mrxtz2026
JF-Expert Member
- Jan 24, 2026
- 609
- 1,314
Uzi huu unaendelea na uchambuzi wa Final Submission katika Kesi ya Uhaini inayomkabili Tundu Antipas Lissu.
Katika sehemu ya kwanza, nilichambua hoja zilizotolewa na Tundu Lissu katika utetezi wake mwenyewe. [ Gusa maandiahi haya kwa kusoma Bandiko hilo ]
Sasa, baada ya upande wa Jamhuri kupitia Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga, kuwasilisha majumuisho yake, ni muhimu kuirudia kesi hii kwa kuziweka hoja za pande zote mbili mezani.
Lengo hapa si kumtetea Lissu wala kuunga mkono Jamhuri. Lengo ni kuchambua hoja, ushahidi na sheria kama zilivyo.
Kwa hiyo katika kila kipengele tutafanya mambo manne:
1. Hoja ya Lissu
2. Hoja ya Jamhuri/Katuga
3. Maneno muhimu yaliyosemwa na kila upande
4. Uchambuzi wa Kisheria na Kiushahidi na mwisho wa kila kipengele tutaacha swali ambalo, kwa mtazamo wa kisheria, linahitaji kujibiwa na Mahakama.
Kesi hii si suala la nani ametoa submission yenye maneno mazito zaidi, Swali kubwa ni moja:
Je, baada ya kuangalia sheria, charge, ushahidi wa pande zote na authorities zilizotajwa, kila element ya kosa linalodaiwa chini ya Kifungu cha 39(2)(d) imeoneshwa na kuthibitishwa kwa kiwango kinachotakiwa katika kesi ya jinai?
Take a note Mapema Kwamba Kwenye uzi huu Ukweli wa kisheria utasemwa hata Pale unapokuwa upande usiotarajiwa au Usiokupendeza.
Take a note Mapema Kwamba uzi huu ni mlefu Sana japokuwa si mlefu kupitiliza lakini Umesema Kila kitu kilichopaswa kusema kwenye Final Submission Tunayotaka kuichambua na Kutoa Tathimini, Kwaiyo Kama utasoma Uzi wote Basi Utakuwa umepata Kila kitu Kuhusu Kesi ya Uhaini inayomkabili Ndugu Tundu Antipus Lissu na utauelewa Kesi hiyo From A to Z.
━━━━━━━━━━━━━━━━━━
1. KIFUNGU CHA 39(2)(d) CHA PENAL CODE: KINASEMA NINI HASA NA MAHAKAMA INAPASWA KUTHIBITISHA NINI?
Kabla ya kuingia kwenye mabishano ya “public”, “deed”, “publication”, “overt act” au maneno yaliyosemwa, tunahitaji kuanzia kwenye sheria yenyewe.
Kifungu cha 39(2)(d) Cha Penal code kinahusu mtu aliye chini ya allegiance kwa Jamhuri anayefanya nia ya ku-effect, kusababisha ku-effect, au ku-instigate, persuade, counsel au advise mtu au kundi la watu kufanya au kusababisha intimidation of the Executive, Legislature or Judiciary, na kisha kudhihirisha nia hiyo kwa publication, overt act au deed.
Kifungu cha 39(2)(d) Cha Penal code Kinatamka Hivi:
39(2) Any person who, being under allegiance to the United Republic, in the United Republic or elsewhere, forms an intention to effect or to cause to be effected, or forms an intention to instigate, persuade, counsel or advise any person or group of person to effect or to cause to be effected, any of the following acts, deeds or purposes, that is to say–
(a) ...............
(b) ...............
(c) ................
(d) the intimidation of the Executive, the Legislature or the Judiciary of the United Republic, and manifests such intention by publishing any writing or printing or by any overt act or deed whatsoever shall be guilty of treason and shall be liable on conviction to be sentenced to death.
Kwenye Kifungu hicho cha 39(2) cha Kanuni ya Adhabu "Penal code " LISSU amefunguliwa Kesi ya Uhaini Chini ya Aya ya (d) Pekee na si Aya ya (a), (b) wala (c).
Kwa kuanza ilikuwa kama ifuatavyo:
HOJA YA LISSU
Hoja ya msingi ya Lissu ni kwamba Jamhuri haiwezi kuishia kuthibitisha kwamba alisema maneno fulani, Bali inapaswa Kuthibitisha wazi Kitendo kinachotakiwa na Kifungu cha 39(2)(d), Yaani Je, Maneno hayo yanatimiza elements zinazotakiwa na s.39(2)(d).?
Kwa lugha rahisi:
Maneno → Maana → Nia → Lengo → Manifestation → Kitendo kinachotakiwa na sheria → Proof beyond reasonable doubt.
Lissu Alisema maneno haya kwenye Final Submission:
Waheshimiwa Majaji katika kesi ya kwanza nilisomewa shitaka la Uhaini kinyume na kifungu cha 39(2)(d) cha Penal Code.
Katika kesi ya pili nilisomewa shitaka la kutoa taarifa za uongo kinyume na kifungu cha 16 cha Sheria ya makosa ya Mtandao. .........
.........
......... Waheshimiwa kifungu kinasema mtu yeyote mwenye utii kwa Jamhuri na akatengeneza nia ya kuwezesha au kusababisha kuwezeshwa au anayetengeneza nia ya kuchochea, kushawishi au kushauri mtu yeyote au kikundi cha watu to effect kimoja wapo kati ya matendo yafuatayo yaani;-
......... What are the essential elements of the offence of treason under that provision of the law.
Jambo la Kwanza ni utiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaani allegiance to the URT.
Jambo la pili ni kwamba kosa lilifanyika ndani ya nchi au kokote kule.
Jambo la Tatu ni kutengenezwa kwa nia ya kutenda kosa la Uhaini haiwezi kuwa nia ya kufanya kitu kingine. The formation of the intention to commit treasonous act.
Na kama ni ya kuchochea lazima huo uchochezi uwe ni wa kufanya kosa la uhaini na sio kuchochea watu kufanya wizi.
Jambo la nne, kama ni kosa la kuchochea basi awe ni mtu mmoja au kikundi cha watu. The target of instigation must be any person or a group of person na sio umma. Ni kikundi cha watu.
Sharti la tano ni kwamba hiyo nia ya kutenda kosa au kushawishi watu ni lazima idhirishwe kwa kuchapisha maandishi au machapisho of any writing or printing or by overt act or deed whatsoever.
Waheshimiwa Majaji sharti la 6 halipo katika kifungu cha 39(2) d bali lipo katika kifungu cha 10(2) kwamba hilo sharti lazima matokeo ya yaliyotakiwa kutokea kwenye hiyo nia ni lazima kuwe na malengo yaliyotakiwa kutokea kutonana na hiyo nia.
Kama sheria imetamka wazi wazi kuwa kosa fulani lazima lioneshe nia basi matokeo ya hiyo nia lazima yaonekane maana yake kama nia ni kuchochea kutengeneza kosa la uhaini lazima matokeo ya hiyo nia yaonekane na kifungu cha 39 kimesema habari ya nia.
Kama nia ilikuwa ni ya kufanya kosa na kosa hakuna maana yake hakuna kosa na nia inakuwa imekufa ndio maana yake.
Hili ambalo nimelisema sasa hivi halikuzungumzwa kabisa kwenye kesi ya Grey Likungu na Khatibu Gandi. Mahakama zote mbili were not drawn on the implication of the current provision of the law ndo maana nilisema mnaenda kuweka precedent ya sheria.
Na vilevile mtaona kwamba the attention of the court in those case were not drawn on the issue of instigation.
Mahakama hii ina hiyo fursa ya kujadili hili na kulitolea mwongozo kwa vyovyote vile Waheshimiwa Majaji you are decision will be developing the law na baada ya kivumbi kutulia tutapata sheria mpya.
Uzito wa innocence sio ya mtu mmoja tu bali ni Precedent.
Waheshimiwa Majaji baada ya kuwa nimeweka hizo parameters za hicho kifungu cha Sheria naomba nipendekeze kwenye masuala ambayo mnatakiwa kuyatolea uamuzi.
*****************************
HOJA YA KATUGA
Katuga anaanzia sehemu hiyo hiyo lakini anasema Jamhuri imevithibitisha elements vinavyotakiwa.
Anategemea s.3(2) ya Evidence Act kuhusu burden ya prosecution na anasema ushahidi wa Jamhuri umefikia kiwango cha beyond reasonable doubt.
Katuga alisisitiza kwamba Jamhuri ndiyo yenye jukumu la kuthibitisha, lakini akasema jukumu hilo limetimizwa.
*****************
Jamhuri/Katuga Alisema maneno haya kwenye Final Submission:
....... Waheshimiwa Majaji, mshtakiwa ameshtakiwa kwa kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, Urekebu wa Mwaka 2022.
Ambapo, Waheshimiwa Majaji, kuhusiana na taarifa ya shitaka hili, inaelezwa kwamba tarehe 23 Aprili 2025, ndani ya Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa chini ya utii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alitengeneza nia ya kuchochea umma kuweza kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, kwa nia ya kuitisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (for the purpose of intimidating the Executive), kwa kudhihirisha nia hiyo kwa kutoa maneno yafuatayo:
‘Wanasema kitu kimoja sahihi hapa, wanasema hivi: Msimamo huu unaashiria uasi, ni kweli, ni kweli kwa sababu tutazuia uchaguzi, hiyo ndiyo namna ya kupata mabadiliko. Kwa hiyo tunaenda kukinukisha, huu uchaguzi tutauvuruga, tutauvuruga kwa sababu tunaenda kukinukisha vibaya sana.’ .......
.......
....... Waheshimiwa Majaji, kifungu ambacho nimekirejea cha 39(2), upande wa Jamhuri tulikifanyia research kama Mahakama ilishawahi kuki-test.
Tafiti zilionyesha kwamba Mahakama zetu katika mashauri ya uhaini ni mashauri ambayo yalishitakiwa chini ya kifungu cha 39(a). ......
....... Waheshimiwa Majaji, kwa kuwa tumejiridhisha kwamba haijawahi kutumika katika Mahakama zetu, tuweze sasa kutafsiri hati ya mashitaka pamoja na kifungu kilichotumika cha 39.
Ili kuweza kuona ni vitu gani Mahakama yenu Tukufu ilianza kuangalia ushahidi, basi ni kitu gani upande wa Jamhuri ulipaswa kuthibitisha. ........
....... Kwa mujibu wa kifungu cha 135 cha CPA, Sura ya 20, Urekebu wa Mwaka 2023, kinaelezea kwamba mashitaka lazima yawe na maelezo ya kosa la shitaka husika pamoja na maelezo ya shitaka.
Ambayo sheria inasema hayo maelezo lazima yatie information ya jinsi shitaka lilivyofanyika.
Lakini kifungu cha 138(a)(iii) kinaelekeza kwamba technical terms hazitakiwi kutumika. .......
........ Waheshimiwa Majaji, tumetumia neno ‘to instigate the public’ kuendana na kifungu cha 135, kufanya hati ya mashitaka kueleweka kuendana na ushahidi wa upande wa Jamhuri ulioutoa.
Waheshimiwa Majaji, kama tulivyoeleza awali, kifungu cha 135 kinataka maelezo ya kosa yaeleweke katika kiwango ambacho mshtakiwa aweze kujitetea na in conformity na ushahidi uliotolewa.
Waheshimiwa Majaji, neno ‘any person’ linafanana na neno ‘public’.
Waheshimiwa, ‘any person’ na ‘a group of people’ yamekuwa included kwenye ‘public’.
Yametafsiriwa katika kifungu cha 5 cha Kanuni ya Adhabu, Waheshimiwa.
Siyo tu akimaanisha watu wote wa Tanzania Bara, lakini hata yule mkazi au anayetumia eneo fulani na any number of those people.
******************************
UCHAMBUZI
Sheria inatoa offence Kisha Jamhuri ina burden. Defence inaweza kupinga interpretation na ushahidi lakini Kwenye hili Mahakama ndiyo inapaswa kuunganisha kila elements na ushahidi wake.
Lissu alipinga Mwanzo kabisa kuwa amefunguliwa Kesi zote mbili Kinyume na Sheria Husika na kwamba Hati ya mashtaka haikumpa yeye kama accused Taarifa za kutosha Kuhusu natural of Offense, Yaani Hati ya mashtaka ilipaswa kusema wazi kwamba Tunakopa Tafsiri ya Neno Fulani kutoka kwenye Kifungu kingine licha ya kwamba unafunguliwa Kesi Chini ya Kifungu kingine.
Katuga alitetea hoja hii na kusema kwamba Kwa mujibu wa Kifungu cha 138(a)(iii) cha CPA Hili kufanya hati ya mashitaka kueleweka kuendana na ushahidi wa upande wa Jamhuri ulioutoa walilazimika kutumia Neno "Public" badala ya Maneno yaliyo kwenye Kifungu Husika ambacho Lissu amefunguliwa Kesi hiyo Chini ya Kifungu hicho.
Uchambuzi wangu kwenye Hili ni kwamba Lissu alipinga moja kwa moja kutumika Kwa Neno "Public", lakini katuga akasema sababu za kutumia Neno "Public" kwenye Hati ya mashtaka badara ya kutumia maneno yaliyo kwenye Kifungu cha 39 (2)(d) cha Penal code Yaani maneno "Any Person or Group of People", ni kufanya Hati ya mashtaka ieleweke kutokana na Ushaidi wa mashtaka utakaotolewa lakini pia Katuga yeye Mwenyewe kwenye Kauli zake alijenga hoja yake hiyo kwa kutumia Kifungu cha 138(a)(iii) kinaelekeza kwamba technical terms hazitakiwi kutumika kama sio Lazima kutumika. ......
Tukiendelea na Uchambuzi wetu Hoja ya muhimu inajitokeza Kwenye Kifungu cha 39(2)(d) kinatumia maneno ‘any person or group of persons’, lakini Hati ya Mashtaka imetumia maneno ‘the public’. Swali ni Je, kama matumizi ya ‘the public’ ni namna tu ya kueleza kwa lugha rahisi, Kwani ‘any person or group of persons’ ni lugha ngumu kueleweka.?
Mimi Binafsi Katika upekuzi wangu wa Sheria nimerejea Kifungu kinachoweka Masharti ya kwamba Hati ya mashtaka iandikwe Kwa lugha Nyepesi yenye kueleweka lakini pia hasa katazo lilowekwa Kuhusu Technical Terms, Yaani 138(a)(iii) cha CPA na CPA yote Kwa Ujumla na kuona Je, Hoja hizi mbili hipi iliyokuwa na Nguvu Kisheria.? Na nimepata kwamba Jamhuri/Katuga alichokuwa Hatua ya kuweka Neno "Public" licha ya kwamba Kifungu cha 138(a)(iii) cha CPA kimekataza lakini hakusema kwenye Hati ya Mashtaka moja kwa moja kwamba Tumekopa technical term or Neno Hilo kutoka kwenye Kifungu kingine licha ya kwamba unafunguliwa Kesi Chini ya Kifungu kingine, Yaani Hapa Katuga alitumia Tafsiri ya Neno "Public" kutoka kwenye Sheria hiyo hiyo ya Penal code Kuanda hati ya Mashtaka, Tafsiri hiyo hipo Chini ya Kifungu cha 5 cha Penal code, kinachosema;
“public” refers not only to all persons within Mainland Tanzania but also to the persons inhabiting or using any particular place, or any number of those persons, and also to such indeterminate persons as may happen to be affected by the conduct in respect to which such expression is used.
Kwaiyo hoja ya Katuga hapa ni kwamba Neno "Public" maana yake ni kama Kifungu cha 5 cha Penal code kilicho toa Ufafanuzi au Tafsiri, Hivyo Basi hoja yake ya kusema "Any Person or Group of people" iliyo Chini ya Kifungu cha 39 (2)(d) ni Sawa na Kile kilichotamkwa kwenye Kifungu cha 5. Kwaiyo kutumia Neno "Public" alikuwa analenga " ..... any number of those persons". Kwa Maana hiyo "Group of people" ni Sawa Sawa na "any number of those persons", Hivyo Basi Katuga kutokea Hapo hakaona ni sahihi kutumia Neno "Public" kwenye Hati ya Mashtaka.
Kwenye hili Kama wewe sio Mtaalamu wa Sheria ukifikilia kiuwepesi unaweza kusema sahihi au si sahihi lakini Mimi Naona ni muhimu kuweka Uchambuzi wangu kidogo na kaswali haka kadogo. Je, Kifungu cha 5 cha Penal code kilichotoa Ufafanuzi au Tafsiri ya Neno Hilo kililenga Tafsiri ya Neno moja kwa moja au kililenga Tafsiri ya Neno Kinyume...?, Pia Je, Kifungu cha 5 kinahusu nini hasa, na lengo lake Kuu ni nini....?
Naomba nichambue maswali yangu niliyoyatoa Hapo juu, Niliposema Tafsiri ya Neno Kinyume Nina maana hii kwamba Kulitafsiri Neno mala mbili mbili, pia Niliposema Kifungu hicho kinahusu nini au kina lengo Gani Basi ni kama ifuatavyo Hapo Chini. Kwanza kabisa Kifungu cha 5 cha Penal code kipo Hivi:
Interpretation:
5. In this Code, unless the context requires otherwise
Katuga nakuita njoo Hapa nikufundishe Sheria Kidogo. Kifungu cha 5 kinahusu Interpretation Yaani Ufafanuzi au Tafsiri ya Maneno, hivyo Basi Kifungu cha 5 chenyewe kinasema Hivi "Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo.", Kifungu Hiki kinalenga Maana yake kwamba "Katika Ufafanuzi au Tafsiri ya Neno lolote litakalotumika kwenye Sheria yote Yaani penal code yote kuanzia Kifungu cha 8 Hadi cha Mwisho ambacho ni 390 ukikutana na Neno "Public", “harm”, “judicial proceeding”, “knowingly”, “night” or “nighttime" or Maneno mengine yeyote Basi rudi kwenye Kifungu hicho cha 5 hili kupata maana ya Neno Hilo", lakini wewe ulichokifanya ni kwamba ndani ya Kifungu cha 39(2)(d) Hakukuwa na Neno "Public" lilokufanya urudi kwenye Interpretation ya Penal code Nzima.
Naomba nifunge Uchambuzi wangu hapa kwamba Katiba na Sheria zina kitu kinaitwa Muongozo wa Jumla, na kitu kingine kinaitwa Ufafanuzi wa Kila Neno lililotumika ndani ya Katiba au Sheria hiyo. na pia Kifungu cha 5 cha Penal code sio Kifungu cha Mwanzo cha Kanuni ya Adhabu kinachotambua Kosa, Kifungu cha Mwanzo kabisa cha Makosa ni Kifungu cha 8 "Ignorance of the law" Yaani "kutokujua Sheria hakukufanya kutokuwa na Hatia".
Kifungu cha 1 Hadi cha 7 ni Vifungu vya ujumla, Yaani Kuhusu Penal code nzima, Ufafanuzi wa Maneno yaliyotumika ndani ya Penal code, Muongozo wa Kimahakama na Mengineyo.
Jamhuri inategemea tafsiri ya "public" iliyopo katika Kifungu cha 5 cha Penal Code. Lakini bado swali linabaki: je, tafsiri hiyo inaweza kutumika kuchukua nafasi ya maneno ‘any person or group of persons’ yaliyowekwa mahsusi na Kifungu cha 39(2)(d), bila kubadilisha maana au upeo wa kosa lenyewe?”
Kwa Maoni yangu kiukweli hapa Katuga Umejenga hoja kwenye Kifungu ambacho Kazi yake ni Interpretation ya Neno utakalolikuta kwenye Kifungu Husika unachotaka kukitumia, sio utumie Interpretation kuongeza Neno jipya wenye Kifungu unachotaka kukitumia. Lakini pia ulichofanya ni Double Interpretation Kwa hoja kwamba Kifungu cha 138(a)(iii) cha CPA kinakupa ruhusa Kuanda hati ya Mashtaka Kwa lugha Nyepesi, hoja hii Naweza Kuiwekea swali dogo Tu; Je, ulidhani Lissu ni Mtu asiejua Sheria Kwa kina Kiasi hatoweze kuelewa Kosa la Kifungu cha 39 (2)(d) cha Penal code, Hivyo umeweka Neno "Public" Hili imuwezeshe kuelewa shtaka.?
NOTE FOR KTG:
Nikirudi Mwanzo kabisa Lissu alibainisha wazi kwamba Hati ya Mashtaka imenyima Taarifa za kutosha Kumuwezesha kuelewa Natural of Offense, Yaani yeye kama Accused anapaswa kuelewa shtaka lake linalomkabili kikamilifu Hili Baadae ajue Namna ya kuja kujitetea kwenye utetezi wake", lakini pia Katuga Baada alitoa hoja zake nyingine kutetea kwamba "Natural ya Offense ilikamilika na kwamba sheria inatoa Njia nyingine kwenye Hilo", kama ifuatavyo:
Katuga:
........ Waheshimiwa Majaji, kama tulivyoeleza awali, kazi ya hati ya mashitaka ni kumu-inform Mshtakiwa.
Ni msimamo pamoja kwamba Mshtakiwa anaweza kuwa further informed kutokana na aina ya mashitaka yake kutokana na ushahidi utakaotolewa na upande wa Jamhuri.
Waheshimiwa, zipo kesi nyingi za kumfanya Mshtakiwa aelewe mashitaka yake.
Daniel Ruhele Vs Jamhuri, Criminal Appeal Number 201 of 2007, TanzLII, 1 March 2012, TZCA 269.
Fixed ( Naomba Tulekebishe Kuhusu marejeo haya ya Hukumu, Pengine ni Makosa ya Muandishi aliyekuwa Mahakamani Wakati Kesi ikiendelea, Marejeo ya Sahihi ya Hukumu iliyorejewa ni. "Damian Ruhele vs Republic (Criminal Appeal No. 501 of 2007) [2012] TZCA 269 (1 March 2012).")
Katika ukurasa wa 5, though katika kesi hii walikuwa wanaona element moja haijawa cured na ushahidi.
Mbali na mashauri mengi, lakini ni moja ya kesi inaonyesha hata kama hujawa informed na charge, lakini ushahidi unaweza kukufanya ujiandae na utetezi.
Mahakama yenu itaangalia nature ya ushahidi wa Prosecution na utetezi.
Je, wakati anajitetea alikuwa haelewi au alikuwa anaelewa anachojitetea? ........
******************************
OF KTG:
Hapa Katuga alitetea hoja hiyo kwamba Sio Lazima kuambiwa au kufahamu Kila kitu pia licha ya kwamba hata kama haujawa Informed na charge so enough lakini Ushaidi wa mashtaka unaweza kukufanya ujiandae na utetezi Wako Bila shida, pia Katuga katetea hoja yake hii Kwa kuweka Marejeo ya Kesi ya Damian Ruhele vs Republic Criminal Appeal No. 501 of 2007 [2012] TZCA 269 (1 March 2012). Na kuiambia Mahakama iangalie Katika ukurasa wa 5 Kuhusu "Without Informed Enough about your Charger can't Affect your Offense Anymore".
Mimi nikaona Hapana let's see it, na Katika kupekuwa pekuwa nikapata haya:
Kwenye Hukumu ya Kesi ya Damian Ruhele Vs Republic Court ilikubali “the charge did not disclose the elements of the offence.” kwasababu evidence ikaonyesha threat hiyo. Na hapo ndipo Court ikaona Threatening was an essential element.
Hapa naomba Kutoa Ufafanuzi kidogo kwanini Mahakama ilitoa uhamuzi kwamba "Even accused not informed Enough doesn't affect the Natural of Offense".
Kwenye picha ya Hapo juu kuna Ushaidi wa wazi unasema:
..... He (the accused) came close to me and said "Leo utanipa **** yako". He got hold of me and laid me down.
Kwa Ushaidi huo Mahakama ikaona Ushaidi imetoa picha ya moja kwa moja kwamba Kitendo kilifanyika, hivyo ikaamua kwamba licha ya Hati ya mashtaka haikuweka Taarifa za kutosha "accused" kumfanya hajue Namna ya kujitetea baadae, kwaiyo alichofanya Kumaliza Chini Yule mwanamke ni kitenda cha maandalizi ya kutaka kumbaka. Hivyo Basi hapa Mahakama ikatoa uhamuzi wa "Even accused not informed Enough about the charger, in the charger Sheet doesn't affect the Natural of Offense".
Tosiishie Tu hapa maana kuna Jambo ambalo lipo hapa Katuga alilizungumzia na ni Kwa mujibu wa Ushaidi wa Utetezi wa Lissu.
Katuga haliteta hoja yake kwa kuongezea Nguvu na Ushaidi wa Shaidi wa Utetezi kwamba, Shaidi aliniambia Mahakama kwamba Lissu Alisema maneno kwamba "kwani wakitukamata watatufanya nini, watatuuwa?, hawatotuuwa Bali watatupa Kesi ya Uhaini", hoja hii inafunga Kabisa Kile ambacho Hukumu ya Marejeo ya Kesi iliyotajwa Hapo juu kwamba mstakiwa alikuwa anajua moja kwa moja Matokeo ya Maneno yake na Kitendo cha Kumaliza Chini Yule mwanamke kilikuwa ni kumbaka. Hivyo Basi Hakukuwa na Haja ya kuweka Kila kitu kwenye Hati ya mashtaka Hili kimuwezeshe yeye kama Accused kuelewa natural of Offense maana alishajua toka Mwanzo matokeo ya Maneno yake na Kitendo chake ni kubaka.
(Kwa wale wasio jua, kwenye Kesi ya Lissu Jamhuri iliiomba Mahakama kurejea Kurasa wa 5 wa Kesi nyingine kabisa iliyowai kutolewa Hukumu na Mahakama hiyo hiyo mwaka 2007 Kati ya Damian Ruhele Vs Republic Ambapo Kesi hiyo ilikuwa inahusu Ubakaji na Kifungo kilikuwa Miaka 30 jera hivyo Basi hoja uliyotolewa kwenye Kesi hiyo ni kwamba. Mahakama hii ilitoa Hukumu hata pale Ambapo Hati ya Mashtaka haikuweka Kila kitu cha Kumuwezesha accused kujitetea baadae kwaiyo Lisu nae katika maneno haliyosema na kama Shaidi wa utetezi alivyosema alijua fika kwamba Kosa litakalokuja mbele yake ni Uhaini, hivyo Basi Katuga na Jamhuri Kwa ujumla wakaona sio Lazima kusema Kila kitu kwenye Hati ya Mashtaka na Mahakama inaweza Kutoa hukumu hata kama Hati hiyo haikuwezesha accused kuelewa Natural of Offense kwasababu Kesi kama hiyo ilishawai kutolewa Hukumu na Mahakama hiyo hiyo, na Mahakama inaweza kurudi kwenye Hukumu hiyo na kuchukuwa hatua zile zile kwenye kesi ya Uhaini ya Lissu.)
Hili twende Sawa naomba Turudi nyuma Kidogo hapa:
Katika kumbukumbu za Mahakama kwenye kesi ya uhaini ya Tundu Lissu, maneno "kwani wakitukamata watatufanya nini, watatuuwa? hawatotuuwa Bali watatupa Kesi ya Uhaini". ni nukuu ya hotuba ya Lissu yenyewe iliyowasilishwa na upande wa Jamhuri kupitia mashahidi kama ACP Amin Mahamba (PW16) na George Bagemu (PW1). Lissu alipojitetea kama shahidi wa kwanza wa utetezi (DW1), alikiri kuyatamka lakini akajenga hoja za kisheria kupinga uzito wake, wakati hatima ya shauri hilo ikisubiriwa kutolewa.
NOTE "UCHAMBUZI WA JUMLA NA TATHIMINI YA KIPENGELE HIKI CHA KWANZA (1)"
Hapa kuna Mambo Kazaa ya kujibiwa na Mahakama:
1. Kwa Maneno hayo Lissu alijua moja kwa moja kuwa anaenda Kutenda Uhaini wa kuitishia Serikali, Yaani Uhaini ulio Chini ya Kifungu cha 39 (2)(d).?
(Hili ndilo lilikuwa hoja ya Katuga mbaka kufikia kuitaka Mahakama Kuikubali Hati ya mashtaka kama ilivyofanya kwenye Kesi ya Damian Ruhele Vs Republic kwamba accused alijua Kitakachotokea Hivyo Basi Hati ya mashtaka haikuwa na ulazima ya kuweka Taarifa za kutosha Kumuwezesha accused kuelewa Natural of Offense kwasababu Lissu alijua kuwa anaenda Kutenda Uhaini Kwa kuitishia Serikali.)
2. Je, Kusema utatenda Jambo Fulani ni Sawa Sawa na kulifanya Jambo Hilo?, Yaani kusema Utatenda Uhaini ni sawa na Kutenda Uhaini huo, kusema nitaiba ni sawa na kuiba kwenyewe, Kusema nitauwa ni Sawa na kuuwa kwenyewe.
3. Je, Jamhuri imeonyesha kila element ya s.39(2)(d), au imeonyesha zaidi kwamba maneno yaliyodaiwa yalisemwa? Yaani imetoa Tafsiri ya Maneno Pekee.
4. Je, definition ya public inaweza kutumika kama mbadala wa “any person or group of persons” bila kubadili scope ya offence? Yaani ni sahihi kubadirisha Neno lilo kwenye Kifungu kilichoshikilia Kesi Husika Hili Uweze Kuthibitisha Makosa unayodai kuwa yametendwa.
5. Je, “public” ni particular inayofafanua allegation, au inabadilisha statutory element yenyewe?
6. Je, matumizi ya “public” yameongeza clarity kwenye charge, au yamebadilisha target iliyowekwa na s.39(2)(d)? Yaani Jamhuri ilishindwa Kuthibitisha Kesi Kwa kutumia maneno halisi yaliyo kwenye Kifungu Husika, Mwisho wakaona Hili tuweze Kuthibitisha Basi tutumie technical terms lakini itabadirisha uhalisia wa Kifungu cha 39(2)(d) na Kuathili na kusaidia Uhaini kuweza kuthibitishiwa.
7. Ikiwa Mahakama itakubaliana na Hoja ya kutumia Kifungu cha 5 Kutoa Neno Public na kuwa mbadala wa Neno any person or group of persons au pia ikikubariana na Hukumu ya Damian Ruhele Vs Republic kwamba Sio Lazima kuambiwa kila kitu Hili kuwezesha Natural of Offense, Basi Mahakama inapaswa Kutoa jibu la maswali Haya:
(A) Hiyo public, "Umma" umethibitishwa na Nani kwamba Ilishawishika na maneno ya Lissu.?
(B) Ikiwa Kitendo cha Kosa ni kuitishia Serikali, kama Kifungu cha 39 (2)(d) cha Penal code kitamkavyo Je, Serikali ilitishika Kwa Maneno Yale ya Lissu.?
(Swali Hili ni muhimu kwasababu linasaidia kufikia beyond reasonable doubt, kwamba Mashaidi wangu Muhimu kadhaa walishindwa kufika Mahakamani Kusema kwamba Serikali ilitishika, pia Lissu Alisema kwamba Taratibu za upelelezi zilikuwa na mashaka kuanzia Mwanzo kwamba Hakukuwa na Mwanasheria, ZPC wa kanda hakufaamishwa kabra, TISS awakufahamu Kuhusu Uhaini huo, DPP akutaalifiwa Kuhusu Shtaka na Mengineyo mengi)
Hili Kutoa Uchambuzi na Tathimini ya Mwisho kabisa kwenye Kipengere cha Kwanza, Kwanza kabisa Tunatakiwa kuangalia Vipengere vinavyofuata.
━━━━━━━━━━━━━━━━━━
2. “STOP THE ELECTION” NI POLITICAL SPEECH AU NI INTIMIDATION OF THE EXECUTIVE?
Hapa ndipo maneno yenyewe yanapoanza kuwa muhimu.
Kwa mujibu wa taarifa za kesi, maneno yanayodaiwa ni pamoja na:
"Tutazuia Uchaguzi" | “we will stop the election”
"Tutavuruga Uchaguzi" | “we will disrupt this election”
"Tutaamasisha uasi" | “we will mobilise rebellion”
HOJA YA LISSU
Lissu Alisema kuna tofauti Katika Context ya Maneno yake Kwa hiyo, neno “Tutazuia uchaguzi” haliwezi kutenganishwa na context yake.
HOJA YA KATUGA
Katuga anaiangalia statement pamoja na mazingira yake na anasema Jamhuri inaona maneno hayo kama manifestation ya nia ya kuitisha Serikali.
Katika submission yake alisoma sehemu ya maneno yanayodaiwa kuwa yalihusu kuzuia na kuvuruga uchaguzi, na akasema hayo ndiyo maneno ambayo Jamhuri imeleta mbele ya Mahakama.
UCHAMBUZI
Hapa kuna tofauti muhimu Kati ya Mipaka ya Kejeri za Kisiasa na Kosa la jinai ambayo Kiukweli Mahakama inapaswa kuangalia Kwa kina Kama kuna Sheria iliyoweka Mipaka Kwenye hili Kwasababu Political speech haimaanishi automatic immunity dhidi ya criminal law.
Lakini pia Political speech kuwa kali hakumaanishi automatic treason, Hapa ndipo tofauti muhimu inapoanzia, kwa sababu Kuna tofauti kati ya:
A. Kusema jambo kali dhidi ya Serikali;
B. Kutaka Serikali ibadilike;
C. Kutaka uchaguzi usifanyike;
D. Kushawishi watu wasishiriki uchaguzi; na
E. Kutengeneza nia ya kuishurutisha/kuitisha Executive, Legislature au Judiciary kwa namna ambayo sheria imeifanya kuwa treason.
Mahakama lazima itafute bridge kati ya maneno yaliyosemwa na specific statutory intention inayotakiwa na s.39(2)(d).
SWALI LA KIMAHAKAMA:
Je, context nzima ya maneno hayo inaonyesha nia ya ku-intimidate Executive, au Jamhuri inahitaji Mahakama ifanye inference hiyo kutoka kwenye maneno yenyewe?
━━━━━━━━━━━━━━━━━━
3. “OVERT ACT” DHIDI YA “DEED”: JE, NI VITU VIWILI TOFAUTI?
Katika Jambo ambalo hata Mimi nilikuwa nimependezwa nalo ni Overt Act/ Deed na ndipo submission ya Katuga inakuwa interesting sana.
HOJA YA LISSU
Lissu anategemea umuhimu wa overt act na authority kama Hatibu Gandhi.
Hoja ni kwamba mere words hazipaswi kuchukuliwa automatically kuwa overt act ya treason bila kuonyesha kitendo kinachohitajika na sheria.
HOJA YA KATUGA
Katuga anasema charge ilichagua “manifestation by his deed”, si “publication” wala “overt act”.
Anategemea neno “or” na s.13 ya Interpretation of Laws Act kusema alternatives hizo zinapaswa kutazamwa disjunctively.
Kisha anasema “Deed ya nini? Kitendo chake cha kutoa na kusambaza maneno.”
UCHAMBUZI
Hapa ndipo tunahitaji kuwa makini sana kwasababu Katuga mwenyewe alirejea Black’s Law Dictionary akitofautisha deed na overt act; baadaye akaeleza deed kama “something that is done”.
Kwa hiyo argument yake si kwamba maneno ni overt act, Argument yake ni uttering the words = deed.
Hilo ni proposition tofauti kabisa. Hatibu Gandhi, kwa upande mwingine, inatukumbusha kwamba proof ya overt act peke yake haitoshi kuthibitisha treason.
SWALI LA KIMAHAKAMA:
Je, “deed” katika s.39(2)(d) inaweza kisheria kujumuisha kitendo cha kutamka maneno, hata pale charge yenyewe imechagua “deed” badala ya “publication” au “overt act”?
. “OR” — KATUGA YUKO SAHIHI KUSEMA ALTERNATIVES HIZI HAZIFANANI?
HOJA YA KATUGA
Katuga ametumia s.13 Interpretation of Laws Act: “or” kwa ujumla huchukuliwa disjunctively, isipokuwa sheria yenyewe ionyeshe similarity.
Kwa hiyo anasema charge haipaswi kuchanganya alternatives hizo.
HOJA YA LISSU
Hoja ya defence ni kwamba manifestation inayodaiwa lazima iendane na wording ya offence yenyewe; si kila kitendo kinachoweza kuitwa “deed” automatically kinatimiza treason.
UCHAMBUZI
Katuga ana point moja ya statutory interpretation hapa: “or” si neno la kupuuzwa.
Lakini hilo halijibu swali la pili; Deed yenyewe ina maana gani ndani ya s.39(2)(d)?
Kusema “or” inatenganisha alternatives hakumalizi definition ya kila alternative Kwa hiyo tuna maswali mawili tofauti:
A. Je, deed ni alternative tofauti na overt act?
B. Kama ndiyo, deed inafikisha nini kisheria?
SWALI LA KIMAHAKAMA:
Mahakama ikikubali kwamba “deed” ni alternative independent, itaitafsiri kwa kiwango gani bila kuipanua criminal liability?
. “UTTERING” — JE, KUTAMKA MANENO NI KITENDO?
HOJA YA KATUGA
Katuga amejenga hoja kwamba “utter” ni verb, na uttering ni kitendo cha kutoa maneno Pia akaunganisha hilo na actus reus + mens rea.
HOJA YA LISSU
Hoja ya defence hapa inahitaji kutenganisha kutamka maneno na kutimiza statutory act ya treason Kwa sababu si kila actus reus ya offence nyingine inakuwa actus reus ya treason.
UCHAMBUZI
Hii ni point ya muhimu sana. Katuga anaweza kuwa sahihi kwamba uttering ni kitendo kwa maana ya grammatical/legal usage.
Lakini swali linalofuata ni kubwa zaidi Je, kwa sababu uttering ni act, basi uttering automatically ni “deed” kwa madhumuni ya s.39(2)(d)?
Hapo ndipo Mahakama inapaswa kufanya statutory analysis.
SWALI LA KIMAHAKAMA:
Je, “uttering” ni act tu, au ni act inayotimiza aina maalumu ya manifestation inayotakiwa na s.39(2)(d)?
━━━━━━━━━━━━━━━━━━
4. PUBLICATION: “NANI ALI-PUBLISH?”
Hoja Kuu inayobishaniwa hapa ni Nani aliyefanya Publication. Kila upande ikatoa hoja zake kama ifuatavyo.
HOJA YA LISSU
Lissu amepinga kwamba kuwepo kwa video online hakuthibitishi kwamba yeye ndiye aliyeifanya publication.
Uzi wa kwanza uliweka distinction kati ya Speaker (Tundu Lissu ) → Recorder (Jambo TV Journalist, Etc) → Uploader (Jambo TV Editor) → Host (Social Media Provider like "Youtube, Instagram, etc") → Sharer (Anyone Individual).
HOJA YA KATUGA
Katuga ameleta maana ya “publish” kama kufanya taarifa ijulikane kwa public na anaunganisha suala la kusambaza maneno na publication.
UCHAMBUZI
Hapa kuna propositions tatu tofauti:
1. Video ilipatikana public.
2. Video ilipublished.
3. Lissu ndiye aliyefanya publication.
Sheria inataka hoja hii iwe imethibitishwa, ikiwa bado prosecution Basi lazima iunganishe accused na act inayodaiwa pia Hoja hizi zinarudi kwenye Ibara ya 18(b) ya Katiba ya mwaka 1977 Ambapo Uhuru huo Unaweza kutumika lakini katika kuitumia Uhuru huo kinaweza kukupelekea kuthibitishiwa kuwa wewe Ndio mmiliki au uliepablish Jambo Husika, Binafsi yangu na Kwa Taaluma yangu ya kisheria Ibara ya 18 inatoa Uhuru wa Maoni na kujieleza Bila kujari Mipaka ya Nchi, hivyo Basi Hakitokea na Mipaka kwamba kuitoa Maoni hayoutakuwa ume publish moja kwa moja,
Ibara ya 18 imesema wazi Mtu yeyote anao Uhuru wa Maoni Bila kujari Mipaka ya Nchi Kwa maana rahisi Hakuna Mipaka wowote utakaowekwa kwenye Mamlaka yeyote kuzuia Uhuru wa kujieleza au kuweka Sheria ya publication kwenye Jambo la Maoni uliyotoa.
SWALI LA KIMAHAKAMA:
Ni ushahidi gani unaomfanya speaker kuwa publisher, badala ya kuwa mtu aliyerekodiwa na publisher mwingine?
. JAMBO TV NA PW17: SHAHIDI ANATHIBITISHA NINI HASA?
PW17 ndie Shaidi mzuri kutoka pande zote mbili, na hapa ndiko umakini unaitajika zaidi
HOJA YA LISSU
Lissu ameipa uzito PW17 kwa sababu alikuwa kwenye mazingira ya tukio, wakati baadhi ya police witnesses walikuwa wanatoa inference kutoka kwenye video au taarifa nyingine.
HOJA YA JAMHURI
Jamhuri haitegemei shahidi mmoja tu. Imeleta witnesses wengi na inasema ushahidi wao kwa pamoja unaonyesha case yake.
UCHAMBUZI
Katika criminal case 17 witnesses ≠ automatically 17 pieces of conclusive proof kwasababu Kila witness anapaswa kupimwa kwa:
SWALI LA KIMAHAKAMA:
Kila shahidi wa Jamhuri anaongeza ushahidi wa element fulani, au baadhi wanarudia inference ileile?
━━━━━━━━━━━━━━━━━━
5. INTENT TO INTIMIDATE VS ACTUAL INTIMIDATION
HOJA YA LISSU
Defence imehoji kama Serikali ilitishwa au kutishika na alleged conduct.
HOJA YA JAMHURI
Hapa lazima tutenganishe intention to intimidate na actual intimidation.
Kifungu kinachozungumziwa kinaweka emphasis kwenye intention na manifestation yake.
UCHAMBUZI
Hii ni sehemu ambayo hatupaswi kuandika kwamba “Rais hakutoa ushahidi, kwa hiyo Jamhuri imeshindwa.” Huo ni conclusion wa haraka ambayo siwezi Kuthibitisha moja kwa moja Hivyo Basi Swali sahihi ni; Actual intimidation ni element inayotakiwa kuthibitishwa na s.39(2)(d), au prosecution inahitaji kuthibitisha intention to intimidate na manifestation yake?
Hilo litategemea wording ya statute na interpretation ya Mahakama.
SWALI LA KIMAHAKAMA:
Je, Jamhuri inahitaji kuthibitisha kwamba Executive iliogopa, au inatosha kuthibitisha kwamba accused alikuwa na nia ya kui-intimidate na akaidhihirisha kwa njia inayotakiwa na sheria?
. KUTOKUITWA KWA RAIS: JE, NI ADVERSE INFERENCE?
HOJA YA LISSU
Lissu alihoji kuhusu kutokutolewa ushahidi na viongozi ambao ungeweza kusaidia Mahakama kuelewa kama Serikali iliona vitendo hivyo kama intimidation.
HOJA YA JAMHURI
Kutokuitwa kwa witness hakumaanishi moja kwa moja kwamba fact inayodaiwa haikutokea.
UCHAMBUZI
Hapa kuna principle muhimu Sana ambayo ni Failure to call a witness ≠ automatic failure of the case Lakini kama witness alikuwa material kwenye element muhimu, Mahakama inaweza kujiuliza kwa nini hakuitwa na nani alikuwa na uwezo wa kumleta.
Kwa hiyo Materiality + availability + burden + existing evidence lazima ziangaliwe pamoja.
SWALI LA KIMAHAKAMA:
Je, huyo witness alikuwa muhimu kuthibitisha element ya offence, au alikuwa witness wa ziada tu?
━━━━━━━━━━━━━━━━━━
6. “NO REFORMS, NO ELECTION”: NI POLITICAL OBJECTIVE AU TREASONOUS OBJECTIVE?
Mambo yanayobishaniwa ni kwamba Maneno kama "No Reforms, No Election", Yalionyesha Nia ya baadae kwamba Tunajiandaa kuzima Uchaguzi Ambapo kufanya Hivyo ndilo kuitishia Serikali Kwa mujibu wa Hati ya Mashtaka.
HOJA YA LISSU
Defence imejaribu kutenganisha political demand ya reforms/election na treason.
HOJA YA JAMHURI
Jamhuri inaiangalia kauli hiyo ndani ya context ya alleged mobilisation na intention ya kuzuia uchaguzi.
UCHAMBUZI
Hapa lazima tuepuke extremes mbili.
Si sahihi kusema “Political speech haiwezi kuwa criminal.” na pia si sahihi kusema: “Political speech yenye nguvu ni treason.”
Swali ni kama political objective hiyo iliambatana na specific statutory intention ya s.39(2)(d).
Naomba tukubariane moja kwa moja kwamba baadhi ya pilitical speechs zinaweza kuwa na kosa la jinai kama uchechoze, Uvunjifu wa maadili ya taifa, na makosa mangine lakini kufika hatua kuwa uhaini sio rahisi wala sio sahihi.
SWALI LA KIMAHAKAMA:
Ni hatua gani inatenganisha political pressure na conduct inayofikia kiwango cha criminal offence?
. ARTICLE 18 NA MIPAKA YA UHURU WA KUJIELEZA
HOJA YA LISSU
Defence imeweka mazingira ya freedom of expression na political speech.
HOJA YA JAMHURI
Uhuru wa kujieleza hauondoi applicability ya criminal law pale conduct inapokidhi offence iliyowekwa na sheria.
UCHAMBUZI
Hapa Article 18 haiwezi kutumika kama “shield” isiyokuwa na mipaka.
Lakini Article 18 nayo haiwezi kupuuzwa wakati Mahakama inatafsiri offence inayogusa political speech Kwa hiyo Mahakama inahitaji kufanya balancing, statutory criminal prohibition ↔ constitutional freedom of expression.
SWALI LA KIMAHAKAMA:
Je, tafsiri ya s.39(2)(d) inayotumika hapa inalinda wording ya offence bila kuifanya iwe pana kiasi cha kuvuka constitutional protection ya political expression?
. CONTEXT YA MANENO: SENTENCE MOJA AU MKUTANO MZIMA?
HOJA YA LISSU
Defence imeonya dhidi ya kuchukua vipande vya maneno na kuviondoa kwenye context.
HOJA YA KATUGA
Katuga anasema maneno yaliyowekwa kwenye charge yana maana na yanaonyesha intention inayodaiwa.
Katika submission yake alihoji pia kama sentensi zilizochaguliwa zinaunda maana kamili katika context yake.
UCHAMBUZI
Hii ni forensic issue, Katika criminal trial, meaning inaweza kutegemea:
Kwa hiyo Mahakama haipaswi kufanya dictionary analysis peke yake Bali kuangalia kla kitu Kuhusu maneno Husika. Hapa naomba tuelewane kidogo kwamba Katika zile kauli alizoongea Tundu Lissu Je, kuchukuwa Neno moja na kuacha lingine kisha kuunganisha Ndio kuweze kumtia hatiani.? Hoja Kuu hapa inayobishaniwa ni maneno yaliyoondolewa Mwanzoni, katikati na Mwishoni Kwa Kila Neno lilowekwa kwenye Hati ya Mashtaka. LISSU anasema maneno yaliyowekwa kwenye Hati si Pekee aliyoyasema kwamba kuna maneno Kati Kati aliyasema ambayo yameondolewa na pengine kama yasingeondokewa Basi Kauli zake zisingekuwa na hoja ya kusema kwamba alikuwa anatishia Serikali.
SWALI LA KIMAHAKAMA:
Je, maana inayodaiwa na Jamhuri ndiyo maana ya kawaida ya statement katika context yake yote, au ni inference inayotokana na kuchagua sehemu fulani?
Kuitisha mkutano ni element ya offence inayodaiwa, au ni mazingira tu yanayotumiwa kuthibitisha intention?
━━━━━━━━━━━━━━━━━━
7. CHARGE, SECTION 135 CPA NA “REASONABLE INFORMATION”
Technical terms zinabishaniwa Kwa Maswali Yale Yale niliyoyauliza kwenye Kipengere cha Kwanza kabisa, Kwamba Matumizi ya Terms zimebadirisha Statutory Wording Au Reasonable Information zimejikita kwenye Natural of Offense.
HOJA YA LISSU
Defence imehoji particulars za charge na matumizi ya terms ambazo zinaweza kubadilisha statutory wording.
HOJA YA KATUGA
Katuga amesisitiza kwamba kazi ya charge ni kutoa reasonable information kuhusu nature ya offence na ametegemea s.135 CPA.
UCHAMBUZI
Hapa ni lazima turekebishe jambo moja muhimu katika uzi wa mwanzo:
s.135 CPA si kifungu kinachounda offence ya treason ni kifungu cha particulars za charge. Offence inatoka Penal Code s.39(2)(d).
Kwa hiyo Penal Code → substantive offence.
CPA s.135 → namna charge inavyopaswa kueleza offence. Hii distinction ni muhimu sana.
SWALI LA KIMAHAKAMA:
Je, charge imeeleza offence kwa particulars zinazompa accused reasonable information bila kubadilisha elements za s.39(2)(d)?
━━━━━━━━━━━━━━━━━━
8. PUBLICATION, DEED NA CYBERCRIMES: JE, SHERIA MOJA INAWEZA KUTOA MAANA KWA KOSA LA SHERIA NYINGINE?
Kwenye Swala la Nani ali-publish Kauli zile alizozitoa Tundu Lissu, kwenye upande wa Kisheria Linaitaji kujibiwa swali la "How can touch the Publication Act between Tundu Lissu and Social Media Journalist (in this case Jambo TV online).? Hapa ndipo suala la Cybercrimes Act linaingia.
HOJA YA JAMHURI
Jamhuri imetumia concept ya publication na dissemination katika kujenga argument yake kuhusu kusambazwa kwa maneno/video.
HOJA YA LISSU
Defence inaweza kuuliza kama definition kutoka sheria nyingine inaweza kuingizwa moja kwa moja kwenye Penal Code.
UCHAMBUZI
Hapa lazima tuwe precise. Cybercrimes Act si sheria inayomhusu mwenye ICT licence pekee. Hiyo argument si sahihi kwa upana huo, Isipokuwa s hemu kubwa ya Sheria hiyo inawahusu wale Tu wenye Leseni Chini ya Mamlaka iliyowekwa, Yaani TCRA.
Kitu cha kuzingatia Kwenye Sheria hii s.3 ya Cybercrimes Act inaanza na formula ya “In this Act…”
Kwa hiyo definition yake ya “publish” ni definition ya matumizi ndani ya Cybercrimes Act, isipokuwa kuwe na legal basis nyingine ya kuitumia kwenye Penal Code.
Hivyo swali halisi ni. Ni kifungu gani kinachoruhusu definition hiyo kuhamishwa na kutumika kupanua maana ya “publication” katika Penal Code s.39(2)(d)?
Hili ni swali tofauti kabisa na kusema Cybercrimes Act haimhusu accused na hapa Article 13(6)(a) inakuwa relevant kama interpretation hiyo ingekuwa inapanua criminal liability badala ya kutafsiri offence iliyopo.
SWALI LA KIMAHAKAMA:
Mahakama inatafsiri Penal Code, au inatumia definition ya sheria nyingine kuongeza scope ya criminal offence?
━━━━━━━━━━━━━━━━━━
9. BURDEN OF PROOF: JE, JAMHURI IMETHIBITISHA KILA ELEMENT?
Hoja zilizobiwhwniwabaada ya Mvutano wote tangia Mwanzo ni je Kwa Mvutano huo, Upande wa mashtaka umethibitisha Kila elements za Kesi ambazo Kifungu cha 39 (2)(d) linaitaji.?
HOJA YA LISSU
Defence inasema prosecution lazima ithibitishe case yake beyond reasonable doubt.
HOJA YA KATUGA
Katuga amerejea s.3(2) Evidence Act na anasema burden hiyo imetimizwa. Pia amesisitiza kwamba beyond reasonable doubt haimaanishi lazima kuwe hakuna “shadow” yoyote.
UCHAMBUZI
Hapa hakuna upande unaobishana kwamba criminal burden iko kwa prosecution. Swali ni application yake.
Mahakama lazima iende element kwa element:
Allegiance?
Intention?
Target?
Purpose?
Manifestation?
Deed/publication/overt act?
Connection ya accused na act?
Kisha iulize:
Je, ushahidi wote ukiwekwa pamoja unaacha reasonable doubt kwenye element yoyote?
SWALI LA KIMAHAKAMA:
Jamhuri imethibitisha offence, au imethibitisha baadhi ya facts ambazo Mahakama inatakiwa kuzifanyia inference?
. HATIBU GANDHI NA GREY LIKUNGU MATAKA: PRECEDENT INASEMA NINI KWELI?
HOJA YA LISSU
Defence inategemea authorities za treason, hasa Hatibu Gandhi na Grey Likungu Mataka, kuonyesha umuhimu wa overt act, intention na statutory ingredients.
HOJA YA JAMHURI
Jamhuri imejaribu kuonyesha kwamba mazingira ya kesi hii na wording ya s.39(2)(d) yanahitaji Mahakama kutofautisha authorities za zamani na facts za kesi hii.
UCHAMBUZI
Hapa hatupaswi kutumia precedent kama slogan.
Tunapaswa kuuliza Ratio ya case ilikuwa nini? Na Facts za case hiyo zinafanana na hizi kwa kiwango gani?
Hatibu Gandhi ni muhimu kwa sababu Court of Appeal ilisisitiza kwamba proof ya overt act peke yake haitoshi bila intention na allegiance.
Lakini haipaswi kutafsiriwa kiholela kuwa “maneno hayawezi kamwe kuwa treason.”
SWALI LA KIMAHAKAMA:
Je, precedents hizo zinazuia interpretation inayotumiwa na Jamhuri, au zinahitaji tu Mahakama kuthibitisha additional elements kabla ya conviction?
━━━━━━━━━━━━━━━━━━
10. MWISHO.
Katika Final Submission Hii Tundu Lissu Alimaliza Kwa kusema Maneno haya:
........ Ni hivi, Waheshimiwa Majaji, kesi ya uhaini ni kesi ngumu sana.
Ukiachilia mbali siasa zake, ambazo pressure zake ndizo zinafanya kesi kuwa ngumu.
Pamoja na kesi kuwa ngumu, nyinyi Majaji mmefanya kazi nzuri sana.
Mmetusikiliza, mmetupa nafasi ya kujitetea.
Hamjanikwaza.
Mmekuwa wavumilivu sana.
Mmefanya kazi kubwa sana na mmefanya kazi nzuri sana.
Nilitaka nisimalize bila kusema haya, pengine hatutakutana tena.
Nilitaka mjue kuwa moyoni mwangu mmefanya kazi nzuri.
Hawa mawakili wangu wa Serikali na wao wamefanya kazi nzuri.
Wamepambana sana mpaka kufika hapa. Pamoja wamekuwa na kesi ya ovyo sana.
Ila wamepambana sana bila kujali nini kitatokea, wamepambana sana.
Nafikiri nawatakieni heri sana.
Asanteni sana.
**********************************
Katika Final Submission Hii Jamhuri/Katuga alimaliza Kwa kusema Maneno haya:
......... Waheshimiwa Majaji, kwa kumaliza kusema hayo, labda na sisi tupate nafasi ya sekunde tano tuweze kuwashukuru.
Kwa kipindi chote cha tangu 22 September 2025 mpaka mwisho wa mwezi September mwaka huu, kwa kutusikiliza mashahidi wetu, tutakuwa tumenyimwa shukrani tusiposema hayo kwa jinsi ambavyo Mahakama imetutreat. Lakini pale ambapo kama binadamu tulikosea...
Waheshimiwa Majaji, tunaomba tumshukuru pia kaka yetu kwa taaluma na umri pamoja; alitukataa kwa kiungwana kwa kipindi chote tulichokuwa naye.
Sisi kwa Jamhuri hatujui na cha ziada kilichojengeka mioyoni mwetu zaidi ya kuthibitisha shtaka na kuacha Mahakama ikatafsiri tuliyoyasema.
*****************************
Ni uchambuzi wangu na Tathmini kwamba, Kwa mujibu wa sheria, ushaidi na Final sabmission hii, Tundu Lissu anahatia katika mikono ya sheria, hivyo basi bila kutoa hukumu ambayo ilipaswa itolewe na mahakama. Maswali yote niliyoyaacha kwa mahakama kama yatajibiwa ipasavyo basi inaweza kumuweka Tundu Lissu kwenye hatia.
Uchambuzi na Tathmini uliyotolewa hapa ni Juhudi za kisomi, Kitaaluma na ni Uchambuzi wa Kisheria wa Mtu mmoja, Yaani Mimi mrxtz2026. Hivyo Basi Siwezi kusema kwamba Huu unaweza kuwa uhamuzi wa Mahakama, Kinyume chake Tusubiri Mahakama Kwa uhamuzi wa Mwisho Kabisa.
Uchambuzi huu umeandaliwa Takribani siku nne (4+) na zaidi. Nawasilisha kwenu Uchambuzi na Tathmini Yangu.
KAMA UTAPENDEZWA UNAWEZA KUSOMA NA HAPA PIA LICHA YA KWAMBA NI NJEE YA MADA HII:
Pendekezo la Katiba Lenye Muundo wa Dola la Tanzania Yenye Mihimili minne. Bandiko hili linahusu muundo Dola lenye mihimili minne ya Kitaifa, Yaani.
1. Baraza la Usimamizi wa Taifa (Muhimili huru wa usimamizi wa msingi yote ya kitaifa, Mamlaka ya kimuungano Kati ya pande mbili za muungano Tanganyika na Zanziar, Mamlaka ya kutoa Tathmini, muongozo na ndie mlinzi wa Ufuasi wa Katiba na Sheria, Tunu za taifa na Maadili ya Taifa, Mlinzi wa Demokrasia na Haki sawa na Mengineyo)
2. Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania (Muhimili wa Pamoja kati ya pande zote mbili, muhimili wa utendaji, utekelezaji wa sera za taifa, dira ya taifa na Usalama na ulinzi wa taifa. Ndio muhimili mkuu kati ya uhusiano wa wananchi na Dola lao)
3. Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania (Muhimili wa Pamoja uwakilishi wa wananchi wa pande zote mbili za muungano katika ngazi ya majimbo, mamlaka ya kutunga sheria na kupitisha bajeti, mamlaka ya mijadara ya muelekeo wa taifa na mipango mikakati ya pamoja na mengnineyo)
4. Mahakama ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania (Muhimili wa pamoja kati ya pamde zote mbili za muungano wenye majikumu ya utoaji haki, hukumu za kisheria, mfasiri wa mwisho wa katiba na sheria, na mengineyo)
Muundo huu unatoa muungozo mzuri wa kutatua matatizo yote ya taifa letu, umoja wetu, na mengineyo mengi, hili kuelewa kiundani kuhusu muundo huu basi hupo kwenye bandiko tajwa hapo juu, na zaidi ya yote Rasimu kamili ya katiba ya muundo huu inapatika kwenye tovuti ya www.katibampya.com

- aliona nini;
- alisikia nini;
- source of knowledge;
- consistency;
- corroboration;
- na element gani ya offence anathibitisha. Hapo ndipo wingi wa mashahidi unatenganishwa na uzito wa ushahidi. Uzi wa kwanza ulikuwa tayari umeweka distinction hiyo.

- maneno kabla;
- maneno baada;
- audience;
- occasion;
- speaker;
- conduct;
- response;
- na circumstances.