Haya jibu nini/kipi/nani aliecode/kilichocode DNA zetu?
Naomba ufuatilie jibu langu kimantiki na kuondoa ushabiki wa kidini.
Sijajua jibu la nini kime cide DNA, lakini jibu lake si Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.
Katika kutafuta jibu, kuna njia nyingi. Njia moja inaitwa "elimination method".
Ukiambiwa, mji mkuu wa Chad, Central Africa ni Washington DC iliyopo Marekani, ukijua kwamba mji mkuu wa nchi ni lazima uwe ndani ya nchi hiyo, na Washington DC ipo Marekani, si Chad, utajua kwamba, Washington DC si mji mkuu wa Chad, hata kabla hujajua mji mkuu wa Chad ni mji gani. Hapi unaweza ku eliminate Washington DC kama mji mkuu wa Chad. Unaondoa jibubla Washington DC, unatafuta jibu la kweli.
Sasa, hata kabla ya kujua jibu la mji mkuu wa Chad ni mji gani, unakuwa ushajua jibu sahihi si Washington DC.
Ukiambiwa kwamba, binti ambaye leo ana miaka mitano, ni mama mzazi wa mwanamme mwenye miaka 60 leo, na wewe unajua mama mzazi ni kazima awe mkubwa kuliko mtoto wake, unaweza kujua kwamba, huyu binti wa miaka mitano hawezi kuwa mama mzazi wa huyu mwanamme mwenye miaka 60. K3a sababu mama yake mzazi huyu mwanamme mwenye miaka 60 hawezi kuwa na miaka michache kuliko hiyo sitini.
Hizi habari mbili za mji mkuu wa Chad kuwa Washington DC, na mama wa mwanamme mwenye miaka 60 kuwa binti wa miaka 5 zina contradiction.
Washington DC kuwa Marekani haiwezi kuwa mji mkuu wa Chad, kwa sababu ina contradict kanuni kwamba mji mkuu wa nchi ni lazima uwe ndani ya nchi hiyo.
Kwa hiyo nikikua Washington DC haupo Chad tu, najua hauwezi kuwa mji mkuu wa Chad, hata kabla sijajua mji mkuu wa Chad ni mji gani.
Vivyo hivyo, nikishajua tu kwamba binti wa miaka 5 ni mdogo kuliko mwanamme wa miaka 60, nitajua kwamba huyu binti hawezi kuwa mama mzazi wa mwanamme mwenye miaka 60. Kwa sababu huyu binti wa miaka 5 kuwa mama mzazi wa mwanamme mwenye miaka 60 kuna contradict kanuni kwamba, mama mzazi wa mtu anatakiwa kuwa mkubwa kuliko huyo mtoto, mama anatakiwa kuwa kazaliwa kabla ya mtoto.
Hapo tunaona kwamba, mtu hahitaji kujua jibu sahihi ili kujua kwamba jibu fulani si sahihi. Na kwamba, katika kutafuta jibu sahihi, tunaweza kuondoa majibubfulani kwamba si ya sahihi.
Kuhusu suala la DNA, bado watu wanatafuta jibu sahihi.
Lakini, kama tunavyoweza kusema Washington DC si mji mkuu wa Chad, au binti wa miaka 5 hawezi kuwa mama mzazi wa mwanamme mwenye miaka 60, tunaweza pia kusema Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hawezi kuwa designer wa DNA.
Kwa sababu.
DNA ina mapungufu. Ikipigwa na radiatio ninafanya mutations zinazosababisha magonjwa. Mungu mwenye uwezo wote ujuzi wote na upendo wote surely angekuwa designer wa DNA angefanya DNA ya viumbe wake anaowapenda iwe much better than this.
The other objectionnis a general versionnof this argument.
1. Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayuko compatible na ulimwengu unaoruhusu mabaya. Yuko mutually exclusive na ulimwengu unaoruhusu mabaya.
2. Maana yake, huwezi kuwa na ulimwengu unaoruhusu mabaya kutokea, halafu hapo hapo Mungu huyu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote akawepo. Maana yake, Mungu huyo akiwepo, ulimwengu unaoruhusu mabaya hauwezi kuwepo, na ulimwengu unaoruhusu mabaya ukiwepo, Mungubhuyo hayupo.
3. Ulimwengu unaoruhusu mabaya upo. Ndiyo huu tunaoishi ndani yake. Una magonjwa, majanga ya kiasili, matetemekonya ardhi, mafuriko, vita, ujambazi, etc.
4. Hivyo, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote hayupo.