Uchambuzi na upelelezi wa tukio la kifo cha padri Francis uanzie hapa

Uchambuzi na upelelezi wa tukio la kifo cha padri Francis uanzie hapa

Nchi hii kuna watu kwa vile wao wameendekeza ngono na hata ukikutana nao utasikia harufu ya ngono wanadhani kila mtu anafanya ngono. Reasoning ya ajabu sana hii!
Mleta maada kaanisha aina za tuhuma
 
Mkuu tusaidiane nyama kwa kweli hapa moyo wangu hautulii natamani ningepewa kibali binafsi kufwatilia kwa kina whts goin on[emoji849] inafikirisha sana
Atwambie kwa nini na kauliwa na nani na wapi na je kwenye aliletwa baada ya kuuliwa au kauliwa hapo hapo
 
Atwambie kwa nini na kauliwa na nani na wapi na je kwenye aliletwa baada ya kuuliwa au kauliwa hapo hapo

IMG-20220419-WA0001.jpg
 
Kuna shida huyu likely kauliwa na wazito
WAUE Ili wapate nini!? Chunguza na wewe uje na majibu yako!
Unaelezwa kisayansi unaleta porojo!

Mauaji ya wazito yanataratibu zake na formula yake! Hata iweje haziwezi kuingiliana!
Hili tukio jepesi sana wala halihitaji PhD ya upelelezi!
Lingekuwa tukio la mauaji taarifa zingeanza kuyumba kuanzia hospital!
Hapo ndipo ingetakiwa uchunguzi uongezewe nguvu
 
Hapa ndipo kanisa linapopataka wakati mgumu,lipotezee habari ipite,au lifuatilie ukweli ujulikane lipate aibu?kwa nini hawa jamaa wasiluhusiwe tu kuoa?

Vatican yenyewe kuna kesi za miaka kibao
Na hivi wazungu hawafichagi unakuta wazee wa miaka hata 70 wanasema walilawitiwa wakiwa wadogo

Na mimi nakazia waoe tu
 
Kwa uzoefu wangu, matumizi mabaya ya pesa (hata kama waumini hawajui hizo pesa zimetoka wapi) na kutembea na wanawake/wake za watu (hata kama waumini wakimwona padri katembelewa na ndugu wa damu wa kike) "ni tuhuma za kawaida sana kwa mapadri".

Sijawahi kuona padri ambaye hana tuhuma kama hizi (awe amefanya au hajafanya) - it doesn't matter. Nina mfano wa padri fulani. Alikuwa na gari linalofanana na gari (Toyota Corolla) la jamaa ambaye alikuwa akifanyakazi Afrika Kusini. Tofauti yake ilikuwa gari la padri lilikuwa na number plate ya njano na plate number nyeusi na la yule mwenye mke lilikuwa na number plate nyeupe na plate number nyekundu. Kwa watu wa kawaida hizi tofauti hazikuwa na maana sana. Walichojali au walichoona wao ni kusema "gari la padri limepaki nyumbani kwa mke wa mtu kwa muda wa wiki moja sasa" na habari hizi zilifika hata kwa Baba Askofu.

Siku moja huyo padri alipita barabara iliyo karibu na nyumba ya huyo bwana, ambaye bado alikuwa likizo na gari lake lilikuwa palepale nyumbani na padri anaendesha hili la kwake. Alipofika karibu na njia inayoenda nyumbani kwa yule bwana, mke wake alikuwepo na watu wengine na alipoona ni padri akamsimamisha. Padri akasimama, lakini hakutoka kwenye gari. Alifungua kioo kumsikiliza huyo mama, ambaye alisema: "Watu wamekuwa wakizusha kuwa gari la padri liko nyumbani kwangu kwa wiki sasa. Mbona anaendesha gari lake hili na lile mbona bado liko pale nyumbani limepaki. Kwani padri ana magari mawili?"

Baada ya kusema hivyo na wale watu baada ya kuona kuwa kumbe lile gari si la padri, wakamwomba radhi, wakisema "hatujakutendea haki hata kidogo, tusamehe padri". Padri alisema tu "endeleeni na ujinga wenu kama unawasaidia" na akaondoka.

Mapadri wamisionari wanatunzwa na shirika lao na parokiani huwa si 'mabwana fedha'. Parokia nyingi za mjini kama Dar es Salaam, kila parokia ina kamati ya fedha na kuna mhasibu wa parokia ambaye siyo padri. Sasa hizo pesa anazoweza kula anazipata kutoka wapi na kwa nani au ni kamati ya fedha iliidhinisha ili azichukue? Na nijuavyo kamati ya fedha inaidhinisha kwa matumizi ya mradi fulani na padri yeye anakuwepo kama mshauri, lakini mambo yote yanafanywa na viongozi wa kamati ya fedha kwa kushirikiana na kamati zingine - mfano kamati ya ujenzi etc.

Hapa najaribu kuona tu namna waumini wanavyoweza kumshusisha padri fulani na matumizi mabaya ya pesa hata bila kujua undani wa matumizi yenyewe. Kwa shirika kama la Wamisionari wa Afrika, paroko anakuwa ni msimamizi tu wa parokia, lakini anakuwa na mapadri wengine wawili anaofanya nao kazi na wote ni sawa hakuna mdogo wala mkubwa. Kwenye nyumba ya mapadri (community ya hao mapadri watatu), kuna pia mkuu wa nyumba na bursar (wale mapadri wengine wawili ambao siyo paroko - mmoja anakuwa mkuu wa nyumba na mwingine anakuwa anaangalia masilahi yao (bursar) kwa mfuko unaotoka shirikani.

Na kwa vile wote watatu wamepangwa kwenye parokia hiyo uamuzi wa uendeshaji wa parokia lazima uridhiwe na mapadri wote wanaofanyakazi pale. Hapa ndipo ninapoona ugumu wa kufuja hela za parokia. Na kwa baadhi ya parokia (kwa vile mapadri wa shirika wanakaa watatu na wote wanatoka mataifa tofauti), kuna baadhi ya mapadri kulingana na huko wanakotoka wana utajiri kwa mfano wale wanaotoka kwenye familia tajiri - familia zao zinaendelea kuwa'support' kwa hali na mali wanapokuwa huku Afrika. Namfahamu padri mmoja kijana alikuwa akitokea Ireland - alipata pesa za urithi - kutoka familia moja tajiri ambayo iliandika 'will' kwamba watakapofariki mali yao yote itakuwa ni kwa ajili ya huyo Fr.

Huyu alikuwa based Afrika Kusini (ninamfahamu) maana ni schoolmate na kwa utaratibu wa Shirika la Wamisionari wa Afrika mali yote anayopata padri fulani ni mali yake binafsi (ingawa anashauriwa kuitumia vizuri na ikiwezekana aweze kuwasaidia wenzake ambao hawana mali au wanatoka familia masikini kadiri atakavyoona yeye).

Hapa juu nimependa kueleza tu namna padri anavyoweza kuwa na shtuma ambazo kimsingi hazina basis. Lakini natambua pia binadamu tuna upungufu wetu na kama shtuma za waumini ni genuine - mimi ni nani wa kusema padri alikuwa hachukui wake za watu au hakutumia vibaya pesa za parokia? Ila nimetaka tu tuwe na caution!
Umefafanuanvizuri
 
Sitaki kuamini kuwa padre alipanda kwenye tank akiwa mzima akajitupa huko ili afe kifo cha maji ambacho kitachukua muda mrefu. Narudia sitaki kuamini kuwa alipanda kwenye tank akiwa mzima halafu akadumbukia huko. Hivi maeneo ya karibu hakuna CCTV Camera? Nyumba yao imepakana na Shule za st . Joseph na Cathedral Bookshop na Tanzania Commercial Bank zamani Bank ya Posta pia kuna Insurance coy jirani. Je kote huku hakuna CCTV? Je wao hawana CCTV? Ngoja nitulie niendelee kusikia ya kusemwa.
 
Katika upelelezi wa matukio kama haya huwezi kuacha kuangazia (last moment ya marehemu)

Marehemu padri Francis katika mahubiri yake ya misa takatifu jumapili ya matawi!
Sehemu kubwa ya mahubiri yake alilalamika jamii kusema vibaya watu, alisisitiza kwamba yeye kama paroko anasemwa vibaya sana na waumini huko mtaani! Tena wanaomsema vibaya wengine waumini wa karibu yake hata baadhi ya viongozi!

Katika kutaka kujua ni yepi haswa padri huyu aliyokuwa akisemwa kuyafanya!

Ilibidi kuhoji baadhi ya waumini wa kanisani kwake wamebainisha machache (yanayosemwa chinichini kama tetesi);

1. Walisema kuna matumizi mabaya ya fedha za waumini chini utawala wake.
2. Kumekuwepo na maneno ya chinichini kwamba anatembea na wanawake.
3. Inadaiwa moja ya mwanamke wake ambaye ni mke wa mtu penzi lilikolea hadi paroko akaamua kumnunulia gari mwanamke huyo anayeishi maeneo ya mbezi Msakuzi (jina kapuni). Baadhi ya waamini wameenda extra mile nakujiuliza kama kweli mwanamke huyo kahongwa gari, je pesa hizo zimetoka wapi? Kuna biashara gani siku hizi ndani ya kanisa inayowapa mapadri kumiliki ndiga za being mbaya na zingine kuhonga kama kweli? Hayo ni miongoni mwa tetesi.

Kwa hayo machache ingawa hayahusiani moja kwa moja tukio la kifo cha padri!
Lakini yanaweza kusaidia kuleta taswira ya kisaikolojia kwenye tukio zima!
Mazingira alipofia yalivyo salama na watu wake yanahamasisha kurudi kwenye (last moment)!
Nyuma ya tanki la maji bado mazingira hayo yanadhihirisha last moment!
Hivyo kuna uwezekano paroko alikuwa kwenye wakati mgumu!.

HUWEZI KUSEMA KIFO CHA PADRI HUYO NI CHA KAWAIDA kwamba watu wasihoji? Kitendo cha kusema kifo chake ni cha kawaida inaleta uchunguzi mwingine kwa watu wenye akili;
Kukutwa kwenye tanki la maji mtu ambaye siye fundi bomba huwezi sema ni kifo cha kawaida labda kama unataka kufumba jambo hilo! Na jambo hilo linaturudisha tena kwenye last moment ya marehemu!

Paroko wa Parokia ya Kanisa Katoliki Mt. Yohanne Paul II, Mbezi Mshikamano, Dar es Salaam, Francis Kangwa amefariki na mwili wake kukutwa kwenye tangi la maji nyuma ya nyumba ya mapadri wa Shirika la Missionaries of Africa iliyopo Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph-Posta DSM.

Upelelezi bado unaendelea!
Alikutwaje humo kwenye tanki.Yaani walihisi vipi kwamba kwenye tanki yumo mtu.

Ni maumivu makubwa sana ikiwa wale ambao tunawategemea watupe msaada wa kisaikolojia ndiyo wanaogeuka wahanga wa kisaikolojia.
 
No. 3 naona ni ugonjwa au allergy kwa maporoko, wachungaji, viongozi wa dini.

Hapa iringa kuna father mmoja wa kanisa hilo hilo la RC Kiyesa naye alibeba jumla mke wa mtu na huyo shemeji yetu anaitwa Christina mumewe ni mc maarufu hapa iringa anaitwa MC Nestory.


Let make investigation about this na ikikamilika tutamwaga kila kitu hapa hapa jukwaani.
Waoe,hakuna mwanaume anayekula vizuri asitooooo........m.............
 
Sitaki kuamini kuwa padre alipanda kwenye tank akiwa mzima akajitupa huko ili afe kifo cha maji ambacho kitachukua muda mrefu. Narudia sitaki kuamini kuwa alipanda kwenye tank akiwa mzima halafu akadumbukia huko. Hivi maeneo ya karibu hakuna CCTV Camera? Nyumba yao imepakana na Shule za st . Joseph na Cathedral Bookshop na Tanzania Commercial Bank zamani Bank ya Posta pia kuna Insurance coy jirani. Je kote huku hakuna CCTV? Je wao hawana CCTV? Ngoja nitulie niendelee kusikia ya kusemwa.
Ata mm sielewi
 
Aisee nidhamu ni ya muhimu sana yaani unaongelea watumishi wa Mungu kama unaongea na wala unga hivi,hekima ni muhimu sana katika kutoa ushauri kumbuka kuna rika zote humu hata kama ni jukwaa huru hakuna asiyejua matusi ila kulinganisha hawa wapakwa mafuta na wahuni nadhani ni bora kukaa kimya maana zaidi watakaa kimya kwakuwa umedhamiria kutumia ubongo wako kuwafedhehesha,Haipendezi
 
Back
Top Bottom