BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 377
- 435
UCHAMBUZI- HURUMA YA RAIS SAMIA, ILIVYOONDOA MATESO YA WATOTO SHULE SHIKIZI.
Na Bwanku M Bwanku.
Leo Ijumaa Februari 25, 2022 kwenye Gazeti la TANZANIA LEO Ukurasa wa 6 nimechambua uamuzi wa Serikali ya Rais Samia kutoa Bilioni 60 kujenga madarasa 3,000 kwenye Vituo Shikizi 970 na kuwaondolea Wanafunzi mateso makali waliyokuwa wanakutana nayo kwa ubovu na uhaba wa miundombinu ya Vituo hivyo kama uhaba wa madarasa hali iliyopelekea watoto kwa muda mrefu kusomea kwenye miti, matope na nyasi.
Shule Shikizi ni vituo vya kutoa elimu kwa wanafunzi wa elimu ya awali mpaka darasa la pili ambao wanakabiliwa na jiografia mbaya kuelekea kwenye shule mama za Msingi. Shule hizi ni saidizi za shule mama za Msingi. Kuna kata, mtaa ama tarafa ina shule lakini kuna wanafunzi wanaishi mbali sana na shule hizo mama, kwahiyo Serikali ikaona ni vema kujenga Vituo hivi Shikizi kwaajili ya wanafunzi wadogo wapate elimu wakiwa karibu na makazi yao halafu wakishakuwa wakubwa kidogo kwa maana wakishafika darasa la 3 hutoka kwenye vituo hivyo Shikizi na kuendelea sasa na Shule Mama za Msingi.
Kuingia kwa Rais Samia alikerwa na hali mbaya ya mateso ya wanafunzi kusomea kwenye mazingira magumu kwenye vituo hivi na hivyo kuamua kutokea hizo Bilioni 60 kujenga madarasa ya kisasa kabisa ili watoto wasomee pazuri na kuondoa kero hiyo ya miaka kwa miaka. Pata NAKALA ya Gazeti hili sasa ili uone mageuzi makubwa aliyoyafanya Rais Samia kwenye Vituo hivi Shikizi kwa muda wake mfupi tu wa miezi 11.