Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Nitafurahi sana Mzee wangu Ms umjibu huyu MM, Hasa katika mistari hii tu aloweka hapa,,

Bursar,

Mimi ni mpenzi wa mijadala.

Nimefunzwa na maalim wangu Sheikh Haruna adab
za minakasha.

Kubwa ni kutoingia katika mjadala kwa kuonyesha kuwa wewe
ni mjuzi kuwapita wenzako.

Usiingie mjadala na mtu alieghadhibioka na mtu atukanae na kutumia
lugha chafu pamoja na kejeli.

Usilazimishwe kujibu kitu.
Shauri nafsi yako kwa kutafuta kusema lile lenye kheri.

Mnakasha uongeze ilm.
Ikiwa hilo halipatikani jitoe.

Wapime watu hawa unaoniomba nisemezanenao je wanaingia wapi katika
usia wa maalim wangu?
 
Ndugu yangu Ritz,

Hayo ndiyo maswali mimi nikijiuliza kila siku.

Bado hujamjua Idd Faiz Mafongo.
Hebu mtazame hapa chini nilivyomweleza katika kitabu:

In the early days the post of the Organising Secretary was always changing hands between Mtemvu (who was TANU’s first organising secretary) Denis Phombeah, Oscar Kambona, Idd Faiz Mafongo and Stephen Mhando.

Hapo hapo alikuwa Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na TANU.
Wakati ule siasa ilikuwa kazi ya hatari sana.

Watu walikuwa hawakimbilii chama maana hakuna ''kula'' ila kutoa tu.

Abdulwahid alikuwa na biashara ya Kituo Cha Mafuta (Filling Station) kituo hiki kipo hadi
leo pale Ilala Boma mkabala.

Abdu alifilisika kwa kupeleka fedha TANU na kulipa mishahara ya baadhi ya watendaji wa chama.

Kuja uhuru kusahauliwa ndiyo ikaja kuwa ijaza yao.
Ukiwataja katika magazeti.

Magazeti yanakusanywa na kutiwa moto.
Mohamed Said, Japokuwa ni vizuri kwa hilo, Ikiwa unataka kila mtu aliyekuwa ndani ya TAA/TANU aenziwe, hivi leo hii watunza fedha wa ccm na wa Chadema hivi leo wewe unawafahamu na wanaenziwa kwa uzito gani katika majukwaa ya siasa?
 
Ritz hata kama wewe ni mpiga debe, hebu changanya na akili kidogo...ni katika nchi gani na ulimwengu upi ambapo mweka hazina wa chama cha siasa anatajwa au kuenziwa kwa mchango wake katika harakati za kisiasa?

Je chama ANC kilichoanzishwa na Zuberi Mtemvu, mweka hazina wake alikuwa nani?

Je chama cha CUF, Chadema, TLP na kile cha cha Mafisadi na wauaji, mbona hawatajwi?

Ingefaa zaidi kama ungemsaidia Mohamed Said kujibu maswali anayoulizwa, acha papara papara! Kwa kukumbusha maswali ni haya kumhusu mzee wake Mohamed, Abdulwahid Sykes, mjukuu wa mlowezi, Mzulu, aliyetumiwa na Wajerumani kuwapiga vita na kuwaua Watanganyika;

  1. Abdulwahid Sykes aliingia kwenye uongozi wa AA mwaka gani kwa mara ya kwanza na kwa wadhifa gani?
  2. Je mwaka 1946, Mwalimu Nyerere alipohudhuria mkutano wa AA Dar es Salaam kama katibu wa tawi la Tabora, Abdulwahid alikuwa na nafasi gani ndani ya AA?
  3. Je, Abdulwahid Sykes alihudhuria huo mkutano uliofanyika mwaka 1946 Dar es Salaam na kwa wadhifa upi ndani ya AA?
  4. Je, Abdulwahid Sykes kama alihudhuria, kwa nini idaiwe ni mwaka saba baadaye, 1953, ndio kakutana na Nyerere kwa mara ya kwanza?
  5. Je, kama mwaka 1946, Abdulwahid Sykes hakuwa na sifa wala wadhifa wa kuhudhuria huo mkutano wa AA, nani kati yake na kaka yake Mwalimu Nyerere alitangulia kwenye siasa?
  6. Je si kweli kuwa Dr. Kyaruzi, aliyefahamiana na Mwalimu Nyerere toka Makerere, ndiye aliongoza mapinduzi ndani ya AA mwaka 1950 na yeye kuchaguliwa Raisi wa kwanza wa TAA?

Mag3,

Kwa hiyo wewe upo hapa kama mpiga debe wa familia ya Nyerere?

Idd Faiz Mafongo,

Siyo mweka hazina tu unajifanya unajua historia wakati hujui kazi alizokuwa anazifanya Mzee Faiz Mafongo ngoja nikupe darsa kidogo kuhusu huyu mzee unayemponda.

Huyu pamoja kuwa mweka hazina wa TANU vilevile aliifanyia kampeni TANU, akifuatana na Nyerere katika safari za awali za kukitangaza chama, akihutubia mikutanoni jukwaa moja na Nyerere. Na yeye na kaka yake Idd Tosiri ndiyo waliompeleka Nyerere kwa binamu yao Sheikh Mohamed Ramia wa Bagamoyo.

Idd Faiz alikwenda mpaka Tanga kutafuta pesa za kuongezea safari ya Nyerere kwenda UNO.

Mlivyokuwa na dharau mnaropoka tu ovyo eti mweka hazina nani atamuenzi.

Hayo maswali yako hayana tija unauliza ili ujifunze.
 
Last edited by a moderator:
Wewe umekuja kwa papara ukala za uso unatafuta pakutokea huna. Hivi ulifikiri nyerere ndio muasisi wa TANU?

Umeisoma hotuba ya Mwalimu Nyerere wakati akiliaga taifa mbele ya wazee wa Dar?
 
huna hoja yakusumbua akili yangu, Lau ungelikuwa gaid kama Mohamed Said ningeshughulika nawewe, by the way unaweza

kujibu hoja kumsaidia Kibwetele (mohamedi) maana wewe nimfuasi wake. sana sana naweza kopi na kukuwekea maswali hapa

nikiona inafaa ukweli nikwamba huna majibu.

Mshume ulimjuwa kabla ya kusoma maandiko ya Mohamed Said?

Au ulizoea kujazwa ujinga kuwa historia ya Uhuru wa Tanganyika ilianzia kwa nyerere na kuishia kwa nyerere?
 
Mag3,

Kwa hiyo wewe upo hapa kama mpiga debe wa familia ya Nyerere?

Idd Faiz Mafongo,

Siyo mweka hazina tu unajifanya unajua historia wakati hujui kazi alizokuwa anazifanya Mzee Faiz Mafongo ngoja nikupe darsa kidogo kuhusu huyu mzee unayemponda.

Huyu pamoja kuwa mweka hazina wa TANU vilevile aliifanyia kampeni TANU, akifuatana na Nyerere katika safari za awali za kukitangaza chama, akihutubia mikutanoni jukwaa moja na Nyerere. Na yeye na kaka yake Idd Tosiri ndiyo waliompeleka Nyerere kwa binamu yao Sheikh Mohamed Ramia wa Bagamoyo.

Idd Faiz alikwenda mpaka Tanga kutafuta pesa za kuongezea safari ya Nyerere kwenda UNO.

Mlivyokuwa na dharau mnaropoka tu ovyo eti mweka hazina nani atamuenzi.

Hayo maswali yako hayana tija unauliza ili ujifunze.
Ndugu yangu kwani shida ipo wapi? Nani kakataa kutambua mchango wa Idd Faiz?

Wapi kadharauliwa?
 
Last edited by a moderator:
Mohamed Said, Japokuwa ni vizuri kwa hilo, Ikiwa unataka kila mtu aliyekuwa ndani ya TAA/TANU aenziwe, hivi leo hii watunza fedha wa ccm na wa Chadema hivi leo wewe unawafahamu na wanaenziwa kwa uzito gani katika majukwaa ya siasa?

Halafu wewe ndiyo unasema mnataka kuandika historia mpya.

Hebu ni tutajie wanachama 20 wa mwanzo wa TANU.
 
Mkuu Maalim Mohamed Said, pamoja na tofauti zetu haswa katika uzushi kwa Nyerere, uchochezi, uwongo na fitna na uchonganishi, siku zote huwa nakupongeza kwa uwezo wako mkubwa wa kusimulia hadithi, natamani ningekuwa nimechumbia kwako ili wajukuu zako wafaidi hadithi za babu, hopping usingewalisha hii sumu ya udini iliyotamalaki katika simulizi zako.

Mmoja kati ya uliowataja kwenye picha hii ni Robert Makange, huyu na Baghdelah, waliwahi kufungwa gerezani kwa kuitumikia TANU.

Asante kutukumbushia. Asante na mleta picha!.
Pasco.

Rashid Heri Baghdelleh.
Angalia ''spelling'' yako unakosea.

Baghdelleh alikuwa rafiki ya baba yangu akija hata nyumbani kwetu.

Mara ya mwisho kaja nyumbani baba hayupo akaacha salamu.
Ndiyo mara yangu ya mwisho kumtia machoni akiwa hai.

Illipigwa simu nyumbani kumuarifu baba yangu kuwa Rashid Heri Baghdelleh
amepata ajali ya gari Arusha na kufariki.

Kwa nini nasema haya hapa ukumbini ni kutaka kuwajuvya kuwa watu hawa
mimi kwa hakika ni wazee wangu.

Tuendelee...

Mwaka 1964 Baghdelleh alikuwa ndiyo Mkuu wa Mkoa Tabora.
Huo ndiyo mwaka babu yangu kafungwa jela Uyui kwa ''kutaka kupindua serikali.''

Baba yangu anamuuliza Baghdelleh ''Vipi Rashid ni kweli mzee alikuwa na mipango
na wanajeshi kuangusha serikali?''

Baghdelleh anatingisha kichwa anamwambia baba, ''Sikiza Said mzee atatoka hakuna
kitu kama hicho wewe nakuomba vuta subra tu...''

Lakini uongo huu ulienezwa sana na baadhi ya watu waliuamini hadi leo.

Ndiyo babu yangu sasa baada ya kutoka kifungoni akawa anawaita baadhi ya watu ''waongo.''

Waongo kwa kuwa walimsingizia alikuwa anaandaa jeshi kupindua serikali ya Nyerere wakati
haikuwa kweli.

Alhamdulilah najua mengi sana katika historia ya nchi hii.
 
Nilikuwepo. Wewe ndio ujazwe ujinga kwa kumsoma. Ulimsikia aliposahau cheo cha Abdul Wahid, au hilo hujasikilizishwa?

Kuwepo sio tiketi yakuelewa kilichozungumzwa, kama hapa tu unakuwa mzito kuelewa, je utaelewa chakusikliza tu bila kusisitizwa na kukaziwa kam tufanyavyo hapa kwako?
 
Hili la MM la kuhamisha "magoli" nimecheka saana. Kinachonishangaza sana mimi, ni kwa nini hotuba za Nyerere au maandishi yake yachukuliwe kama uhalisia yaani alichosema au alichoandika ndio cha kweli na kinachosemwa au kuandikwa na wengine kinachambuliwa na kuonekana ni uwongo na uzushi. kwa nini?

Nyerere, kama binadamu wengine, akisema au akiandika lazima tuchambue. Ya maana na ya kweli tunakubali ni sawa, lakini tusimeze kila alichoandika au kusema.

Nakumbuka enzi ya zidumu...
 
Mag3,

Kwa hiyo wewe upo hapa kama mpiga debe wa familia ya Nyerere?

Idd Faiz Mafongo,

Siyo mweka hazina tu unajifanya unajua historia wakati hujui kazi alizokuwa anazifanya Mzee Faiz Mafongo ngoja nikupe darsa kidogo kuhusu huyu mzee unayemponda.

Huyu pamoja kuwa mweka hazina wa TANU vilevile aliifanyia kampeni TANU, akifuatana na Nyerere katika safari za awali za kukitangaza chama, akihutubia mikutanoni jukwaa moja na Nyerere. Na yeye na kaka yake Idd Tosiri ndiyo waliompeleka Nyerere kwa binamu yao Sheikh Mohamed Ramia wa Bagamoyo.

Idd Faiz alikwenda mpaka Tanga kutafuta pesa za kuongezea safari ya Nyerere kwenda UNO.

Mlivyokuwa na dharau mnaropoka tu ovyo eti mweka hazina nani atamuenzi.

Hayo maswali yako hayana tija unauliza ili ujifunze.

Idd Faiz alitoa fedha vilevile katika hazina ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika akatia katika
mfuko wa TANU kwa ajili ya safari ya Nyerere UNO, New York 1955.
 
Umeisoma hotuba ya Mwalimu Nyerere wakati akiliaga taifa mbele ya wazee wa Dar?
Ha ha ha!

Usichokijua ni kuwa katika ile hotuba wengi wamefunguka macho pale nyerere mwenyewe alipokuwa anakiri kuwa hata jina la TANU alilikuta tayari limeshafikiriwa.

Swali langu kwako wewe unayetaka kutuandikia historia inayotugusa zaidi ya watu milioni 40, una uhusiano gani na Julius nyerere?
 
Halafu wewe ndiyo unasema mnataka kuandika historia mpya.

Hebu ni tutajie wanachama 20 wa mwanzo wa TANU.

Allah anafanya mambo yake kwa njia za ajabu sana.

Marehemu Abdu Sykes alipotezwa kabisa katika historia ya kudai uhuru.

Katika uhai wake alikwepa sana kusema kuwa TANU kaianzisha yeye au
hata hiyo ofisi ya TANU kajenga baba yake.

Abdu akasahauliwa kwa takriban miaka 20 hadi nilipomwandika katika gazeti
na gazeti likasakwa na kuchomwa moto.

Hebu tazama leo Abdu alivyokuwa midomoni mwa watu.

Kila mtu anataka kujua huyu Abdulwahid Sykes alikuwa nani na kafanya nini
katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Allah ana maajabu.
Allah amerejesha hadhi na heshima yake baada ya miaka mingi kupita.

Ana mjukuu wake anaitwa Abdulwahid Kleist Sykes kila anapokutana na
mimi haishi kufurahi.

Ananambia siku moja darasani Canada katoa kitabu cha babu yake anawaonesha
wenzake...

''I come from a very prominent family in Tanzania read this book.''
Abdulwahid mjukuu anatamba darasani.

Nacheka namwambia, ''Abdu learn from your namesake he was a very humble person...''
 
Kuwepo sio tiketi yakuelewa kilichozungumzwa, kama hapa tu unakuwa mzito kuelewa, je utaelewa chakusikliza tu bila kusisitizwa na kukaziwa kam tufanyavyo hapa kwako?

Naona wewe bado hujaelewa kuwa nyerere aliwekwa nyumbani kwa Abdulwahid. Au nalo ulilijuwa kabla ya kumsoma MS?
 
nyerere_departing_for_UNO.jpg

Safari ya UNO.

Mag3,

Anasema hawa ni wasaidizi wa Nyerere tu. Yericko, yeye anasema Maliale ndiyo alitoa mchango mkubwa wa safari ya Nyerere kwenda UNO.
Idd Faiz Mafongo kulia kwa Nyerere leo anafananishwa na mweka hazina wa Chadema na CUF.
 
Last edited by a moderator:
Jamaa yako Mag3, Msome ndiyo nimemjibu anakuambia mweka hazina umuenzi wa nini?
Kijana, ungekaa pembeni kidogo kwani hakuna unachochangia cha maana...msaidie mentor wako kujibu maswali aliyoulizwa. Wakati nasubiri majibu kwa maswali yangu sita ya mwanzo, nimeongezea na la saba...maswali yenyewe ni haya;

  1. Abdulwahid Sykes aliingia kwenye uongozi wa AA mwaka gani kwa mara ya kwanza na kwa wadhifa gani?
  2. Je mwaka 1946, Mwalimu Nyerere alipohudhuria mkutano wa AA Dar es Salaam kama katibu wa tawi la Tabora, Abdulwahid alikuwa na nafasi gani ndani ya AA?
  3. Je, Abdulwahid Sykes alihudhuria huo mkutano uliofanyika mwaka 1946 Dar es Salaam na kwa wadhifa upi ndani ya AA?
  4. Je, Abdulwahid Sykes kama alihudhuria, kwa nini idaiwe ni mwaka saba baadaye, 1953, ndio kakutana na Nyerere kwa mara ya kwanza?
  5. Je, kama mwaka 1946, Abdulwahid Sykes hakuwa na sifa wala wadhifa wa kuhudhuria huo mkutano wa AA, nani kati yake na kaka yake Mwalimu Nyerere alitangulia kwenye siasa?
  6. Je si kweli kuwa Dr. Kyaruzi, aliyefahamiana na Mwalimu Nyerere toka Makerere, ndiye aliongoza mapinduzi ndani ya AA mwaka 1950 na yeye kuchaguliwa Raisi wa kwanza wa TAA?
  7. Mkutano wa kwanza wa kuizindua AA mwaka 1929, ulifanyika nyumbani kwa nani na chini ya uongozi wa nani?
Uzuri moja wa ukweli ni kuwa uongo hauthubutu kukaa nao chumba kimoja...ukweli ukidhihirika uongo huoooo...hutokomea huko huko gizani kuliko maskani yake ya siku zote hata kama uliweza kudumu kwa miaka 15.
 
Back
Top Bottom