Uchambuzi na upelelezi wa tukio la kifo cha padri Francis uanzie hapa

Uchambuzi na upelelezi wa tukio la kifo cha padri Francis uanzie hapa

Katika upelelezi wa matukio kama haya huwezi kuacha kuangazia (last moment ya marehemu)

Marehemu padri Francis katika mahubiri yake ya misa takatifu jumapili ya matawi!
Sehemu kubwa ya mahubiri yake alilalamika jamii kusema vibaya watu, alisisitiza kwamba yeye kama paroko anasemwa vibaya sana na waumini huko mtaani! Tena wanaomsema vibaya wengine waumini wa karibu yake hata baadhi ya viongozi!

Katika kutaka kujua ni yepi haswa padri huyu aliyokuwa akisemwa kuyafanya!

Ilibidi kuhoji baadhi ya waumini wa kanisani kwake wamebainisha machache (yanayosemwa chinichini kama tetesi);

1. Walisema kuna matumizi mabaya ya fedha za waumini chini utawala wake.
2. Kumekuwepo na maneno ya chinichini kwamba anatembea na wanawake.
3. Inadaiwa moja ya mwanamke wake ambaye ni mke wa mtu penzi lilikolea hadi paroko akaamua kumnunulia gari mwanamke huyo anayeishi maeneo ya mbezi Msakuzi (jina kapuni). Baadhi ya waamini wameenda extra mile nakujiuliza kama kweli mwanamke huyo kahongwa gari, je pesa hizo zimetoka wapi? Kuna biashara gani siku hizi ndani ya kanisa inayowapa mapadri kumiliki ndiga za being mbaya na zingine kuhonga kama kweli? Hayo ni miongoni mwa tetesi.

Kwa hayo machache ingawa hayahusiani moja kwa moja tukio la kifo cha padri!
Lakini yanaweza kusaidia kuleta taswira ya kisaikolojia kwenye tukio zima!
Mazingira alipofia yalivyo salama na watu wake yanahamasisha kurudi kwenye (last moment)!
Nyuma ya tanki la maji bado mazingira hayo yanadhihirisha last moment!
Hivyo kuna uwezekano paroko alikuwa kwenye wakati mgumu!.

HUWEZI KUSEMA KIFO CHA PADRI HUYO NI CHA KAWAIDA kwamba watu wasihoji? Kitendo cha kusema kifo chake ni cha kawaida inaleta uchunguzi mwingine kwa watu wenye akili;
Kukutwa kwenye tanki la maji mtu ambaye siye fundi bomba huwezi sema ni kifo cha kawaida labda kama unataka kufumba jambo hilo! Na jambo hilo linaturudisha tena kwenye last moment ya marehemu!

Paroko wa Parokia ya Kanisa Katoliki Mt. Yohanne Paul II, Mbezi Mshikamano, Dar es Salaam, Francis Kangwa amefariki na mwili wake kukutwa kwenye tangi la maji nyuma ya nyumba ya mapadri wa Shirika la Missionaries of Africa iliyopo Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph-Posta DSM.

Upelelezi bado unaendelea!
Vitombi wa wake za watu sina huruma nao bora limekufa
 
Kwani wanabaka? Kumbuka hata wewe mkeo hujamkuta bikira!
Akiwa huko barabarani hana alama ..akikubali anapigwa pum....kwahiyo lawama ziko pande zote
Huyu ni padre ukitomba mke we mtu kuuliwa halali yako, kutoka kapteni kwenda Meja tunazawadi ya discovery au Lexus Kali, ni kama mgoni
 
Wewe ni mmoja wa hao viongozi??

Kama sio mmoja wao hufai kujibu hivyo.
Hakuna huo utaratibu mtu akikuika hufukuzwa! Awe mwanamke au mwanamme na waliofukuzwa wapo wengi tu mtaani kwa makosa ya kingono na kwenda kinyume na kanisa
 
Haya wale wakujisifia hakuna mambo ya ajabu ajabu katoliki waje watambe na huku
Mzee tofautisha mtu na taasisi,Kanisa Katoliki km taasisi haina shida,lkn watu waliomo humo ndio wanaweza kuwa na mapungufu ya hapa na pale kwasababu nao ni binadamu.Ikiwa wachungaji wenye wake hufanya ufuska vipi kwa Padre ambaye hana mke hebu wekeni mizani.
 
Kujiombea mwenyewe ni bora zaidi kuliko kumuombea binadamu mwingine. Nitafutie mstari ambao Yesu aliomba kuombewa na mtu mwingine ili iwe mifano ya kuombea wengine.
Wewe au mimi unaweza kujifananisha na Yesu kweli! ,mimi namwomba Yesu nae ananiombea kwa Mungu Baba,hao viongozi wa kiroho wote tunawaombea nao wanatuombea

Yak 5:16​

Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.
 
Hivi hawa mapadri na maaakofu wa katoliki si hawaruhusiwi kuwa na wanawake kabisa.?
 
Hapa ndipo kanisa linapopataka wakati mgumu,lipotezee habari ipite,au lifuatilie ukweli ujulikane lipate aibu?kwa nini hawa jamaa wasiluhusiwe tu kuoa?
Uchunguzi litafanya kanisa au vyombo vya ulinzi na usalama?.Kuhusu kuto kuoa hiyo haiwezi kubadilishwa kwasababu hicho kiapo kipo Kibiblia,lkn pia makosa ya watu wachache hayawezi kupelekea kubadilisha taratibu za kanisa,hivi wewe ukiwa baba nyumbani kwako,ukiwa umejiwekea taratibu zako mfano muda wa watoto kurudi nyumbani ni saa kumi na mbili,je,utabadili utaratibu huo kisa kuna watoto wameshindwa kufuata utaratibu??.
 
Hayo ni mambo ya mtu binafsi Padre ni binadamu kama binadamu wengine so akijisikia anambato tu swala ni heshima na busara Roman katoliki hutumia kuhandle mambo yake huwezi kulinganisha na mambo ya Konde huko
Kumbe kanisa katoliki huwa linajua mapadri na maaakofu wanatomb.a tomba kwahiyo wana namna zao za kuhandle issues siyo? Sasa huu si unafiki si muowe tu?
 
Wewe au mimi unaweza kujifananisha na Yesu kweli! ,mimi namwomba Yesu nae ananiombea kwa Mungu Baba,hao viongozi wa kiroho wote tunawaombea nao wanatuombea

Yak 5:16​

Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.
 
Kwa uzoefu wangu, matumizi mabaya ya pesa (hata kama waumini hawajui hizo pesa zimetoka wapi) na kutembea na wanawake/wake za watu (hata kama waumini wakimwona padri katembelewa na ndugu wa damu wa kike) "ni tuhuma za kawaida sana kwa mapadri".

Sijawahi kuona padri ambaye hana tuhuma kama hizi (awe amefanya au hajafanya) - it doesn't matter. Nina mfano wa padri fulani. Alikuwa na gari linalofanana na gari (Toyota Corolla) la jamaa ambaye alikuwa akifanyakazi Afrika Kusini. Tofauti yake ilikuwa gari la padri lilikuwa na number plate ya njano na plate number nyeusi na la yule mwenye mke lilikuwa na number plate nyeupe na plate number nyekundu. Kwa watu wa kawaida hizi tofauti hazikuwa na maana sana. Walichojali au walichoona wao ni kusema "gari la padri limepaki nyumbani kwa mke wa mtu kwa muda wa wiki moja sasa" na habari hizi zilifika hata kwa Baba Askofu.

Siku moja huyo padri alipita barabara iliyo karibu na nyumba ya huyo bwana, ambaye bado alikuwa likizo na gari lake lilikuwa palepale nyumbani na padri anaendesha hili la kwake. Alipofika karibu na njia inayoenda nyumbani kwa yule bwana, mke wake alikuwepo na watu wengine na alipoona ni padri akamsimamisha. Padri akasimama, lakini hakutoka kwenye gari. Alifungua kioo kumsikiliza huyo mama, ambaye alisema: "Watu wamekuwa wakizusha kuwa gari la padri liko nyumbani kwangu kwa wiki sasa. Mbona anaendesha gari lake hili na lile mbona bado liko pale nyumbani limepaki. Kwani padri ana magari mawili?"

Baada ya kusema hivyo na wale watu baada ya kuona kuwa kumbe lile gari si la padri, wakamwomba radhi, wakisema "hatujakutendea haki hata kidogo, tusamehe padri". Padri alisema tu "endeleeni na ujinga wenu kama unawasaidia" na akaondoka.

Mapadri wamisionari wanatunzwa na shirika lao na parokiani huwa si 'mabwana fedha'. Parokia nyingi za mjini kama Dar es Salaam, kila parokia ina kamati ya fedha na kuna mhasibu wa parokia ambaye siyo padri. Sasa hizo pesa anazoweza kula anazipata kutoka wapi na kwa nani au ni kamati ya fedha iliidhinisha ili azichukue? Na nijuavyo kamati ya fedha inaidhinisha kwa matumizi ya mradi fulani na padri yeye anakuwepo kama mshauri, lakini mambo yote yanafanywa na viongozi wa kamati ya fedha kwa kushirikiana na kamati zingine - mfano kamati ya ujenzi etc.

Hapa najaribu kuona tu namna waumini wanavyoweza kumshusisha padri fulani na matumizi mabaya ya pesa hata bila kujua undani wa matumizi yenyewe. Kwa shirika kama la Wamisionari wa Afrika, paroko anakuwa ni msimamizi tu wa parokia, lakini anakuwa na mapadri wengine wawili anaofanya nao kazi na wote ni sawa hakuna mdogo wala mkubwa. Kwenye nyumba ya mapadri (community ya hao mapadri watatu), kuna pia mkuu wa nyumba na bursar (wale mapadri wengine wawili ambao siyo paroko - mmoja anakuwa mkuu wa nyumba na mwingine anakuwa anaangalia masilahi yao (bursar) kwa mfuko unaotoka shirikani.

Na kwa vile wote watatu wamepangwa kwenye parokia hiyo uamuzi wa uendeshaji wa parokia lazima uridhiwe na mapadri wote wanaofanyakazi pale. Hapa ndipo ninapoona ugumu wa kufuja hela za parokia. Na kwa baadhi ya parokia (kwa vile mapadri wa shirika wanakaa watatu na wote wanatoka mataifa tofauti), kuna baadhi ya mapadri kulingana na huko wanakotoka wana utajiri kwa mfano wale wanaotoka kwenye familia tajiri - familia zao zinaendelea kuwa'support' kwa hali na mali wanapokuwa huku Afrika. Namfahamu padri mmoja kijana alikuwa akitokea Ireland - alipata pesa za urithi - kutoka familia moja tajiri ambayo iliandika 'will' kwamba watakapofariki mali yao yote itakuwa ni kwa ajili ya huyo Fr.

Huyu alikuwa based Afrika Kusini (ninamfahamu) maana ni schoolmate na kwa utaratibu wa Shirika la Wamisionari wa Afrika mali yote anayopata padri fulani ni mali yake binafsi (ingawa anashauriwa kuitumia vizuri na ikiwezekana aweze kuwasaidia wenzake ambao hawana mali au wanatoka familia masikini kadiri atakavyoona yeye).

Hapa juu nimependa kueleza tu namna padri anavyoweza kuwa na shtuma ambazo kimsingi hazina basis. Lakini natambua pia binadamu tuna upungufu wetu na kama shtuma za waumini ni genuine - mimi ni nani wa kusema padri alikuwa hachukui wake za watu au hakutumia vibaya pesa za parokia? Ila nimetaka tu tuwe na caution!
Mkuu yote hayo ya nini?
Mapadre waoe tu, mihemuko ya mwili uliotengenezwa na Mungu ni kaaazi kwer kwer!
 
Huyu ni padre ukitomba mke we mtu kuuliwa halali yako, kutoka kapteni kwenda Meja tunazawadi ya discovery au Lexus Kali, ni kama mgoni
Nchi hii kuna watu kwa vile wao wameendekeza ngono na hata ukikutana nao utasikia harufu ya ngono wanadhani kila mtu anafanya ngono. Reasoning ya ajabu sana hii!
 
Padri wengi wana tabia mbaya sana hasa kuchukua wake za watu
 
Back
Top Bottom