Uchambuzi wa Mkataba wa kuendesha bandari ya Dar es Salaam kati ya Tanzania na Dubai

Huu mkataba unaiingiza rasmi Tanzania kwenye biashara za Kimataifa.

Wenye uelewa wa biashara za Kimataifa watalielewa hilo.


Mambumbumbu wa biashara mtabaki bandari imeuzwa, imeuzwa.

Imeuzwa kupelekwa wapi?
Baelezee baelezeeee!
 
Nawakumbusha watanzania tuachane na CCM sasa manake tunaelekea pabaya sana.
 

Attachments

  • C664DB2B-CB31-4CC9-B649-28FBDD076BF4.jpeg
    55.3 KB · Views: 8
  • 5E1F868E-08D8-4D96-9746-726C1E03437D.jpeg
    150.5 KB · Views: 10
  • 0987988A-4CDC-4E19-AAD7-CF50995D3148.jpeg
    131.1 KB · Views: 9
  • 6F7C0BB4-C0D7-4891-A754-9B031EE7BE13.jpeg
    75.7 KB · Views: 10
  • FD697942-454D-43D8-8E98-EBB44C542640.jpeg
    55.1 KB · Views: 9

IBRAHIM JEREMIAH
S.L.P 602
SONGEA
06/06/2023

KATIBU WA BUNGE, OFISI YA BUNGE
10 BARABARA YA MOROGORO
S.L.P 941,
40490 TAMBUKARELI
DODOMA

YAH. KUPINGA AZIMIO LA UBINAFSISHWAJI WA BANDARI KWA KAMPUNI YA DP WORLD

Ndugu
Husika na Kichwa cha barua hapo Juu,

Mimi ni Mtanzania ambaye nimeguswa na suala hili na kimsingi nina wajibu wa kutoa maoni yangu ili Taifa letu lisiingie matatizoni,

Jambo hili limezua taharuki kwa Watanzania wengi waliosoma na kusikia taarifa hii kwasababu Bandari ni jambo linalohusu Umma,

Lakini pia mchakato huu umekuwa wa haraka na ushirikishwaji wa wananchi umekuwa mdogo sana, hivyo umesababisha kuongeza mashaka zaidi kwa Watanzania,

Hivyo nashauri mkataba huu ubatilishwe kwasababu hizi zifuatazo,

Bandari ni moyo wa Uchumi wa nchi na Kitovu kikubwa cha mapato yetu hivyo kwa umuhimu na Unyeti wake ni muhimu maeneo haya yasibinafsishwe na yakaendelea kuendeshwa na Watanzania wenyewe,

Kupitia uwekezaji huu umetolewa ufafanuzi kuwa Ubinafsishaji wao utaleta mapato kwa asilimia 233,

Imani yangu ni kuwa kupatikana kwa mapato haya hakutumii miujiza,
Ikiwa tutawekeza na kuongeza umakini katika usimamiaji tunaweza kupata mapato zaidi ya asilimia ambazo zimesemwa na wawekezaji,

Athari za Kiulinzi na Kiusalama
Ikiwa Bandari itaendeshwa na Kampuni binafsi kwa asilimia 100 kutakuwa na athari kubwa za kiulinzi na Kiusalama,

Hivi karibuni zimesambaa taarifa za Wanyama wa Afrika kupelekwa Dubai, lakini yapo madini, madawa ya kulevya, Pembe za ndovu na vitu vinginevyo vinavyosafirishwa kwa magendo,
Kama tutaruhusu Ubinafsishaji maana yake hata kama tutatoa ulinzi kutokana na Rushwa bado walinzi wetu wataitumikia Kampuni ya kiarabu,

Uwekezaji ni Biashara
Na hakuna Kampuni inayowekeza ili kupata hasara hivyo faida itakayopata Kampuni hii itawanufaisha waarabu wa Dubai,

Kwa lugha rahisi waarabu watachukua Pesa yetu na kwenda kujengea kwao, Jambo ambalo halitainufaisha nchi yetu,

Lipo suala la Ajira,
Ubinafsishaji huu utaleta tatizo la ajira kwa Watanzania kwasababu Waarabu hupenda kuajiri watu wao,

Waajiriwa wa nafasi kubwa katika Kampuni nyingi za Kiarabu hapa nchini huwa ni waarabu, Watanzania wa asili wengi huajiriwa kwenye nafasi za Utwana, nafasi za chini hivyo itapelekea Watanzania kutonufaika na uwekezaji huu na hivyo uwekezaji utawanufaisha waarabu zaidi katika soko la ajira,

Pia Dubai ni nchi ya Kidini hivyo utaratibu wa uajiri katika kampuni hii utakuwa wa Kidini Jambo ambalo si utamaduni wetu na litapelekea kukosekana kwa umoja wa Kitaifa na kuleta athari za kidini,

Mkataba huu ni wa muda mrefu,
Mikataba ya muda mrefu inaleta athari baadae ikiwa awamu zijazo zitakuwa na mpango tofauti katika shughuli za uendeshwaji wa Bandari,

Nyote ni mashahidi kuwa tumekuwa tukipitia wakati mgumu katika kubadilisha na kuvunja mikataba mingi ya muda mrefu iliyosainiwa kipindi cha nyuma ambayo haililetei tija Taifa mfano mikataba ya Madini na Makinikia ambapo madini yetu yamekuwa yakichukuliwa nje pasipo kutuletea tija yoyote hivyo ni muhimu mikataba hii ya muda mrefu tuisitishe na tuwe na utaratibu wa kufanya mikataba ambayo inakuwa ndani ya muda wa viongozi wa wakati huo ili isilete athari kwa Serikali zijazo na vizazi vijavyo,

Kuipa Kampuni ya Taifa jingine kuendesha Bandari kutalishushia heshima Taifa letu, Mkataba huu unakwenda kututukana na kutudhalilisha kimataifa kwasababu tutaonekana tumeshindwa kujiongoza wenyewe hususani kwenye rasilimali hii muhimu ambayo haitakiwi kufanyiwa mnada na mzaha wa namna hii,

Utofauti wa tamaduni za utendaji kazi na tamaduni zetu,
Dubai wanafanya kazi Jumatatu mpaka siku ya Alhamisi, siku ya Ijumaa inakuwa kama mapumziko lakini pia katika mwezi wa Ramadhani shughuli huwa zinasimama na kazi zinafanywa kwa nusu siku tofauti na hapa kwetu ambapo shughuli zinafanywa wakati wote,
Kwa kiasi fulani Dubai wanafanana sana kitamaduni na Zanzibar kuliko huku Bara hivyo kutakuwa na mtafaruku wa Kitamaduni hususani katika sehemu inayohusu Umma kama hii,

Kwa haya machache niliyoyoaanisha nashauri mapendekezo haya yasipitishwe na mkataba huu uvunje kabla ya kuja kutuletea athari Watanzania!

Wako katika kupigania maslahi ya Taifa
IBRAHIM JEREMIAH
 

Attachments

  • IMG_0515.MP4
    7.7 MB
unajua kwanini katika Nchi zenye Uraia pacha kuna baadhi ya haki hawapewi wenye huo Uraia wa pili?
Hakuelewa ulichosema kuhusu uraia pacha. Labda nimurahisishie hapa

Mzanzibari hawezi iuza Zanzibar
Mzanzibari anawezaiuza Tanganyika
Mtanganyika hawezi iuza Tanganyika
Mtanganyika anaweza iuza Zanzibar

Sasa point to note, ni haki zipi alizonazo Mzanzibari kwa Tanganyika na ni haki zipi alizonazo Mtanganyika kwa Zanzibar.
 
Huu mkataba unaiingiza rasmi Tanzania kwenye biashara za Kimataifa.

Wenye uelewa wa biashara za Kimataifa watalielewa hilo.


Mambumbumbu wa biashara mtabaki bandari imeuzwa, imeuzwa.

Imeuzwa kupelekwa wapi?
Thibitisha kwa kuleta facts kama za mtoa Mada.
 
Mnaingizwa mkenge na nketa mada na nyinyi mnauvaa kichwa kichwa, Mleta mada ameleta vipande tu vya mkataba na kuwalisha maoni yake.

Aweke mkataba kamili.

Huyu ni wale wale tu, kina ndugai na bashiru.
Kama unao bi Mkubwa tunaomba utuwekee hapa ili tuuone na kuusoma. Itapendeza.
 
Kama unao bi Mkubwa tunaomba utuwekee hapa ili tuuone na kuusoma. Itapendeza.
Hao waluouleta vipande vipande humu wanao, cha kujiuliza, kwanini wanaleta vipande vipande wanavyotaka wao tu?
 
Mkuu kama unao mkataba mzima kwa nini usiubandike wote hapa ili tusome neno kwa neno na msitari kwa msitari? Hivi vipande vipande tunashimdwa kuelewa lengo lake hasa ni nini?
 
Tumekwisha! Waarabu wanarudi na biashara yao ya utumwa! Halafu kumbe ni bandari zote za tanganyika!
Huyu typist aliyejinyakulia urais atatufikisha pabaya.
Hebu ona anavyoyaleta kwa ushauri wa majambazi haswa! Ile sheria ya kuimarisha TISS na kuwanyanganya polisi mamlaka inakuja makusudi kusaidia ujambazi usio na uwajibikaji. Watanzania hatujawahi kupigana lakini tuko mpakani for sure!
TUKATAE KUHUJUMIWA NA MAJAMBAZI mafia wa kiarabu!
 
Wee bibi udini unakuendesha mbio mno khaaah, au nawee hao wa huko Dubai ni wajomba zako???
 
Huu mkataba unaiingiza rasmi Tanzania kwenye biashara za Kimataifa.

Wenye uelewa wa biashara za Kimataifa watalielewa hilo.

Mambumbumbu wa biashara mtabaki bandari imeuzwa, imeuzwa.

Imeuzwa kupelekwa wapi?
Ila kule kwenu zenj hamuhitaji biashara za kimataifa! mnataka kubaki na bububu kama ilivyo eti eh!!!
 
Huo mkataba hata mie kwa akili zangu ndogo na sijui sheria, ila baada ya kuusoma tena kifungu kidg hapo hapo niliuona hauna maana, ndo iwe yeye Rais??

Acheni kutetea kila kitu bhana. Khaaaah
 
Ila kule kwenu zenj hamuhitaji biashara za kimataifa! mnataka kubaki na bububu kama ilivyo eti eh!!!
Kumbe ubaguzi tu unakusumbuwa, wewe kwenu wapi?

"Kule zenji" kama huelewi mkataba na Dubai walianza na eyapoti, wa bandari ukafatia.

Mbona ni zamani sana mpaka imekuwa historia, wewe ulikuwa umelala?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…