figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 28,132
- 64,416
Dar es Salaam.
Taarifa waqliyoitoa Chama cha ACT-Wazalendo walipokuwa wanaongea na Waandishi wa habari. kuwa litafungua mashauri mahakamani kupinga baadhi ya vifungu vya Sheria ya Fedha ya Mwaka 2026 limefungua mjadala mpya kuhusu nafasi ya siasa za upinzani katika usimamizi wa fedha za Umma na utawala wa sheria.
Luhaga Mpina, ambaye sasa ni Naibu Waziri Mkuu katika Baraza Kivuli la ACT-Wazalendo, ambaye ameibua hoja kadhaa akidai kuwa baadhi ya vifungu vya sheria hiyo vinakiuka Katiba, vinahalalisha matumizi yasiyo ya uwazi ya fedha za umma na vinaongeza mzigo kwa wananchi. Huku akiangazia hujuma katika uagizaji wa Mafuta.
Kwa mtazamo wa haraka, inaweza kuonekana kuwa hatua ya kwenda mahakamani ni mwelekeo mpya baada ya Mpina kuhamia ACT-Wazalendo. Hata hivyo, uchambuzi wa kauli zake za nyuma unaonyesha kuwa hoja zake nyingi zinafanana na zile alizokuwa akizitoa alipokuwa mbunge kupitia CCM.
Pia soma: Serikali kuilipa Symbion Tsh Billion 356 | JamiiForums Tanzania Serikali kuilipa Symbion Tsh Billion 356
Mwaka 2022, wakati wa mjadala wa makadirio ya bajeti bungeni, Mpina aliibua hoja kuhusu malipo ya zaidi ya Sh356 bilioni yaliyokuwa yakidaiwa kulipwa kwa Kampuni ya Symbion. Alitaka malipo hayo yasifanyike mpaka uchunguzi wa kina ufanyike na Bunge lipate maelezo ya kutosha kuhusu mkataba huo, hatua zilizochukuliwa dhidi ya waliohusika na kiwango cha kodi ambacho kampuni hiyo ilikuwa imelipa au kudaiwa.
Katika mchango wake, alisisitiza kuwa fedha za umma hazipaswi kutolewa bila uwazi na kwamba mikataba yenye dosari inapaswa kuchunguzwa na, inapobidi, kufutwa. Aidha, alihoji kwa nini taasisi zinazosimamia ushindani na masoko hazikuwa zikichukua hatua dhidi ya vitendo alivyodai vilichangia kupanda holela kwa bei za bidhaa.
Pia soma: Maswali magumu ya Luhaga Mpina bungeni kuhusu Symbion kulipwa Bilioni 350 huku wananchi wakibaki na umasikini | JamiiForums Tanzania Maswali magumu ya Luhaga Mpina bungeni kuhusu Symbion kulipwa Bilioni 350 huku wananchi wakibaki na umasikini
Miaka minne baadaye, akiwa Naibu Waziri Mkuu katika Baraza Kivuli la ACT-Wazalendo, Mpina amerudi na hoja zinazobeba maudhui yanayofanana. Safari hii, badala ya kuzungumzia mkataba mmoja, analenga Sheria ya Fedha ya Mwaka 2026. Anasema baadhi ya vifungu vya sheria hiyo vinakiuka Katiba, vinahalalisha misamaha ya kodi isiyo na uwazi, vinawezesha matumizi yasiyo halali ya fedha za mifuko maalumu na vinaongeza mzigo wa kodi kwa wananchi.
Pia soma: Mpina: ACT Wazalendo tunaenda mahakamani kupinga Sheria ya Fedha 2026 | JamiiForums Tanzania Mpina: ACT Wazalendo tunaenda mahakamani kupinga Sheria ya Fedha 2026
Kwa mujibu wa msimamo wa ACT-Wazalendo, chama hicho kinatarajia kufungua mashauri mahakamani kikitaka vifungu vinavyopingwa vifutwe pamoja na kudai fedha zilizotumika au kuchukuliwa kinyume cha sheria zirejeshwe.
Licha ya msimamo huo mkali, chama hicho pia kimetambua maeneo ambayo Serikali ilifanya marekebisho kufuatia maoni yaliyotolewa bungeni. Miongoni mwa maeneo hayo ni kuondolewa kwa baadhi ya tozo zilizokuwa zimependekezwa kwenye muswada wa awali, jambo ambalo ACT-Wazalendo limesema ni hatua chanya.
Katika muswada, Serikali ilianzisha tozo ya Sh10 kwa kila kilogramu ya sukari ya ndani na ya nje kwa ajili ya kugharamia Mfuko wa Bima ya Afya. Tulitoa maoni Serikali iondoe na Serikali imefanya marekebisho kwa kuondoa tozo hiyo, badala yake imeweka tozo ya Sh20 kwa sukari inayoingizwa nchini, tunakubaliana,” allisema Luhaga Mpina.
Mpina alisema ACT- Wazalendo itaendelea kutumia njia zote halali za kikatiba na kisheria kuhakikisha fedha za wananchi zinalindwa, sheria zinaheshimiwa na Serikali inawajibika kwa kila uamuzi unaogusa maisha ya Watanzania.
“Msimamo wa Chama cha ACT -Wazalendo ni kwamba, vifungu vya 10, 22, 83 na 94 vya muswada vifutwe ili kuliwezesha Taifa kunufaika na rasilimali zake na kuondoa utoaji holela wa misamaha ya kodi unaopoteza mapato mengi ya Serikali.”
Hoja za sekta ya mafuta na madai ya ruzuku
Mbali na Sheria ya Fedha, Mpina amekuwa akielekeza macho yake katika sekta ya mafuta, akidai kuwepo kwa tofauti kati ya bei za mafuta katika soko la dunia na bei za ndani nchini.
Amesema bei ya mafuta ghafi ilishuka kutoka Dola za Marekani 112.9 kwa pipa hadi Dola 87.3, sawa na takribani asilimia 22, lakini akahoji kwa nini wananchi hawakushuhudia punguzo la kiwango hicho katika bei za rejareja.
Aidha, Mpina amedai kuwa Serikali ilitangaza kutoa ruzuku ya Sh259 kwa lita mwezi Mei 2026 na Sh535 kwa lita mwezi Juni 2026 ili kupunguza bei ya mafuta, lakini akahoji kutokuwepo kwa tangazo rasmi la Serikali (GN) na akasema bei hazikushuka kama ilivyotarajiwa.
Historia ya hoja zake kuhusu sekta ya mafuta
Msimamo wa Mpina kuhusu usimamizi wa sekta ya mafuta ulianza kujitokeza mapema zaidi. Mwaka 2022, akiwa Mbunge wa Kisesa kupitia CCM, alimkosoa aliyekuwa Waziri wa Nishati, , akidai kuwa hatua zilizochukuliwa katika usimamizi wa bei za mafuta na baadhi ya tozo hazikufuata taratibu za kisheria na zilisababisha Serikali kupoteza mapato.
Pia Waweza kusoma: Luhaga Mpina amlipua Waziri Makamba, amtuhumu kwa Uhujumu Uchumi. Atoa wito kwa TAKUKURU kumchukulia hatua
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mpina alidai kuwa uamuzi wa kuondoa tozo ya Sh100 kwa lita ya mafuta bila kufuata utaratibu uliowekwa kisheria ulisababisha Serikali kupoteza takribani Sh30 bilioni ambazo zilikuwa zimeidhinishwa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22. Kutokana na madai hayo, alitoa wito kwa kufanya uchunguzi na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria.
Aidha, alimkosoa Waziri huyo kwa kile alichodai kuwa hakutoa majibu ya kina kuhusu sababu za kupanda kwa bei za mafuta na athari zake kwa mfumuko wa bei nchini.
Kauli hizo zimekuwa sehemu ya mjadala mpana kuhusu uwazi wa mifumo ya bei na matumizi ya fedha za umma katika sekta ya nishati.
Pia soma:
Thread 'Mpina aibua Kashfa ya MAFUTA dhidi ya TPDC na VITOL' Mpina aibua Kashfa ya MAFUTA dhidi ya TPDC na VITOL
Hoja za Mpina Mwaka 2022 alitaka uchunguzi kabla ya fedha za umma kutumika. Mwaka 2026 anataka mahakama ipime uhalali wa vifungu vya sheria vinavyosimamia ukusanyaji na matumizi ya fedha hizo.
Wachambuzi wa siasa wanaweza kutafsiri hali hii kwa namna mbili. Upande mmoja unaweza kuona kuwa Mpina ameendelea na msimamo wake wa muda mrefu wa kutetea uwajibikaji wa Serikali bila kujali chama alichopo. Upande mwingine unaweza kuona kuwa nafasi yake mpya ndani ya upinzani imempa uhuru mkubwa wa kutumia hatua za kisheria ambazo asingezichukua alipokuwa ndani ya chama tawala.
Endapo ACT-Wazalendo itafungua rasmi shauri mahakamani, hoja zitakazowasilishwa na uamuzi wa mahakama vitatoa picha pana zaidi kuhusu nguvu ya madai hayo na athari zake kwa utungaji wa Sheria ya Fedha katika miaka ijayo.
Nampongeza sana Mpina kwa kutokuteteleka katika kutetea wananchi bila kujali vitisho vilivyopo.
Pia soma: Mpina acharuka bungeni | Mwananchi https://share.google/tjvbE3ncf8tp0ikZy
Nini maoni yako?