SERA YA ELIMU na AFYA:
Mimi niseme kidogo juu ya nini watafanya CCM kama ilivyo ktk ilani yao ya 2015 - 2020 katika sekta za elimu na afya pamoja na uongo na makelele anayoendelea kupiga mgombea wao Bwana Magufuli.
ELIMU:
Magufuli anasema [ana ahidi] kuwa ataboresha elimu hususani kwa kutoa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kwa wakati (!!!??), kutoa elimu bure ya msingi na sekondari hadi kidato cha nne. Kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa walimu na wanafunzi kwa kujenga madarasa, maabara na nyumba za walimu na pia kununua madawati. Mwisho anaahidi kuwa ataboresha maslahi kwa maana ya mishahara ya walimu!!
Mimi ktk eneo hili hebu niwaulize wanaCCM mliopo humu pamoja na mgombea wenu wa urais bwana Pombe
Kwamba mnajua na mko aware kuwa walimu wa nchi hii kupitia chama chao cha walimu (CWT) kimetoa "ultimatum" kwa serikali hiihii aliyomo Magufuli ya mwezi mmoja kuwa ilipe madeni yao ya malimbikizo ya mishahara, uhamisho, masomo, likizo nk yanayokadiriwa kufikia bilioni 70 nchi nzima?? Anajua kweli azungumzacho au anapiga kelele tu huyu??
Hivi utawezaje kuahidi jambo/kitu kipya iwapo cha zamani hujakitekeleza? Ni uwendawazimu, upumbavu au ulofa?
Hebu toeni jibu ktk hili kabla ya kuwafanya walimu wa nchi hii wajinga na mapoyoyo!!
Kuhusu kuboresha miundo mbinu ya madarasa, nyumba za walimu na maabara.
Hivi Magufuli na wana CCM wa kwenye mitandao mnafahamu kuwa wakati Edward Lowassa alipokuwa PM wenu alisimamia vyema sana hili na kabla hajaamua kuachia ngazi aliacha miundo mbinu ya madarasa, nyumba za walimu na maabara zikiwa ktk hatua mbalimbali za ujenzi?
Mnajua kuwa Mara baada ya jamaa kuondoka ni kama aliondoka na mpango mzima huo?
Mnajua kuwa mpaka leo hii majengo hayo ambayo ni maboma sehemu nyingi tangu wakati huo (2008) hakuna kilichoendelea na sasa mengine yanabomoka?
Mnajua kuwa katika mpango huu, Sera ilikuwa wananchi waibue mradi au waanzishe ujenzi hadi boma la jengo lisimame na serikali imalizie hatua inayofuata (kupaua, kupiga ripu, rangi na kuweka vifaa vya ndani kama ni darasa basi madawati, maabara - vifaa vya maabara)? Fedha za kazi hii ziko wapi, zilienda wapi?
Mnafikiri Ni kwa nini hata Kikwete mwishoni kwa mwaka Jana alipoibuka na ujenzi wa maabara ktk shule zote za Kata bila kuwa na bajeti wananchi wa maeneo mengi walikuwa reluctant, waligoma kuunga mkono mradi huo?
Jibu ni kuwa walishagundua kuwa serikali ya CCM ni ya waongo na mafisadi
Sasa tuambieni mgombea wenu anajua Na kulitambua hili kweli?
Kwa nini anatoa ahadi zilezile tena? Tafadhali tupeni kwanza mrejesho wa mlichotekeleza ktk yale mliyotuaahidi tangu mwaka 2005 na si kutufanya wajinga!!
Nitarejea kwa sekta ya afya....