Uchambuzi huru: Hotuba ya Rais Samia Suluhu ya Aprili 22, 2021

Mkuu umepotea sana sana. Kwa nini? Au vijana wa sasa na mada zao za ki-Yanga na Simba zinakukwaza? Umetoa hoja nzuri sana sana. Tanzania itajengwa na watanzania na siyo wawekezaji kutoka nje. Hawa wanaoitwa wawekezaji wengi siyo watu wazuri. Mimi hofu yangu ni kuwa mheshimiwa Samia ameanza kuonyesha atawapigia magoti kitu ambacho ni hatari sana.
 
Kwa hiyo miradi yote hiyo ilikuwa mikopo sio? Yaani zile shule za kata na zahanati ambazo Wananchi walijitolea kujenga kwa nguvu kumbr nyie mmekula hela mkidai ni hesabu ya mikopo? Mkuu stick to the question, sijasema JK hakufanya kitu isipokuwa maswali yenu jui ya ongezeko la deni nilitolea maelezi ambayo binafsi yangu ukiniuliza sioni kitu hata kimoja kilichodtahili kukopa feeha nje. Kazi kubwa ya Serikali ni kujenga miundombinu na binafsi sikuiona. Barabara za Dar labda lkn Dar Arusha ilikuwa mbovu, Dar - Mwanza ilikuwa.mbovu na finyu. Dar - Mbeya usiseme. Ajali kukicha. Kuna takwimu za mwaka 2008 ( kama sikosei) tulifikia vifo 20,000 kwa mwaka! Vingi Kuliko hata Ukimwi..samahani lakini..
 
Bora wakongwe mrudi maana mmewaachia jukwaa makuwadi wa siasa hadi kuna kera. Binafsi ninamuombea SSH aongoze yeye nchi hata kama atakosea kuliko kujikuta "wafulani" wanaongoza kwa mlango wa nyuma.
Kikwete is on the steering wheel now. For me this is a sad news.
 
Tunakubaliana kwa vingi nakutofautiana kwa machache katika haya...Ila it doesnt matter kama ni Chines au westerns long as tunashindwa ku bargain na kufikia winwin situation ambayo haiji bila wenye ujuzi na taaluma kuchukua haya majukumu.

Tatizo ni sote kugeuka kuwa waimba chorus tu bila kuwa na critical and analytical mind hasa kwa ile cadre inayohotajika kusimama imara dhidi ya wengi ambao hawakupata nafasi ya kujua lugha ile mataifa makubwa wanaiongea.

Infact hakuna free lunch duniani na hakuna atakaye kuletea share yako kwenye silver plate na wala si kwakupiga makelele mengi ndiyo utawatisha wapigaji...Let us be responsible, wewe na mimi kwa faida ya nchi yetu na vizazi vyetu
 
Unaposema Dar-Mwanza ilikuwa mbovu una maana gani?, Yote ilikuwa mbovu au kuna vipande vilikuwa vibovu?

Unaposema Dar-Mbeya ilikuwa mbovu, uba maana kuwa kutoka Dar hadi Iringa ilikuwa mbovu?

Naona Unageneralize sana mzee bila kuwa na facts

Wakati wa JK ujenzi wa hizo barabara alisisimamia Magufuli huyohuyo unayemsifu na ndizo zilizimfanya akajulikana zaidi na kupendwa na watu kwa jinsi alivyopiga kazi kwenye hayo mabarabara.

Ajali zilichochewa na mambo mengi ikiwemo kutotii ile sheria ya spidi 50
Ajali hazikupungua kipibdi cha Magufuli eti kwa kuwa yeye Alizibomoa hizo barabara na kuzijenga upya bali ninkwa kuwa aligeuza faini za barabarani dili yaani chanzo cha mapato, kwa hiyo tochi za matrafiki zikawa kila pahala
 
Kusema kweli nilisepa kutokana na vijana hawa wa Dotkom maanake kwanza hawana adabu. Haqajui.kujenga hoja kazi yao matusi tu. Unaandika hoja anarudi na matusi unashindwa kujua imetoka wapi halfu hugundua athari za hizi ni athari na hulka zitokanazo na Unazi.

Mzee mzima nikaona isiwe taabu, nijikate mapema maanake nikianza nami matusi kuna wanangu na wajukuu humu halafu watasema duuuh Babu yetu vipi tena. Huwa napitia mara moja moja kuwasoma.
 
Mkuu hakuna kitu kizima nusu nusu aidha ni kibovu au kizima. Nyumba yenye nyufa na inayovuja maji ya mvua, huwezi kusema sio mbovu ila kuna sehemu ndio mbaya.

Kifupi huwezi kulinganisha kabisa wakati wa JK na Magufuli unless unataka kuleta Unazi wa Simba na Yanga. Anyway, naishia hapa naona tunatoka nje ya mada..
 
Hapo palikuwa na upungufu binafsi wa mhusika. Naweza pia kusema JPM hakuwa na itikadi rasmi inayoeleweka na badala yake alichokuwa anafanya ni maono na misukumo yake binafsi.
Nini maana ya Itikadi na unaitafsiri kwa sera na falsafa zipi?
 
Duh kweli wewe kiboko

Kwa hiyo wewe falsafa yako ni kuwa mtu akijenga Barabara ya lami nzuuri Dar mpaka Shinyanga, kwako hiyo siyo mali kitu mpaka tu hiyo ingekuwa imefika Mwanza?

Hoja yako ni Muflisi kwa sababu, nchi haiwezi kujengwa na Mtu mmoja, Akija rais mwingine atamalizia Shinyanga Mwanza

By the way, Kikwete alijenga mtandao wa lami wa kuunganisha mikoa yote TZ bara, alibakisha mikoa Sita tu ikiwemo Manyara na Kigoma. Na huyohuyo Magufuli wako ndiye aliyesimamia ujenzi huo!. Sasa wewe unakuja kuona yule aliyemalizia hiyo mikoa Sita eti kafanya kazi kubwa kuliko aliyejenga ya mikoa 20. Logic yako ya ajabu kweli hapa.

Ninaweza kukuwekea document hapa iliyoandaliwa na Waziri Magufuli mwaka 2015 akionyesha Mafanikio ya miradi ya Ujenzi wa serikali ya Kikwete kuanzia 2005 hadi 2015 uone Jinsi Yule Mkwere alivyofanya mambo makubwa kwenye sekta ya Ujenzi, na ameondoka madarakani huku mirwdi mingine akiwa aneshaitafutia fedha, ameishaifanyia upembuzi yakinifu na mingine ikiwa inaendelea na Ujenzi, Magufuli kama rais kaikuta inaendelea. Sasa kukamilika kwa miradi hiyo kipindi cha Magufuli haimaanishi kuwa yeye ndo kahustle kuiplan na kuitafutia Funding!. No!

Mkandara soma huu uzi hapa chini!, Download document nzina niliyiattach kwenye huo uzi uone miradi aliyoacha JK amekamilisha, aliyoacha ameifanyia upembuzi yakinifu na aliyoacha inajengwa

 
Mkuu nimesafiri njia zote hizo, ilifikia kwenda Mwanza tunazungukia Kenya. Mbeya safari karibu 24 hrs, Arusha karibu siku nzima ukifika hoi. Sasa hivo vipande vipande mnavyotaka kusema ni vipi. Unatoka Dar hujafika Chalinze pale Mlandizi mashimo halafu umnatuambiwa fedha za Mkopo! Ilifika watu walikuwa qanapanda ndege haijalishi kiasi gani nsio.maana bei za ticket za ndege zilirushwa. Makampuni mengi ya nje yakaingia qalipoona firsa hizi. Dar - Mwanza ilikuwa ghali kuliko uruke kutoka Chicago kwenda New York hahahaha! watu haqakujali kwa sababu michongo ya kuibia Seeikali ilikuwa wanjewanje.. Acheni maslhala kama sii Magufuli naapa kwa Mungu, CCM isingerudi Madarakani 2015 ..
 
@Mkandara ,unachambua hotuba ya Mh. Rais Samia au unamuongelea mwendazake JPM!!??
Naona Magufuli nyingi zaidi ya kilichoongelewa na Mh. Rais.
 
Soma hiyo document niliyokuwekea hapo nchini uone jinsi nchi ilivyokuwa inatimka vumbi kwa ujenzi kipindi cha JK

Achana na hearsay

By the way ni JK ndiye aliyetuondolea aibu ya kupitia Kenya kwenda Kagera
 
Reactions: Pep
Aaah kubabake [emoji23][emoji23]
 

Kama wewe unaamini kuwa 1984 Nyerere aliiacha nchi kwenye hali nzuri sana kiuchumi sina neno la kukuongezea.

Isipokuwa ninachofahamu ni kuwa Nyerere alikuwa amehangaika sana kutafuta misaada na mikopo nafuu akaishia kukutana na kikwazo cha IMF. Wafadhili wakubwa hata marafiki wa Tanzania hawakuwa tayari kumpa misaada mikubwa nje ya muafaka na IMF. Yeye aligoma kabisa kusaini mkataba na IMF akaamua kung’atuka.

Nilisoma kuwa AHM alipoingia madarakani kama Rais, wadau mbalimbali na media walimuuliza Mwalimu kama atakuwa radhi mrithi wake AHM asaini mkataba na IMF kama Rais wa JMT. Akasema hana tatizo kabisa na hilo ilimuradi sio yeye!

Nyerere alijua vizuri sana masharti ya IMF kwamba yangeathiri sana legacy yake hasa mashirika ya umma yaliyokuwa yameshikilia uchumi wa taifa. Lakini alijua hakuna namna. Itabidi AHM asaini mkataba na IMF na kuutekeleza. Ilikuwa dhahiri kwamba mashirika kama TRC, ATC, TANESCO, n.k. yaliyokuwa yakiendeshwa bila ufanisi, rushwa kwa wingi, nepotism, n.k. yangetetereka na mengine kufa.

Kwa taarifa yako, ATCL bado haijafufuliwa. Kilichofanyika ni serikali kujitwisha mzigo wa kununua na kumiliki ndege angalau kuweka taswira ya uhai wa ATCL. Ndege sio kigezo cha uhai wa shirika ya ndege. Kama alivyosema Rais Mh. SSH, hatua za kufufua shirika zitachukuliwa rasmi ili kulipa uhai wa kibiashara.

Miradi mingine ya umeme, reli, n.k. bado ni miradi. Tusubiri kuona hatua zitakazochukuliwa kuikamilisha na kuiendesha kwa ufanisi. Nina hakika hata Magufuli angekuwepo isingeendeshwa “KIJAMAA” kama enzi za Nyerere. Na angethubutu kufanya hivyo angekwama mapema sana. Hata North Korea yenyewe leo hii inashiriki uchumi wa kibepari kwa kuibia sana. Makampuni ya US na Ulaya yanazalisha bidhaa huko kwa kutumia mgongo wa China kukwepa vikwazo vya UN.

Kuhusu wizi wa Magufuli nakuachia ubishane na hao waliokuambia. Sina hizo siri.
 
Kuna story moja, sijui kama ni kweli au story tu, lakini ujumbe wake ni muhimu kuuelewa.

Inamhusu waziri mmoja mkubwa wa Nigeria, nafikiri alikuwa waziri wa fedha.

Alikuwa waziri shupavu kupinga rushwa, nchi haijawahi kuona waziri shupavu kama huyo, alikuwa anasema sana kukemea rushwa.

Ikafika wakati akaanza mpaka kwenda benki za kimataifa kunegotiate hela za Nigeria zirudishwe, alikuwa hataki mchezo.

Akaenda Uswizi, akazwa anazunguka mabenki, akafanya uchunguzi kutafuta benki yenye usiri kabisa Uswizi.

Akaipata, akaenda kuonana na CEO wa benki.

Akamwambia anataka majina ya Wanaijeria wote wenye hela kwenye hiyo benki, na vyanzo vyao vya mapato.

CEO akamwambia siwezi kukupa majina hayo.

Akasema nipe majina, ukinipa nitakutafutia deal kubwa sana na serikali ya Nigeria iweke hela zake kwenye benki yako, utapata faida sana.

CEO akawmambia siwezi kukupa majina, nafuata kanuni za faragha za kibenki.

Waziri akamwambia nitatengeneza deal na serikali ya Nigeria kwamba ukiripoti hela za wizi zilizoibiwa Nigeria tutakupa kiasi fulani katika hizo hela.

CEO akakataa, akasema hawezi kuzisaliti kanuni za faragha za kibenki.

Basi yule Waziri akamwambia CEO, huyu hapa Dr. Adebayo Adedeji wa African Development Bank, ukitupa majina tutakupa deal kubwa sana la Benki ya Maendeleo ya Africa, uweke hela za mabilioni mengi sana ya ADB.

CEO akakataa kutoa majina, akasema siwezi kusaliti kanuni za faragha za kibenki.

Waziri akasema sawa, wewe ndiye niliyekutafuta.

Nimekuja na mimi nataka kuweka mamilioni ya dola yangu kwenye benki yenu, lakini kabla ya kuweka kwanza nilikuwa nakupa mtihani nione kama watu wakija kutaka majina ya wateja wenu unaweza kutoa au hutatoa.

What's my point?

Ukiwa so caught up na habari za "mabeberu this, mabeberu that" na kushikwa na theatrics za viongozi wa Afrika wanaojinadi kupigana na mabeberu, unaweza kuchotwa kirahisi na watu wanaoshirikiana na hao mabeberu.

Mtu anaweza kujitengenezea image nzuri kuwa anapingana na mabeberu, kumbe na yeye anajipandisha bei tu apige hela kubwa zaidi.

Tunatakiwa kuwa makini sana tusiingie katika mtego wa simple narratives.

Kuna mabeberu wengine weusi wenzetu Watanzania, na kuna watu wa nchi za nje wanaoweza kutusaidia kupigana na ubeberu.

Kwa hiyo tujadili mambo kwa nuance, sio kwa a broad painting brush.
 
Naamini kabisa hii transition itatupa mwelekeo kama nchi, msije mkampoteza Mh. Kwa tamaa za miradi binafsi, hili hatutalikubali please and please come rain come sunshine....
Mkuu 'Ame'
Nimefuatilia maandishi yako kwenye mada hii, na nadhani nimeelewa vizuri unachkiandika hapa; ambacho mimi ninakubaliana nacho kabisaaaaa!

Ila, usijidanganye, ukadhani viongozi tulionao wana fikra kama ulizonazo wewe; na wala usidhani kwa hali ya wananchi wa Tanzania ilivyo, unaweza ukaitegemea kuzuia chochote.
Akitokea JK mwingine sasa hivi huko CCM, usidhani kuna mtu yeyote atakayenyanyua kidole. Utaanza kuona watu wanajipanga kwenye mstari kuimba nyimbo zake na kumwonyesha yeye ni kama malaika.

Inaumiza sana.

Iwe ni kwa bahati tu, tumpate kiongozi mwenye kuyaamini haya yanayopigiwa kifua na mkuu 'Ame' na wengine kama akina 'Mkandara' na akina 'Kalamu1' - hiyo itakuwa ni bahati yetu nzuri tu na sio kwa utashi wa waTanzania..., sijui kwa nini.
Lakini mtu huyo asiwe kama Marehemu Magufuli, kwa yale mabaya yake!

Sijui tutampataje mtu wa aina hiyo. Najua wapo..., lakini hawataki kujitokeza mbele waliokoe taifa letu.
 
katika miaka ya 90 Cgina ilikuwa na tenda ya kununua skrepa za computer za jeshi (USA). Waamerika hawakutambua kuwa wao walikuwa wanaenda kuzusambaratisha na kuiba siri za teknoljia kutoka hard drve. Walikujatambua wachina wameishaiba siri nyingi.

Dah [emoji23][emoji23][emoji23]

Kweli tumechelewa sana ndugu zangu
 
Naam [emoji1544][emoji1544]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…