Hakika nachagua kipi cha kujibu kipi cha kukinyamazia.
Mimi sihitaji kushawishi mtu kuniamini.
Mbona hili nishalisema sana humu?
Kwani kuna faida gani kwa mimi kuaminika kile nisemacho khasa
wakati huu ambapo kitabu kiko sokoni huu mwaka wa 15 na
''reviews'' zimekamilka.
Japo nilitaka nikuache uendelee kuandika bila kukosolewa lakini kwa ajili ya vijana wanaoingia humu itakuwa si kuwatendea haki kuacha usema vitu visivyo na mantiki (illogical).
Mtu anapotoa madai (claim) wakati huo huo anataka watu waamini madai yake. Huwezi kutoa madai bila -wakati huo huo- kudai imani.
Mtu akisema "gari lile ni bovu" anatoa dai kuwa 'gari ni bovu' lakin implicitly anataka watu waamini kuwa gari ni bovu. Sasa watu wakiliona gari na kwa kuangalia nje hawaoni 'ubovu wowote' basi yule aliyetoa dai (claim) kuwa gari ni bovu anajukumu la kkwanza la kuwapa ushahidi wa dai lake - evidence of his claim. Hii ni kanuni za msingi kabisa katika mantiki (principles of logic). Sasa huyu aliyetoa dai ana uhuru wa kuleta ushahidi na anaweza kuleta ushahidi wa kila aina autakao. Lakini katika kuleta ushahidi watu wataanza kuamini kama ataleta ushahidi wa kuamini (credible proof).
Kwa mfano: Anaweza ksuema "gari ni bovu kwa sababu Bw. Sudi kaniambia ni bovu"
Sasa watu wanaweza kuamua huyu Bw. Sudi ni nani hadi aaminike. Itabidi tuulize "Sudi ni nani". Atatuambia ni "fundi Mekanika na ndiye aliyegundua matatizo ya gari lenyewe" Sasa akisema hivyo, tunavutwa kuamini madai yake kwani ushahidi aliotoa ni credible. Lakini akisema "Bw. Sudi ni fundi cherehani alisikia gari lina ngurumo fulani hivi ndio aliniambia" basi ushahidi wake bado hautoshi kutufanya tuamini kuwa gari ni bovu.
Sasa, kwenye mantiki (logic) kila dai linahitaji kuaminiwa na katika kuaminiwa kila dai linahitaji ushahidi ama wa kimantiki, factual, scientific, historical au hata mathematical n.k. Ukisema kwa mfano "Nyerere aliua maelfu ya Wanyaturu" ni dai hilo na linadai facts na hivyo linataka kuaminiwa. Sasa kwa vile mtu kasema hivyo huwezi kudakia na kuanza kutangaza "Nyerere aliua maelfu ya Wanyaturu"!
Mfano mzuri wa hili ni madai kuwa "Maelfu ya watu walikufa wakati wa operesheni ya vijiji vya ujamaa". Dai hili utakutana nalo kwenye maandishi mengi sana ya waandishi wa Magharibi (Western authors) na limekuwa likirudiwa hata na waandishi wetu wasomi. Lakini kila siku tunauliza hawa maelfu waliokufa ni kina nani? Walizikwa wapi? hadi leo hajatokea mtu na kutupa namba inayokaribia maelrfu ya watu lakini wanataka tuamini tu kwa sababu mtu fulani alisema huko zamani!
Nasema hivi kwa sababu hoja zako zote unazotoa humu zinadai imani; zinataka kushawishi watu waamini. Tatizo ni kuwa hutaki kuweka ushahidi kwanini watu waamini! Japo unasema unaandika siyo ili watu waamini lakini ukweli kama usingetaka watu waamini usingeandika - hii inaitwa logical contradiction!
Unapodai Nyerere alishiriki katika kuiua EAMWS unatoa dai zito ambalo unataka watu waliamini;
Unapodai Nyerere aliingizwa katika siasa na kina Abdul Sykes mwaka 1953 unataka watu waamini;
Unapodai Nyerere alikuja kwa marra ya Kwanza jijin iDar mwaka 1952 na alikuwa hajulikani unataka watu waamini;
Unapodai kuwa kulikuwa na kundi la Waislamu waliotaka kumuondoa Nyerere madarakani kwa sababu ya Ukristu wake unataka watu waamini;
Unapodai kanisa lilikula njama dhidi ya Uislamu ili kuudhoofisha unataka waamini kuwa ni kweli;
Unapodai kuwa Benjamin Mkapa alikula njama dhidi ya Waislamu unataka watu waamini kuwa ni kweli;
Unapodai kuwaBAKWATA iliundwa na Nyerere siyo na Waislamu wazalendo unataka watu waamini;
Unapodai kwenye kichwa cha habari cha kitabu chako kuwa kuna historia ya iliyofichwa ya Waislamu unataka watu waamini kuwa ni kweli;
Sasa, hakuna dai lolote ambalo umelitoa iwe humu au kwenye maandishi yako mengine ambalo halidai kuaminiwa! Tatizo linapokuja ni kuwa watuw anasema "tupe sababu ya kuamini unachosema" unageuka na kusema:
Mimi sihitaji kushawishi mtu kuniamini.
Mbona hili nishalisema sana humu?
It is oddly incredible that such an assertion can be made by someone claiming to have written an 'historical account' of what 'really' happened. It is more incredible that there are some people - who look like sane - believe in that account and praise you for that! Absrudities have many colors but yours sir, surpass them all!
Don't make a claim if you can't back it up! But if you make one; prove.
Mojawapo ya aya ninazozipenda kwenye Qurani ni hii:
Yaani;
2:111. Na walisema: Hataingia Peponi ila aliyekuwa Yahudi au Mkristo. Hayo ni matamanio yao. Sema: Leteni ushahidi wenu kama nyinyi ni wasema kweli.
Sasa utaona kuwa hata Qurani haikubali madai bila ushahidi! Walikuwa watu wanasema wakati wa Mtume kuwa hatoingia mtu peponi isipokuwa awe Myahudi au Mkristo, sasa Mtume anaambiwa waambie "lete ushahidi wenu kama nyinyi wasema kweli".
Mzee Said kama huna ushahidi usitoe madai; ila ukitoa madai 'bring your proof'!