Uchawi au Majini hayapo! Nani ameshawahi kukutana na jini

Uchawi au Majini hayapo! Nani ameshawahi kukutana na jini

Unaelewa kwamba hata haya maandishi uliyotumia kuandika "mantiki uwezo huo haina" yametumia mantiki?

Yani, huwezi kuikwepa mantiki, mpaka unapotaka kuiponda mantiki, inakubidi utumie mantiki.

Unaelewa kwamba bila mantiki hoja zako za kusema Mungu yupo zinavunjika?

Unaelewa kwamba ukiiponda mantiki unafungua mlango wa kuleta fake news yoyote ile hapa?
Hakuna mantiki yoyote niliyo tumia hapo,sababu maneno na kuhoji au uandishi ulikuwepo kabla ya hiyo Mantiki.

Mantiki ni fani tu iliyo kuja kuwekwa na Aristoto na kujipangia kanuni za namna ya kuhoji kwa mtazamo wake yeye,ambao una madhaifu mengi sana.
 
Baadhi wanasema kuna majini wazuri na majini wabaya, wazuri hua wanasali na kumuomba mungu na wabaya hadi ma atheist wapo

Wapo wanaodai kua kuna elimu juu ya utengenezaji wa hivyo viumbe.

Kuna siku nilisikia redioni mkufunzi akitoa somo namna ya kuita jini kwa kutamka maneno fulani hivi ya kiarabu.

Yale maneno niliyanukuu vyema nikawa naya practice maana mdau alisema unatakiwa uende njia panda usiku wa maneno kisha utamke hayo maneno

Nikiwa na tumaini kua leo ndio siku ambayo najithibitishia kua majini yapo, nikafika njia panda nikaanza kuyatamka hayo maneno kwa kuyarudia rudia zaidi ya mara 100 lakini hakukua na respond yeyote kutoka third party system

Wakati nikiendelea kutamka yale maneno nilishtukizwa na roba flani matata upande wa nyuma, mwanzo nilidhani ni ujio wa jini kumbe ni kibaka wa mtaa na alikua anapiga patrol

Aisee nilimlaumu sana yule jamaa wa redioni
basi huyo aliyekupiga rob ndio jini au shetani.Shetani unavyodhani ni jitu la kutisha lakini shetani anaweza kuja katika maumbo tofauti tofauti.Hata wewe ukishafanya mambo yasiyompendeza mungu tayari umeshakuwa shetani.Shetani ni dhana ya mambo hasi au negative na malaika ni dhani ya mambo chanya au positive.
Ulipokuwa unaomba kutamka hayo maneno mungu aliona akuonyeshe jini kwa mtindo huo take care
 
unasema lugha inahukumu!? katika comments zangu pitia nimekupa mfano ulio wazi!

halafu hua ukiulizwa swali ukashindwa kujibu hua unasema "swali ni la uongo" huu ujinga alikufundisha nani!? yaani mtu yoyote atakushangaa sana eti swali la uongo! unataka istilahi za kuuliza maswali usilete konakona istilahi pekee ya swali ni lijibiwe ! sasa ww unataka kuuliza maswali katika mtindo elekezi wa majibu yako!

na nnadhani ukiendelea na huu upuuzi utakosasifa ya kuingia mjadala na mimi! maana kazi ya kujadiliana na wewe itakua sawa nakumkanda mbwa kizazi
Mpaka najiuliza kwanini hujibu swali la msingi ?

Onyesha nafasi na uwezo wa nini kuratibu suala la DNA ?

Hapa ndiyo nakuonyesha uongo wa swali lako. Sababu tamko "nini ?" Linatumika kwa kisicho na maarifa.

Si umelazimisha nini,ikae katika kuratibu na kusanifu mambo,onyesha ukweli wa hilo,tuambie hiko nini kimewezaje kuratibu na kusanifu DNA na ilikuwaje ? Ukiweza kujibu swali hilo kwa ufasaha basi swali lako litakuwa la kweli.
 
Kuna nadharia za ajabu sana Africa ambazo huwezi ziona dunia ya kwanza.
Uchawi ni nini. Nani ambaye anaweza kutupa prove uchawi upo? Nani alimuona mchawi? Nani anaujua uchawi? Uchawi una nguvu gani?

Hayo Majini ni nini? Hakuna cha majini wala babu yake na majini?
Hizo ni drama za kufikirika.

Utasikia kuna majini. Ushawahi kuliona! Utasikia majini majini ni viumbe visivyoonekana kama hayaonekani umejuaje kama yapo.
Majini na uchawi ni dhana za kufikilika

Lete Proof hapa.

Hakuna cha majini wala uchawi

Kutoamini haimaanishi kwamba haupo! Nikikuuliza una roho most likely utaniambia unayo au sio? Je nikikwambia thibitisha utaweza?

Sent using Jamii Forums mobile app
Roho uliiona wapi?
 
YESU alipotoa mapepo kutoka kwa yule mtu wakatoka na kwenda kuwaingia wale nguruwe na nguruwe wakapata wazimu wakaenda korongoni wakatumbukia wakafa wote hilo unasemaje.Wewe ni nani usikubali kuwa hawa viumbe wapo?
Kama unabisha hebu njoo huku Tanga na Sumbawanga tukubeep kidogo halafu utarudi dar kufuta huu uzi
 
Naona unatangaza viashara zako bila kodi ,hivi kwanini uislam unahusishwa sana na uchawi na majini?naona ile shanga nyeusi huwa wanatembea wakishwali wakiihesabu
 
We jamaa Mzushi tu

mchawi gani unatumia hadi whatsapp, profile picha umemuweka morison mzee wa kukera akiwa amepiga uzi mpya??

Nakupa task tumia uchawi wako fanya uweze kuipata namba yangu ya whatsapp niliyotumia kuangalia profile yako, ukiweza hilo tunafunga huu uzi na rasmi naanza kuamini uchawi
Hahahahaa mm ni simba dam dam na sijasema kama mm ndio naroga

Karibu mwanza mkuu
 
haya kuna hii hapa kati ya dunia na mbingu kipi kilianza!?

hapa anasema

29. Yeye ndiye aliye kuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi. Tena akazielekea mbingu, na akazifanya mbingu saba. Naye ndiye Mjuzi wa kila kitu. (2:29)

yaan kua alianza na ardhi kisha akazigeukia mbingu ndo akaziumba( kifupi imeanza ardhi ikafata mbingu)

halafu huku tena anasema

Are you the harder to create, or is the heaven that He built?
He raised the height thereof and ordered it;
and He has made dark the night thereof, and He brought forth the morn thereof.
And after that, He spread out the earth. -- Sura 79:27-30

hapa ameanzia mbingu halafu akamalizia ardhi!

vipi hiyo sio contradiction!? au tuendelee na zingine!?
Nimecheka sana.

Naposema hakuna "contradictions" katika Qur'aan tuna maanisha.

Anasema Allah mtukufu :

27. . Je! Ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliye ijenga!

28. Akainua kimo chake, na akaitengeneza vizuri.

29. Na akautia giza usiku wake, na akautokeza mchana wake

30. Na juu ya hivyo ameitandaza ardhi. (an-Naaziat :27-30)

Aya hizi hazionyeshi ya kuwa mbingu ndiyo ilianza kujengwa,bali inatoa taarifa juu ya uwezo wa Allah katika uumbaji. Ndiyo maana aya ya 27, inasema yeye ndiye mjenzi.

Aya ya 30 inaonyesha wazi kabisa na limetumika tamko la wakati uliopita la "ameitengeneza yaani aliitengeneza" ardhi,yaani vivyo hivyo yaani yeye ndiye aliitengeneza ardhi,na ndani ya mbingu na ardhi akaweka usiku na mchana.
 
Hakuna mantiki yoyote niliyo tumia hapo,sababu maneno na kuhoji au uandishi ulikuwepo kabla ya hiyo Mantiki.

Mantiki ni fani tu iliyo kuja kuwekwa na Aristoto na kujipangia kanuni za namna ya kuhoji kwa mtazamo wake yeye,ambao una madhaifu mengi sana.
Mantiki ilikuwapo kabla ya Aristotle.

Unapotumia herufi za alphabet, tayari umetumia mantiki ya pangilio wa herufi.

Unapohesabu kwa namba, tayari umetumia mantiki ya hesabu.

Sasa unataka kusema Aristotle ndiye kanzisha kuandika na kuhesabu?
 
Unajua kama mantiki ni fani ? Yaani unawezaje kuitofautisha mantiki na hesabu ?

Mantiki haikuwepo kabla ya Aristoto,usiwe muongo.

Kutumia herufi za alfabeti na kuzipangilia zi kweli kwamba umetumia mantiki.

Si kweli.

Nakuuliza swali dogo sana,mantiki ilikuwepi kama fani au ilikuwepo kama nini kabla ya Aristoto na ulikuwa unaijuaje kama hii ni mantiki,kisha uje kuniambia nini maana ya "Mantiki".

Na mimi nitakifundisha Mantiki ni nini...?
 
Naona unatangaza viashara zako bila kodi ,hivi kwanini uislam unahusishwa sana na uchawi na majini?naona ile shanga nyeusi huwa wanatembea wakishwali wakiihesabu
Shauri yako watakuja wazee wa albadili
 
Nimecheka sana.

Naposema hakuna "contradictions" katika Qur'aan tuna maanisha.

Anasema Allah mtukufu :

27. . Je! Ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliye ijenga!

28. Akainua kimo chake, na akaitengeneza vizuri.

29. Na akautia giza usiku wake, na akautokeza mchana wake

30. Na juu ya hivyo ameitandaza ardhi. (an-Naaziat :27-30)

Aya hizi hazionyeshi ya kuwa mbingu ndiyo ilianza kujengwa,bali inatoa taarifa juu ya uwezo wa Allah katika uumbaji. Ndiyo maana aya ya 27, inasema yeye ndiye mjenzi.

Aya ya 30 inaonyesha wazi kabisa na limetumika tamko la wakati uliopita la "ameitengeneza yaani aliitengeneza" ardhi,yaani vivyo hivyo yaani yeye ndiye aliitengeneza ardhi,na ndani ya mbingu na ardhi akaweka usiku na mchana.

nlichojifunza kutoka kwako ni kua uko tayari kukana kwa kila kitu! mpaka hapa umeshakosa sifa za kujibizana na mimi! kazi ya kua unacheza mdundo wa singeli kwa ku dab! nmekuachia wewe mwenyewe!

aya zinajieleza vizuri tu ila unakuja na maelezo yako ya namna ya kuielewa wakati hizo aya ziko clear zinasema nini!
 
Hapana, nimeona nguvu za giza kwa macho yangu mawili.

Mwanzoni nilikuwa najidai mimi ni msomi na mbishi juu ya haya mambo lakini nilipoyashuhudia ubishi ukanitoka.

Wala sio ugonjwa wa akili.
America,Australia Canada England kote wasomi wabobezi wanafanya study juu ya masuala haya nami nipo pia katika utafiti pia hakika ni utafiti mgumu kupindukia maana katika tafiti utakapokosea tu huweza kuyagharimu maisha yako Instantly.
 
basi huyo aliyekupiga rob ndio jini au shetani.Shetani unavyodhani ni jitu la kutisha lakini shetani anaweza kuja katika maumbo tofauti tofauti.Hata wewe ukishafanya mambo yasiyompendeza mungu tayari umeshakuwa shetani.Shetani ni dhana ya mambo hasi au negative na malaika ni dhani ya mambo chanya au positive.
Ulipokuwa unaomba kutamka hayo maneno mungu aliona akuonyeshe jini kwa mtindo huo take care
Kibaka maarufu mtaani anayejulikana hadi maskani kwake ndio jini?

Ebu kua serious
 
Mambo ya kiroho hayachunguzwi kisayansi
No umekoseaa, research continue in every corner of the world.

N.b:-Remember this is a science, inahusisha hesabu Kali za fizikia za elimu na maesabu anga,kiukweli bila elimu hii hata safari za mwezini au mars haziwezekani kabisa.
"The education beyond"
 
Elimu ni pana usiyoyajua kuhusu dunia ni mengi.
 
No umekoseaa, research continue in every corner of the world.

N.b:-Remember this is a science, inahusisha hesabu Kali za fizikia za elimu na maesabu anga,kiukweli bila elimu hii hata safari za mwezini au mars haziwezekani kabisa.
"The education beyond"
Research zipo za aina nyingi.
Hata mambo ya kiroho yana research zake.Ni mpaka uwe na elimu hio.
 
Back
Top Bottom