zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,930
Mojawapo ya aya ninazozipenda kwenye Qurani ni hii:
Yaani;
111. Na walisema: Hataingia Peponi ila aliyekuwa Yahudi au Mkristo. Hayo ni matamanio yao. Sema: Leteni ushahidi wenu kama nyinyi ni wasema kweli.
Sasa utaona kuwa hata Qurani haikubali madai bila ushahidi! Walikuwa watu wanasema wakati wa Mtume kuwa hatoingia mtu peponi isipokuwa awe Myahudi au Mkristo, sasa Mtume anaambiwa waambie "lete ushahidi wenu kama nyinyi wasema kweli".
Mzee Said kama huna ushahidi usitoe madai; ila ukitoa madai 'bring your proof'!
Siku za nyuma nilishawahi kukupa darsa kuhusu kunukuu aya za Qur'an ili usipotoshe umma. Leo narudia somo ingawa ni tofauti kidogo na lileeeee, nna uhakika unalikumbuka.
Ukinukuu aya za Qur'an uwe makini kuweka sura na aya, hapa wewe umeweka namba ya aya tu (111), kumbuka, kwa hii ulitakiwa uandike Qur'an 2:111 ikimaanisha ni sura ya pili na aya ya 111. Kumbuka, zipo sura zaidi ya moja zenye aya ya 111.