Uchambuzi huru: Hotuba ya Rais Samia Suluhu ya Aprili 22, 2021

I cannot say never...Lakini tumpe mama benefit of doubt ni mapema sana kuhukumu; ila nilishajiapiza sintaondoka dunia hii kama msindikizaji ipo siku nayo yaja tena si mbali sana kama si mimi kizazi changu nchi hii haitakaa irudi kwenye ufisadi....nadhani sipo ndotoni ebu tuendelee tuone!
 
Basi ulishindwa kutimiza wajibu wako maana CAG katuonyesha wazi, serikali ya mwendazake ilijaa ufisadi na upigaji.

Na upigaji aliotuonyesha CAG ni just tip of the iceberg, je angekagua mamununuzi ya hizo ndege si pangechimbika?
 
Reactions: Ame
Kama nilivyosema nakubalina kabisa na wewe kwa mengi ila amini nimeishi na hawa ndugu zetu, nimefanya nao kazi tangu ni kiwa kinda kabisa age ya 25 years....Linapokuja maslahi ya jamii yao na mataifa yao imeshakuwa kama ugonjwa they never count us as beneficiaries....At personal level ni watu wazuri sana honest wenye integrity ila nadhani wamekuzwa kuamini sisi hatustahili kama wao. Hata akijitahidi vipi bado hawezi kubali kuwa sawa na sisi...Hofu hii ndiyo inayowapelekea kutoamini kutoa fursa ya sisi kujitegemea hata siku moja kwakua wanajua tukishafanikiwa pengine watapunguza heshima yao.

Chamsingi ni kweli, uki negotiate vizuri wana ka ustaarabu fulani hivi kakukubali ila si kwa level ile ya kukufanya uachane kabisa na utegemezi.
 
Basi ulishindwa kutimiza wajibu wako maana CAG katuonyesha wazi, serikali ya mwendazake ilijaa ufisadi na upigaji.

Na upigaji aliotuonyesha CAG ni just tip of the iceberg, je angekagua mamununuzi ya hizo ndege si pangechimbika?
Pengine!
 
@Mkandara ,unachambua hotuba ya Mh. Rais Samia au unamuongelea mwendazake JPM!!??
Naona Magufuli nyingi zaidi ya kilichoongelewa na Mh. Rais.
Well nachambua kulingana na jinsi mnavyopeleka Mjadala huu maanake nimeona watu wengi bado wanataka kulinganisha sio tu Magufuli na Samia bali hata Viongozi walotangulia kama JK .

Nami sina budi kuweka mawazo yangu haswa pale tunapo tofautiana. Mama Samia alisema Yeye na Magufuli kitu kimoja kwa maana ya kwamba YEYE mama Samia alishiriki kikamilifu katika maandalizi ya dira na mwelekeo pamoja na kila Maamuzi ya Utekelezaji aloyafanya rais Magufuli. Muda wote walikuwa pamoja yeye ubavuni mwake. Kwa wale wanaomlaumu Magufuli basi lawama hizo hata yeye zinamhusu. Lakini wapi kiswahili cha ndani kiliwashinda kutafsiri..

Nami katika bandiko langu nikasema sioni kama wako kitu kimoja! kutokana na hotuba yake siku aloapishwa, na labda sikuongezea pia hotuba yake nyingine siku ya kupokea taarifa ya CAG. Alisistiza sana mageuzi na wala sii maboresho ya dira na mwelekeo! Wazi kabisa alichukua mkondo mwingine hivyo.safari yetu haikuwa ile ya Uchaguzi mkuu 2020 tena.

Toka pale nilimsoma tofauti kabisa na Mambo yaakaanza kwenda kushoto Kulia, mvurugano kila kona, Wanafiki nao wakajitokeza wazi Bungeni, kuna Mkuu wa Mkoa fulani huko kusini, alidiriki hata kusema picha ya rais Magufuli ishushwe hata kabla Mama Samia kuapishwa! Haya yote yametokea within 15 days baada ya Magufuli kuzikwa. I was pissed off, nikamfikiria sana Mama Janet na familia Wanajisokiaje huko waliko? I wouldn't blame her for whatever decisions she has made since!

Na Wakati yote haya yanatokea, Mama Samia anazidi ku pose na mipasho - 'Ukinizungua Tutazinguana!' Sijii ngoma zinachezwa Mitandaoni blaa blaa blaaa yaani mambo ya Mwambao na Kibaokata! Pengine huo ndio Uhuru wa Kujieleza lakini siku zote Uhuru una mipaka yake jamani..
 
Na mm pengine natafuta nafasi hiyo...Moyo wa binadamu una siri sana...I concur!
 
Huu ni ufupisho wa hotuba na wala si uchambuzi
 
Kama ilivyo ada sitachoka kutoa darasa kwa watu wanojadili vitu kwa sababu wamesikia kwa watu wakisema ama wamesoma pahala. ATCL haijafufuka kivipi wakati shirika.lipo, ndege zinaruklshwa na marubani Waajiriwa wa ATCL! Au kufufuka mpaka uhakiki na vidole kama Wafuasi wa Yesu? Hahahaha it's joke.

Ukiachana na Vita ya Uganda, mwaka 1980 hadi 1983, Dunia nzima kulikuwa na Economic Depression yaani kulikuwa na recesssion kali sana duniani, na kwa mara ya kwanza kabisa pipa la mafuta ghafi lilifika Usd 100. Since then hatujawahi kupitia rwcession wqla hatua kama hiyo ndio maana watu wengi hawakumbuki tulikotoka. Ebu Wauulize watu, mara ya mwisho Kimbunga kupita Tz ilikuwa mwaka gani? Utashangaa majibu utapakayo pata maana watakupa mafuriko ya Jangwani.. Hahahaha

Ni wakati huo huo nchi zote maskini zilipigwa na wimbi kubwa la Kiuchumi na pengine kuwa mwisho wa nchi za Kikomunist.

Marekani yenyewe wanamshukuru Reagan mpaka kesho kwa msimamo wake kupitisha Sheria kali ya Uzalendo - Patroit act yaani Mmarekani haruhusiwi kununua nje ya nchi lakini wao wnauza nje. Pia aliwanua kwa kuuza Ngada US wakifanya Money laundy ku finance vikundi vya Sandinista huko Amerika ya Kusini. Marekani (CIA) wakinunua Cocaine kutoka Colombia na kuuza kwa cartel wa US kisha wanachukua fedha na kununua silaha ambazo wanazipeleka huko Nicaragua kusini - A Game changer!

Kwa hiyo Mwalimu aliufanya Ujamaa wetu kama vile mzazi anavyomlea mwanaye anayetambaa. Leo bro unashangaa Mwalimu kutuvika diapers na kutulisha kwa kijiko, akatse tusile nyumba tusozijua.. Mtoto kulelewa na kijiji sii vibaya lakini huwezi kumpa mchawi mwanao amlee! Hizo ni methali zenye nidjamu ya woga wa kumpoteza mwana bora afe wa jirani...sijui unanipata pata?

Kwa hiyo Magufuli asingeweza kuendesha UJAMAA wa Mwalimu na hata Ubepari wa miaka ya 60s hadi 80s sio huu wa leo. Biden hawezi kuiongoza Marekani kwa sera za Jimmy Carter. Umaskini aloukuta Nyerere sio sawa kabisa na Umaskini tulokuwa nao leo. Hivyo itachekesha sana kama Magufuli naye angejaribu kutuvika diapers na kutulisha kwa kijiko ilhali sasa hivi sisi ni midume ya kutafuta Wachumba (Soko huria) Just common sense..

 
Amechambua na kulinganisha kisha kutoa mawazo yake! Hajatumia lugha ya kuudhi, amesema anachoamini yeye! Anachoamini si lazima kiwe sahihi na si lazima tukikubali! Ni mawazo mbadala!
 
Tatizo mabeberu huangalia maslahi yao tu!! Inabidi kuwa tafu sana kushughulika na mabeberu! Wakikuona ni mjanja wanakupigia hesabu ya kukuondoa!!
 
Basi ulishindwa kutimiza wajibu wako maana CAG katuonyesha wazi, serikali ya mwendazake ilijaa ufisadi na upigaji.

Na upigaji aliotuonyesha CAG ni just tip of the iceberg, je angekagua mamununuzi ya hizo ndege si pangechimbika?
Mimi ningeomba hizi taarifa za CAG siku moja zinyanyambuliwe vizuri ili zieleweke.

Haiingii akilini hata mara moja, matarakimu yote yale anayoyatoa kila mwaka uwe ni upigaji; halafu cha kusikitisha zaidi, kila anapomaliza kuyatangaza, na watu kuyapigia mayowe kwa muda, kila kitu kinarudi pale pale kama kawaida, kana kwamba hakuna lolote lililotokea.

Huoni yeyote akiwajibishwa, na wala juhudi za serikali kurekebisha chochote.

Mwishowe, imenibidi nihitimishe kwamba huu ni aina fulani ya usanii mtupu!
 
CAG hapeleki watu mahakamani.
Yeye anafanya kazi na kuiachia serikali au Bunge vichukue hatua. sasa serikali isipochukua hatua au bunge kutochukua hatua, wa kulaumiwa siyo CAG
 
CAG hapeleki watu mahakamani.
Yeye anafanya kazi na kuiachia serikali au Bunge vichukue hatua. sasa serikali isipochukua hatua au bunge kutochukua hatua, wa kulaumiwa siyo CAG
Naelewa vyema, kwamba sio kazi ya CAG kupeleka watu mahakamani, lakini si kuna vyombo stahiki?

Mimi sijamlaumu CAG; sijui ni vipi umenielewa hivyo!
 
Mkuu,nakubaliana nawe.Lakini,hao wazungu hawawezi kutulazimisha.Tunahiari kukubali au kukataa.Katika diplomasia ya uchumi sisi kama nchi lazima tuzingatie "the so called win-win situation." Tunategemeana.
 
Kuwa exposed ina maana gani kwako na ushamba ni nini?!
 
Nasikia uchungu sana nikisoma uzi huu...yale machozi na zile kanga watanzania walizokuwa wanazitandika barabarani walizimaanisha...hata km JPM hakuwapa shilingi....maana kupata kiongozi mzalendo km JPM nimajaliwa na sasa kaondoka what next, business as usual ama?!
Nikiwaza viongozi waliokuwa majasiri km JPM hawakulast nabaki kuwa na maswali mengi sana..

ukiangalia alivyopigwa vita na baadhi ya watanzania...huku watu wengi huko nje wakimsifu wazungu kwa weusi..maswali yananizidi..
Tatizo ni sisi wanyewe watanzania tunasobotage power/maendeleo kwa mgongo wa mabepari kwa shule na degrees walizotumezesha au ni nini?!
Hapa namkumbuka Bob Marley alisema halaumu kwanini hakuenda shule maana angekuwa ignorant..na yet akawa maarufu kwa nyimbo zake za kupinga ubepari na mwisho wake wote tunaujua

vitu vingine haviihitaji rocket science jamani

Sokoine alisema ili usinyanyasike jitahidi ulime kwa bidii ukiwa na chakula chako hakuna atakae kunyanyasa...there is no free lunch jamani...tunaomba viongozi walikuwepo madarakani kwa Sasa mfanyemaamuzi yatakayo tukomboa kutoka kwenye umaskini...uwekezaji uwe wenye tija huku tukijikita kwenye mikakati yakujikomboa wenyewe....mkoloni alituacha kwa jembe la mkono na baadhi bado kilimo nihicho cha msimu..sitaki kuamini km hatuna wataalamu wakilimo wakutosha...hatuna uwezo kufungua viwanda vidogo km vya akina Tanga Fresh,katani,pamba tutengeneze nguo zetu,ngozi - viatu etc

Kuhusu mbegu jamani tuwe waangalifu GMO sio kabisa nadhani tumenusurika kwa Corona sababu ya lishe yetu..,tukiruhusu hizo mbegu zao..I believe ni one big trap..the next pandemic itakuwa balaa..nawakilisha maoni yangu

tusitukanane watanzania tupendane tujibu hoja kwa hoja hamna alikuwa zaidi ya mwingine wote tunajitahidi kujenga nchi yetu,tuwe kitu kimoja maana Mungu wetu ni mmoja

Mungu atubariki Watanzania wote
Mungu mbariki Raisi wetu
 
Mkuu,nakubaliana nawe.Lakini,hao wazungu hawawezi kutulazimisha.Tunahiari kukubali au kukataa.Katika diplomasia ya uchumi sisi kama nchi lazima tuzingatie "the so called win-win situation." Tunategemeana.
Mkuu hili neno 'win- win situation' ni mtego tu inategemea wewe utalielewaje.

Wakati wa JK tuliambiwa ni win win situation. Aki define Ukitaka kula lazima nawe uliwe.. Enzi ya JPM kuna wengine wanasema TUTA-wafukuza Wawekezaji! Hii kutangulizi TUTA wakati hao Wawekezaji bado wapo imna wanazidi kuingia ilinipa wasiwasi kutoka ndani zaidi kuliko nje. Leo tunasikia Tutalegeza masharti ya Uwekezaji...yale yaleeee
 
Daaah Uzuri hiyo ni hadithi japo inafikirisha! Ukweli unabakia Ukisha umwa na nyoka kuogopa majani yakikugusa sii kosa! Tembea sehemu za wazi zaidi kulizo zenye kiza na majani..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…