UCHAMBUZI: Ikulu kujiingiza katika kesi ya Msigwa ni matokeo kukosa maarifa?

Kwa kifupi ikulu imejaa wapuuzi tu na uthibitisho ndo huo. Kuingia ikulu yeyote anaweza kuingia kama atasimamiwa na dola.
 
Kwa busara Mhe. Rais asingetakiwa kumtolea mfungwa faini. Pili isingekuwepo na Press Conference wakati wa kutoa zile fedha. Fedha zile zingetolewa kimya kimya bila mtu kufahamu. Naona kama imeleta sintofahamu kwa kiasi fulani.
 
Yaani Mimi ningekuwa Rais, ningefanya haya mawili:-
1. Fedha ya kumlipia Msigwa ningeituma kwa familia ya Binti Acqulina, kuwapa pole kwa yaliyotokea, na kulaani kabisa tukio lile baya lililoacha kovu na kumbukumbu mbaya katika nchi yetu.

2. Kutumia Mamlaka yangu kama Rais wa nchi, ningetoa msamaha kwa wanasiasa wote wa upinzani kwa hatia iliyowapeleka gerezani, bila ya kulipa fine yoyote, kusamehana yote yaliyopita, kufungua ukurasa mpya wa maandalizi ya uchaguzi ujao, uwe huru na wa Amani, upendo na Mshikamano.

Tujenge nchi, ugomvi na visasi vya kila mara visiwe na nafasi katika nchi yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
imedhibitika jiwe ni mshamba aki,hata kama aliombwa na ndugu kwa nini mpaka aite makamera na ikulu ikaweke kambi pale. si angewapa hao ndugu tu wakaenda kulipa?
 
imedhibitika jiwe ni mshamba aki,hata kama aliombwa na ndugu kwa nini mpaka aite makamera na ikulu ikaweke kambi pale. si angewapa hao ndugu tu wakaenda kulipa?
UMESEMA UKWELI.....HATUJAWAHI KUWA NA RAIS WA NAMNA HII KATIKA NCHI YETU. VERY PATHETIC.....KILA MAHALI ANADHARAULIKA. RWANDA TAYARI WAMESHAMFANYA LAUGHING STOCK.....KENYA NDIYO USISEME.....ZIMBABWE ETC KILA MAHALI ANACHEKWA.
 
Mtazamo wako

Unaweza kuwa wa kisomi sana

Ila alichofanya JPM amekuwa man of the match kwa raia wengi sana
NDUGU KWANI LAZIMA KILA UZI UCHANGIE ??? MENGINE YAKUPITE UKIYAJIBU UNAKUWA UNAJIDHALILISHA BILA KUJUA. MAJIBU YAKO YAMETAFSIRI MENGI KUKUHUSU POLE SANA.
 
Kama ni mtu alimshauri afanye uamuzi aliofanya basi namshauri rais wangu asikae apokee tena ushauri kutoka kwa huyo mtu.

Eti man of the match kwa raia wengi,wapi hao? Labda kama unatania au unafanya kejeli.
​
Nimeamini kwanini mwanzoni rais hakuhitaji washauro
 
Kwa mambumbumbu kama wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app

Naona kwa akili zako umehamishia vita kwangu

Haujaeleww kabisa post yangu

Nakubaliana kabisa kuwa anything that has been done na JPM kinaweza kisiwe acceptable kwako!?

Kwenye context ya kisiasa HAO UNAOITA MBUMBUMBU ndio wako wengi sana na ndio wanaotoa maisha

Jpm hajafanya kila mtu akubali!! Ila watakaokubali na kushabikia positively ni wengi

Sasa kwa akili yako, mimi kuweka huo ukweli umeniona mbumbumbu na sio analyst, haina shida pia😂😂
 
Ya akina Ngoswe tuwaachie akina Ngoswe, nani alijua akina Msigwa wameoa mtoto wa kumzaa Meko? Siasa inawafanya wakaziane mishipa ya shingo lakini wakifika nyumbani wanashikana mikono. Leo ndio nimegundua kwa nini Meko alihudhuria msiba wa Dada wa Msigwa na kutoa fuko lile la pesa.
 
Hoja Nzito kabisa zafaa kujibiwa na Msingwa wa Ikulu tu.
 
Una jua, hata ilipo fika Yesu ana karibia kusulibiwa aliwaambia wanafunzi wake kwamba mmoja wao atamsaliti, lakini wote walikana. Na pesa Yuda akapokea. Ila baadae Yuda alijuta kwa lile tendo
Kwa viongozi wa Chadema Ccm na serikali yake inaujua ukweli wa hii kesi kwamba ni ya kuhushi sasa huruma za wananchi zina wasuta. Yana kuwa yale ya Yuda. Ila bado sisi tuta wapaka mafuta Chadema ili andiko litimie..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa ndedere walishadlfeli tangu 2015 hawawezi kufanya siasa tena wapinzani wanapambana na dola
 
Kama ni mtu alimshauri afanye uamuzi aliofanya basi namshauri rais wangu asikae apokee tena ushauri kutoka kwa huyo mtu.

Eti man of the match kwa raia wengi,wapi hao? Labda kama unatania au unafanya kejeli.
​
Hahahaa jamaa anajipa matumaini maana aibu hio yataka moyo kuihimili.
 
Mtazamo wako

Unaweza kuwa wa kisomi sana

Ila alichofanya JPM amekuwa man of the match kwa raia wengi sana
Labda amekuwa man of the match kwako..

Ilishawahi semwa kuwa MKUBWA WETU NI BINGWA WA KUTENGENEZA ISHU THEN ANARUDI KWA MLANGO MWINGINE KUJA KUTATUA ISHU ALIYOITENGENEZA NA AKAONEKANA KAMA MKOMBOZI... "YESU" wetu
 
Ulipotaja .... nanukuu.... mwendo huu wa kushabikia matukio kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ni kujifurahisha tu kupunguza shinikizo la damu... mwisho wa kunukuu... NILIDHANI WEWE UNGETUMIA NJIA NYINGINE KUYASEMA HAYA... |Kumbe na wewe walewale tu... Nyani haoni..............................
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…