Katika masomo ambayo niliishia njiani ilikuwa kusomea urubani wa ndege!
Ndege ni chombo cha usafiri kinachoongoza kwa usalama kuliko vyombo vingine!
Ukubwa wa ajali ya ndege hutegemea na uzembe wa mamlaka zingine saidizi!
Ndege ina injini zaidi moja, mfano zilizopo Tanzania nyingi zina injini tatu!
Injini moja ikifeli haizuii ndege kutua kwa kutumia injini nyingine kwa dharula!
Ajali ya precision air huko Bukoba, Rubani kafanya kazi yake kwa usahihi kabisa!
Ndege inapoaanza safari huhifadhi oksjeni ya kutosha kulingana na ukubwa wa ndege!
Hewa hiyo ndiyo hutumika na abiria wawapo angani hadi wafikapo safari!
Ndege inapowashwa ndipo mitambo ya hali ya hewa kwenye ndege nayo hufanya kazi!
Ndege ikizimwa hata hewa hukosekana inakuwa sawa na chupa iliyofungwa!
Hivyo kama ndege hutegemea Hali ya hewa kupaa na kutua maana yake kazi ya rubani ni kuhakikisha anaipaisha au kuitua kulingana na Hali!
Tukio la precision linampa pongezi kubwa rubani kwamba baada ya hali kuwa mbaya!
Jambo la kwanza ilikuwa kuangalia yuko umbali gani kutoka ardhini! Karibu au mbali
Kama angekuwa juu sana na hali ikawa mbaya kutokana na hitilafu za chombo kuna namna nyingine ya kuokoa abiria
Lakini kama yuko mbali na chombo ni kizima lakini shida ni mawasiliano Basi hupaswa kutua uwanja uliyokaribu au kurudi!
Shida ni hapo akiwa karibu na ardhini halafu hali ya hewa iwe mbaya ambayo kuendelea na safari angani haiwezekani na mawasiliano ni mabovu!
Njia pekee ya rubani katika hali hiyo ni kupunguza risk! Yaani kuhakikisha anaitua ndege porini, jangwani au ziwani/baharini!
Rubani wa precision alifanikiwa sana kutua ndege salama! Shida yoyote ambayo huhatarisha uhai katika mazingira hayo ni ukosefu wa huduma saidizi! (Poor rescue team with modern technology)
Kama nilivyosema hapo awali ndege hutegemea hewa iliyotoka nayo ili watu wapumue!
Sasa ikitua baharini kama hakujapasuliwa kioo hewa haipiti watu ni rahisi kuzimia (faint)
Pia wanaowahi kuja kuokoa wakizibua vibaya maji huingia na watu hukanyagana kutokana na kutaka kuokolewa haraka!
Tukio la precision rubani kafanya kazi yake. Vyema! Mengine ni uzembe wa rescue team!
Wavuvi wamefanya wanachoweza kujitolea! Uzembe ni kwa mamlaka za uokoaji!
Kwa ajali za kuruka na parachute bado abiria wanaweza toka wote kwenye Ndege angani! Lakini huku duniani wakaenda kutua juu ya mbuga ya wanyama kama hakuna msaada watakufa hata juu ya mchongoma!
Usafiri wa ndege ni salama angani! Kuna rubani namba moja, rubani namba mbili, Technician Fundi rubani namba tatu usalama ni mkubwa kwa waongozaji hata mmoja akilala.
Matatizo yapo huku chini duniani namna ya uokoaji!
Na baada ya kugundua hili ni tatizo maboresho ya kizazi cha ndege kuelea kinafanyiwa kazi, ili hata ndege ikifa angani yenyewe nzima nzima iwe na parachute la kuelea taratibu, na ikitua baharini iweze pia kuelea kama meli!!
Lakini kwa sasa tatizo kubwa ni uokoaji kwa wakati! Vifo vingi ni uzembe kwa waokoaji!