share
JF-Expert Member
- Nov 22, 2008
- 6,063
- 10,479
Kila mtu ameshangazwa na kilichofanywa na utawala wa Magufuli (Magufuli adminstration) ya kukimbilia kulipa faini isiyowahusu!
Michango ya kumtoa Msigwa ilishatosha na leo ilikuwa wawalipie wafungwa watatu wa CHADEMA, sasa kwa mshangao wa kila mtu, anatokea mtu mmoja anawa-overtake wahusika kwenda kutoa mchango usio wahusu...
Hiyo ni tabia ya kijinga na isiyo na mantiki yoyote inayoendelea kuwashangaza wahusika wenyewe (CHADEMA), Mhusika mkuu (Mbunge Msigwa-Mfungwa), wananchi wote wenye akili timamu na hata wengine waliotumwa kupeleka hiyo faini.
Kwa utaratibu unaofahamika, kama kuna mtu yeyote ameguswa na hayo yanayoendelea angepeleka mchango wake kwenye kamati zinazohusika...
Kama hapendi kutajwa basi angeomba awe " Anonymous" yaani asitajwe wakati anawasilisha michango au mchango wake lakini kilichotokea ni "real a laughing stock" asiyehusika anajua hahusiki na anajua wapi mahali pa kupeleka michango au angalau basi kuwahusisha wahusika au kuwapa taarifa lakini badala yake wanakimbilia huko jela kumtoa mfungwa ambaye pesa zake wahusika wameshalipia, isitoshe wanakwenda na utitiri wa waandishi wa habari(press) na maandamano ya magari mengi"(???)
Labda wanaweza kutueleza nia yao ni nini? Kama kweli walikuwa na nia ya kumtoa huyo mfungwa (Msigwa) kwani lazima waite waandishi wa habari? Je ilikuwa lazima mkurugenzi wa Ikulu asimame mbele ya Camera kuonyesha risiti za malipo ya faini? Inasaidia nini? Je kulikuwa na ugumu gani wa kuwasiliana na viongozi wa CHADEMA kuwaeleza kuwa wasihangaike na faini ya Msigwa kwa sababu tayari ipo kuliko kuwasumbua kwenda kupeleka faini na siku hiyo hiyo mnapeleka na ninyi? Hapo kuna shida tena siyo ndogo! Huyu Polepole anakimbizana na ujinga, ni hopeless na kama yeye ni architecture wa haya mambo basi ana shida kubwa ya ufikiri.
Kama kuna lilifichika basi litaonekana......Hadi sasa nia yao ni PUBLICITY STUNT labda kuna mengine zaidi, Time will tell. Hivi hii aibu ya kumlazimisha mfungwa apande migari yenu halafu akawakatalia mtaipeleka wapi?
AIBU aibu, Rais wa wanyonge anayemlipia mfungwa mmoja kutoka jela, vipi wale wananchi wake wengine? Au hawastahili....kwa sababu hawana ndugu aliye rais. Some people need to grow up
Umesema vizuri mno. Some people need to grow up. Hiki ni kituko cha karne.