Uchaguzi 2020 Uchambuzi: Hotuba ya Tundu Lissu kutangaza nia ya Kugombea Urais - Juni 8, 2020

Uchaguzi 2020 Uchambuzi: Hotuba ya Tundu Lissu kutangaza nia ya Kugombea Urais - Juni 8, 2020

Hao waliokamatwa na kuachiwa mnao ushahidi kuwa hawakufanya malosa ya uhujumu uchumi? Na kama ni hivyo mbona kuna watanzania wengi wanafanya biashara halali hawajakamatwa? Au ndio kuipaka matope serikali? Yaani huna kosa alafu usingiziwe bure?

Unauliza au unapigia jibu mstari?
 
Hoja dhaifu sana ! maneno huumba , anayoyasema Lissu ndiyo atakayotenda , hivyo ndio ilivyo , Kwa mfano , Dr Magufuli amenukuliwa dunia nzima akiwaambia marafiki zake kabla ya kuwa Rais kwamba , nanukuu , " NIKIWA RAIS MTALIMIA MENO " mwisho wa kunukuu , je kwa sasa watu hawalimii meno ?

Toa mfano japo mmoja wa alichosema Lissu kwa maslahi mapana ya nchi aksimamia kutekelezwa - maneno huumba
 
Lissu amekuja kipindi muafaka ambacho kama taifa tunahitaji katiba mpya ya wananchi, tunahitaji mabadiliko makubwa katika mfumo wa utawala na sheria zetu! Tunahitaji kufuta karibu 60% ya sheria zetu! Wanaombeza wambeze, lakini ukweli utabaki palepale ndiye tiba ya mahala tulipo kwama!
 
Amani iwe nanyi Wadau.

kama wote mnavyojua leo ndo siku ile ambayo watanzania kwa pamoja wameweza kushuhudia hotuba ya kwanza kutoka kwa gwiji la upinzani, ndugu Tundu Antipas Lissu. Hotuba iliyokuwa imejaa utulivu, akili, busara na hekima iliyotukuka.

Kama kawaida CCM walipanga yao, kwanza walipanga vijana wao kushambulia kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo facebook na Youtube ili tu kujaribu kuonesha umma na dunia kuwa Lissu hakubaliki ila kiukweli Lissu kwa hotuba ya leo ameonesha kuwa amejiandaa vizuri na amejipanga vizuri kuwa Raisi wa Tanzania mwaka 2020.

Lissu ameweza kuelezea kwa kifupi na kueleweka sana hoja zote zilizotikisa kwenye miaka hii Mitano ambazo sio tu Chadema ila hadi CCM na watanzania kwa ujumla zimewagusa sana.

Hakuna ambae hajui kuwa wafanyabiashara wakubwa na wakati wamenyanyaswa sana kwenye kipindi hiki cha miaka Mitano, kwenye hili Lissu kapiga mulemule, hakuna ambayo hajui kuwa awamu ya tano imeharibu sana kwenye uchumi, kilimo na diplomasia, kwenye haya tena Lissu kapiga mulemule.

Alipomaliza Lissu ni pale alipoelezea kwa jinsi gani suala la kuonea watu na kukiuka katiba limekuwa linaumiza watu na hapa tena Lissu amepiga mulemule.

Mwisho kuonesha jinsi gani amekomaa, pamoja na kupigwa risasi 16 amesema amesamehe na hatolipa kisasa. Hapa Lissu kawa sawa na Mandela aliyewasamehe makabulu na Papa John Paul 2 aliye msamehe kijana aliyempiga risasi. Lissu ameonesha amekomaa sio tu kiuongozi ila hata kihekima na busara.

Hotuba ya leo ya Lissu imegusia mambo mengi ikiwemo kurekebisha mfumo wa sheria na vyombo vya ulinzi na usalama ili vifanye kazi kwa weredi. Lissu kusema kweli kumaliza yote.

Ukweli lazima tuseme , Ingawa vyombo vya Habari vya Tanzania ikiwemo Azam , ITV na vingine vikubwa kuogopa hata kurusha Habari ya Lissu kutangaza nia leo. Ila hotuba yale imesikika na imewasisimua watu wengi nikiwemo mie. CCM wametumia mbinu ya kuvitisha vyombo hivi kwa makusudi ila Naona nguvu ya Lissu ni kubwa sana kuliko hujuma dhidi yake.

Itoshe kusema Lissu amethibitisha kuwa anatosha akiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2020

Kura yangu anayo akipitishwa na Chadema.

Ushauri kwa Chadema. Isambazeni video ya leo ya Lissu kwenye mitandao mbalimbali kuanzia Insta, Facebook, Twitter na Whatsup’ watu wengi waione maana mkitegemea vyombo vya Habari vya Tanzania vilivyobanw na Ccm mtapoteza.

Jioni Njema!
Huu uchambuzi umejikiga kwenye fikla zako Binafsi

Ni sehemu gani ha huu uchambuzi umeonesha Lissu akigusa maswala ya Kitaifa?
Zaidi zaidi unetaja Shelia na Magufuli.
 
maxresdefault.jpg


pole sana kwa matatizo yaliompata Mh Mbowe kwa kushambuliwa na vijana wahuni.

Jana umehutubia kwa njia ya mtandao kwa kueleza hisia zako juu ya kutaka kuwania nafasi y uraisi kupitia CHADEMA. Ni jambo zuri sana na kupongeza kwa hilo.

Sasa nadhan ni wakat wa wewe kuja kuungana na wana chedema wenzako katika kampeni na sio kufanya hayo unayo yafanya ya ww kukaa huko ugenini na kuhutubia.

Bado najiuliza Inamaana wewe Tundu lisu kila kitu utafanya online
utajaza form online
utafanya kampeni online
kura zako zitahesabiwa online
utamatokea ya uchaguzi online
utaapishwa online
utaongoza nchi online

Njoo kwenye uwanja wa vita utangaze sera zako ukiwa hapa Tanzania.wewe mwenyewe mwoga kuja unaishia kulalamika serikali dhalimu alafu unakaa mbali kuilalamikia serikali kila kukicha.
 
Uweke ushahidi huku wenzako wanatafuta kinga ya kutokushitakiwa. Au unadhani hiyo kinga wanaitaka kwa bahati mbaya?
Kushitakiwa watashitakiwa ila utaratibu wa kuwashitaki ndio umeboreshwa. Yaani unapeleka mashitaka kupita kwa Ag.
 
Back
Top Bottom