UCHAMBUZI: Hoja za NECTA kufuta utaratibu wa kutangaza shule bora na wanafunzi bora hazina mantiki kwa 100%

Sasa why watunge mtihani mmoja kama wanajua Kuna disparity ya quality?

Huyo Mkenda smart kwa lipi? Hakuna hata SoMo la kilimo au viwanda sekondari alafu wanaongelea Tanzania ya viwanda na kilimo wanadhank man power inatokea wapi?

Acheni exaggerate watu wanao under perform, hoja ni kwamba kama una grade basi wangeweza sema Serikali top 10 na private top 10!! Hapo angekua smart.

Nakumbuka walikua wana grade matokeo ya form 6 kwa shule zenye wanafunzi below 40 na above 40 Ili kulinganisha sample zinazofanana.

Sasa kuacha gap ndio Kila mtu ata claim ameongoza kitaifa maana anajua hauna namna ya kuthibitisha!! Mtarudi Tena kuanza kukemea ilihali tatizo mmelileta wenyewe.
Eeh!! Swala ni watu wanaondaliwa katika mazingira tofauti na kuja kufanya mtihani mmoja sio sawa.

Mkenda huwezi kumlaumu kwani yeye ndo hawezi kufanya reforms za haraka katika elimu ni taratibu kaanza na hilo .
 
Haswaa.
Nimekuelewa vyema na umeelewa vyema mada yangu hapa.
 
Siku ya leo, baraza la taifa la mitihani nchini Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne na kufuta utaratibu wa muda mrefu wa kutoa orodha na mtiririko wa ubora wa shule kulingana na kiwango cha ufaulu na pia limefuta utaratibu wa kutangaza wanafunzi bora wa mitihani hiyo. NECTA imetoa sababu kuu mbili za wao kufanya hivyo, ambazo ni;
-Kutangaza shule bora ni kutangaza biashara kwa shule hizo.

-Hakuna usawa baina ya shule moja na nyingine katika mazingira ya utoaji elimu hivyo hawapaswi kushindanishwa.

Kwa kuwa JF ni Kisima cha maarifa na uchambuzi huru, Mimi binafsi hapa hapa nitazipinga hoja zote hizo mbili kwa kuchambua kwa kina hoja kwa hoja.

1. Hoja ya kutangaza biashara.
Kwanza kabisa hoja hii imekaa kiupande mmoja, ni hoja ya kibaguzi kwa 100% na kuumiza wasiohusika kwa 100%. It is a double standard decision. Sababu za kibiashara zimewalenga wamiliki wa shule binafsi (zimewabagua) na hapo hapo zinazinyima fursa shule za serikali pasipo sababu (zime wahukumu pasipo kuhusika). Pili ni hoja ya nusu nusu mnoo, kwa kuwa NECTA hiyo hiyo ndio imekuwa ikitoa hadharani matokeo yote ya shule moja moja yenye kuakisi ubora wa shule husika, hata kama NECTA haitaweka mtiririko rasmi wa ubora bado mtu yoyote makini (hata asiye makini) anaweza kuchambua na kuonyesha zipi ni shule kumi bora zaidi kulingana na mtiririko wa kimatokeo ulivyo. Na katika hili, mtu au taasisi tofauti (vikiwemo vyombo vya habari) vinaweza kuja na uchambuzi wenye kukinzana na kuzaa upotoshaji. Kifupi tu, NECTA imejivua jukumu lake na sasa inakwenda kuruhusu mtu au taasisi yoyote kujitangazia ubora wake kimatokeo, hata kama ni kwa upotoshaji. Na tutegemee matangazo ya kibiashara (yenye chembe chembe za upotoshaji) kwa kwa kutumia matokeo ya NECTA yakichipuka na kuongezeka maradufu. Mwisho katika hili, NECTA haipaswi kukwepa kuteketeleza majukumu yake, kisa tu inaogopa kivuli cha kuonekana inatangazia biashara shule bora. Vipi kama shule hizo 10 bora ningekuwa ni shule za serikali tu?

2. Hoja ya mazingira yasiyolingana katika utoaji elimu hapa nchini.
Nadhani huenda hii ni hoja ya kipumbavu kupita maelezo kuwahi kutolewa na NECTA. Kwanza kabisa kuweka hoja sawa, sote yanapaswa kufahamu kuwa, NECTA haiwajibiki popote katika kutengeneza, kuboresha au kuyapima mazingira ya utoaji elimu hapa Tanzania, hivyo hawapaswi kuyasemea chochote mazingira hayo maana sio jukumu lao.

Pili NECTA wanawajibika kuandaa, kusimamia, kusahihisha na kutoa matokeo ya mitihani. Kama NECTA wanaona na kuamini kuwa mazingira ya utoaji elimu hapa Tanzania hayako sawa baina shule na shule na yanaathiri matokeo yao, ni kwanini waandae mitihani mmoja kwa wote au usahihishaji na utoaji wa alama za ufaulu uwe sawa?
Kwanini suala la utofauti wa mazingira baina ya shule moja na nyingine liwe ni hoja wakati wa kutangaza ubora wa shule tu, lakini isiwe ni hoja ya msingi wakati wa kutunga mitihani, kusahihisha na kuweka alama za ufaulu?
we kinachokusumbua ni nini mpaka povu lote hili. Inaonekana una maslahi flani mmezoea mbeleko. Iacheni taasisi iamue inavyoona inafaa, tukijua wa wanafunzi bora 10 kati ya wanafunzi laki 5 inatusaidia nini. Kuja shule bora 10 kuna ligi? Matokeo yako kwenye mtandao fuatilia matokeo ya shule ambazo una-interest nazo msiingize taasisi ya serikali ktk maslahi yenu. Kwangu mimi wamechelewa sana kufuta upuuzi ule
 
Eeh!! Swala ni watu wanaondaliwa katika mazingira tofauti na kuja kufanya mtihani mmoja sio sawa.

Mkenda huwezi kumlaumu kwani yeye ndo hawezi kufanya reforms za haraka katika elimu ni taratibu kaanza na hilo .
Ndio maana sisi tumewakosoa NECTA kwa kufuta utaratibu wa kutangaza shule bora huku wakija na hoja dhaifu mnoo.

Huwezi kusema mchuzi wa nguruwe ni haramu halafu hapo hapo useme nguruwe ni halali.
 
Serikali imejidhatiti kwa watu wote tambua na utoaji elimu uko katika kiwango kidogo kuanzia mazingira na Mishahara kwa walimu kwa maana iyo kiwango dunia cha elimu kinachotolewa kwa upande wao .

Ukija kw wanafunzi wa private haswa top ten niambie ada wanayolipwa na hata hata wanafunzi wazazi wao wanaweza kuwapeleka kusoma hata marekani pesa ipo ila sio hawa St kayumba wengi hali mbovu wakina sie..
Jaribu kuzunguka katika shule kati ya KEMOS na tafuta ambayo imefeli sana then angalia mazingira .
..
Bado unazunguka hujaelewa hoja za mtoa mada,,,kwanini wapimwe kwa mtihani mmoja angali mazingira ni tofauti??
 
we kinachokusumbua ni nini mpaka povu lote hili. Inaonekana una maslahi flani mmezoea mbeleko. Iacheni taasisi iamue inavyoona inafaa, tukijua wa wanafunzi bora 10 kati ya wanafunzi laki 5 inatusaidia nini. Kuja shule bora 10 kuna ligi? Matokeo yako kwenye mtandao fuatilia matokeo ya shule ambazo una-interest nazo msiingize taasisi ya serikali ktk maslahi yenu. Kwangu mimi wamechelewa sana kufuta upuuzi ule
Rudi usome tena hoja zangu kisha uzichambue, mambo yangu binafsi huyajui na hata ukiyajua hayatakusaidia.
 
Bado unazunguka hujaelewa hoja za mtoa mada,,,kwanini wapimwe kwa mtihani mmoja angali mazingira ni tofauti??
Ndo maana huwezi kuwaweka sawa katika kupanga list ,ndo kafuta ni hatua na tangu mwanzo walikuwa wanajua kwamba hawatokuwa sawa Kwa zile wanasoma mazingira tofauti
 
Ndio maana sisi tumewakosoa NECTA kwa kufuta utaratibu wa kutangaza shule bora huku wakija na hoja dhaifu mnoo.

Huwezi kusema mchuzi wa nguruwe ni haramu halafu hapo hapo useme nguruwe ni halali.
Ndo maana wamtenga hawawezi kuwachanganya wanajitambua sasa
 
Siku ya leo, baraza la taifa la mitihani nchini Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne na kufuta utaratibu wa muda mrefu wa kutoa orodha na mtiririko wa ubora wa shule kulingana na kiwango cha ufaulu na pia limefuta utaratibu wa kutangaza wanafunzi bora wa mitihani hiyo. NECTA imetoa sababu kuu mbili za wao kufanya hivyo, ambazo ni;
-Kutangaza shule bora ni kutangaza biashara kwa shule hizo.

-Hakuna usawa baina ya shule moja na nyingine katika mazingira ya utoaji elimu hivyo hawapaswi kushindanishwa.

Kwa kuwa JF ni Kisima cha maarifa na uchambuzi huru, Mimi binafsi hapa hapa nitazipinga hoja zote hizo mbili kwa kuchambua kwa kina hoja kwa hoja.

1. Hoja ya kutangaza biashara.
Kwanza kabisa hoja hii imekaa kiupande mmoja, ni hoja ya kibaguzi kwa 100% na kuumiza wasiohusika kwa 100%. It is a double standard decision. Sababu za kibiashara zimewalenga wamiliki wa shule binafsi (zimewabagua) na hapo hapo zinazinyima fursa shule za serikali pasipo sababu (zime wahukumu pasipo kuhusika). Pili ni hoja ya nusu nusu mnoo, kwa kuwa NECTA hiyo hiyo ndio imekuwa ikitoa hadharani matokeo yote ya shule moja moja yenye kuakisi ubora wa shule husika, hata kama NECTA haitaweka mtiririko rasmi wa ubora bado mtu yoyote makini (hata asiye makini) anaweza kuchambua na kuonyesha zipi ni shule kumi bora zaidi kulingana na mtiririko wa kimatokeo ulivyo. Na katika hili, mtu au taasisi tofauti (vikiwemo vyombo vya habari) vinaweza kuja na uchambuzi wenye kukinzana na kuzaa upotoshaji. Kifupi tu, NECTA imejivua jukumu lake na sasa inakwenda kuruhusu mtu au taasisi yoyote kujitangazia ubora wake kimatokeo, hata kama ni kwa upotoshaji. Na tutegemee matangazo ya kibiashara (yenye chembe chembe za upotoshaji) kwa kwa kutumia matokeo ya NECTA yakichipuka na kuongezeka maradufu. Mwisho katika hili, NECTA haipaswi kukwepa kuteketeleza majukumu yake, kisa tu inaogopa kivuli cha kuonekana inatangazia biashara shule bora. Vipi kama shule hizo 10 bora ningekuwa ni shule za serikali tu?

2. Hoja ya mazingira yasiyolingana katika utoaji elimu hapa nchini.
Nadhani huenda hii ni hoja ya kipumbavu kupita maelezo kuwahi kutolewa na NECTA. Kwanza kabisa kuweka hoja sawa, sote yanapaswa kufahamu kuwa, NECTA haiwajibiki popote katika kutengeneza, kuboresha au kuyapima mazingira ya utoaji elimu hapa Tanzania, hivyo hawapaswi kuyasemea chochote mazingira hayo maana sio jukumu lao.

Pili NECTA wanawajibika kuandaa, kusimamia, kusahihisha na kutoa matokeo ya mitihani. Kama NECTA wanaona na kuamini kuwa mazingira ya utoaji elimu hapa Tanzania hayako sawa baina shule na shule na yanaathiri matokeo yao, ni kwanini waandae mitihani mmoja kwa wote au usahihishaji na utoaji wa alama za ufaulu uwe sawa?
Kwanini suala la utofauti wa mazingira baina ya shule moja na nyingine liwe ni hoja wakati wa kutangaza ubora wa shule tu, lakini isiwe ni hoja ya msingi wakati wa kutunga mitihani, kusahihisha na kuweka alama za ufaulu?
Umetumwa na hizo shule zinazochuja wanafunzi ili mradi tu zionekane ziko vizuri MPUUZI mkubwa wewe KIMA
 
Ndo maana huwezi kuwaweka sawa katika kupanga list ,ndo kafuta ni hatua na tangu mwanzo walikuwa wanajua kwamba hawatokuwa sawa Kwa zile wanasoma mazingira tofauti
Mkuu umeyaona matokeo na kuyachambua?
Walichokifanya NECTA ni kutupa matokeo yote halafu sisi wenyewe tuyape ubora!! Tukipotosha?
Logic iko wapi?
 
Enzi zetu waliokosa nafasi Shule za Serikali walikwenda Private kama Sangu, Highland etc. Hizi mbwembwe za kutangaza results kwenye Makamera hazikuwepo.
Kabisa ,ni ujuha eti kulinganisaha shule za feza na shule zetu ambazo hazina utamaduni wa kuchuka wanafunzi .Pale feza wakiona huwezi pata division one wanakuhamishia feza international
 
Ndo maana huwezi kuwaweka sawa katika kupanga list ,ndo kafuta ni hatua na tangu mwanzo walikuwa wanajua kwamba hawatokuwa sawa Kwa zile wanasoma mazingira tofauti
Kama huwezi kuziweka shule zote sawa katika upangaji ubora, ni vipi uzitungie mtihani mmoja, usahishe na kuzipa alama katika viwango sawa?
 
Zote zinazoshika top ten ni zile za St na nyinginezo tofauti na za vidumu. Sasa za kule atokapo ndiyo zinakuwa mkiani kabisa. Uzuri mmoja awamu hii ikimalizika tutarudi kwenye ushindani wa hizi shule kama kawaida. Leo nimechungulia shule za kibabe na matokeo kabisa yaonesha ndiyo top ten wao hata kama hazijatangazwa. Hivyo awamu hii wajiangalie Sana kwenye eneo le Elimu bara maana shule za kikrisro ndiyo zinaongoza zikifuatiwa na zinazomilikiwa na Trustees. Wivu huo waache. Mjukuu wangu shule ya Katoliki wako 138 wote ni Div I za single digits na chache Sana double digits. Mmoja wao amepata 3 alikuwa na matatizo ya kiafya toka form One. Ninashukuru Mafather hawakumuondoa wakapambama naye mpaka amepata 3. Halafu MTU anaacha kuzipambanisha kisa eti mazingira tofauti. Ñao waboreshe mazingira yao. Pesa ya kujengea tu madarasa wanatafuna, madawati wanatafuna, vyoo wanatafuna wanajenga uchichoro wa Choo. Yaani ni aibu Sana.
 
Ukitaka kujua ubora wa skuli uitakayo kila matokeo yakitoka fanya kutafuta mwenyewe siyo serikali ikuwekee ubaoni na kukutangazia skuli yako.

Wewe amka na walimu wako fanyeni recruit search alafu iteni media zote pigeni ukunga.
 
Kwa mantiki yake, Je ni sahihi kutunga mtihani mmoja wa kumpima mwanafunzi wa Feza na Kata?
Ni sahihi ,duniani kote hakuna mitihani tofauti kwa ngazi sawa ya kidato ila kulinganisha shule inayochu
 
Back
Top Bottom