SoC03 Uchambuzi: Namna ambavyo ubovu wa mifumo endeshi ya kiutawala inavyofifisha utawala bora na namna ya kuuendea utatuzi wake ili kuleta mabadiliko

Stories of Change - 2023 Competition

Almalik mokiwa

Senior Member
Joined
Jun 5, 2020
Posts
147
Reaction score
157
Kwa mataifa mengi duniani, imekuwa kawaida watawala kutumia mifumo ya kiutawala inayokiuka misingi ya utawala bora. Katika kukuza na kudumisha utawala unao zingatia zaidi uhuru wa kujieleza, uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa mahakama, uwazi, haki na umoja, ushirikishwaji wa wananchi na utawala wa sheria, dhana ya uwajibikaji siyo ya KUEPUKIKA. Na hii ndio huchora tafsiri halisi ya dhana ya utawala bora.

Tanzania ni moja ya nchi zenye viashiria vya kudhoofika kwa misingi ya utawala wa sheria, uhuru wa kujieleza, uhuru wa mahakama, kusheheni kwa matukio ya ufisadi na rushwa, kukosekana kwa uwazi, uwajibikaji MBOVU wa viongozi wa umma, ushirikishwaji hafifu wa wananchi katika kuamua, kudhoofika kwa uhuru wa vyombo vya habari na kuzorota kwa umoja na haki unaotokana na migongano ya tofauti za kiitikadi. Uchambuzi huu utaenda kugusa moja kwa moja ni kwa namna gani mifumo ya uendeshaji wa kiutawala umekuwa ukikiuka misingi ya utawala bora, na namna ya kuuendea utatuzi wake ili kuhuisha na kusimika nguzo ya utawala bora.

Licha ya Tanzania kutumia mfumo endeshi wa kidemokrasia kama nyenzo kuu ya kupitia ili kudumisha utawala ambao unaitanabaisha serikali kuwa serikali ya watu, inayoipa mamlaka makubwa wananchi katika kufanya maamuzi, lakini bado imeonekana kuwa ni demokrasia iliyochujwa kutokana na ubabaishaji katika kufatwa kwa kanuni zake.

Mambo machache, yanayo dhoofisha utawala bora ni kama ifuatavyo;

Kudhoofu kwa uhuru wa vyombo vya habari;
Tanzania imekuwa ikiingia katika ukakasi juu uhuru wa vyombo vya habari, ambapo umeonekana kuzorota kutokana na kujitokeza kwa matukio mbalimbali ambayo yamekuwa yakitishia usalama wa waandishi wa habari. Mwishoni mwa mwaka 2017, vichwa vya habari vya magazeti mbali mbali nchini, viliripoti taarifa ya kupotea katika mazingira ya kutatanisha kwa mwandishi machachari wa habari za uchunguzi aliyekuwa akihudumu katika gazeti la Mwananchi, ndugu Azory Gwanda. Matukio hayo yamekuwa yakiendelea kujitokeza ambapo waandishi wengine hasa wa habari za uchunguzi, kama Stan Katabalo, Daudi Mwangosi, Josephat Isango na Ben Sanaane kupotea na maisha yao kuwa katika mashaka. Waandishi hawa machachari wameonekana kuingia mashakani hasa baada ya kuonekana wakihoji juu ya utendaji na uwajibikaji wa viongozi wa umma. Kutungwa kwa sheria kandamizi za habari zinazowapa karaha waandishi wa habari na kufifisha utendaji na uwajibikaji wao katika kuuhabarisha umma. Mfano , sheria ya makosa ya kimtandao ya 2015 pamoja na kanuni za maudhui ya mtandaoni ya mwaka 2018.

IMG-20230730-WA0078.jpg

Picha kutoka StockImages

Kuzorota kwa uwazi, uwajibikaji na ushirikishwaji wa wananchi
Kumekuwa na ushirikishwaji mdogo wa wananchi katika kushiriki kwenye shughuli za maendeleo ya nchi, kama vile ushiriki katika uundaji wa bajeti ya taifa, kama katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilivyo ainisha katika ibara ya 8, vile vile kudogodeshwa kwa ushiriki wa umma katika kufanya maamuzi juu ya ulinzi na utunzaji wa rasilimali zao kumekuwa kukionyesha ukinzani baina ya watawala na dhana ya utawala bora. Mfano azimio la Bandari, na kuidhinishwa kwa makubaliano ya ubinafsishaji wa bandari kwa DP world bila kusikilizwa na kuchambuliwa kwa kina kwa maoni ya wananchi, kumechora tafsiri halisi ya kupunjwa kwa ushirikishwaji wa wananchi katika kufanya maamuzi.

DEMOCRACY.jpg

Picha kutoka PA times

Kukiukwa kwa misingi ya utawala wa Sheria na kuongezeka kwa vitendo vya ufisadi na Rushwa
Yapo matukio tofauti tofauti yanayo dhihirisha ukiukwaji wa utawala wa sheria, ambapo viongozi wameonekana kujiingiza katika matendo yasio randana na sheria za nchi yetu, tunaweza kujikumbusha kupitia zuio la mikutano ya vyama vya siasa lililowekwa kinyume na sheria za vyama vya siasa. Kutofatwa kwa misingi ya utawala wa sheria kumesababisha kuongezeka kwa vitendo vya ufisadi, kwani wanao husishwa na vitendo hivyo wamekuwa wakitoa RUSHWA ili wasiwajibishwe na sheria kutochukua mkondo wake.
IMG-20230730-WA0086.jpg

Picha kutoka AdobeStock

NAMNA YA KUUENDEA UTATUZI WAKE ILI KUKUZA DHANA YA UTAWALA BORA KWA MANUFAA YA JAMII.

Uchambuzi wa makala hii umelenga kuleta utatuzi juu ya masuala yanayo zorotesha dhana ya utawala bora na kusimamisha nguzo ya utawala wenye tija katika jamii, ili jamii ipate kunufaika.

Kuundwa kwa mifumo ya uwajibishwaji wa viongozi
Mifumo hiyo inaweza kuwa, utunzi wa sheria ya kuwachukulia hatua viongozi wote wa umma wanaohusishwa na ufisadi kutoka katika ripoti ya mkaguzi wa hesabu za serikali (CAG) kama vile, kifungo cha maisha na kutaifishwa kwa mali za mshitakiwa wa makosa ya ufisadi. Mwaka 2021 ripoti ya CAG ilimtuhumu mkurugenzi mtendaji wa bandari kwa kumhusisha na ufisadi wa fedha za umma bilioni 3.7 na kuishiwa kusimamishwa kazi tu.

b32890f32a9906f55320423e4da0f538.jpg

Picha kutoka Daily News

Mabadiliko katika mitaala ya elimu, yenye kulenga kuwajenga vijana kuwa WAZALENDO
Vijana ndio nguzo na muelekeo wa leo na kesho ya taifa lolote duniani, taasisi za kielimu zinapaswa kuwalea vijana katika makuzi ya kizalendo, kuwafanya vijana kuwa viziwi wa kutosikia sauti zenye maudhui ya kupewa RUSHWA, vipofu wasioona ubora katika kujibinafsisha na kujilimbikizia mali za umma, viwete wasio weza kuuendea ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma, mbadala wake, wawe wakali pale rasilimali zao zinapoguswa na walowezi. Vilevile, taasisi za elimu ziweke somo la sheria kuwa la lazima, kwa lengo la kuwaandaa vijana kuwa weledi katika kuzielewa vyema sheria za nchi yao, hii itasaidia katika kudumisha ulinzi wa rasilimali na kuhuisha utawala wa sheria.

Hero - Transforming Education (11).jpg

Picha kutoka UNICEF

Matumizi ya sanaa katika kuchochea utawala bora
Mtawala mwenye maono ya kulifikisha taifa au taasisi katika nchi ya ahadi, iliyo na miti ya mitende, mito ya maziwa na harufu ya Haluwa, anapaswa kufanya uwekezaji mkubwa katika sanaa, kuwaondolea vikwazo vyote kwa wasanii wenye roho ya ujasiri wa kudadavua athari za uwajibikaji mbovu wa viongozi wa umma na kukosoa vikali vitendo vya RUSHWA na UFISADI kupitia kutanua na kuupigia chepeo UHURU WA KUJIELEZA. Hii itachangia katika kukuza utawala bora.
shutterstock_187662866-1.jpg

Picha kutoka East Side Online

Kuundwa kwa mfumo wa kielektroniki unaoupa umma fursa ya kuweka maoni juu ya viwango vya utendaji na uwajibikaji wa viongozi wa umma
Mfumo huu utaweza kuonyesha utendaji wa viongozi kupitia viwango vilivyopendekezwa na umma, kiongozi ambae anaonekana kuwa na viwango vya chini zaidi anapaswa kuondolewa na kubadilisha kuweka mwingine ambae ataendana na kasi ya mahitaji ya wanajamii. Hii itachochea uwajibikaji wa viongozi wa umma.

IMG-20230730-WA0091.jpg

Picha kutoka Adobe Stock

Mwisho; Ili kudumisha utawala bora mahakama zinapaswa kuwa huru kupitia kupunguza mamlaka ya rais kuteua majaji, mbadala wake iundwe tume ya majaji kwaajili ya kuteua majaji.
 
Upvote 55
Taifa makini ni lenye vijana makini ambao baadaye huwa wazee wenye busara na makini, ili uwe kiongozi wa juu kwa nchi yetu ni lazima uwe mtu wa makamo. Ukiwa kijana hohehae na unapenda uongozi tutegemee kuwa na kiongozi mbumbumbu katika siku za usoni. Andiko zuri sana kijana, nakuona mbali sana....✍
Shukrani sana🙏
 
Andiko limesheheni na linajieleza kwa ustadi mkubwa, I wish VIONGOZI wa umma wangelisoma Ili liwachome na wabadilishe mienendo yao Kwa ajili ya Tanzania Bora. HONGERA kaka Kwa makala hii fupi but full of content!!!
Ahsante sana kaka Daudi🙏
 
Hii iko sahihi, na ndio maana tunadai utawala bora. Utawala bora unaanzia moyoni mwetu, na kwangu mimi na wewe. Ili kuondoa hili, tunapaswa kuisafirisha jamii ya kizazi chetu kwa kuwajenga watoto wetu wakue katika mazingira ya ya kuithamini haki na kweli. Hii itapunguza uchawa. Ukirejea katika andiko hili, nimeeleza namna ya kuwajenga vijana katika misingi hii. Ahsante.
Haya mkuu all the best, katika mapendekezo uliyotoa,nimependa hili la kuwaajibisha viongozi kupitia mahakama au kwa wale mafisadi kutaifisha mali zao. Kwangu mimi this is only effective solution kwa utawala bora. Hayo mengine kama yapo yanafuata baada ya hili. Sioni hio electric system ikifanya kazi kwa nchi corrupted kama Tanzania. Na wala sioni kuwafundisha watoto wetu haki na kweli kama itaondoa tatizo kama bado ufisadi upo. Sio kwamba wabadhirifu wa mali za Umma hawajui haki na kweli, ni wanafanya makusudi. Leo umfundishe mtoto kusimamia haki na kweli anaingia kwenye ajira anakuta au anaona viongozi wakifisadi na HAWAFANYWI LOLOTE, usidhanie akipata nafasi huyu mtu hatokuwa tempted kuiba na yeye. It should be top down process na sio bottom up proccess, tuanze na Viongozi ku deal nao kwenye ufisadi, tight laws kama China, then kila mwananchi akiobserve atakua responsible.Hivi hivi seriously tunacheza makida makida. Again all the best
 
Shukrani sana. Ubarikiwe🙏
 
Uchambuzi makini, akili
Kwa mataifa mengi duniani, imekuwa kawaida watawala kutumia mifumo ya kiutawala inayokiuka misingi ya utawala bora. Katika kukuza na kudumisha utawala unao zingatia zaidi uhuru wa kujieleza, uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa mahakama, uwazi, haki na umoja, ushirikishwaji wa wananchi na utawala wa sheria, dhana ya uwajibikaji siyo ya KUEPUKIKA. Na hii ndio huchora tafsiri halisi ya dhana ya utawala bora.

Tanzania ni moja ya nchi zenye viashiria vya kudhoofika kwa misingi ya utawala wa sheria, uhuru wa kujieleza, uhuru wa mahakama, kusheheni kwa matukio ya ufisadi na rushwa, kukosekana kwa uwazi, uwajibikaji MBOVU wa viongozi wa umma, ushirikishwaji hafifu wa wananchi katika kuamua, kudhoofika kwa uhuru wa vyombo vya habari na kuzorota kwa umoja na haki unaotokana na migongano ya tofauti za kiitikadi. Uchambuzi huu utaenda kugusa moja kwa moja ni kwa namna gani mifumo ya uendeshaji wa kiutawala umekuwa ukikiuka misingi ya utawala bora, na namna ya kuuendea utatuzi wake ili kuhuisha na kusimika nguzo ya utawala bora.

Licha ya Tanzania kutumia mfumo endeshi wa kidemokrasia kama nyenzo kuu ya kupitia ili kudumisha utawala ambao unaitanabaisha serikali kuwa serikali ya watu, inayoipa mamlaka makubwa wananchi katika kufanya maamuzi, lakini bado imeonekana kuwa ni demokrasia iliyochujwa kutokana na ubabaishaji katika kufatwa kwa kanuni zake.

Mambo machache, yanayo dhoofisha utawala bora ni kama ifuatavyo;

Kudhoofu kwa uhuru wa vyombo vya habari; Tanzania imekuwa ikiingia katika ukakasi juu uhuru wa vyombo vya habari, ambapo umeonekana kuzorota kutokana na kujitokeza kwa matukio mbalimbali ambayo yamekuwa yakitishia usalama wa waandishi wa habari. Mwishoni mwa mwaka 2017, vichwa vya habari vya magazeti mbali mbali nchini, viliripoti taarifa ya kupotea katika mazingira ya kutatanisha kwa mwandishi machachari wa habari za uchunguzi aliyekuwa akihudumu katika gazeti la Mwananchi, ndugu Azory Gwanda. Matukio hayo yamekuwa yakiendelea kujitokeza ambapo waandishi wengine hasa wa habari za uchunguzi, kama Stan Katabalo, Daudi Mwangosi, Josephat Isango na Ben Sanaane kupotea na maisha yao kuwa katika mashaka. Waandishi hawa machachari wameonekana kuingia mashakani hasa baada ya kuonekana wakihoji juu ya utendaji na uwajibikaji wa viongozi wa umma. Kutungwa kwa sheria kandamizi za habari zinazowapa karaha waandishi wa habari na kufifisha utendaji na uwajibikaji wao katika kuuhabarisha umma. Mfano , sheria ya makosa ya kimtandao ya 2015 pamoja na kanuni za maudhui ya mtandaoni ya mwaka 2018.View attachment 2704166
Picha kutoka StockImages

Kuzorota kwa uwazi, uwajibikaji na ushirikishwaji wa wananchi: Kumekuwa na ushirikishwaji mdogo wa wananchi katika kushiriki kwenye shughuli za maendeleo ya nchi, kama vile ushiriki katika uundaji wa bajeti ya taifa, kama katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilivyo ainisha katika ibara ya 8, vile vile kudogodeshwa kwa ushiriki wa umma katika kufanya maamuzi juu ya ulinzi na utunzaji wa rasilimali zao kumekuwa kukionyesha ukinzani baina ya watawala na dhana ya utawala bora. Mfano azimio la Bandari, na kuidhinishwa kwa makubaliano ya ubinafsishaji wa bandari kwa DP world bila kusikilizwa na kuchambuliwa kwa kina kwa maoni ya wananchi, kumechora tafsiri halisi ya kupunjwa kwa ushirikishwaji wa wananchi katika kufanya maamuzi.
View attachment 2704180
Picha kutoka PA times

Kukiukwa kwa misingi ya utawala wa Sheria na kuongezeka kwa vitendo vya ufisadi na Rushwa; Yapo matukio tofauti tofauti yanayo dhihirisha ukiukwaji wa utawala wa sheria, ambapo viongozi wameonekana kujiingiza katika matendo yasio randana na sheria za nchi yetu, tunaweza kujikumbusha kupitia zuio la mikutano ya vyama vya siasa lililowekwa kinyume na sheria za vyama vya siasa. Kutofatwa kwa misingi ya utawala wa sheria kumesababisha kuongezeka kwa vitendo vya ufisadi, kwani wanao husishwa na vitendo hivyo wamekuwa wakitoa RUSHWA ili wasiwajibishwe na sheria kutochukua mkondo wake.
View attachment 2704183
Picha kutoka AdobeStock

NAMNA YA KUUENDEA UTATUZI WAKE ILI KUKUZA DHANA YA UTAWALA BORA KWA MANUFAA YA JAMII.

Uchambuzi wa makala hii umelenga kuleta utatuzi juu ya masuala yanayo zorotesha dhana ya utawala bora na kusimamisha nguzo ya utawala wenye tija katika jamii, ili jamii ipate kunufaika.

Kuundwa kwa mifumo ya uwajibishwaji wa viongozi; Mifumo hiyo inaweza kuwa, utunzi wa sheria ya kuwachukulia hatua viongozi wote wa umma wanaohusishwa na ufisadi kutoka katika ripoti ya mkaguzi wa hesabu za serikali (CAG) kama vile, kifungo cha maisha na kutaifishwa kwa mali za mshitakiwa wa makosa ya ufisadi. Mwaka 2021 ripoti ya CAG ilimtuhumu mkurugenzi mtendaji wa bandari kwa kumhusisha na ufisadi wa fedha za umma bilioni 3.7 na kuishiwa kusimamishwa kazi tu.
View attachment 2704187
Picha kutoka Daily News

Mabadiliko katika mitaala ya elimu, yenye kulenga kuwajenga vijana kuwa WAZALENDO; Vijana ndio nguzo na muelekeo wa leo na kesho ya taifa lolote duniani, taasisi za kielimu zinapaswa kuwalea vijana katika makuzi ya kizalendo, kuwafanya vijana kuwa viziwi wa kutosikia sauti zenye maudhui ya kupewa RUSHWA, vipofu wasioona ubora katika kujibinafsisha na kujilimbikizia mali za umma, viwete wasio weza kuuendea ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma, mbadala wake, wawe wakali pale rasilimali zao zinapoguswa na walowezi. Vilevile, taasisi za elimu ziweke somo la sheria kuwa la lazima, kwa lengo la kuwaandaa vijana kuwa weledi katika kuzielewa vyema sheria za nchi yao, hii itasaidia katika kudumisha ulinzi wa rasilimali na kuhuisha utawala wa sheria.
View attachment 2704191
Picha kutoka UNICEF

Matumizi ya sanaa katika kuchochea utawala bora; Mtawala mwenye maono ya kulifikisha taifa au taasisi katika nchi ya ahadi, iliyo na miti ya mitende, mito ya maziwa na harufu ya Haluwa, anapaswa kufanya uwekezaji mkubwa katika sanaa, kuwaondolea vikwazo vyote kwa wasanii wenye roho ya ujasiri wa kudadavua athari za uwajibikaji mbovu wa viongozi wa umma na kukosoa vikali vitendo vya RUSHWA na UFISADI kupitia kutanua na kuupigia chepeo UHURU WA KUJIELEZA. Hii itachangia katika kukuza utawala bora.
View attachment 2704193
Picha kutoka East Side Online

Kuundwa kwa mfumo wa kielektroniki unaoupa umma fursa ya kuweka maoni juu ya viwango vya utendaji na uwajibikaji wa viongozi wa umma; Mfumo huu utaweza kuonyesha utendaji wa viongozi kupitia viwango vilivyopendekezwa na umma, kiongozi ambae anaonekana kuwa na viwango vya chini zaidi anapaswa kuondolewa na kubadilisha kuweka mwingine ambae ataendana na kasi ya mahitaji ya wanajamii. Hii itachochea uwajibikaji wa viongozi wa umma.
View attachment 2704196
Picha kutoka Adobe Stock

Mwisho; Ili kudumisha utawala bora mahakama zinapaswa kuwa huru kupitia kupunguza mamlaka ya rais kuteua majaji, mbadala wake iundwe tume ya majaji kwaajili ya kuteua majaji.
Akili imetulia, uchambuzi makini, hongera saana familia.
 
Aiseee...nataman watawala wapitie hapa watake some notes for reference....maana umeeleza kila kitu na solution umetoa....what a brain....Tanzania tuna hazina kubwa ya vijana....najivunia Tanzania yangu
 
Kaka Mokiwa upo vizuri kazi imenyooka.
Kongole kwako na utafika mbali kupitia kalamu kama si maarifa uliyonayo.
 
Mwisho; Ili kudumisha utawala bora mahakama zinapaswa kuwa huru kupitia kupunguza mamlaka ya rais kuteua majaji, mbadala wake iundwe tume ya majaji kwaajili ya kuteua majaji

Andiko limenyooka sana, ukisoma huchoki kama story flani hivi ila imejaa ukweli ndani yake , hongera kwako ndugu muandishi umetisha sana
 
Back
Top Bottom