Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Ha ha ha!

Usichokijua ni kuwa katika ile hotuba wengi wamefunguka macho pale nyerere mwenyewe alipokuwa anakiri kuwa hata jina la TANU alilikuta tayari limeshafikiriwa.

Swali langu kwako wewe unayetaka kutuandikia historia inayotugusa zaidi ya watu milioni 40, una uhusiano gani na Julius nyerere?
Inawezekana leo ndio umeona historia ya uhuru wetu mkuu?
 
Ndugu yangu,huww sijibu maswali ya kejeli.

Tusonge mbele mkuu

Mimi sifanyi kejeli ndugu yangu nimekuuliza tu tutajie wanachama 20 wa mwanzo wa TANU unaniambia hujibu kejeli. Hakuna kejeli apo ndiyo tunafahamishana historia yetu.
 
Naona wewe bado hujaelewa kuwa nyerere aliwekwa nyumbani kwa Abdulwahid. Au nalo ulilijuwa kabla ya kumsoma MS?

Tupo hapa tangu 12/1/2013, pole sana kwakuchelewa kujiunga na mjadala huu, nakusihi rudia kusoma uzi huu na post zake zote, hayo yote yamejibiwa vema
 
Bursar,

Mimi ni mpenzi wa mijadala.

Nimefunzwa na maalim wangu Sheikh Haruna adab
za minakasha.

Kubwa ni kutoingia katika mjadala kwa kuonyesha kuwa wewe
ni mjuzi kuwapita wenzako.

Usiingie mjadala na mtu alieghadhibioka na mtu atukanae na kutumia
lugha chafu pamoja na kejeli.

Usilazimishwe kujibu kitu.
Shauri nafsi yako kwa kutafuta kusema lile lenye kheri.

Mnakasha uongeze ilm.
Ikiwa hilo halipatikani jitoe.

Wapime watu hawa unaoniomba nisemezanenao je wanaingia wapi katika
usia wa maalim wangu?

Nimekusoma Mzee wangu MS
 
Ndugu yangu,huww sijibu maswali ya kejeli.

Tusonge mbele mkuu

Mimi sifanyi kejeli ndugu yangu nimekuuliza tu tutajie wanachama 20 wa mwanzo wa TANU unaniambia hujibu kejeli. Hakuna kejeli apo ndiyo tunafahamishana historia yetu.
 
Kijana, ungekaa pembeni kidogo kwani hakuna unachochangia cha maana...msaidie mentor wako kujibu maswali aliyoulizwa. Wakati nasubiri majibu kwa maswali yangu sita ya mwanzo, nimeongezea na la saba...maswali yenyewe ni haya;

  1. Abdulwahid Sykes aliingia kwenye uongozi wa AA mwaka gani kwa mara ya kwanza na kwa wadhifa gani?
  2. Je mwaka 1946, Mwalimu Nyerere alipohudhuria mkutano wa AA Dar es Salaam kama katibu wa tawi la Tabora, Abdulwahid alikuwa na nafasi gani ndani ya AA?
  3. Je, Abdulwahid Sykes alihudhuria huo mkutano uliofanyika mwaka 1946 Dar es Salaam na kwa wadhifa upi ndani ya AA?
  4. Je, Abdulwahid Sykes kama alihudhuria, kwa nini idaiwe ni mwaka saba baadaye, 1953, ndio kakutana na Nyerere kwa mara ya kwanza?
  5. Je, kama mwaka 1946, Abdulwahid Sykes hakuwa na sifa wala wadhifa wa kuhudhuria huo mkutano wa AA, nani kati yake na kaka yake Mwalimu Nyerere alitangulia kwenye siasa?
  6. Je si kweli kuwa Dr. Kyaruzi, aliyefahamiana na Mwalimu Nyerere toka Makerere, ndiye aliongoza mapinduzi ndani ya AA mwaka 1950 na yeye kuchaguliwa Raisi wa kwanza wa TAA?
  7. Mkutano wa kwanza wa kuizindua AA mwaka 1929, ulifanyika nyumbani kwa nani na chini ya uongozi wa nani?
Uzuri moja wa ukweli ni kuwa uongo hauthubutu kukaa nao chumba kimoja...ukweli ukidhihirika uongo huoooo...hutokomea huko huko gizani kuliko maskani yake ya siku zote hata kama uliweza kudumu kwa miaka 15.
Mkuu hao vijana wafuta viatu wa Shehe Mohamed Said ikiwezekana usiwajibu tu,wanayumbisha mjadala tu huu.

Tuendelee na Shehe wao angalau yeye anajaribu kujibu baadhi ya hoja na kujenga hoja pia.
 
Tupo hapa tangu 12/1/2013, pole sana kwakuchelewa kujiunga na mjadala huu, nakusihi rudia kusoma uzi huu na post zake zote, hayo yote yamejibiwa vema

Mbona haya ni marudio tu, labda wewe hujuwi kuwa nyuzi nyingi zilifungwa, futwa na baadhi zikarudishwa zingine zimeyayushwa. Usidhani wewe ndio muasisi wa hizi kejeli zenu zinazowasuta nafsi zenu, zipo siku nyingi na wala huna jipya ulilolileta. Bado hujaja hata na moja la kukosoa maandiko ya MS na kuleta mbadala. Naona mara Somalia mara Nigeria, vipi Biafra mbona hukupataja?
 
Hapa Naona mnapeana za USO ila mnaniuzi wengine kuingiza Imani za kidini na itikadi za kichama mnaongelea history na sio politic.
 
Ndugu yangu,huww sijibu maswali ya kejeli.

Tusonge mbele mkuu
Hivi leo? siye wewe uliyekuwa ukimkejeli Mohamed Said na kudai kuwa imo katika kanuni za mijdala hapa JF?
Yericko Nyerere said:
je utaelewa chakusikliza tu bila kusisitizwa na kukaziwa kam tufanyavyo hapa kwako?
Delusion of grandeur!
Yericko Nyerere said:
Inawezekana leo ndio umeona historia ya uhuru wetu mkuu?
Hayo ni maoni au swali? eleweka...ikiwa huwezi kuelezea sentensi moja na kueleweka vipi utakuja kueleweka wakati ukiiandika historia ya Tanzania? au unafikiri kuwa na jina la nyerere tu kuna kupa wewe haki ya kuwaandikia Watanzania wote historia yao?

Swali bado lipo palepale; una uhusiano gani na julius nyerere?
 
mkuu hao vijana wafuta viatu wa shehe mohamed said ikiwezekana usiwajibu tu,.

Tuendelee na shehe wao angalau yeye anajaribu kujibu baadhi ya hoja na kujenga hoja pia.

achana na hizo kejeli,jibu lile swali linauliza ya kwamba>> unaamua nawewe kuandika historia ya kumtetea mzee wako julius,je,wewe una uhusiano gani na nyerere??
 
Hakika nachagua kipi cha kujibu kipi cha kukinyamazia.

Mimi sihitaji kushawishi mtu kuniamini.
Mbona hili nishalisema sana humu?

Kwani kuna faida gani kwa mimi kuaminika kile nisemacho khasa
wakati huu ambapo kitabu kiko sokoni huu mwaka wa 15 na
''reviews'' zimekamilka.

Japo nilitaka nikuache uendelee kuandika bila kukosolewa lakini kwa ajili ya vijana wanaoingia humu itakuwa si kuwatendea haki kuacha usema vitu visivyo na mantiki (illogical).

Mtu anapotoa madai (claim) wakati huo huo anataka watu waamini madai yake. Huwezi kutoa madai bila -wakati huo huo- kudai imani.

Mtu akisema "gari lile ni bovu" anatoa dai kuwa 'gari ni bovu' lakin implicitly anataka watu waamini kuwa gari ni bovu. Sasa watu wakiliona gari na kwa kuangalia nje hawaoni 'ubovu wowote' basi yule aliyetoa dai (claim) kuwa gari ni bovu anajukumu la kkwanza la kuwapa ushahidi wa dai lake - evidence of his claim. Hii ni kanuni za msingi kabisa katika mantiki (principles of logic). Sasa huyu aliyetoa dai ana uhuru wa kuleta ushahidi na anaweza kuleta ushahidi wa kila aina autakao. Lakini katika kuleta ushahidi watu wataanza kuamini kama ataleta ushahidi wa kuamini (credible proof).

Kwa mfano: Anaweza ksuema "gari ni bovu kwa sababu Bw. Sudi kaniambia ni bovu"

Sasa watu wanaweza kuamua huyu Bw. Sudi ni nani hadi aaminike. Itabidi tuulize "Sudi ni nani". Atatuambia ni "fundi Mekanika na ndiye aliyegundua matatizo ya gari lenyewe" Sasa akisema hivyo, tunavutwa kuamini madai yake kwani ushahidi aliotoa ni credible. Lakini akisema "Bw. Sudi ni fundi cherehani alisikia gari lina ngurumo fulani hivi ndio aliniambia" basi ushahidi wake bado hautoshi kutufanya tuamini kuwa gari ni bovu.

Sasa, kwenye mantiki (logic) kila dai linahitaji kuaminiwa na katika kuaminiwa kila dai linahitaji ushahidi ama wa kimantiki, factual, scientific, historical au hata mathematical n.k. Ukisema kwa mfano "Nyerere aliua maelfu ya Wanyaturu" ni dai hilo na linadai facts na hivyo linataka kuaminiwa. Sasa kwa vile mtu kasema hivyo huwezi kudakia na kuanza kutangaza "Nyerere aliua maelfu ya Wanyaturu"!

Mfano mzuri wa hili ni madai kuwa "Maelfu ya watu walikufa wakati wa operesheni ya vijiji vya ujamaa". Dai hili utakutana nalo kwenye maandishi mengi sana ya waandishi wa Magharibi (Western authors) na limekuwa likirudiwa hata na waandishi wetu wasomi. Lakini kila siku tunauliza hawa maelfu waliokufa ni kina nani? Walizikwa wapi? hadi leo hajatokea mtu na kutupa namba inayokaribia maelrfu ya watu lakini wanataka tuamini tu kwa sababu mtu fulani alisema huko zamani!

Nasema hivi kwa sababu hoja zako zote unazotoa humu zinadai imani; zinataka kushawishi watu waamini. Tatizo ni kuwa hutaki kuweka ushahidi kwanini watu waamini! Japo unasema unaandika siyo ili watu waamini lakini ukweli kama usingetaka watu waamini usingeandika - hii inaitwa logical contradiction!

Unapodai Nyerere alishiriki katika kuiua EAMWS unatoa dai zito ambalo unataka watu waliamini;
Unapodai Nyerere aliingizwa katika siasa na kina Abdul Sykes mwaka 1953 unataka watu waamini;
Unapodai Nyerere alikuja kwa marra ya Kwanza jijin iDar mwaka 1952 na alikuwa hajulikani unataka watu waamini;
Unapodai kuwa kulikuwa na kundi la Waislamu waliotaka kumuondoa Nyerere madarakani kwa sababu ya Ukristu wake unataka watu waamini;
Unapodai kanisa lilikula njama dhidi ya Uislamu ili kuudhoofisha unataka waamini kuwa ni kweli;
Unapodai kuwa Benjamin Mkapa alikula njama dhidi ya Waislamu unataka watu waamini kuwa ni kweli;
Unapodai kuwaBAKWATA iliundwa na Nyerere siyo na Waislamu wazalendo unataka watu waamini;
Unapodai kwenye kichwa cha habari cha kitabu chako kuwa kuna historia ya iliyofichwa ya Waislamu unataka watu waamini kuwa ni kweli;

Sasa, hakuna dai lolote ambalo umelitoa iwe humu au kwenye maandishi yako mengine ambalo halidai kuaminiwa! Tatizo linapokuja ni kuwa watuw anasema "tupe sababu ya kuamini unachosema" unageuka na kusema:
Mimi sihitaji kushawishi mtu kuniamini.
Mbona hili nishalisema sana humu?

It is oddly incredible that such an assertion can be made by someone claiming to have written an 'historical account' of what 'really' happened. It is more incredible that there are some people - who look like sane - believe in that account and praise you for that! Absrudities have many colors but yours sir, surpass them all!

Don't make a claim if you can't back it up! But if you make one; prove.

Mojawapo ya aya ninazozipenda kwenye Qurani ni hii:

2_111.png


Yaani;

2:111. Na walisema: Hataingia Peponi ila aliyekuwa Yahudi au Mkristo. Hayo ni matamanio yao. Sema: Leteni ushahidi wenu kama nyinyi ni wasema kweli.

Sasa utaona kuwa hata Qurani haikubali madai bila ushahidi! Walikuwa watu wanasema wakati wa Mtume kuwa hatoingia mtu peponi isipokuwa awe Myahudi au Mkristo, sasa Mtume anaambiwa waambie "lete ushahidi wenu kama nyinyi wasema kweli".

Mzee Said kama huna ushahidi usitoe madai; ila ukitoa madai 'bring your proof'!
 
Yericko Nyerere,

Tupe basi habari za Mashado kidogo bila kumnukuu Mohamed Said. Au japo za Dosa Aziz.


Nakuhakikishia huwezi, thumma huwezi.
 
Last edited by a moderator:
TANU ilikuwa na watu wa aina yake hujapatapo kuona.
Nyerere aliipa jina ile hali ya mapenzi na udugu "the TANU spirit."

Angalia udugu wa Abdu na Nyerere.
Mama yake Abdu ndiyo akifua nguo za Abdu na Nyerere.

Hapo wako "retreat" Kirk Street kwa Bi Mluguru.

Angalia uhusiano wa baba na mtoto kati ya Mzee Mshume na Nyerere.

Sasa njoo kwa Dossa "the bank" Aziz na Nyerere.
Dossa anamsifia Nyerere anasema alikuwa mtu muadilifu sana hafuji fedha.

Wakati mwingine anakataa kupanda taxi na masurufu Dossa kampa.

Yako mengi.

Huu haukuwa uhusiano wa "master-servant."
Huwezi kumwita Idd Faiz, Abdu, Dossa au Mshume "wasaidizi."

Huo ni wizi wa fadhila na kuwakosea adabu watu hawa.
Kidogo tunachoweza kuwalipa ni kutunza heshima zao.
 
hadi hapa tulipofikia sijaona ni nani miongoni mwao,na hata tuseme wote wakiungana kwa umoja wao kama wana uwezo wa kuandika kitabu chenye mantiki na uwezo wa kutenza nguvu za hizo wanazoziita ngano za moh said,wote wanatia huruma tuh,as time goes tunaona kuongezeka kwa wingi wa kejeli tuh,na uchache wa hoja zao.
 
Mkuu hao vijana wafuta viatu wa Shehe Mohamed Said ikiwezekana usiwajibu tu,wanayumbisha mjadala tu huu.

Tuendelee na Shehe wao angalau yeye anajaribu kujibu baadhi ya hoja na kujenga hoja pia.

Yericko Nyerere,

Unazidi kujivunjia tatizo umejaa dharau na kibri wewe mwenyewe umetoka kusema huwa hujibu kejeli halafu wewe huyo huyo unawaandikia wenzako kejeli.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom