajima ambao wanamdharau mama Samia kwa sababu tu yeye ni mwanamke. Wanaoana eti hatoshi kuiongoza nchi. Kwa hiyo, wanajitahdi kuleta chokochoko na kumvuruga kusudi aache kujikita kuongoza nchi aanze kujishughulisha nao. Hii ni hujuma kubwa sana. Wabunge wengi waliochangia hoja kwenye klipu hapo juu, wamessikitsishwa mno na kitendo hiki cha baadhi ya watanzania wasioitakia mema nchi hii kufanya juhudi za kumkwamisha mama Samia. Hili halikubaliki hata kidogo.

Tatu, kitendo cha kamanda IGP Simon Sirro kugoma kumkamata Gwajima na kumfungulia mashtaka ya uhujumu uchumi kinaashiria kuwa kamanda Sirro yupo upande wa kundi linalomhujumu Rais Samia. Naomba mama Samia amfute kazi mara moja au amshauri ajiuzuru bila shuruti ili ampishe ateue IGP mwingine. Huwezi kuwa Amiri Jeshi Mkuu halafu kipande kimoja cha jeshi kikagoma kukutii ukabaki salama. Lolote laweza kutokea.

Nahitimisha kwa kusema adhabu hii aliyopewa Gwajima ni ndogo sana kwani suala lake limekuwa likifanyika kwa muda mrefu na kwa kurudiarudia. Ameonyesha dharau kubwa sana kwa rais wetu hasa pale alipomtuhumu kwamba alifanya chanjo ya maigizo na kwamba amehongwa na mabeberu ili kuleta chanjo ya kuwaua watanzania. Ilipaswa huyu bwana apewe adhabu kali zaidi.

Na akama Spika aliposhauri, naomba chama chake kiangalie uwezekana wa kumfuta uanachama ili liwe fundisho kwa wengine wasioheshimu mamlaka. Laiti kama mbunge wa upinzani ndiye anayefanya upotoshaji huu anaofanya Gwajima, nadhani angekuwa hata ameishauawa na watu wasioijulikana. Lakini kwa kuwa ni mbunge mwenzao ndio maana wamempa adhabu nyepesi.

Taarifa zaidi kuhusu sakata hili unaweza kulipata kwenye uzi huu hapa chini:

Ikiwa makato kwenye miamala ya simu, LUKU na mabenki hayatabadilika nini kifanyike?

Nawasilisha.​
Jamaa wewe idiot. Gwajima hana kosa, hata Mh. Rais Mama Samia anajua kabisa. Wabunge uelewa mdogo. Hivi inakuwaje kitu cha majaribio kiwe lazima. Ukitaka kujua wewe mleta hoja ni mjinga na lijinga na pimbi wewe kumbuka Rais mama Yetu alisema chanjo ni hiari na Gwajima katumia hiyo hiyo hiari. Sasa mlivyowajjnga mnademika tu.
 
Askofu Gwajima makosa yake yapo wazi mkuu. Ndio maana sijarudia kuyachambua kwa kuwa clips zake za upotoshaji zimesamabaa sana na kwa muda mrefu.
 
Kamati ukiwauliza watajibu the same. So kwa nini unadhani wamekosea?
 
Jamaa wewe idiot. Gwajima hana kosa, hata Mh. Rais Mama Samia anajua kabisa. Wabunge uelewa mdogo. Hivi inakuwaje kitu cha majaribio kiwe lazima. Ukitaka kujua wewe mleta hoja ni mjinga na lijinga na pimbi wewe kumbuka Rais mama Yetu alisema chanjo ni hiari na Gwajima katumia hiyo hiyo hiari. Sasa mlivyowajjnga mnademika tu.
Nani kakulazimisha mkuu? Askofu Gwajima anajua fika kuwa chanjo ni hiyari lakini yeye kila siku amekuwa akiwagomesha wafuasi wake wasichanjwe badala ya kuwaacha watumie hiyari hiyo kuamua wao wenyewe ama wachanjwe au wasichanjwe. Natumaini sasa umeelewa hoja yangu.
 
Wewe mtoa mada uwezo wako wa kuchambua mambo mdogo sana.Tulitegemea utaishauri serikali imjibu Gwajima kisomi,lakini unashabikia udikiteta wa kijinga.Tuko karne ya kulumbana kwa hoja,siyo tawala za kifalme.
 
Kwema wakuu? Naingia kwenye hoja moja kwa moja bila kupindisha maneno. Leo tarehe 31/08/2021 bunge la JMT limetoa adhabu ndogo kwa wabunge wawili wa CCM – ndugu Jerry Silaa wa Ukonga na ndugu Josephat Gwajima wa Kawe. Bunge limetoa azimio la kuwasimamisha mikutano miwili ya Bunge.

Wengi tuliofuatilia maamuzi yale ya bunge tumebaki vinywa wazi kwani kuna mambo mengi yamefichwa ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya. Watanzania wamefichwa mambo mengi sana kufuatia adhabu hii ilyotolewa kwa wabunge hawa wa CCM.

Naomba nianze kuchambua adhabu iliyotolewa kwa Silaa na sababu zilizotolewa na kamati kuhusu adhabu husika. Hoja ya Silaa ilikuwa kwamba wabunge wanalipwa pesa nyingi sana ambazo hazikatwi kodi na hili hufanyika kwa makusudi ili wasilipe kodi stahiki kwa serikali kama wafanyakazi na watanzania wengine wanavyolipa.

Kwa bahati mbaya sana, Silaa amehukumiwa kwa kusema ‘uongo’ bila kamati kuonyesha ukweli ni upi. Kinachoonekana wazi ni kuwa kamati imeamua kufunika kombe ili mwanaharamu apite. Hawataki kusema ukweli kwa sababu wakisema ukweli wananchi watakuwa wakali kwani wananchi wanabebeshwa mzigo mkubwa wa kodi na tozo, huku wabunge wakila bata. Na kwa masikitikko makubwa, pamoja na mishahara minene wanayolipwa kuna mbunge aliwahi kudiriki kusema kuwa mishahara yao ni midogo na kuwa walipwe kwa dola. Nchi hii haitakuja kuisha maajabu.

Wananchi wamjia juu mbunge anayesema posho, mishahara yao haitoishi

Kwa mujibu wa taarifa zilizowahi kutolewa na Mh Zitto Kabwe mwaka 2017 wakati akiwa mbunge wa Kigoma Mjini, mshahara wa mbunge ni Tsh 3.8 kwa mwezi, posho ya ubunge ni milioni 8 kwa mwezi, posho ya kujikimu ni Tsh 120,000 kwa siku, kukaa kikao cha bungeni posho ni Tsh 200,000 kwa siku. Bado kuna fedha kwa ajili ya mfuko wa jimbo ambayo ni milioni 46 lakini hii hutegemeana na jimbo lenyewe na mbali na hapo kuna posho ya jimbo.

Kwa kuwa huu ulikuwa mshahara wa mwaka 2017 na kwa kuwa kila mwaka wabunge hujiongezea mishahara kimyakimya, kuna uwezekano mshahara wa mbunge kwa sasa upo juu sana kuliko tunavyofikiri.

Huu ndio ufafanuzi ambao ulipaswa kutolewa na kamati ya Bunge kwa umma wa watanzania ili kukata mzizi wa fitna. Lakini wameamua kukaa kimya ili wananchi wasijue jinsi wanavyokwepa kodi kwa kujilimbikizia posho za kukufuru huku wakijilipa kimshahara uchwara ambacho hukatwa kodi uchwara isiyotosha kuchangia chochote kwenye uchumi wa taifa.

Mimi nafikiri Silaa yupo sahihi sana anaposema kuwa wabunge hawalipi kodi. Kama kweli wabunge wa CCM wanataka kushiriki ulipaji kodi, hizo posho za kufuru wanazojilipa zihamishiwe kwenye mshahara ili zikatwe kodi. Sote tunafahamu kuwa posho huwa hazikatwi kodi. Ndio maana wameamua ku-divert mshahara kwenda kwenye posho ili wakwepe kodi. Hawa jamaa ni wahujumu uchumi wallah!

Kabla sijaenda mbali sana naomba nirejee kwenye suala la Gwajima na hoja nyingine zilizoibuka kutokana na kauli zake tata za kuwakataza watanzania kuchanjwa. Kukaangwa kwa Gwajima ni haki kabisa kwa makosa aliyofanya kuwapotosha wananchi kuhusu chanjo. Nasikitika tu amepewa adhabu ndogo sana licha ya kuwa kosa alilofanya ni zaidi ya uhujumu uchumi. Ni uuaji wa makusudi.

Je ni funzo gani tulilopata kutokana na adhabu hizi kwa wabunge wa CCM? Mosi, funzo kubwa ni kuwa kuna baadhi ya wanaCCM hawapendi uongozi wa mama Samia kwa sababu wanazozijua wao wenyewe (Ushahidi: Sikiliza clip hapo juu). Hawa ni wale masalia wa mwendazake waliojipa jina na MATAGA na kujifanya kuwa wao ni watanzania zaidi kuliko wengine. Dawa yao inachemka.

Pili, kuna baadhi ya watanzania aina ya Gwajima ambao wanamdharau mama Samia kwa sababu tu yeye ni mwanamke. Wanaoana eti hatoshi kuiongoza nchi. Kwa hiyo, wanajitahdi kuleta chokochoko na kumvuruga kusudi aache kujikita kuongoza nchi aanze kujishughulisha nao. Hii ni hujuma kubwa sana. Wabunge wengi waliochangia hoja kwenye klipu hapo juu, wamessikitsishwa mno na kitendo hiki cha baadhi ya watanzania wasioitakia mema nchi hii kufanya juhudi za kumkwamisha mama Samia. Hili halikubaliki hata kidogo.

Tatu, kitendo cha kamanda IGP Simon Sirro kugoma kumkamata Gwajima na kumfungulia mashtaka ya uhujumu uchumi kinaashiria kuwa kamanda Sirro yupo upande wa kundi linalomhujumu Rais Samia. Naomba mama Samia amfute kazi mara moja au amshauri ajiuzuru bila shuruti ili ampishe ateue IGP mwingine. Huwezi kuwa Amiri Jeshi Mkuu halafu kipande kimoja cha jeshi kikagoma kukutii ukabaki salama. Lolote laweza kutokea.

Nahitimisha kwa kusema adhabu hii aliyopewa Gwajima ni ndogo sana kwani suala lake limekuwa likifanyika kwa muda mrefu na kwa kurudiarudia. Ameonyesha dharau kubwa sana kwa rais wetu hasa pale alipomtuhumu kwamba alifanya chanjo ya maigizo na kwamba amehongwa na mabeberu ili kuleta chanjo ya kuwaua watanzania. Ilipaswa huyu bwana apewe adhabu kali zaidi.

Na akama Spika aliposhauri, naomba chama chake kiangalie uwezekana wa kumfuta uanachama ili liwe fundisho kwa wengine wasioheshimu mamlaka. Laiti kama mbunge wa upinzani ndiye anayefanya upotoshaji huu anaofanya Gwajima, nadhani angekuwa hata ameishauawa na watu wasioijulikana. Lakini kwa kuwa ni mbunge mwenzao ndio maana wamempa adhabu nyepesi.

Taarifa zaidi kuhusu sakata hili unaweza kulipata kwenye uzi huu hapa chini:

Ikiwa makato kwenye miamala ya simu, LUKU na mabenki hayatabadilika nini kifanyike?

Nawasilisha.​
akili yako haiko sawasawa,, unawaza leo na maisha yako ww bila kufikili kesho na wtt wako watakuwaje!!!kaa kimya mkuu,,,fikilia kabla ya kuandika huu upuuzi!!...gwajima alitaka majibu sahihi ya maswali yake kuhusu chanjo hajajibiwa mpk saiv,, au ww utujibu bas ili tumuhukum ngwj
 
'The same' what? Ina maana hata kamati inaamini na kuukbali upotoshaji wa Gwajima? La hasha!
Kwa Jerry. Gwajima alikuwa na hoja zake kama alivyokuwa Jerry. Kamati haijajibu kuonesha ukweli ni upi kwa wote wawili.

Ila umehoji kwa Jerry na kwa Gwajima umepitisha hukumu. Anyway may be naongea mambo magumu. Tuyaache tu!
 
Wewe mtoa mada uwezo wako wa kuchambua mambo mdogo sana.Tulitegemea utaishauri serikali imjibu Gwajima kisomi,lakini unashabikia udikiteta wa kijinga.Tuko karne ya kulumbana kwa hoja,siyo tawala za kifalme.
Gwajima aliposema kwamba mama Samia amehongwa hela na wazungu ili alete chanjo ya kuwaua watanzania na kwamba aliigiza kuchanja, Gwajima ametoa ushahidi wowote mbele ya kamati kuhusu huu upotoshaji? Usimtetee mjinga huyu na tapeli mkubwa wa kidini. Mungu anakuona.
 
Kwa Jerry. Gwajima alikuwa na hoja zake kama alivyokuwa Jerry. Kamati haijajibu kuonesha ukweli ni upi kwa wote wawili.

Ila umehoji kwa Jerry na kwa Gwajima umepitisha hukumu. Anyway may be naongea mambo magumu. Tuyaache tu!
Gwajima alisema hadharani kuwa mama Samia amehongwa fedha na mabeberu na kuwa aliigiza kuchoma chanjo. Ushahidi gani ametoa kutetea upotoshaji wake huu?
 
Gwajima aliposema kwamba mama Samia amehongwa hela na wazungu ili alete chanjo ya kuwaua watanzania na kwamba aliigiza kuchanja, Gwajima ametoa ushahidi wowote mbele ya kamati kuhusu huu upotoshaji? Usimtetee mjinga huyu na tapeli mkubwa wa kidini. Mungu anakuona.
Kama una chuki binafsi na Gwajima sema.Vinginevyo unabashiri tu,kwani Gwajima alitaja jina au cheo cha mtu.
 
akili yako haiko sawasawa,, unawaza leo na maisha yako ww bila kufikili kesho na wtt wako watakuwaje!!!kaa kimya mkuu,,,fikilia kabla ya kuandika huu upuuzi!!...gwajima alitaka majibu sahihi ya maswali yake kuhusu chanjo hajajibiwa mpk saiv,, au ww utujibu bas ili tumuhukum ngwj
Pinga hoja kwa kutumia hoja, usimshambulie mto mada bila sababu za msingi.
 
Back
Top Bottom