Uchambuzi: Adhabu kwa wabunge Silaa na Gwajima ni funzo kubwa kwa watanzania

Gwajima alisema hadharani kuwa mama Samia amehongwa fedha na mabeberu na kuwa aliigiza kuchoma chanjo. Ushahidi gani ametoa kutetea upotoshaji wake huu?
Hivi umeelewa hata ulichohoji kwenye andiko lako mwenyewe? Ndio maana nikahoji logic yako ina matege. Unachowahoji kamati kwa Jerry ndio unachokifanya kwa Gwajima. Kama hujaelewa na hapa nitawaachia wenye uwezo zaidi wa kuelewesha
 
Hivi umeelewa hata ulichohoji kwenye andiko lako mwenyewe? Ndio maana nikahoji logic yako ina matege. Unachowahoji kamati kwa Jerry ndio unachokifanya kwa Gwajima. Kama hujaelewa na hapa nitawaachia wenye uwezo zaidi wa kuelewesha
Je, Gwajima anaposema kuwa chanjo zina madhara na kwamba zitawafanya watu kuwa mazombi ana ushahidi wowote wa kisayanzi? Je, yeye amewahi kuwa zombi baada ya kuchanja? Usitetee jambo usilolijua mkuu. Kama huna hoja ni bora ukae kimya.
 
Je, Gwajima anaposema kuwa chanjo zina madhara na kwamba zitawafanya watu kuwa mazombi ana ushahidi wowote wa kisayanzi? Je, yeye amewahi kuwa zombi baada ya kuchanja? Usitetee jambo usilolijua mkuu. Kama huna hoja ni bora ukae kimya.
Nadhani hatutafika mahala. Ulichohoji kwa slaa kilifanyika kwa Gwajima? Kama hakikufanyika kwa nini umehoji kwa Jerry na kumhukumu Gwajima? Kama wewe umefanya hivi na unaona sawa vipi kuihoji kamati?

Kwa lugha rahisi huna moral authority ya kuhoji kamati. Unachowahukumu nacho ndicho unachokifanya. Na kama uko sahihi logical conclusion ni kuwa hoja yako ni self defeating!
 
tpaul

Kila malipo ya fedha yaliyohalali upaswa kulipiwa kodi... Kama Bunge linalipa tax kwa basic salaries bado wanatunyonga! Posho zote wanazolipwa lazima zilipiwe kodi.

Labda grant funds sio lazima kulipiwa kodi... Sina hakika sana na hili kwani utegemea zaidi sera za serikali husika
 
Wabunge hawa wa CCM wanatupunja sana mkuu. Posho zao hazikatwi kodi na pia mafao yao huwa hayakatwi kodi. Wanatuumiza sana. Sijui wanatuonaje.
 
NI ZAIDI YA KUMKOSOA HASA PALE MKOSOAJI ANASEMA RAIS KAHONGWA.
 
Furaha yetu SSI ni kuwaona ccm wakiparaganyika wao kwa wao Mana walidhani wakiwa wao pekee bungen bila wapinzani hatakuwa na mawazo kinzani na Bado watauwana Hawa. Gwajima kaza baba kwa hoja zako tuko nyuma yako
 
Wanasema gwajima awape evidence Kama chanjo Ina madhara
Wakati wao hawana evidence za usalama wa chanjo
Wanasema gwajima anawashawishi wananchi kukataa chanjo ambayo ni hiyari
Wao wapo busy kutuhamasisha tuchanjwe akat Ni hiyari
Wanasema gwajima amewatukana kua wamepewa pesa Hana ushahidi
Na huku wanajua chanjo zimekuja na msaada wa kiasi Kikubwa cha pesa ๐Ÿ˜ณ
Mungu anawaona
Yaani siyapendi mabunge hayo
 
Umezunguka kote lakini hoja yako ni Mch. Gwajima...

Yeyote anayecheza na mtumishi wa Bwana Mungu Yehova anacheza, kisasi na hasira na moto wa Mungu...

Hii vita ni mtifuano wa falme mbili moja ikiwa dhaifu kabisa yaani;

Ufalme wa ulimwengu huu unaotawaliwa na Ibilisi/shetani akitumia wanadamu waovu, serikali na taasisi za uovu duniani...

VS

Ufalme wa mbinguni/Mungu chini ya mfalme Yesu Kristo akiwakilishwa duniani hapa na watumishi wake wanaadamu waaminifu kina Mch. Gwajima na kina sisi...

Unaweza kuona kama dhaifu na isiyo na nguvu yoyote inaweza kuishinda yeye nguvu. Yaani eti itokee shetani amshinde Mungu Muumba...!

Mwisho nakuhakikishia jambo moja kuwa, watashindwa tena kwa aibu isiyo na kifani...!!
 
Like serious, bunge linaacha kujadiri mambo ya msingi wanamjadiri Gwajima na slaa tena kwenye jambo la hiari !!?
Duh hii ndo Tz!
Kuna mpumbavu kasema anaifahamu vyema Israel kuliko Gwajima. Eti wakati Yesu anatembea na mke wake toka Nazareti kwenda Yerusalemu kuhesabiwa.

Madhara ya chanjo yashaanza kujidhihirisha ๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†
 
Mkuu mbona unatumia nguvu nyingi sana kumtetea FAKE prophet?
 
Wakubwa hofu yao kufungua mengine mengi jinsi wanavyoitafuna keki ya nchi hii bila huruma.
Unajua marupurupu ya mawaziri, majaji, na Raisi?
 
Wewe na hao wabunge hamna tofauti ni wale wale tu. Hebu na wewe thibitisha Gwajima alipokosea
 
Mkuu mbona unatumia nguvu nyingi sana kumtetea FAKE prophet?
Najua nisemacho. Najitambua vizuri sana. Sina shaka na mtumishi wa Bwana Yesu Kristo Mch. Gwajima. Wewe kama unaamini ni "fake prophet", dhambi hiyo hainihusu bali na iwe juu yako mwenyewe...!

By the way, hata Yesu Kristo aliitwa majina hayahaya pengine mabaya zaidi ya haya...

Aliwahi kuitwa "mkuu wa mapepo"...

Kisa cha kuitwa majina haya?

Ni kwa sababu alikuwa anapigania haki za watu, alikuwa anatibua maslahi ya watawala wa serikali za kidunia...

Walitumia nguvu za serikali za dunia hii. Wakamshtaki kwa mashtaka ya uongo na kumhukumu adhabu ya kifo lakini HAKUFA, YU HAI HATA LEO naye ndiye mtetezi wetu na apiganaye kwa ajili ya yetu...

Mwisho wake ukawaje?

Wote waliohusika kumsemea uongo na kumhukumu Yesu Kristo mwisho wao ilikuwa ni aibu tupu mpaka leo...

Ndivyo itakavyokuwa kwa hawa wanaotaka kutesa damu isiyo na hatia...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ