UCHAMBUZI: Hoja za NECTA kufuta utaratibu wa kutangaza shule bora na wanafunzi bora hazina mantiki kwa 100%

Siku ya leo, Baraza la Taifa la Mitihani Nchini Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne na kufuta utaratibu wa muda mrefu wa kutoa orodha na mtiririko wa ubora wa shule kulingana na kiwango cha ufaulu na pia limefuta utaratibu wa kutangaza wanafunzi bora wa mitihani hiyo. NECTA imetoa sababu kuu mbili za wao kufanya hivyo, ambazo ni;

-Kutangaza shule bora ni kutangaza biashara kwa shule hizo.

-Hakuna usawa baina ya shule moja na nyingine katika mazingira ya utoaji elimu hivyo hawapaswi kushindanishwa.

Kwa kuwa JF ni Kisima cha maarifa na uchambuzi huru, Mimi binafsi hapa hapa nitazipinga hoja zote hizo mbili kwa kuchambua kwa kina hoja kwa hoja.

1. Hoja ya kutangaza biashara
Kwanza kabisa hoja hii imekaa kiupande mmoja, ni hoja ya kibaguzi kwa 100% na kuumiza wasiohusika kwa 100%. It is a double standard decision. Sababu za kibiashara zimewalenga wamiliki wa shule binafsi (zimewabagua) na hapo hapo zinazinyima fursa shule za serikali pasipo sababu (zime wahukumu pasipo kuhusika).

Pili ni hoja ya nusu nusu mno, kwa kuwa NECTA hiyo hiyo ndio imekuwa ikitoa hadharani matokeo yote ya shule moja moja yenye kuakisi ubora wa shule husika, hata kama NECTA haitaweka mtiririko rasmi wa ubora bado mtu yoyote makini (hata asiye makini) anaweza kuchambua na kuonyesha zipi ni shule kumi bora zaidi kulingana na mtiririko wa kimatokeo ulivyo.

Na katika hili, mtu au taasisi tofauti (vikiwemo vyombo vya habari) vinaweza kuja na uchambuzi wenye kukinzana na kuzaa upotoshaji. Kifupi tu, NECTA imejivua jukumu lake na sasa inakwenda kuruhusu mtu au taasisi yoyote kujitangazia ubora wake kimatokeo, hata kama ni kwa upotoshaji. Na tutegemee matangazo ya kibiashara (yenye chembechembe za upotoshaji) kwa kwa kutumia matokeo ya NECTA yakichipuka na kuongezeka maradufu. Mwisho katika hili, NECTA haipaswi kukwepa kuteketeleza majukumu yake, kisa tu inaogopa kivuli cha kuonekana inatangazia biashara shule bora. Vipi kama shule hizo 10 bora ningekuwa ni shule za serikali tu?

2. Hoja ya mazingira yasiyolingana katika utoaji elimu hapa nchini
Nadhani huenda hii ni hoja ya kipumbavu kupita maelezo kuwahi kutolewa na NECTA. Kwanza kabisa kuweka hoja sawa, sote yanapaswa kufahamu kuwa, NECTA haiwajibiki popote katika kutengeneza, kuboresha au kuyapima mazingira ya utoaji elimu hapa Tanzania, hivyo hawapaswi kuyasemea chochote mazingira hayo maana sio jukumu lao.

Pili NECTA wanawajibika kuandaa, kusimamia, kusahihisha na kutoa matokeo ya mitihani. Kama NECTA wanaona na kuamini kuwa mazingira ya utoaji elimu hapa Tanzania hayako sawa baina shule na shule na yanaathiri matokeo yao, ni kwanini waandae mitihani mmoja kwa wote au usahihishaji na utoaji wa alama za ufaulu uwe sawa?

Kwanini suala la utofauti wa mazingira baina ya shule moja na nyingine liwe ni hoja wakati wa kutangaza ubora wa shule tu, lakini isiwe ni hoja ya msingi wakati wa kutunga mitihani, kusahihisha na kuweka alama za ufaulu?
Ni upuuzi tuu usio na meingi
 
Tusiingize chuki za kijinga kwenye serikali ya wananchi
Ni jambo la aibu serikali kuwa na chuki na shule ilizozisajili zinazofanya vizuri
Hizi chuki za kijinga ndo zilikuwepo kwenye awamu Fulani kwenye sekta binafs tuzikatae
Akili ndogo sana hiyo uliyotumia hapo.

Serikali ina uwezo wote na mamalaka ya kufanya lolote, so kutolewa tamko lile nyie wenye skuli mnazodhani ni bora kuliko nyingine msidhani ni chuki.

Kataa roho hiyo inayokwambia kila jambo linaloletwa na serikali lenye kuleta mabadiriko ni chuki, hiyo ni roho ya ibilisi kijana wangu!.
 
Kama NECTA wanaona na kuamini kuwa mazingira ya utoaji elimu hapa Tanzania hayako sawa baina shule na shule na yanaathiri matokeo yao, ni kwanini waandae mitihani mmoja kwa wote au usahihishaji na utoaji wa alama za ufaulu uwe sawa?

Kwanini suala la utofauti wa mazingira baina ya shule moja na nyingine liwe ni hoja wakati wa kutangaza ubora wa shule tu, lakini isiwe ni hoja ya msingi wakati wa kutunga mitihani, kusahihisha na kuweka alama za ufaulu?
Mkuu wangu, kwa hii hoja nimekupata vizuri sana. Kama kweli NECTA wanafahamu mazingira hayafanani basi watunge mitihani miwili.....mmoja wa mazingira mazuri na mmoja wa mazingira mabaya.
 
Mimi nakasirika sana, kwanini shule za kanisa zinafanya vyema kuliko za kata? Shule inaitwa Taifa, performance yake kama Taifa Stars ✨, halafu shule inaitwa St. Francis performance yake kama Argentina 🇦🇷 mabingwa wa dunia.

Hamjui inaumiza kiasi gani. Afadhali hata UMUGHAKA ana option, either afe yeye au afe Rehema
Matokeo yamekuvuruga, UMUGHAKA anahusikaje huku 😅 😅 😅 😅 😅 😅
 
Siku ya leo, Baraza la Taifa la Mitihani Nchini Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne na kufuta utaratibu wa muda mrefu wa kutoa orodha na mtiririko wa ubora wa shule kulingana na kiwango cha ufaulu na pia limefuta utaratibu wa kutangaza wanafunzi bora wa mitihani hiyo. NECTA imetoa sababu kuu mbili za wao kufanya hivyo, ambazo ni;

-Kutangaza shule bora ni kutangaza biashara kwa shule hizo.

-Hakuna usawa baina ya shule moja na nyingine katika mazingira ya utoaji elimu hivyo hawapaswi kushindanishwa.

Kwa kuwa JF ni Kisima cha maarifa na uchambuzi huru, Mimi binafsi hapa hapa nitazipinga hoja zote hizo mbili kwa kuchambua kwa kina hoja kwa hoja.

1. Hoja ya kutangaza biashara
Kwanza kabisa hoja hii imekaa kiupande mmoja, ni hoja ya kibaguzi kwa 100% na kuumiza wasiohusika kwa 100%. It is a double standard decision. Sababu za kibiashara zimewalenga wamiliki wa shule binafsi (zimewabagua) na hapo hapo zinazinyima fursa shule za serikali pasipo sababu (zime wahukumu pasipo kuhusika).

Pili ni hoja ya nusu nusu mno, kwa kuwa NECTA hiyo hiyo ndio imekuwa ikitoa hadharani matokeo yote ya shule moja moja yenye kuakisi ubora wa shule husika, hata kama NECTA haitaweka mtiririko rasmi wa ubora bado mtu yoyote makini (hata asiye makini) anaweza kuchambua na kuonyesha zipi ni shule kumi bora zaidi kulingana na mtiririko wa kimatokeo ulivyo.

Na katika hili, mtu au taasisi tofauti (vikiwemo vyombo vya habari) vinaweza kuja na uchambuzi wenye kukinzana na kuzaa upotoshaji. Kifupi tu, NECTA imejivua jukumu lake na sasa inakwenda kuruhusu mtu au taasisi yoyote kujitangazia ubora wake kimatokeo, hata kama ni kwa upotoshaji. Na tutegemee matangazo ya kibiashara (yenye chembechembe za upotoshaji) kwa kwa kutumia matokeo ya NECTA yakichipuka na kuongezeka maradufu. Mwisho katika hili, NECTA haipaswi kukwepa kuteketeleza majukumu yake, kisa tu inaogopa kivuli cha kuonekana inatangazia biashara shule bora. Vipi kama shule hizo 10 bora ningekuwa ni shule za serikali tu?

2. Hoja ya mazingira yasiyolingana katika utoaji elimu hapa nchini
Nadhani huenda hii ni hoja ya kipumbavu kupita maelezo kuwahi kutolewa na NECTA. Kwanza kabisa kuweka hoja sawa, sote yanapaswa kufahamu kuwa, NECTA haiwajibiki popote katika kutengeneza, kuboresha au kuyapima mazingira ya utoaji elimu hapa Tanzania, hivyo hawapaswi kuyasemea chochote mazingira hayo maana sio jukumu lao.

Pili NECTA wanawajibika kuandaa, kusimamia, kusahihisha na kutoa matokeo ya mitihani. Kama NECTA wanaona na kuamini kuwa mazingira ya utoaji elimu hapa Tanzania hayako sawa baina shule na shule na yanaathiri matokeo yao, ni kwanini waandae mitihani mmoja kwa wote au usahihishaji na utoaji wa alama za ufaulu uwe sawa?

Kwanini suala la utofauti wa mazingira baina ya shule moja na nyingine liwe ni hoja wakati wa kutangaza ubora wa shule tu, lakini isiwe ni hoja ya msingi wakati wa kutunga mitihani, kusahihisha na kuweka alama za ufaulu?
Kwa nini shule bora zipatikane kwenye majiji na ile mikoa yenye ushawishi ina maana sehemu zingine hazistahili kuuonja huo utamu wa ubora?
 
Wapo sahihi. Watoto wanatoka mazingira tofauti. Wote hao wanapambania mtihan mmoja. Wewe mwingine unasa huku una njaa mazingira magumu wemzako wanasoma na sosej zinaozea kwenye ma lunch box kwa kukosa hewa maana kachemshiwa nyumban na kapewa na elfu kumi ya kula shule.
 
Bado hujajadili hoja hapo juu na wala hujajibu hoja. Uko nje ya mada.

Kama mazingira ya kielimu ni tofauti, kwanini NECTA watunge mtihani mmoja kuwapima wote?
Kwan utaratibu wa kutangaza umeanza lini? Upo kwnye katiba? Em tuamlngalie matokeo ya kwanza baada yabuhuru .
 
Siku ya leo, Baraza la Taifa la Mitihani Nchini Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne na kufuta utaratibu wa muda mrefu wa kutoa orodha na mtiririko wa ubora wa shule kulingana na kiwango cha ufaulu na pia limefuta utaratibu wa kutangaza wanafunzi bora wa mitihani hiyo. NECTA imetoa sababu kuu mbili za wao kufanya hivyo, ambazo ni;

-Kutangaza shule bora ni kutangaza biashara kwa shule hizo.

-Hakuna usawa baina ya shule moja na nyingine katika mazingira ya utoaji elimu hivyo hawapaswi kushindanishwa.

Kwa kuwa JF ni Kisima cha maarifa na uchambuzi huru, Mimi binafsi hapa hapa nitazipinga hoja zote hizo mbili kwa kuchambua kwa kina hoja kwa hoja.

1. Hoja ya kutangaza biashara
Kwanza kabisa hoja hii imekaa kiupande mmoja, ni hoja ya kibaguzi kwa 100% na kuumiza wasiohusika kwa 100%. It is a double standard decision. Sababu za kibiashara zimewalenga wamiliki wa shule binafsi (zimewabagua) na hapo hapo zinazinyima fursa shule za serikali pasipo sababu (zime wahukumu pasipo kuhusika).

Pili ni hoja ya nusu nusu mno, kwa kuwa NECTA hiyo hiyo ndio imekuwa ikitoa hadharani matokeo yote ya shule moja moja yenye kuakisi ubora wa shule husika, hata kama NECTA haitaweka mtiririko rasmi wa ubora bado mtu yoyote makini (hata asiye makini) anaweza kuchambua na kuonyesha zipi ni shule kumi bora zaidi kulingana na mtiririko wa kimatokeo ulivyo.

Na katika hili, mtu au taasisi tofauti (vikiwemo vyombo vya habari) vinaweza kuja na uchambuzi wenye kukinzana na kuzaa upotoshaji. Kifupi tu, NECTA imejivua jukumu lake na sasa inakwenda kuruhusu mtu au taasisi yoyote kujitangazia ubora wake kimatokeo, hata kama ni kwa upotoshaji. Na tutegemee matangazo ya kibiashara (yenye chembechembe za upotoshaji) kwa kwa kutumia matokeo ya NECTA yakichipuka na kuongezeka maradufu. Mwisho katika hili, NECTA haipaswi kukwepa kuteketeleza majukumu yake, kisa tu inaogopa kivuli cha kuonekana inatangazia biashara shule bora. Vipi kama shule hizo 10 bora ningekuwa ni shule za serikali tu?

2. Hoja ya mazingira yasiyolingana katika utoaji elimu hapa nchini
Nadhani huenda hii ni hoja ya kipumbavu kupita maelezo kuwahi kutolewa na NECTA. Kwanza kabisa kuweka hoja sawa, sote yanapaswa kufahamu kuwa, NECTA haiwajibiki popote katika kutengeneza, kuboresha au kuyapima mazingira ya utoaji elimu hapa Tanzania, hivyo hawapaswi kuyasemea chochote mazingira hayo maana sio jukumu lao.

Pili NECTA wanawajibika kuandaa, kusimamia, kusahihisha na kutoa matokeo ya mitihani. Kama NECTA wanaona na kuamini kuwa mazingira ya utoaji elimu hapa Tanzania hayako sawa baina shule na shule na yanaathiri matokeo yao, ni kwanini waandae mitihani mmoja kwa wote au usahihishaji na utoaji wa alama za ufaulu uwe sawa?

Kwanini suala la utofauti wa mazingira baina ya shule moja na nyingine liwe ni hoja wakati wa kutangaza ubora wa shule tu, lakini isiwe ni hoja ya msingi wakati wa kutunga mitihani, kusahihisha na kuweka alama za ufaulu?
Sababu za kumtoa Mbobezi Dr. Charles Msonde kama nahisi zimepatikana!
 
Mimi nakasirika sana, kwanini shule za kanisa zinafanya vyema kuliko za kata? Shule inaitwa Taifa, performance yake kama Taifa Stars ✨, halafu shule inaitwa St. Francis performance yake kama Argentina 🇦🇷 mabingwa wa dunia.

Hamjui inaumiza kiasi gani. Afadhali hata UMUGHAKA ana option, either afe yeye au afe Rehema
Mnajiuliza maswali ya hoovyooo!
 
Tambua kwa namna yeyote ile huwezi kulinganisha sasa tuje kweny za serikali zimazofanya vizuri kama Tabora boys ,ilboru.

Je izo shule zinareflect jamii za izo shule zilipo kwa watu wa mkoa wa shule izo zilizopo ndo wanajua sana...point👉 serikali kupitia mitihani ya elimu ya msingi wale vipanga ndo wanaenda kujumuika kutoka shule tofauti kwa hao wanaandaliwa sawa na kuchukua wachezaji wakali kuweka timu moja then upambanisha na timu Haina wachezaji class ya juu.

Ni kwamba hata uchukue za serikali tayar ilboru Wanaenroll vipanga kutoka sehemu nyingi za Tanzania ..private nao wamechukuw vipanga ivyo ivyo Tena na kuwajengea mazingira mazuri Zaid.

Katika kuja kucompara tayar ushajua wa kwanza atakuwa yupi maana wale weny akili wote wamawekwa sehemu moja.

Labda private wao na list yao na government yao ..hata hao government wale vipanga wanakuwa wako shule kama kibaha, ilboru ,Tabora boys& girl wawe na list yao ya kupambana ..Shule za kata ziwe na list yao.
Mkuu una hoja.
 
Mkenda ni smart na izo hoja ulizoweka anaweza pangua zote hata Mimi binafsi naweza kuzipangua.

Unajua umafia wa kweny biashara iwe bidhaa au elimu? Unajua izo shule wanafunzi wanalipa shilling ngapi then uje kufananisha na elimu bure? Mkenda na wenzie michezo yote wanaijui wapo kweny game kitambo hawajai kurupuka sio rahisi.

Mazingira ya izo shule na st kayumba unayajua.

Nakupa home work 👉 Kaangali motisha ya walimu wa izo shule kabla ya wanafunzi then uje hapa kuleta jibu.
Kwani Kuna kitu kinabadilika?? Maana km shule yako imefelisha imefelisha tu!!! Hakuna kipya hapo!!!
Wale private wakifaulu wamefaulu tu
 
Back
Top Bottom