Uchambuzi: Kwanini Rais Samia hakukataa kusalimiana na Mange

mange alimtukana hayati makufuli ndio maana mama samia hakukataa kumsalimia mange kwani mpaka sasa mwigulu na wengine katika serikali ya awamu sita inamsema vibaya hayati makufuli lakini rais hasemi lolote. sasa mseme yeye uone
 
Kama ukiangalia tukio zima kwa umakini utagundua ile picha imepigwa kuwaridhisha ndugu watazamaji, kila mmoja kati ya rais na mange walikuwa eitha wanaogopana au manhe alikuwa anafeel gilty wakati SSH alikuwa na kinyongo ilikuwa ni picha ya kulazimisha huku mjini wanasema ni picha ya kijino pembe.
 
Nimekomea point namba 3 tu huna maana hujui unachokiandika

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Rais hajainyesha picha nzuri kukaribiana na huyo mwanamke asiye na staha mange inajenga picha mbaya Sana
Yaani raha sana, unatukana uwezavyo mpaka unagaragara, alafu akija kiongozi mwingine unasogea kwake kwa kujipendekeza na kujionyesha mwema.

Wanadamu a.k.a watanzania tunakutetea na kusema "aombaye upewa na abishae ufunguliwa" yaani waafrika hasa watanzania ukiwafahamu hawakupi shida.

👉🏾 Naendelea kujifunza tabia ya Mtanzania.
 
Mda wa visasi na kufukua makaburi viliishia Chato
 
...Kweli. Hata 'Body Language' zao zilikuwa zipo zipo tu....!
 
Umeongea vizur Ila Kuna sehemu umevuruga na kujivuruga.

Maswali haya ukinijibu nitaweza kuamin ulicho andika kwa 100%

1.Kwanza una ushahidi au uhakika gan kwamba mangi kaomba msamahaa na kujirudi?

Pili, kwann useme mangi anajutia makosa, Kwan amekwambia yeye anafl Gilt? Kwann umuite mwana mpotevu?

Tatu, kwann usifikirie uenda Samia nae alitaka kumwambia mwanangu isamehee serikali yako usiishambulie Tena tumejirekebisha?

Nne, kile kitambaa Cha kijan Kama bango flan hv, alichokuwa ameshika Mangi mala gafra kikarudishwa nyuma, kilikuwa na ujumbe gan
 
Mange anatakiwa abadilike,,unaweza fikili uyu siyo muisilamu na minguo yake ya ajabu ajabu.

Kuhusu mama kusalimiana na mange sioni kama ni tatizo mzehe. Kwaiyo ugomvi wake na magufuli mama unamuhusu nini!!!! mlitaka asipokee salamuyake!!!! Uisilamu hauko hivyo mzehe.


Narudia tena ,,,wewe dada kimambi acha umagharibi na kuiga tamaduni zao za kipumbafu,,jiheshimu, vaanguo zinazoendana na imani yako. Siku ukichomoka hawataweza kukusaidia hao, wewe na matendo yako ndiyoo yatakusaidiya dadaa.
 
Naona CCM wanatafuta mada mbadala. Tafuteni wajinga mje kujadili nao huu upuuzi. Ila mada na ajenda muhimu bado zitabaki pale pale
 
Wengi tunakumbuka hekaheka za Mange Kimambi dhidi ya Hayati Rais John Joseph Pombe Magufuli jinsi alivyokutana na matusi, kejeli na dhihaki mbaya kutoka kwa Mange Kimambi ambaye ana wafuasi wake wanaomtumia taarifa. Magufuli alipigwa mtungo wa matusi kutoka kwenye combination ya Mange Kimambi aliyejikita Instagram na Kigogo 2014 aliyejikita Twitter.

Combinenga hii ya Mange Kimambi na Kigogo 2014 iliweza kumtikisa Magufuli lakini bado Magufuli aliweza kusimama thabiti kama Chuma au Jiwe, licha ya kipindi chake cha urais kukumbwa na jangwa kubwa la dunia la COVID19, na Magufuli alisimama imara dhidi ya ugonjwa huo na kukataa Nchi isiingie Karantini (kufunga mipaka ya nchi na Raia kukaa ndani ya nyumba tu), jambo hili na msimamo huu wa Magufuli haukutegemewa na Mataifa mengi na mashirika ya afya kwa sababu kwa kipindi icho Nchi nyingi zilikuwa zimeshajikita kukaa Karantini na raia kujifungia ndani. Mange Kimambi na Kigogo 2014 wakatumia huo ugomjwa na maamuzi yake kama mwanya wa kuchonganisha serikali ya Magufuli na pamoja mashirika ya afya duniani. Jambo lililopelekea nchi nyingi kutaka kujua kwa nini Tanzania haijaingia karantini. Chama pinzani cha kisiasa cha Chadema nao hawakua nyuma, walifanya juu chini kuutikisa utawala wa Magufuli ikiwemo kumtumia Mwanasiasa Antipas Lissu kueneza habari mbaya za serikali ya Tanzania na jinsi inavyopambana na COVID19. Ulitengenezwa uadui mkubwa kwa John Pombe Magufuli, akipigwa mtungo wa matusi na kejeli za mitandaoni kutoka kwa Mange Kimambi, Kigogo 2014 na Antipas Lissu. Lakini Mwamba Magufuli akasimama thabiti kama mwanaume na kuiongoza nchi vyema, akafanikiwa kutawala tena hawamu ya pili mpaka siku umauti uliomchukua kutokana na changamoto ya kiafya aliyokuwa nayo toka ujana. Baada ya umauti kumkuta baadhi ya watu walisherehekea umauti wake, huku raia wengi wakihudhunika kwa kumpoteza shujaa aliyebadilisha hali ya maisha ya watanzania wengi.

Baada ya Rais Samia kuchukua madaraka kwa kurithi kiti cha urais kutoka kuwa makamu wa urais, watu wengi walifurahia sana, kwanza kuwa rais wa kwanza wa mwanamke, na mambo kaza wa kaza. Kiongozi huyu aliingia na kufanya mabadiliko ya baadhi ya viongozi ambao wengi waliitwa kama Sukuma gang au wafuasi wa Magufuli, na akawateua na kuwarudisha viongozi ambao walienguliwa na Rais Magufuli. Watu wakaanza kusema anaondoa mambo ya Magufuli na kurudisha ya Kikwete, wengine wakisema anaendeleza ya Magufuli. Kwa ufupi wale wote waliokuwa wanamdhihaki na kumtusi Magufuli walianza kumsifia Rais samia. Kina Mange Kimambi, Kigogo 2014, na Lissu wote walionekana kumsifia Rais Samia, japo muda mwingine walionekana kumchafua.

Hali imeanza kubadilika sasa baada ya Mange Kimambi kuanza kurudisha mashambulizi ya matusi ya kipindi kile cha Magufuli na kuanza kumtusi Rais Samia. Matusi ambayo ni makubwa sana na hayapaswi hata kuandikwa hapa.

Kiongozi wa chama kikuu serikalini cha CCM Paul Makonda ambaye amehudumu nafasi mbalimbali serikalini hivi karibuni amekuja na kudai kuwa baadhi ya viongozi na mawaziri wanawalipa watu mitandaoni hili waweze kumtukana Rais Samia, na kwa asilimia kubwa anawafahamu majina na wakiendelea atampatia Rais hayo majina. Paul Makonda aliyasema hayo baada ya kukithiri matusi ya mitandaoni kutoka kwa Mange Kimambi yanayorushwa kwenda kwa Rais Samia. Inasemekana, kwa mujibu wa kauli ya Paul Makonda, Mange Kimambi analipwa na baadhi ya viongozi na mawaziri kumtukana Rais.

Hii shida iliwahi kumkuta Magufuli na Sasa Rais Samia.
 

From the outside looking in, things appeared to be hunky-dory.

The outlook was rosy.

Smiling faces everywhere. Photo ops and all that jazz.

But now it’s back to ‘square one’.

Insults everywhere. Accusations galore!

So what happened?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…