Nakupa kazi hii onyesha wapi Qur'aan inajipinga yenyewe kisha nikuulize maswali,ukijibu maswali yangu nakuwa mkana Mungu.
Hapo hap unayo yasema haya hata Qur'aan huijui. Nasubiri hizo Contradiiction unazo dai,na tuzijadili moja baada ya nyingine. Mwenzako alikimbia anaye jiita Kiranga,anaweka kisha hataki kuzijadili.
54. Hakika Mola Mlezi wenu ni Mwenyezi Mungu aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Kisha akatawala juu ya Kiti cha Enzi. Huufunika usiku kwa mchana, ufuatao upesi upesi. Na jua, na mwezi, na nyota zinazo tumika kwa amri yake. Fahamuni! Kuumba na amri ni zake. Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.
(7:54)
hyo inasema kua dunia imetengenezwa kwa siku 6.
halafu huku anasema hivi pia!
9. Sema: Hivyo nyinyi mnamkataa aliye umba ardhi katika siku mbili, na mnamfanyia washirika? Huyu ndiye Mola Mlezi wa walimwengu wote. 9
10. Na akaweka humo milima juu yake, na akabarikia humo na akakadiria humo chakula chake katika siku nne. Haya ni sawa kabisa kwa wanao uliza. 10
11. Kisha akazielekea mbingu, na zilikuwa moshi, akaziambia hizo na ardhi: Njooni, kwa khiari au kwa nguvu! Vyote viwili vikasema: Tumekuja nasi ni wat'iifu. 11
12. Basi akazifanya mbingu saba kwa siku mbili, na akazipangia kila mbingu mambo yake. Na tukaipamba mbingu ya chini kwa mataa na kwa ulinzi. Hichi ndicho kipimo cha Mwenyezi Mungu Mwenye Kujua. (41:9-12)
tukizichambua hizi aya ukijumlisha siku 2 za kuumba ardhi, halafu 4 za kuumba milima na kuweka chakula, halafu 2 zingine za kutengeneza mbingu, yaani 2+4+2=8 sasa hapa hyo quran huoni inajipinga!? yaan inasema mungu kaumba katika siku 6 ila katika kuelezea process zimekuja siku 8[emoji16][emoji16][emoji16] bado mnataka kuniambia kitabu kama hiki kimekamilika!?