Kwa uzoefu wangu, matumizi mabaya ya pesa (hata kama waumini hawajui hizo pesa zimetoka wapi) na kutembea na wanawake/wake za watu (hata kama waumini wakimwona padri katembelewa na ndugu wa damu wa kike) "ni tuhuma za kawaida sana kwa mapadri".
Sijawahi kuona padri ambaye hana tuhuma kama hizi (awe amefanya au hajafanya) - it doesn't matter. Nina mfano wa padri fulani. Alikuwa na gari linalofanana na gari (Toyota Corolla) la jamaa ambaye alikuwa akifanyakazi Afrika Kusini. Tofauti yake ilikuwa gari la padri lilikuwa na number plate ya njano na plate number nyeusi na la yule mwenye mke lilikuwa na number plate nyeupe na plate number nyekundu. Kwa watu wa kawaida hizi tofauti hazikuwa na maana sana. Walichojali au walichoona wao ni kusema "gari la padri limepaki nyumbani kwa mke wa mtu kwa muda wa wiki moja sasa" na habari hizi zilifika hata kwa Baba Askofu.
Siku moja huyo padri alipita barabara iliyo karibu na nyumba ya huyo bwana, ambaye bado alikuwa likizo na gari lake lilikuwa palepale nyumbani na padri anaendesha hili la kwake. Alipofika karibu na njia inayoenda nyumbani kwa yule bwana, mke wake alikuwepo na watu wengine na alipoona ni padri akamsimamisha. Padri akasimama, lakini hakutoka kwenye gari. Alifungua kioo kumsikiliza huyo mama, ambaye alisema: "Watu wamekuwa wakizusha kuwa gari la padri liko nyumbani kwangu kwa wiki sasa. Mbona anaendesha gari lake hili na lile mbona bado liko pale nyumbani limepaki. Kwani padri ana magari mawili?"
Baada ya kusema hivyo na wale watu baada ya kuona kuwa kumbe lile gari si la padri, wakamwomba radhi, wakisema "hatujakutendea haki hata kidogo, tusamehe padri". Padri alisema tu "endeleeni na ujinga wenu kama unawasaidia" na akaondoka.
Mapadri wamisionari wanatunzwa na shirika lao na parokiani huwa si 'mabwana fedha'. Parokia nyingi za mjini kama Dar es Salaam, kila parokia ina kamati ya fedha na kuna mhasibu wa parokia ambaye siyo padri. Sasa hizo pesa anazoweza kula anazipata kutoka wapi na kwa nani au ni kamati ya fedha iliidhinisha ili azichukue? Na nijuavyo kamati ya fedha inaidhinisha kwa matumizi ya mradi fulani na padri yeye anakuwepo kama mshauri, lakini mambo yote yanafanywa na viongozi wa kamati ya fedha kwa kushirikiana na kamati zingine - mfano kamati ya ujenzi etc.
Hapa najaribu kuona tu namna waumini wanavyoweza kumshusisha padri fulani na matumizi mabaya ya pesa hata bila kujua undani wa matumizi yenyewe. Kwa shirika kama la Wamisionari wa Afrika, paroko anakuwa ni msimamizi tu wa parokia, lakini anakuwa na mapadri wengine wawili anaofanya nao kazi na wote ni sawa hakuna mdogo wala mkubwa. Kwenye nyumba ya mapadri (community ya hao mapadri watatu), kuna pia mkuu wa nyumba na bursar (wale mapadri wengine wawili ambao siyo paroko - mmoja anakuwa mkuu wa nyumba na mwingine anakuwa anaangalia masilahi yao (bursar) kwa mfuko unaotoka shirikani.
Na kwa vile wote watatu wamepangwa kwenye parokia hiyo uamuzi wa uendeshaji wa parokia lazima uridhiwe na mapadri wote wanaofanyakazi pale. Hapa ndipo ninapoona ugumu wa kufuja hela za parokia. Na kwa baadhi ya parokia (kwa vile mapadri wa shirika wanakaa watatu na wote wanatoka mataifa tofauti), kuna baadhi ya mapadri kulingana na huko wanakotoka wana utajiri kwa mfano wale wanaotoka kwenye familia tajiri - familia zao zinaendelea kuwa'support' kwa hali na mali wanapokuwa huku Afrika. Namfahamu padri mmoja kijana alikuwa akitokea Ireland - alipata pesa za urithi - kutoka familia moja tajiri ambayo iliandika 'will' kwamba watakapofariki mali yao yote itakuwa ni kwa ajili ya huyo Fr.
Huyu alikuwa based Afrika Kusini (ninamfahamu) maana ni schoolmate na kwa utaratibu wa Shirika la Wamisionari wa Afrika mali yote anayopata padri fulani ni mali yake binafsi (ingawa anashauriwa kuitumia vizuri na ikiwezekana aweze kuwasaidia wenzake ambao hawana mali au wanatoka familia masikini kadiri atakavyoona yeye).
Hapa juu nimependa kueleza tu namna padri anavyoweza kuwa na shtuma ambazo kimsingi hazina basis. Lakini natambua pia binadamu tuna upungufu wetu na kama shtuma za waumini ni genuine - mimi ni nani wa kusema padri alikuwa hachukui wake za watu au hakutumia vibaya pesa za parokia? Ila nimetaka tu tuwe na caution!