Uchambuzi: Bomba la mafuta ya wizi Ungindoni, Kigamboni

[emoji23][emoji23][emoji23] tatizo ni resources za kutengeneza hiyo movie. Kutengeneza movie ya kisasa inahitajika pesa ndefu sana. Pesa itakayokuwezesha kupata vifaa vya kisasa kabisa na actors wazuri wenye kipaji.
Lakini muhimu kuliko vyote ni "pesa".
Movie tunazoziona huko Ulaya zimegharimu mabilioni ya shillingi. Mfano kuna movie inaitwa "The Italian Job", hii movie naipenda sana na ni kati ya movie bora sana kwangu. Unaambiwa movie hii iligharimu kiasi cha dola milioni 3 ambazo ni sawa na Bilioni 6.8 za Tanzania.
Sasa jiulize, hapa Tanzania nani yuko tayari kuwekeza hiyo pesa kwenye movie???????
Ukinipa nusu yake tu sihangaiki tena nakula bata[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]haya ndio mawazo ya wengi
 
Episode one
Anaonekana tajiri mmoja yuko ofisini anasoma magazeti mara anakutana na habari ya watu waliokamatwa wakiiba mafuta kwenye nyumba moja mtaani..hao walitoboa bomba na kujiunganishia..anatabasamu na kuendelea na habari nyingine

Miezi sita baadae anaonekana kwenye ofisi yake akisoma magazeti, anakutana na habari kama ile ya wizi wa mafuta lakini safari hii ni upigaji mkubwa zaidi tena mpigaji akiwa ni tajiri aliyeibuka ghafla.. Anamfahamu kiasi , ananyanyua simu kumpigia lakini inaita bila kupokelewa...
Itaendelea
Nasubiri epsode 2😃
 
Kwani hawafanyagi oil reconcilliation huenda ata watu wa bandari wanajua..coz mafuta yanayoshushwa ndiyo yanapaswa kufika kwenye bohari...sasa huu ujinga unatokeaje?
 
Ukipiga hesabu tanker 10 za lita 10,000 akiuza lita kwa buku anaingizamilioni mia moja kwa siku mkuu sio milioni kumi
 
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya muunganiko! MATAGA pia natumai hamjambo!

Rejea mada hii: BLINDSPOT: Uchochoro wa kupiga popote

Kukamatwa kwa bomba hili kwa bahati nasibu tuu ni mwendelezo wa ufunuo wa udhaifu wa serikali ya awamu ya tano iliyojinasibu kudhibiti wizi, rushwa, upigaji na ubadhilifu...! Ukijua hivi wenzako wanajua vile na kinyume chake.

Leo nitaandika mada ndefu kidogo kuhusiana na hili kwakuwa kwa namna moja au nyingine linagusa usalama wa nchi na ya kwamba kwenye hili hatupaswi kuaminiana ama kumuamini yoyote hata awe na pesa na ukwasi kiasi gani.

Tukumbuke ya kwamba waliofanikisha kujenga lile bomba la wizi wa mafuta toka bomba la serikali si watu wa kawaida bali ni mtandao wa watu wenye akili kubwa,hela, vitendea kazi vya kisasa, wataalam wa kuchimba, wasoma ramani nknk

Hebu tupitie dondoo hizi:

1. Eneo la upigaji ni nyumba ya kupanga/kupangishwa
Ni eneo la kimkakati kutokana na ujenzi wake! Eneo kubwa lililozungushiwa ukuta mrefu kotekote! Ndani kukiwa na nyumba moja tuu.. Je kuna uhusiano gani kati ya mmiliki na mpangaji? Je hawezi kuwa mtu mmoja mwenye sura mbili!? Cha kushangaza zaidi eneo linatazamana na serikali ya mtaa Ungindoni, kinachowatenganisha ni barabara tu![emoji2815][emoji3]

2. Usalama wa nchi na raia
Kigamboni ni eneo la kimkakati kwenye usalama wa nchi na raia pia na serikali imewekeza sana kule, kuna kambi ya jeshi na ofisi za vitengo vya usalama.. Lilipaswa kuwa eneo la kuogopwa na wapigaji wakubwa! Sasa ninini kilitokea hapa mpaka watu wanatoboa ardhi mpaka kulifikia bomba na kunyonya mafuta kwa miaka miwili kasoro bila kustukiwa na organ za usalama?

3. Mfadhili na mmiliki wa huu mradi si mtu mdogo asilani
Na pengine ni mojawapo wa matajiri wenye kumiliki kadi ya kijani na mfadhili wa chama na viongozi wake. Pengine ni mmojawapo wa matajiri anayeheshimiwa na pengine kuogopwa na viongozi wetu na pengine ana miliki cheti cha mlipakodi mkubwa mzuri kupitia miradi mingine aliyoanzisha kwa kutumia pesa za kutakatisha za wizi wa mafuta.

4. Kikosi kazi kilichotekeleza ule mtobozano ni kikosi toka nje ya nchi kwa vyovyote kilichokuwa na kila nyenzo ya kisasa zikisaidiwa na mashine za kutoboa visima virefu In fact kazi ilifanywa na watu wachache na mitambo ya kisasa kwa kutumia computer tu. Yaani vitu vinasetiwa toka umbali wa bomba lilipo, uchorongaji nknk. Watu wako kwenye AC na vikombe vya NIDO kama wanaangalia movie.

Hakuna jambo linalokosa asili. Ilianza kule Tegeta nadhani kuna watu walikamatwa kwenye nyumba nao wakiwa wamejiunganishia bomba lao toka bomba kuu na wakawa wanakula maisha kwa kwenda mbele. Hawa walikuwa level one au shule ya msingi.

Akaja kukamatwa tajiri aliyeibuka ghafla, Princess Muro akiwa na mabasi ya kusafirisha abiria mengi tu na vituo vya mafuta vilivyokuwa vinachipua kama uyoga. Kumbe huyu naye alikuwa kajiunganishia bomba lake la mafuta toka bomba kuu la serikali. Alikamatwa na kufilisiwa nadhani. Huyu ni level two au shule ya sekondari.

Huyu aliyekamatiwa vitu vyake Kigamboni yeye tunamuweka level 3 au chuo kikuu alisoma makosa ya waliotangulia akafanya marekebisho mengi akafanya yake!

Je, kutakuwa na level 4? Muda utasema!

Uzalendo ni kitu kikubwa sana. Uzalendo ni zaidi ya kuvaa scalf na nguo zenye rangi ya taifa, uzalendo ni zaidi ya kusimama majukwaani na kuhubiri. Ule wizi wa Kigamboni una mkono wa Watanzania wengi tu mle ndani na wengine pengine wakiwa na dhamana ya ulinzi na usalama wa nchi lakini wote wakapiga kimya!

Aakari waliokamata ile gari iliyopelekea kubumbuluka kwa wizi huu mkubwa sijui watapewa zawadi gani. Lakini hata hivyo pamoja na serikali kuishia kutaifisha ile nyumba na magari na ile mitambo sidhani kama wamiliki halali wa ule wizi watakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria, sana sana watakamatwa vijana wetu wasiojua mengi.

Kama hujui jamaa kapiga bei gani kwenye huu wizi angalia hizi hesabu. Na kama zikija kupatikana hesabu halisi huu unaweza kuja kuwa upigaji mkubwa kuja kutokea Tanzania.

Nakupa hesabu kwa uchache tuu na bei ya chini kabisa:

Kama kwa siku alivuna tanker kumi tu za lita elfu 10 kila moja na akaenda kuuza kila lita moja kwa sh. 1000 tu,
  • Kwa siku moja alikuwa anaingiza kwa uchache milioni 10 kumi za Kitanzania
  • Kwa wiki milioni 70
  • Kwa mwezi milioni 280
Piga kwa mwaka au miezi 20 aliyofanya kazi

Sitaki kuongelea ya Mkuu wa Wilaya ambaye alikuwa hajui jina hata moja ya vile vifaa vilivyotumika pale. Hivi kwanini hawakumuandaa? Walimkurupusha tu au alikurupuka? Hivi kweli DC anashindwa kusema hata welding machine?

Eneo lote lilikuwa na camera na ulinzi mkali 24/7, hivyo miliiki alikuwa anaona kila kitu. Mpaka DC na timu yake yote alionekana bila chenga. Hii ni big mistake! Walimpa nafasi bora sana ya kujipanga ama kukimbia.

Anyway, upigani ni jadi hasa kwa Taifa kama Tanzania na pengine hili nalo litapita kama mengine yote.
DC alikuwa na haraka ya kuripoti ukitilia maanani uteuzi wa Ma DC ndio unafuata.Alitaka apate point ndio maana unaona ni kama amekurupuka hivi na kuifanya taarifa nzima ionekane kama haikuandaliwa vyema. Au hawana uhakika.
 
😂😂😂 tatizo ni resources za kutengeneza hiyo movie. Kutengeneza movie ya kisasa inahitajika pesa ndefu sana. Pesa itakayokuwezesha kupata vifaa vya kisasa kabisa na actors wazuri wenye kipaji.
Lakini muhimu kuliko vyote ni "pesa".
Movie tunazoziona huko Ulaya zimegharimu mabilioni ya shillingi. Mfano kuna movie inaitwa "The Italian Job", hii movie naipenda sana na ni kati ya movie bora sana kwangu. Unaambiwa movie hii iligharimu kiasi cha dola milioni 3 ambazo ni sawa na Bilioni 6.8 za Tanzania.
Sasa jiulize, hapa Tanzania nani yuko tayari kuwekeza hiyo pesa kwenye movie???????
Siyo kuwekeza utamuuzia nani mtaani unakuta walisha burn 😂😂
 
Kwani hawafanyagi oil reconcilliation huenda ata watu wa bandari wanajua..coz mafuta yanayoshushwa ndiyo yanaoswa kufika kwenye bohari...sasa huu ujinga unatokeaje?
Hizi connection zina insiders haiwezekeni kitu sensitive kama bomba hilo la mafuta likose leakage sensors au moisture sensors

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ruth Msafiri kafika yard nyeupe, au ndio ilikuwa kwenda tu kukuonyesha kwa Mama baada ya kushiba ili PDF ijayo asomeke

Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app
kama kweli alikuwa serious basi tunataka kuona mwisho wa sakata hili.
na pia tunataka kuona wahusika wote ktk sakata hili wanakamatwa, hatutegemei kuona wanakamatwa walinzi tu halafu wahusika wanatokomea.
 
Kimyakimya sasa.. Changamoto mtaji
Mtaji sio tatizo kabisa, ongea na wauza mafuta ya jumla wao Wana hela na vifaa na utaalamu, wewe tafuta nguvu kazi iliyo tayari kujitoa akili na usiri. Usisahau malipo yao ni cash ukiwarusha ujue imekula kwako.

Pia hakikisha polisi wanaingia kwenye payroll kuanzia RPC na wasaidizi wake pamoja na kukaa vizuri na Mwenyekiti wa mtaa na kusaidia CCM hata kujenga ofisi na michango mbalimbali ya chama.

Muhimu sana usisahau kusaidia ujenzi wa misikiti na makanisa ikiwemo ujenzi wa madrasa na ujenzi wa miundombinu ya maji ili vifaa vyako visijulikane vinatumika kufanya nini.

Toa misaada ya madawati, vitabu vya shule za primary, anzisha ligi ya mpira, usiajiri mtu mwenye asili ya Asia kabisa jitahidi kuweka mzungu aonekane mwekezaji watu wa Asia wanajulikana ni magumashi kuanzia wahindi Hadi wachina.

Toa misaada kwenye vituo vya watoto yatima ikiwemo ufadhili wa watoto kadhaa kwa kuwalipia ada na mahitaji yao ya shule.

Fungua kampuni ya kuchimba visima na ujenzi wa mabomba. Pata vibali vyote ili wasikusumbue.

Hakikisha kwenye board of directors anakuwepo mchungaji au sheikh na mstaafu wa serikalini ambaye alikuwa na cheo cha juu.

Haya yote hayamalizi milioni 400, Ila faida yake you will thank me later 😃😃😃😃
 
Mtaji sio tatizo kabisa, ongea na wauza mafuta ya jumla wao Wana hela na vifaa na utaalamu, wewe tafuta nguvu kazi iliyo tayari kujitoa akili na usiri. Usisahau malipo yao ni cash ukiwarusha ujue imekula kwako.

Pia hakikisha polisi wanaingia kwenye payroll kuanzia RPC na wasaidizi wake pamoja na kukaa vizuri na Mwenyekiti wa mtaa na kusaidia CCM hata kujenga ofisi na michango mbalimbali ya chama.
Akili kubwa[emoji1548][emoji1548][emoji1548][emoji736]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kilichonishangaza ile habari haijapewa uzito mkubwa sana katika media kubwa, ukisikia uhujumu uchumi ndio ule sasa,

Kingine kuhusu Mh Dc kutojua vifaa vile sio kosa lake, sio fani yake na anaweza kusahau
 
Kaka kuna kitu kinaitwa summary meeting/ briefing kabla kiongozi hajaenda eneo la tukio kwakuwa huko atakutana na vyombo vya habari na anaweza kuulizwa maswali.. Hivyo hizo meeting naye huwa huru kuuliza ili kupata uelewa wa jambo husika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya muunganiko! MATAGA pia natumai hamjambo!

Rejea mada hii: BLINDSPOT: Uchochoro wa kupiga popote

Kukamatwa kwa bomba hili kwa bahati nasibu tuu ni mwendelezo wa ufunuo wa udhaifu wa serikali ya awamu ya tano iliyojinasibu kudhibiti wizi, rushwa, upigaji na ubadhilifu...! Ukijua hivi wenzako wanajua vile na kinyume chake.

Leo nitaandika mada ndefu kidogo kuhusiana na hili kwakuwa kwa namna moja au nyingine linagusa usalama wa nchi na ya kwamba kwenye hili hatupaswi kuaminiana ama kumuamini yoyote hata awe na pesa na ukwasi kiasi gani.

Tukumbuke ya kwamba waliofanikisha kujenga lile bomba la wizi wa mafuta toka bomba la serikali si watu wa kawaida bali ni mtandao wa watu wenye akili kubwa,hela, vitendea kazi vya kisasa, wataalam wa kuchimba, wasoma ramani nknk

Hebu tupitie dondoo hizi:

1. Eneo la upigaji ni nyumba ya kupanga/kupangishwa
Ni eneo la kimkakati kutokana na ujenzi wake! Eneo kubwa lililozungushiwa ukuta mrefu kotekote! Ndani kukiwa na nyumba moja tuu.. Je kuna uhusiano gani kati ya mmiliki na mpangaji? Je hawezi kuwa mtu mmoja mwenye sura mbili!? Cha kushangaza zaidi eneo linatazamana na serikali ya mtaa Ungindoni, kinachowatenganisha ni barabara tu![emoji2815][emoji3]

2. Usalama wa nchi na raia
Kigamboni ni eneo la kimkakati kwenye usalama wa nchi na raia pia na serikali imewekeza sana kule, kuna kambi ya jeshi na ofisi za vitengo vya usalama.. Lilipaswa kuwa eneo la kuogopwa na wapigaji wakubwa! Sasa ninini kilitokea hapa mpaka watu wanatoboa ardhi mpaka kulifikia bomba na kunyonya mafuta kwa miaka miwili kasoro bila kustukiwa na organ za usalama?

3. Mfadhili na mmiliki wa huu mradi si mtu mdogo asilani
Na pengine ni mojawapo wa matajiri wenye kumiliki kadi ya kijani na mfadhili wa chama na viongozi wake. Pengine ni mmojawapo wa matajiri anayeheshimiwa na pengine kuogopwa na viongozi wetu na pengine ana miliki cheti cha mlipakodi mkubwa mzuri kupitia miradi mingine aliyoanzisha kwa kutumia pesa za kutakatisha za wizi wa mafuta.

4. Kikosi kazi kilichotekeleza ule mtobozano ni kikosi toka nje ya nchi kwa vyovyote kilichokuwa na kila nyenzo ya kisasa zikisaidiwa na mashine za kutoboa visima virefu In fact kazi ilifanywa na watu wachache na mitambo ya kisasa kwa kutumia computer tu. Yaani vitu vinasetiwa toka umbali wa bomba lilipo, uchorongaji nknk. Watu wako kwenye AC na vikombe vya NIDO kama wanaangalia movie.

Hakuna jambo linalokosa asili. Ilianza kule Tegeta nadhani kuna watu walikamatwa kwenye nyumba nao wakiwa wamejiunganishia bomba lao toka bomba kuu na wakawa wanakula maisha kwa kwenda mbele. Hawa walikuwa level one au shule ya msingi.

Akaja kukamatwa tajiri aliyeibuka ghafla, Princess Muro akiwa na mabasi ya kusafirisha abiria mengi tu na vituo vya mafuta vilivyokuwa vinachipua kama uyoga. Kumbe huyu naye alikuwa kajiunganishia bomba lake la mafuta toka bomba kuu la serikali. Alikamatwa na kufilisiwa nadhani. Huyu ni level two au shule ya sekondari.

Huyu aliyekamatiwa vitu vyake Kigamboni yeye tunamuweka level 3 au chuo kikuu alisoma makosa ya waliotangulia akafanya marekebisho mengi akafanya yake!

Je, kutakuwa na level 4? Muda utasema!

Uzalendo ni kitu kikubwa sana. Uzalendo ni zaidi ya kuvaa scalf na nguo zenye rangi ya taifa, uzalendo ni zaidi ya kusimama majukwaani na kuhubiri. Ule wizi wa Kigamboni una mkono wa Watanzania wengi tu mle ndani na wengine pengine wakiwa na dhamana ya ulinzi na usalama wa nchi lakini wote wakapiga kimya!

Aakari waliokamata ile gari iliyopelekea kubumbuluka kwa wizi huu mkubwa sijui watapewa zawadi gani. Lakini hata hivyo pamoja na serikali kuishia kutaifisha ile nyumba na magari na ile mitambo sidhani kama wamiliki halali wa ule wizi watakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria, sana sana watakamatwa vijana wetu wasiojua mengi.

Kama hujui jamaa kapiga bei gani kwenye huu wizi angalia hizi hesabu. Na kama zikija kupatikana hesabu halisi huu unaweza kuja kuwa upigaji mkubwa kuja kutokea Tanzania.

Nakupa hesabu kwa uchache tuu na bei ya chini kabisa:

Kama kwa siku alivuna tanker kumi tu za lita elfu 10 kila moja na akaenda kuuza kila lita moja kwa sh. 1000 tu,
  • Kwa siku moja alikuwa anaingiza kwa uchache milioni 100 kumi za Kitanzania
  • Kwa wiki milioni 700
  • Kwa mwezi bilion 2.8
Piga kwa mwaka au miezi 20 aliyofanya kazi

Sitaki kuongelea ya Mkuu wa Wilaya ambaye alikuwa hajui jina hata moja ya vile vifaa vilivyotumika pale. Hivi kwanini hawakumuandaa? Walimkurupusha tu au alikurupuka? Hivi kweli DC anashindwa kusema hata welding machine?

Eneo lote lilikuwa na camera na ulinzi mkali 24/7, hivyo miliiki alikuwa anaona kila kitu. Mpaka DC na timu yake yote alionekana bila chenga. Hii ni big mistake! Walimpa nafasi bora sana ya kujipanga ama kukimbia.

Anyway, upigani ni jadi hasa kwa Taifa kama Tanzania na pengine hili nalo litapita kama mengine yote.
Mkuu wezi ni hao hao serikali amini nakwambia, hapo wanaondoana wezi wa awamu ya 5 wanaanza wa awamu ya 6. Ni hiyo hiyo serikali nakwambia. Ukitaka kujua kuibia serikali ni ngumu anza ww mipango ya kuiba tu lazima utakamatwa mara moja.
 
Back
Top Bottom