Uchambuzi: Tundu Lissu na Chadema: Waathirika wa Siasa za Unafiki na Ukaidi wa Sheria

Kayugumis

Senior Member
Joined
Jun 6, 2022
Posts
160
Reaction score
172

Kinachomuangusha Tundu Lissu leo ni genge la wanafiki waliomzunguka na kumdanganya kwa muda mrefu kuwa ana nguvu, ushawishi, na uwezo wa kufanya yasiyowezekana. Hili ndilo genge ambalo lilimweleza kuwa ana mamlaka ya kuzuia uchaguzi mkuu wa kikatiba kwa sababu tu yeye hajaridhika – jambo ambalo halina mantiki wala msingi wa kisheria.

Leo hii, haohao waliomshawishi kuwa ana uwezo wa kuzuia uchaguzi mkuu ndio haohao wametoweka kimya kimya, wakimuacha Lissu akihangaika peke yake kujibu tuhuma nzito za uhaini kwa kauli zake zisizokuwa na busara alizozitoa akidhani Watanzania watamfuata tu kila atakalosema – hata yale ya kijinga.

Tundu Lissu sasa anavuna alichopanda – matokeo ya kuzungukwa na wanafiki waliomwaminisha kuwa wako naye bega kwa bega hata pale anapovunja sheria. Walimwaminisha kuwa Watanzania ni wajinga kiasi cha kutangazia nia ya kufanya uhaini na bado wakamshangilia. Amebaki peke yake; genge la wanafiki limemuacha solemba.

Lissu pia ameikaba koo Chadema. Chama chao sasa hakijui la kufanya wala pa kuanzia. Ni wao waliosema wazi kuwa "bila mabadiliko ya kisiasa hakuna uchaguzi" mwaka huu. Ni wao hao waliokataa kutia saini fomu za maadili ya uchaguzi – sharti la kisheria linalotakiwa ili kushiriki uchaguzi mkuu. Lakini sasa wanajitokeza kulalamika kwamba wamezuiwa kushiriki uchaguzi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Huu si unafiki wa wazi?

Baada ya mikakati ya hovyo na siasa za porojo kushindwa, viongozi wa Chadema sasa wanageukia wananchi – wakiwalaumu kwa “kutokuonyesha hasira” baada ya Lissu kukamatwa. Ni jambo la kushangaza, hasa ikizingatiwa kuwa ni Lissu huyu huyu aliyewahi kumsanifu Freeman Mbowe na kusema kwamba akihamasisha maandamano anaishia kuandamana na binti yake tu. Leo hii amekamatwa, na Watanzania wanaendelea na maisha yao kama kawaida. Hii ndiyo ishara kuwa Watanzania hawadanganyiki tena.

Hili ni fundisho kwa wanasiasa wanaotegemea mitandao ya kijamii kupanga siasa zao, wakishawishiwa na watu wasio na sura wala majina mitandaoni – ambao hata hawajitokezi barabarani bali hukaa kupost tu. Ni wakati sasa kwa Lissu kupunguza siasa za mtandaoni na kuachana na ushauri wa wanaharakati walioko ughaibuni. Ashuke chini, atangamane na Watanzania wa kawaida walio hapa nchini.

Ukweli ni mmoja – si Tundu Lissu, si Chadema, wala wanaharakati wa ndani au nje ya nchi wenye uwezo wa kuzuia uchaguzi unaofanyika kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Uchaguzi utafanyika mwaka huu, Watanzania watapiga kura, na wale wanaoona hawapo tayari kushiriki, wabaki pembeni bila kuvuruga haki ya wengine kutekeleza wajibu wao wa kiraia na kidemokrasia.

Kwa viongozi wa Chadema, huu ni wakati wa kufanya maamuzi ya msingi: Je, wanaamini kuwa bila wao hakuna uchaguzi? Kama jibu ni ndiyo, basi waache kuuhadaa umma na vyombo vya habari vya kimataifa kuwa wamezuiwa kushiriki. Huwezi kuzuiwa kushiriki uchaguzi ambao wewe mwenyewe ulitangaza kuwa hautakuwapo kama matakwa yako hayatatimizwa.

Mwisho kabisa, nawaasa Watanzania waendelee kuwa waangalifu. Wakatae kuingizwa kwenye mitego ya kisiasa inayowekwa na watu wachache wenye ajenda binafsi. Wasikubali kuvunja sheria kwa lengo la kutimiza tamaa za watu ambao maslahi yao binafsi ni muhimu zaidi kwao kuliko amani, utulivu na maendeleo ya nchi yetu.
 
Lissu anaamini kwenye siasa za vurugu na migomo. Unfortunately waliozifuata mwanzoni wakapata madhara au usumbufu walitelekezwa na hao hao wanasiasa wakapambana na masaibu peke yao. Ingawa yeye pia ni mhanga wa imani yake at least alipata sapoti toka kwa wadau mbalimbali nje na ndani wakiwemo wafuasi wake na wa hali zote.

Kuna haja ya kubadili mbinu zake za kisiasa ili avutie watu wengi badala ya siasa za pinga pinga.
 
Kabakwe
 
Unajifanya unataka watu wafuate Sheria na huku wewe hautendi haki unabambika watu kesi za uongo unatarajia nini?
 
Maelezo Mengi Bila udhibitisho upuuzi mtupu.

Unasema watu wanalia wamezuiwa nani kalia?

Unasema watu Wana walalamikiwa wa Tz hawajaonyesha ushirikiano alivyokamatwa LISSU nani kalalamika Hilo??

In short kupitia andiko hili imejidhirisha ni Kwa Namna Gani Elimu ambayo inatolewa na Sisiemu Kwa zaiid ya Miaka 60 haiwasaidii wa Tanzania.

Ulichokiandika hata mtoto wako alie la Saba hawez kusema mbele za watu.
 
Andishi refu lakini halina taafifu ya kutoa elimu ya maana kwa waTz wanaosoteshwa na mifumo kandamizi ya kiutawala isiyofuata haki kwa raia walio wengi.

Upo hapa kupromote uchawa wako tu na hauna wasi wasi wowote.

Je wananchi wafanye nini kwenye mtanziko huu wa kidemokrasia uliopo sasa nchini mwetu?

Lissu na kesi yake si mfano wa maana kuweza kumnyooshea vidole kwa sasa, kama vile eti kafanya makosa ya kweli ya jinai kwa tuhuma zake, kila mTz anazijua hila za wazi za kesi hii.

Kejeli zako kwamba Wananchi hawakumfuata nyuma kumnasua mikononi mwa Polisi kina logic gani kwa mkomavu wa kisheria?

Na mambo ya kiini macho cha ubambikizaji wa kesi hii huelewi yameasisiwa na nani, au umekuja kupima upepo wa wadau?

Silioni kosa lolote la kijinai la Lissu alilolitenda nje ya kisiasa, Muda ni mwalimu mzuri utaongea na baadaye yatapita na kuisha.

Tusichoshane bhana, wewe ni mtu mzima unalielewa vizuri andiko lako la kichawa limelenga nini.

Haki ya waTz itapatikana kwa njia ambazo Mwenyezi Munga kazipanga tuzipate kwa kuzipitia waTz iwe kwa kupitia Lissu ama kwa njia zingine na mwanga umeanza kuonekana.

Hatuwezi kutegemea ukombozi wa nchi ukaletwa na Ccm iliyofeli miaka yote 60+

Tuwape shime raia wote wa nchi hii wanaoonesha juhudi za kuleta mabadiliko ya kweli.
 
Maelezo marefu ya ki sisiemu sheria gani anazovunja?
 
Gazeti limejaa pumba
 
Huu ni uharo kabisa. Samia anamgwaya sana Lissu na alitumia hela na nguvu za dola kuhakikisha hashindi uenyekiti lakini ameshindwa kumzuia,akaja na plani B la kuwatumia G 55 nayo imebuma sasa kaja na plan C ya kumtungia kesi ya mchongo ya uhaini nayo pia atashindwa na kuvuna aibu. Kinachofuata upinzani utahamia huko huko CCM kwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…