Margaret Winston
New Member
- May 13, 2025
- 1
- 2
Habari wanajamii,
Mimi ni mdau ninayepanga kuanzisha mradi wa ufugaji endelevu na salama kiafya hapa Dodoma. Lengo kuu la mradi huu ni kuzalisha bidhaa za mifugo kama nyama, maziwa, mayai na kadhalika ambazo ni bora kiafya na salama kwa matumizi ya jamii.
Malengo ya mradi huu ni pamoja na:
Kwa sasa, nafanya utafiti wa changamoto na fursa zilizopo kwenye sekta ya ufugaji salama na endelevu ili kuhakikisha mradi unakidhi mahitaji halisi ya jamii. Ningependa tushirikiane mawazo na uzoefu wenu kuhusu changamoto mnazokutana nazo. Tafadhali changia kwa kujibu maswali yafuatayo:
Ninashukuru sana kwa muda wako na mawazo yako. Ushirikiano wako utasaidia sana kuboresha utafiti huu na kuhakikisha mradi unaanza kwa mafanikio makubwa hapa Dodoma.
Karibuni tushirikiane mawazo ili kuboresha ufugaji endelevu, salama kiafya, na rafiki kwa mazingira, huku tukitengeneza ajira na kutoa mafunzo kwa jamii yetu!

- ✅ Kuzalisha Chakula Salama kwa Jamii: Kupitia ufugaji unaozingatia mbinu bora za kiafya kwa ajili ya matumizi salama ya nyama, maziwa, mayai, na bidhaa nyingine.
- ✅ Kuchangia Usalama wa Chakula: Kwa kutoa bidhaa za mifugo zilizo bora kwa afya ya jamii.
- ✅ Kujenga Ufahamu kuhusu Chakula Bora: Kutoa elimu kwa wafugaji na wanajamii kuhusu ufugaji endelevu na salama.
- ✅ Kusaidia Kutunza Mazingira: Mradi unazingatia matumizi bora ya ardhi na ufugaji rafiki kwa mazingira. Kwa mfano, kinyesi cha mifugo kinatumika kama mbolea ya asili katika mashamba, kupunguza matumizi ya mbolea za viwandani ambazo zina madhara kwa ardhi.
- ✅ Kutoa Mafunzo na Programu za Uwezeshaji: Mradi unatoa mafunzo kwa wafugaji na wanajamii juu ya mbinu bora za ufugaji endelevu, utunzaji wa mifugo, na uzalishaji salama.
- ✅ Kujenga Fursa za Ajira: Kupitia programu za mafunzo na uzalishaji, mradi unalenga kuajiri ili kuchochea kipato na kujenga uwezo wa kujiajiri.
Kwa sasa, nafanya utafiti wa changamoto na fursa zilizopo kwenye sekta ya ufugaji salama na endelevu ili kuhakikisha mradi unakidhi mahitaji halisi ya jamii. Ningependa tushirikiane mawazo na uzoefu wenu kuhusu changamoto mnazokutana nazo. Tafadhali changia kwa kujibu maswali yafuatayo:
MASWALI YA KUJADILI:
1️⃣ Kuhusu Wewe:
- Unajishughulisha na nini? (Ufugaji, Kilimo, Biashara, nk)
- Umekuwa kwenye shughuli hizo kwa muda gani?
2️⃣ Changamoto Unazokutana Nazo:
MTUMIAJI
- Kama mtu ambaye ni mtumiaji wa chakula kinachotokana na mifugo (nyama, maziwa, mayai, na kadhalika), unapata faida au athari gani kiafya?
- Je, unajali chakula hicho kimeandaliwaje hadi kufikia meza yako?
- Kama mtu unayetaka kujiingiza kwenye ufugaji, ni changamoto zipi kubwa unakutana nazo?
- Ni changamoto zipi kuu unazokutana nazo kwenye ufugaji wa mifugo?
- Je, changamoto hizi zinaathiri vipi kipato chako au uzalishaji wako?
3️⃣ Suluhisho Unazotumia kwa Sasa:
MFUGAJI
- Kwa sasa, unalishaje mifugo yako?
- Je, unalipia huduma au bidhaa zozote kusaidia kwenye ufugaji wako?
- Kama ndiyo, kwa kiasi gani?
- Ni huduma zipi au bidhaa zipi unazolipia? (Mfano: Chakula cha mifugo, vifaa vya ufugaji, huduma za daktari wa mifugo, chanjo, n.k.)
4️⃣ Unachopenda na Usichopenda:
- Uwe mfugaji au mtumiaji, je, ubora wa bidhaa zinazotokana na mifugo unakuridhisha?
- Kwa Mfugaji:
- Ni mambo gani unapenda kuhusu ufugaji wako wa sasa?
- Ni mambo gani ungependa yabadilishwe au kuboreshwa ili kukusaidia zaidi katika ufugaji wako?
- Kwa Mtumiaji wa Bidhaa za Mifugo:
- Ni mambo gani unapenda kuhusu bidhaa za mifugo unazotumia sasa (nyama, maziwa, mayai, na kadhalika)?
- Ni mambo gani hupendi kuhusu bidhaa hizo?
- Ungependa kuona mabadiliko gani kwenye ubora au upatikanaji wa bidhaa hizo?
5️⃣ Uwezo wa Kifedha:
- Ikiwa kutakuwa na suluhisho bora zaidi la kutatua changamoto zako, ungependa kuliwekeza?
- Ni kiwango gani cha bei kingekuwa sahihi kwako?
6️⃣ Mapendekezo ya Kuboresha:
- Kwa Mfugaji:
- Ungependa kuona nini tofauti ili shughuli zako za ufugaji zifanikiwe zaidi?
- Je, ungependa kushiriki kwenye mafunzo ya ufugaji endelevu na salama kiafya?
- Kwa Mtumiaji wa Bidhaa za Mifugo:
- Ungependa kupata elimu juu ya jinsi chakula kinavyotayarishwa ili kiwe salama na bora kiafya?
- Kwa kiwango gani upo tayari kujifunza kuhusu umuhimu wa chakula bora na usalama wake kwa afya yako?
- Je, ungependa kushiriki kwenye semina au mafunzo kuhusu uandaaji salama wa bidhaa za mifugo?
HITIMISHO: