Uchambuzi; Usafiri wa ndege ni salama kuliko usafiri mwingine wowote, ajali ya precision lawama kwa waokoaji. Hongera rubani

Mtoa mada umeeleza vizuri. Kuna video fulani alionekana mkuu wa mkoa akisema bado mawasiliano na rubani yanaendelea (wakati ho ndege ilishaanguka kwenye maji). Ina maana Rubani aliitua ndege salama kwenye maji. Kilichokosekana ni msaada wa uokozi baada ya hapo.
Kama msaada hata wa kuivuta ungefika haraka, milango ingefunguliwa wakati imeshavutwa hadi kwenye kina kifupi, lakini iliobidi ifunguliwe haraka ili angalau waweze kuwahi kuwatoa watu - kuzuia watu wasife kwa kukosa hewa.
Inawezekana lilifanyika kosa kama la wakati wa MV Bukoba - kuitoboa na kusababisha kuzama kwa haraka. Hapa walifungua milango maji yakajaa ndani (hawakuwa na la kufanya zaidi maana wataalamu wa uokoaji hawakuwepo)
Soma thread hii Shujaa wa uokozi ajali ya Precision alijikuta yupo wodini
 
Rubani kafanya sehem yake, msaada ndo umekosekana kutokana na poor rescue team
Hilo walisema weye yakhe, serikali yako haiwez kukubali makosa, watamtafuta tu wa kumwekea zigo la misumari kichwani awe hai au kafariki.
 
Hakika 100%
 
Tumeaibisha taifa kwakweli kwa uzembe ule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…