UCHAMBUZI: Hoja za NECTA kufuta utaratibu wa kutangaza shule bora na wanafunzi bora hazina mantiki kwa 100%

UCHAMBUZI: Hoja za NECTA kufuta utaratibu wa kutangaza shule bora na wanafunzi bora hazina mantiki kwa 100%

Wewe kwa akili yako umeona ni sawa aanze na kuondoa ushindani wa ubora wa elimu na kuficha takwimu?
Badala ya kuanza na kuboresha mazingira kwanza
Usiunge tu mkono sio kila kiongozi anakuwa sahihi
Sipo sahihi kwa mtazamo wako ..ila tambua haijalishi kwa kiasi gani lakini watu wanatokea mazingira tofauti kama Wana elimu nzuri zinazotolewa huko ni kwamba sio kila mtoto wa kitanzania anaweza kumudu kimantiki ya uchumi ... Serikali yetu haswa na umaskini wa nchi yetu Haina kiwango cha juu cha elimu haswa miundombinu.

Angalia hoja ivi then
1. Shule za private Zinachagua wale vipanga kupigia interview je serikali ifanye ivyo na hao wataofeli kwamba wamedisqualify kusoma unaona itakuwa sawa? Serikali inachukua wote wasome maana ni huduma sio biashara.

2.Uchumi(Ada) hata wwe sijajua uchumi wako ila hakuna asiyependa mwanae asome feza ila hali ya uchumi hairuhusu hata boarding wanakula vizuri yaani Maisha safi vocation za kumwaga ...huku st kayumba hamna cha maana labda muenda mapango ya Amboni.

3.serikali yenyewe ilishachagua shule za vipaji mfano Tabora ,ilboru wale weny ufaulu mkubwa kutoka darasa la Saba wanapelekwa huko na efforts zilizopo katika shule izo si za mchezo ,je hao wengine huoni kuwekwa shule za kata ni wengi wao ni kuzidi kuwekewa mazingira ya kupata zero.

4.Niambia tajiri gani anajiamini mwanae ana akili akampeleka kusoma shule za kata ?
 
Hivi na zile bajeti za chai vitafunwa semina kusafiri alizoondoa Jpm kwenye maofisi bado zipo au.?? Hivi na mambo mengine muhimu ndio vitu vya kuangalia sio kupoteza muda kwenye hayo matokeo.
 
Siku ya leo, baraza la taifa la mitihani nchini Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne na kufuta utaratibu wa muda mrefu wa kutoa orodha na mtiririko wa ubora wa shule kulingana na kiwango cha ufaulu na pia limefuta utaratibu wa kutangaza wanafunzi bora wa mitihani hiyo. NECTA imetoa sababu kuu mbili za wao kufanya hivyo, ambazo ni...
Na huko kwenye taasisi ya wahandisi (ERB) kila mwaka kwenye Annual day yao hutoa zawadi Kwa wanafunzi wahitimu Bora Kwa kila fani Kwa kila mwaka. Kwa maoni yangu hii nayo Haina maana labda kama mtihani ungekuwa ni ule ule Kwa vyuo vyote na siyo kama ilivyo sasa Kwa kila chuo kuwa na mtihani wake hata kama iko moderated.

Mawazo yangu ni kwamba kila chuo kitoe wanafunzi wake Bora harafu wapewe mtihani mmoja kwenye mazingira sawia Ili washindanishwe na kumpata aliye Bora zaidi. Vinginevyo Kwa hali ya sasa Haina maana yoyote.
 
Huu uamuzi wa hovyo kwa namna fulani utapunguza morali miongoni mwa walimu na shule zetu, hawa jamaa simply wanataka iwe business as usual, mkifaulu wengi mtajua wenyewe, na mkifeli wote mtajua wenyewe, hawajui maana ya motisha kabisa.

Huu uamuzi kwa upande mwingine naona utaziathiri zaidi zile shule zinazofanya vibaya, kwani sasa matokeo yao mabovu yatakuwa siri, walimu hawataona aibu shule zao kufelisha wengi, wakuu wa wilaya na mikoa hawatawajibika, wala hapatakuwepo na jitihada zozote za kubadilisha hali.
Itakuwa siri vipi wakati matokeo yapo kwenye tovuti!?

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
 
Mleta mada anahoja za msingi Sana.

Kwanza naunga mkono uamuzi wa NECTA japo hapo kwenye sababu zilizotolewa zinahitaji maboresho kidogo.

Ila nimeona baadhi ya wachangiaji wanazungumzia suala la upotoshaji kwamba shule inaweza sema ni ya kwanza wakati sio ya kwanza.

Sasa kwa hiyo hoja ndio pia naungana na NECTA kufuta huo utaratibu sababu watafuta shule za watoto wao wajikite kuangalia ufaulu na sio shule imekuwa ya ngapi. Hapo jambo la muhimu ni ufaulu na sio nafasi ya Shule.

Hata kama umeambiwa shule ni ya kwanza, wewe kama mzazi angalia ufaulu na ukiridhika peleka mtoto wako.

Kwa sababu shule inaweza kuwa ya kwanza ila kwa wajinga. ( Ndio ile mjinga kawa wa kwanza kwa wajinga wenzake)
 
Mimi naona wapo sahihi kwa 100% kufuata upumbuvu huo kwa kuwa ubora wa Elimu aliyo ipata mtu tutaupima mtu anapo kuwa mtaani anavyo mudu mazingira yake na kusaidia wengine.

Watu wanaiba mitihani na kuweka mikakati ya udanganyifu na wengine wamefaulu mpka kuitwa maprofefa lakini anadai chuo kikuu alichokuwa anafanyia kazi ambapo ni chuo kikuu maarufu palikuwa jalalani kwa sababu tuu ya kacheo ka uwaziri.
Kutotangaza ni sawa na Wala Haina shida japokuwa inaweza kuwa na msukumo wa Utanganyika na Uzanzibari. Nakumbuka wakati wa sherehe mojawapo sikumbuki kama ni ya mapinduzi au vipi huko Zanzibar ambayo pia JPM alihudhuria.

Wakati akihutubia aliwasifia mabinti wazuri wa kizanzibar lakini akasema tatizo lao ni Kwa shule za Zanzibar kufeli sana kwenye mitihani hasa ya form 4.

Alifanya rejea ya MATOKEO ya mwaka huo Kwa shule nyingi za Zanzibar zikiwa zimeburuza mkia kulinganisha na za bara. Nadhani wazenji wengi wanaona kama kutangaza kunawadhalilisha ingawaje pia Kuna shule kadhaa Toka Zenji zinafanya vyema.
 
Hii point ya Mtihani mmoja umeishikilia Bango sana. Washauri pia hao unawatetea wapokee wanafunzi direct kutoka Wizara ya Elimu/ Tamisemi bila kuwachuja kwa level wanayotaka wao.
Nitakujibu hapa hapa.
Hiyo hoja ya kuwa na mtihani mmoja ninaishikia bango kwa kuwa ndio msingi unao kinzana na hoja hafifu za NECTA. Kama NECTA wanaamini utofauti wa kimazingira katika utoaji elimu unaathiri moja kwa moja matokeo ya mitihani, kwanini wasilizingatie hilo tangu wakati wa kutunga na kusahisha mitihani, badala ya kuja kulizingatia wakati kutangaza washindi?
 
Mnaoneje Serikali iweke utaratibu wa Shule zote Private and Government zipate selection ya Watoto directly kutoka Wizara ya Elimu/ Tamisemi???
Mkuu kitu ambacho hukifahamu ni hichi.
1. Hapo zamani watoto wengi waliokuwa wanakwenda kusoma shule za private ni wale waliofeli darasa la saba.

2. Kuongezeka kwa shule za serikali hususani za kata huku ada ikiwa sawa na bure kulipelekea shule nyingi za private kukosa wanafunzi (kudorora) na chache kubakia na wanafunzi.

3. Kwa zama hizi za sasa, mzazi anayepeleka mtoto wake shule za private anasukumwa na sababu zake binafsi sana (kama imani, swaga), ubora wa shule husika huku mfukoni akiwa vyema.

Sasa katika tafakari hiyo jenga hoja yako.
 
Mkenda ni smart na izo hoja ulizoweka anaweza pangua zote hata Mimi binafsi naweza kuzipangua...
Kwani mazingira ya shule hizo boss yameanza kubadilika kipindi cha hivi karibuni? Mbona serikali kuhusu mazingira ni yale yale tu auhisi labda kuna sababu nyingine?
 
Mimi nakasirika sana, kwanini shule za kanisa zinafanya vyema kuliko za kata? Shule inaitwa Taifa, performance yake kama Taifa Stars ✨, halafu shule inaitwa St. Francis performance yake kama Argentina 🇦🇷 mabingwa wa dunia.

Hamjui inaumiza kiasi gani. Afadhali hata UMUGHAKA ana option, either afe yeye au afe Rehema
Hahahahaha
 
Shida ni kutokutoa ajira tu, ajira zinaenda kwa urafiki ,undugu, ukabila ,
 
Huu uamuzi wa hovyo kwa namna fulani utapunguza morali miongoni mwa walimu na shule zetu, hawa jamaa simply wanataka iwe business as usual, mkifaulu wengi mtajua wenyewe, na mkifeli wote mtajua wenyewe, hawajui maana ya motisha kabisa.

Huu uamuzi kwa upande mwingine naona utaziathiri zaidi zile shule zinazofanya vibaya, kwani sasa matokeo yao mabovu yatakuwa siri, walimu hawataona aibu shule zao kufelisha wengi, wakuu wa wilaya na mikoa hawatawajibika, wala hapatakuwepo na jitihada zozote za kubadilisha hali.
Huu uamuzi ni mzuri
Kwani shule nyingi zinapambana kuiba mitihani na kukaririsha wanafunzi badala ya kufundisha
Elimu imekuwa kwa ajili ya mitihani sio kwa ajili ya kumsaidia mtoto
 
Mkenda ni smart na izo hoja ulizoweka anaweza pangua zote hata Mimi binafsi naweza kuzipangua.

Unajua umafia wa kweny biashara iwe bidhaa au elimu? Unajua izo shule wanafunzi wanalipa shilling ngapi then uje kufananisha na elimu bure? Mkenda na wenzie michezo yote wanaijui wapo kweny game kitambo hawajai kurupuka sio rahisi.

Mazingira ya izo shule na st kayumba unayajua.

Nakupa home work 👉 Kaangali motisha ya walimu wa izo shule kabla ya wanafunzi then uje hapa kuleta jibu.
Suluhisho ni kuboresha mazingira ili zifanye vizuri, siyo hizi cheap politics mnazozileta. Mnaua elimu. Mnaua motivation.
 
Bado hujajadili hoja hapo juu na wala hujajibu hoja. Uko nje ya mada.

Kama mazingira ya kielimu ni tofauti, kwanini NECTA watunge mtihani mmoja kuwapima wote?
Kama sababu ni mazingira, basi waruhusu na mitihani itungwe na shule husika, kama vyuo vikuu. Hii serikali inaua elimu, na taifa consequently.
 
NECTA walitaka shule binafsi zijitangaze vipi ili kupata wanafunzi wengi kama sio kutumia ubora wa matokeo ya ufaulu wa mitihani ya NECTA?

NECTA inaogopa shule kushindana katika kutoa elimu bora?

NECTA haiamini matokeo ya mitihani yao kama kipimo muhimu na sahihi cha kuzipima shule katika kutoa elimu bora?
Wewe unaamini matokeo ya mtihani ni kipimo sahihi cha uelewa wa mwanafunzi?

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom