Uchawi au Majini hayapo! Nani ameshawahi kukutana na jini

KItabu gani kinasema hivyo? Tupe kifungu cha kusapoti usemacho
 

swali halitakiwi kua "nani ameweka genetic code katika DNA" bali linatakiwa kua "imewezekanaje DNA" kua coded!? na imekua coded na nini?

swali la nani linakua sio valid maana linalenga katika kuitaja nafsi!

nini ni generalisation ambayo inajumlisha nani kifupi "nani" ni swali ambalo linatakiwa kuja baada ya "nini".

kortini hua wanatumia neno "speculating" kuashiria kua muulizaji anauliza swali linalopelekea jibu alilonalo! yaani swali linakudirect kabisa kwenye jibu la muulizaji! ndo maana swali la "nani" sio valid!

bisha tu, mana ndo kazi yako!
 

kutumia aya za kitabu chenye contradiction haina mantiki yaani ni sawa na kutumia uongo kuthibitisha uongo!
Quran inajipinga yenyewe hvyo huwezi kuitumia katika kusapoti hoja yako! hvyo hoja ni dhaifu
 
Ufahamu wako ni Mdogo Sana kuhusu dunia tulia.
 
Alikuwaje! Prove.. Hakuna majini
Njoo tukupeleke chuo cha uchawi temeke na syllabus zipo na notice zake zipo.Unasoma uchawi darasani miaka 5 kwa theory na vitendo then uganga miaka 2 unapewa degree cheti kabisa
 

unataka mfano wa kuonesha nani ipo ndani ya nini!?

mfano huu hapa!

nyumbani kwangu nafuga kuku, paka na mbwa, pia nna watoto hapahapa kwangu! nmeacha sahani ya nyama nje nkaingia ndani baada ya nusu saa narudi nakuta vipande vya nyama havipo kumbuka hapo nje uani kuna mbwa watoto wanacheza paka na kuku pia! sasa natakiwa kujiuliza nani kachukua vipande vya nyama!? au kujiuliza nini kimechukua!?

swali la kwanza linatakiwa kua nini maana kuna variety of options ambazo ni paka mbwa watoto au kuku! nkipata jawabu kua ni watoto basi ntauliza nani!? ili kujua yupi alichukua vipisi vya nyama!


nadhani nmejaribu kukuonesha vema!
 
Onyesha kama mahubiri si uthibitisho. Niambie kilicho andikwa kwenye aya ni uhalisia au siyo uhalisia ?

Kisha kosoa nilicho kiandika. Ukiweza naacha mjadala na nakuwa na fikra kama zako.

sio kila kitu ni uhalisia!
 
Njoo tukupeleke chuo cha uchawi temeke na syllabus zipo na notice zake zipo.Unasoma uchawi darasani miaka 5 kwa theory na vitendo then uganga miaka 2 unapewa degree cheti kabisa

chuo kipo temeke sehemu gani!? tupe jina la chuo!
 

Eti "Third part system" hahahahah ujue we comedy sana
 
Una hoja dhaifu sana. Ndiyo maana nilitaka ujadili aya,na huwa ukijaribu kujibu maswali yangu unaangukia pua,hili nakuonyesha na nilishakuonyesha tangu huko nyuma katika mijadala mingine.

Niliwahi kukwambia ya kuwa suala la ukana Mungu hamjaanza nalo nyinyi,hili weka akilini,walikuwepo na bado watakuwepo. Aya imewajumuisha nyote wenye fikra kama hizo,ndiyo maana ikawataja wao kwa tamko la kufidisha ujumla,kiistilahi tunasema "Umuuman".

Kwahiyo hakuna logic inayoweza kukosoa. Lakini umeonyesha udhaifu mkubwa sana katika hili,sababu aya iko wazi inawauliza wakana Mungu,wanao kataa kuhusu uumbaji,na hapa ndipo ithbati ilipo.

Nilisema hivi ukiweza kukosoa hiyo aya naacha huu mjadala. Sasa kama hata hujui kama wewe ni mkana Mungu,huu mjadala haukufai. Unapoteza muda wako bure.

Kwahiyo swali langu bado liko pale pale. Nasubiri ukosoaji wako.
 
Kwa sababu inawezekana wewe ni mfiadini uliyeamua kwamba hata ukioneshwa Mungu wako ana contradiction hutakubali.

Ukioneshwa kwamba Mungu wako hayupo, utakubali?

Au utang'ang'ania ushabiki wa ki Mujahedeen tu?
Hali ina tabia moja ya ajabu saba,huwa ina mili popote.

Wewe onyesha hilo kama uone nitakataa haki au kinyume chake.

Nasubiri uonyeshe.
 
swali halitakiwi kua "nani ameweka genetic code katika DNA" bali linatakiwa kua "imewezekanaje DNA" kua coded!? na imekua coded na nini?
Lugha ina hukumu kijana. Hakuna lugha inakubali kiulizi cha swali "nini ?" katika jambo lenye mfumo na utaratibu maalumu.

Unajia nini inasimama kumaanisha nini ? Ushawahi kusoma somo la adabu za kuuliza maswali na namna ya kuuliza maswali ?

Ili uone ya kuwa swali lako ni la uongo. Tupe majibu kwa mujibu wa swali lako,kisha tuonyeshe uwezekano wa nini kufanya jambo hilo. Yaani nionyeshe hiyo nini ilivyoweza kufanya hivyo. Ukiweza kufanya hivyo naacha huu mjadala.
swali la nani linakua sio valid maana linalenga katika kuitaja nafsi!
Onyesha nje ya nafsi na kisichokuwa na nafsi kutenda na kusanifu jambo. Tofauti yangu na yenu ni kuwa mimi naongelea uhalisia nyinyi mnaleta dhana na dhahania. Lazima muumie.
nini ni generalisation ambayo inajumlisha nani kifupi "nani" ni swali ambalo linatakiwa kuja baada ya "nini".
Thibitisha hili kwa kutoa mfano. Onyesha hilo kwa kuweka nani na nini,na nani iwe baada ya nini ? Hivi sijui kama huwa mnafikiria haya mambo,au mnajiandikia.
 
kortini hua wanatumia neno "speculating" kuashiria kua muulizaji anauliza swali linalopelekea jibu alilonalo! yaani swali linakudirect kabisa kwenye jibu la muulizaji! ndo maana swali la "nani" sio valid!

bisha tu, mana ndo kazi yako!
Jenga hoja na kosoa,usilete tuhuma baada ya kushindwa hoja.
 
kutumia aya za kitabu chenye contradiction haina mantiki yaani ni sawa na kutumia uongo kuthibitisha uongo!
Quran inajipinga yenyewe hvyo huwezi kuitumia katika kusapoti hoja yako! hvyo hoja ni dhaifu
Nakupa kazi hii onyesha wapi Qur'aan inajipinga yenyewe kisha nikuulize maswali,ukijibu maswali yangu nakuwa mkana Mungu.

Hapo hap unayo yasema haya hata Qur'aan huijui. Nasubiri hizo Contradiiction unazo dai,na tuzijadili moja baada ya nyingine. Mwenzako alikimbia anaye jiita Kiranga,anaweka kisha hataki kuzijadili.
 
Unasikitisha sana,niliposema hili hamliwezi nilimaanisha.

Mfano wako hauonyeshi kwenye nini kuna nani,bali mfano wako umemili kwenye nini. Ndiyo maana umezunguka sana. Hata mimi naweza kuweka msingi wa swali katika nani mwanzi mwisho,ila naweza kuonyesha ujumla wa nani kuzalisha nini.

Nakupa mifano miwili,wa nani kuzalisha nini kwa hususia na nini kuzalisha nani kadhalika,ila swali langu ni ujumla wa nani ndani yake kuna nini,ndiyo maana nili hoji huko mwanzo mtuonyeshe tu hali wezekano au ishara tu ya nini kuweza kumiliko ufahamu na usanifu.

1. Humo ndani kuna nani ? (Nini kuna nani)

2. Kichwani mwako umeweka nini ? (Nani kuna nini)

Swali langu la msingi ni kuonyesha nini kuna nani yenye ufahamu na kuratibu mambo. Muwe mnaelewa hoja. Hili swali huwezi kujibu bali hata wakubwa zako hawawezi kujibu,mwenzako amelikikbia.
 
Hahahaha dah Hadi njaa imeisha sasa
 
Upo mjini unasema hakuna uchawi. Nenda usukumani huko shinyanga. Ukishafika kijijini sema hakuna uchawi na hakuna mtu wa kunifanyia kitu. Utakalopata uje utuhadithie hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…