Uchambuzi: Bomba la mafuta ya wizi Ungindoni, Kigamboni

Uchambuzi: Bomba la mafuta ya wizi Ungindoni, Kigamboni

Tatizo uzalendo wetu wa kitanzania hauwezi kuufananisha na Uzalendo wa Mmarekani.
kwanini kuna tofauti?
wezetu uzalendo kwa nchi yao unapandikizwa/kufundishwa kwa watoto kuanzia chekechea, tena unafundishwa na wazalendo walio iva.
sisi huku tunaanza kumfundisha Uzalendo mtu aliye kubuhu kwenye wizi!!, ubadhirifu!!!
uozo! uozo kila mahali.
unaweza kuta mpaka ikafikia kufahamika uhalifu huo wa wizi wa mafuta kuna mtu miongoni mwa wakubwa karukwa au kanyimwa mgao ndipo kaamua kuchomoa betri!!!
Uzalendo kwa Taifa letu uanze kufundishwa kwa bidii kuanzia chini kabisa sambamba na elimu ya Maadili hapo ndipo kizazi chetu kitafurahia matunda ya rasilimali za Taifa letu.
hata hivyo wapo viongozi wachache ambao kweli ni wazalendo wa kweli, na hao ukichunguza sana maadili yao yanatokana na historia ya elimu aliyo ipata/shule alizo soma n.k, japo na wao hufika wakati wanazidiwa nguvu na mfumo corrupts na hivyo huachia goli.
watu wachafu na waovu ni wengi zaidi kuliko watu wema na waadilifu. hii ni hatati sana.
 
Wabongo wataweza wapi netflix [emoji2]
Nilikuwa na wazo kama lako. Hii issue ikipata script writer mzuri na mtaji wa kutosha basi itakuwa bonge la movie.
Episode one
Anaonekana tajiri mmoja yuko ofisini anasoma magazeti mara anakutana na habari ya watu waliokamatwa wakiiba mafuta kwenye nyumba moja mtaani..hao walitoboa bomba na kujiunganishia..anatabasamu na kuendelea na habari nyingine

Miezi sita baadae anaonekana kwenye ofisi yake akisoma magazeti, anakutana na habari kama ile ya wizi wa mafuta lakini safari hii ni upigaji mkubwa zaidi tena mpigaji akiwa ni tajiri aliyeibuka ghafla.. Anamfahamu kiasi , ananyanyua simu kumpigia lakini inaita bila kupokelewa...
Itaendelea
 
Changamoto ni connection na siyo Mtaji,kuna watu wako na mitaji yao,lakini wanaishia kwenda kuchukua magunia ya mchele huko Kyela!!
Hahaha au nyanya Iringa
 
Wizi wa Mafuta Kigamboni ni Uhujumu Uchumi daraja la kwanza.
nilivyo ona tu njia za uhalifu huo basi nikakumbuka historia ya Guzman na mtandao wake wa kihalifu walivyo chimba handaki la km.1 na kutokezea ktk chumba cha gereza alicho kuwa amefungiwa Guzman na kufanikiwa kumtorosha.
lkn mchongo huo ulishirikisha watu kibao, wamiliki wa ardhi, majirani, wapita njia, wachunga mifugo, wakulima, wahudumu, wakuu,wawindaji, wapiga doria n.k n.k n.k
 
Episode one
Anaonekana tajiri mmoja yuko ofisini anasoma magazeti mara anakutana na habari ya watu waliokamatwa wakiiba mafuta kwenye nyumba moja mtaani..hao walitoboa bomba na kujiunganishia..anatabasamu na kuendelea na habari nyingine

Miezi sita baadae anaonekana kwenye ofisi yake akisoma magazeti, anakutana na habari kama ile ya wizi wa mafuta lakini safari hii ni upigaji mkubwa zaidi tena mpigaji akiwa ni tajiri aliyeibuka ghafla.. Anamfahamu kiasi , ananyanyua simu kumpigia lakini inaita bila kupokelewa...
Itaendelea
😂😂😂 tatizo ni resources za kutengeneza hiyo movie. Kutengeneza movie ya kisasa inahitajika pesa ndefu sana. Pesa itakayokuwezesha kupata vifaa vya kisasa kabisa na actors wazuri wenye kipaji.
Lakini muhimu kuliko vyote ni "pesa".
Movie tunazoziona huko Ulaya zimegharimu mabilioni ya shillingi. Mfano kuna movie inaitwa "The Italian Job", hii movie naipenda sana na ni kati ya movie bora sana kwangu. Unaambiwa movie hii iligharimu kiasi cha dola milioni 3 ambazo ni sawa na Bilioni 6.8 za Tanzania.
Sasa jiulize, hapa Tanzania nani yuko tayari kuwekeza hiyo pesa kwenye movie???????
 
Back
Top Bottom