Ritz hata kama wewe ni mpiga debe, hebu changanya na akili kidogo...ni katika nchi gani na ulimwengu upi ambapo mweka hazina wa chama cha siasa anatajwa au kuenziwa kwa mchango wake katika harakati za kisiasa?
Je chama ANC kilichoanzishwa na Zuberi Mtemvu, mweka hazina wake alikuwa nani?
Je chama cha CUF, Chadema, TLP na kile cha cha Mafisadi na wauaji, mbona hawatajwi?
Ingefaa zaidi kama ungemsaidia Mohamed Said kujibu maswali anayoulizwa, acha papara papara! Kwa kukumbusha maswali ni haya kumhusu mzee wake Mohamed, Abdulwahid Sykes, mjukuu wa mlowezi, Mzulu, aliyetumiwa na Wajerumani kuwapiga vita na kuwaua Watanganyika;
- Abdulwahid Sykes aliingia kwenye uongozi wa AA mwaka gani kwa mara ya kwanza na kwa wadhifa gani?
- Je mwaka 1946, Mwalimu Nyerere alipohudhuria mkutano wa AA Dar es Salaam kama katibu wa tawi la Tabora, Abdulwahid alikuwa na nafasi gani ndani ya AA?
- Je, Abdulwahid Sykes alihudhuria huo mkutano uliofanyika mwaka 1946 Dar es Salaam na kwa wadhifa upi ndani ya AA?
- Je, Abdulwahid Sykes kama alihudhuria, kwa nini idaiwe ni mwaka saba baadaye, 1953, ndio kakutana na Nyerere kwa mara ya kwanza?
- Je, kama mwaka 1946, Abdulwahid Sykes hakuwa na sifa wala wadhifa wa kuhudhuria huo mkutano wa AA, nani kati yake na kaka yake Mwalimu Nyerere alitangulia kwenye siasa?
- Je si kweli kuwa Dr. Kyaruzi, aliyefahamiana na Mwalimu Nyerere toka Makerere, ndiye aliongoza mapinduzi ndani ya AA mwaka 1950 na yeye kuchaguliwa Raisi wa kwanza wa TAA?