Kinengunengu
JF-Expert Member
- May 3, 2021
- 1,716
- 4,375
KItabu gani kinasema hivyo? Tupe kifungu cha kusapoti usemacho
Vitabu vya dini vinakuambia mababu na mabibi zako wote waliozaliwa kabla ya Yesu na Mtume, na hata waliozaliwa baada lakini hawakuwajua wageni hawa na dini zao kwa sababu ya umbali huko Africa watachomwa na moto wa milele na Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, kwa kuwa hawakumjua huyo Mungu, kwa kuwa hawakupewa ufunuo wa vitabu hivyo vya dini kumjua huyo Mungu.
Unaamini hili nalo?